Bashe: Si Lowassa pekee aliyeonewa CCM

Bashe: Si Lowassa pekee aliyeonewa CCM

acha wehu ukimuonea mtu nimipango yamungu?
Hata hivyo Nikuulize Mungu yupi ?
Labda anayeala makaburini ?

Kwanza hizi ni tawala za wanadamu
yeyote iwe kwa hila au haki anaweza
kufanya chochote au kupata
cheo chochote !

Waachie waccm mada yao waijadili
 
Mbona Lowassa anaandikwa sana kwenye media tangu juzi, jamani lakini umri unabadilisha watu, kuna mtu wangu wa karibu akikuwa na Lowassa UDSM miaka hiyo, anasema super tall alikuwa hashikiki kwenye basket ball.
 
Kama ni kweli basi huyu jamaa huwa nampenda sana kwakuwa anamsimamo sana
Yaani misimamo kwako ni kuiponda ccm!! Aise hiki kizazi ni balaa. Vyuo vifutwe tu kibaki udsm pekee mana vyuo hivi vingine ni shida wanachukua had I div 3 ndo mana reasoning ya humu jf ni mdogo sana kama huyu kiwavi jeshi
 
Nimemisi Siasa jamani...uchaguzi wa 2015 ulikuwa na vitimbwi vyake
 
Hakuna aliyeonewa CCM, mabadiliko na kasi aliyoleta Rais Magufuli ndio imerudisha imani ya wananchi kwa chama cha CCM. Watanzania hawakuwa tayari kuendelea kutawaliwa na Wanamtandao
 
Mwenye habari kamili atuwekee hapa
Dar es Salaam. Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amesema anaamini Edward Lowassa hakuenguliwa kwa haki na CCM katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama hicho, na kwamba waziri mkuu huyo wa zamani si pekee ambaye amekumbana na uonevu kama huo.

Bashe, ambaye ameingia bungeni kwa mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana akipeperusha bendera ya CCM, pia amesema kashfa zote zinazoikumba Serikali hutengenezewa suluhisho kwa malengo fulani na si kutafuta muafaka wa haki.

Kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Bashe, ambaye alikuwa kambi ya Lowassa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM, alisema ingawa hana uhusiano tena wa kisiasa na kada huyo, anaona tukio lake kuwa ni historia ya kutotendea haki wanachama wengi wa CCM. “Si Lowassa pekee, wako wengi,” alisema Bashe katika mahojiano hayo.
 
Back
Top Bottom