Bashe: Si Lowassa pekee aliyeonewa CCM

Bashe: Si Lowassa pekee aliyeonewa CCM

Alexandry Nemesi

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2014
Posts
1,508
Reaction score
590
Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amesema anaamini Edward Lowassa hakuenguliwa kwa haki na CCM katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama hicho, na kwamba waziri mkuu huyo wa zamani si pekee ambaye amekumbana na uonevu kama huo.

Bashe, ambaye ameingia bungeni kwa mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana akipeperusha bendera ya CCM, pia amesema kashfa zote zinazoikumba Serikali hutengenezewa suluhisho kwa malengo fulani na si kutafuta muafaka wa haki.

Kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Bashe, ambaye alikuwa kambi ya Lowassa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM, alisema ingawa hana uhusiano tena wa kisiasa na kada huyo, anaona tukio lake kuwa ni historia ya kutotendea haki wanachama wengi wa CCM. “Si Lowassa pekee, wako wengi,” alisema Bashe katika mahojiano hayo.

Chanzo: Mwananchi
 
ARUSHA .......inaelekea Lema atapita vizuri saana
Dar/Ilala.....Rhemtullah
Mikopo ya chuo itaibua kura nyingi za chuki.
 
Mbunge wa Nzega,Mh.Hussen Bashe,Amenukuliwa na Gazeti la Mwananchi toleo la leo,Akisema kuwa si Edward Lowassa Pekee aliyeonewa Ndani ya CCM.
hana mpango wa kugombea 2020 hi inaitwa potelea mbali
 
Back
Top Bottom