Bashe: Si Lowassa pekee aliyeonewa CCM

Bashe: Si Lowassa pekee aliyeonewa CCM

We vip yaani unamshauri jamaa awe mnafiki?....

Ni bora kuongea ukweli kuliko kuwa mnafiki na kuja na ID fake kulalamika jamii forum.....

Tabia yako inatakiwa iwe ndio uharisia wa unachokitaka na unayoyafanya .....
 
Aweza kuwa chachu ya mabadiliko uko uko haliko. Bashe kaza usiwe mnafiki.
 
Inamaana hata makufuli ana support unafiki..??!!
 
Msemakweli ni mpenzi wa Mungu.Kama anachokisema ni kweli basi Mungu atamlinda.
 
Ndio tunashangaa kama PM na Makamu wa Rais walikatwa, nini EL ambaye hakuwa na wadhifa wowote!!
Kuna siku Ritz alisema hapa kwamba huko CDM Lowassa hana cheo lakini anafunguliwa mlango wa gari na wenyekiti wa Chama!!
 
Shauri yake malaika mkuu hapendi kusikia hilo jina la lowassa

Atawekwa mahala salama ooohhoo!!
 
KWANI Lowassa alichukua fomu peke yake? Huko alikokwenda CHADEMA yeye aliwatendea wenzake haki?

Dr. Slaa na Profesa Lipumba walizuiwa hata kuchukua fomu ingawa waliweka nguvu na muda wao mwingi kujenga vyama hivyo, je hiyo ni haki?

Mkuki kwa nguruwe, kwa Lowassa uchungu sana.
 
Kwani BASHE anasubiri nini SI AENDE TU MOJA KWA MOJA alupoenda MSHIKAJI sio kuzungumza vitu vilivyopita
 
hahaa bashe bana lakini huko tunakoelekea ,bashe atakuja KUMTETEA LOWASA HADI RICHMUND ALIONEWA,
akina lisu, msigwa, mbowe na bavicha walimtukana Nao pia wao walimuonea, na je huko CDM akikatwa bashe atamlaumu MBOWE pia
 
Bashe ndio mpenzi wa mungu.
Juma ni wakala wa shetani katumwa kutufanya tuishi kama mashetani.
 
Huyu kaka ni msema ukweli lakini kitakachomharibia ni kuwa katika chama cha wasiopenda kuambiwa ukweli
Sijui ni kwanini ashamie kwenye chama cha wasema kweli.

Mbona anajikosesha amani kwa kukaa na chama hiki.

Bashe Jiunge na wapenda haki na wasema kweli wenzio.
 
...hata Dr. Salim hakutendewa haki mwaka 2005 wakati jk anateuliwa kugombea..huyu huyu jk akaja kutomtendea haki lowassa mwaka 2015....kuna watu huko ccm dhambi waliyotenda itakuja kuwatafuna tu...kama si wao basi ndugu/watoto wao..
 
Lowassa hakuonewa hata kidogo. Alikichukiza chama chake na hata Mungu wa mbinguni. Kitendo cha kuanza kampeni mapema kuanza kuwapa watu pesa halafu kuwaambia waje kujifanya wanakuomba ugombee urais kilikuwa ni maudhi kwa CCM. Halafu Januari 2015 alitoa shilingi 500,000 kwa kila mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na shilingi 1,000,000 kwa kila mjumbe wa NEC ya CCM. Yeye alidai ni zawadi ya mwaka mpya lakini CCM waliona ni rushwa. Mambo mengine yote ya nyuma waweza kusahau. Lakini hayo mawili yalitosha kabisa kumtosa. Kumuudhi Mungu ni kule kuwarubuni watumishi wa Mungu wachungaji na mashehe na kuwapa pesa ili nao waende kwake kumwomba agombee urais. Mungu hawezi kufurahia mtu tajiri ambaye anatumia ufukara wa watumishi wake kufanikisha malengo yake ya kisiasa. Halafu kitendo cha Lowassa ambaye ni Mkristo kuingia msikitini na kuvalishwa kama Ustaadh ili tu apate kura za Waislam ni kumdhihaki Mungu kwa sababu leo huwezi kuwa Mwislam na Mkristo wakati huo huo. Ushenzi huu Mungu asingeruhusu ufanikiwe. Lowassa kapigwa chini na Mungu mwenyewe pamoja na CCM yake kwa makosa yake mwenyewe.
Du umenena vizuri. Kwa hiyo hata Magufuri anapoenda kwa waislamu na kuvalishwa kibandiko na kanzu ana mkufuru Mungu? Halafu ajabu anatwambia eti tumuombee, sasa tumuombee kwa mungu gani? Mungu wa waislamu au wa wakristo? kufuru hiyo kwa mungu itamuangusha 2020 na dalili zimeanza kuonekana.
 
Bashe ana haki ya kusema anachokiamini. Inashangaza sana kuona chama kinamlazimisha mtu kufikiri na kuongea jinsi wanavyotaka wakuu wa chama???

Namuunga mkona bashe
 
Back
Top Bottom