Bashe: Kama mnataka kutukata kodi mkateni na Rais

Bashe: Kama mnataka kutukata kodi mkateni na Rais

Hivi ukiongea ukweli ndani ya CCM umekuwa team lowassa, CCM Mungu awarehemu msiwe waoga kiasi hicho, rais aonyeshe uzalendo wake kwa kulipa kodi, hizo exemptions zote zifutwe na sheria zirekebishwe wote walipe, tofauti na hapo basi na wananchi masikini wapate hizo exemptions.
 
Kuna watu hubaki vile walivyo bila kujali wapo wapi.

Watu wanaongea wanachofikiri na sio kuongea Ili kufurahisha watu
 
Huo ndio ukweli huwezi kukata kodi kwa kiinua mgongo cha wabunge ukamuacha spika na wengine aliowataja bashe..
Spika naye si Mbunge? Mawaziri si wabunge pia?? What am I not understanding here?
 
Huyu bashe bado ni mfuasi wa Lowasa mpaka sasa hivi..Magufuli akipewa uenyekiti aanze nae huyu mamluki kumshughulikia
Tuliyategemea maneno kama haya kutoka kwa sana ccm, maana Bashe kaongea ukweli
 
Huyu bashe atawasumbua, hapa anakubali kwamba wakatwe kodi lakini wigo uwe mpana zaidi na usio onevu kwa kuwakata na wanasiasa wengineo akiwemo rais. Mawazo yake yanashabihiana na UKAWA!
Mkuu kuna siku niliweka uzi juu ya uimara wa bashe, kuwa bashe kapotea kuwa mbunge wa ccm lkn sikueleweka lkn naona sasa watu wameanza kuelewa
 
Bashe one of us....
Nimemkumbuka sana Ester Bulaya wa ccm alikuwa hivi...na hakuwa mnafiki....ukweli ni ukweli..uongo ni uongo.

KWELI ITATUWEKA HURU
 
Huyu bashe bado ni mfuasi wa Lowasa mpaka sasa hivi..Magufuli akipewa uenyekiti aanze nae huyu mamluki kumshughulikia
Yaani kama hao aliowataja hawalipi kodi basi TZ tusahau habari za maendeleo kabisa.
Kiongozi yeyote hata awe nani anapaswa kuwa mfano kwa kulipa kodi.
Kama kiongozi halipi kodi atakua anawanyonya watu wake, atawambiaje walipe kodi?
Anawezaje kutungia watu sheria ya kulipa kodi ili hali yeye mwenyewe halipi hiyo kodi?
Anawezaje kumuadhibu mtu asiyelipa kodi wakati yeye mwenyewe halipi kodi?
Hayo ni baadhi tu ya maswali ya kujiuliza kama tunataka nchi yetu iendelee.
 
Nyie na Bashe wenu wote vichwa maji ndio maana mnaropoka! Bashe anasema kuwa sheria ndio inatoa wigo wa Rais kuto kukatwa kodi halafu papo hapo anasema Rais naye akatwe kodi..hivi huyu Bashe akili ataipata lini? Hivi kuwa mfuasi wa Lowasa kuna mfanya mtu awe kama nyumbu?

Hivi Bashe nani kamkataza kupeleka hoja ya marekebisho ya sheria ili Rais awe ana katwa kodi? Ninani alitunga sheria hiyo kama si wao wenyewe? Ni nani wa kuirekebisha kama si wao wenyewe? Hivi Bashe maumivu ya Lowasa yatamuisha lini?

Mkuu mshauri kama anataka apeleke hoja ya marekebisho ya sheria ili Rais awe ana katwa kodi, kwanza naamini Rais mwenyewe ni mtu wa wanyonge kama kashusha mishahara kwa wale wa mil 40, ataijali tu na hii sheria ili wanaokuja wote kwenye hicho kiti wawe wanalipa kodi, tumpe muda mambo ni mengi.
 
Huyu bashe bado ni mfuasi wa Lowasa mpaka sasa hivi..Magufuli akipewa uenyekiti aanze nae huyu mamluki kumshughulikia
Wataibuka akina bashe wengine mkuu.
Alichokisema siyo kibaya. Hakuna mantiki walipa kodi wawe walala hoi tu. Hata nchi zilizo endelea watu wote wanalipa kodi. Fikilia eti wakuu wa mikoa hawalipi kodi, wakuu wa wilaya hawalipi kodi sababu za kutolipa kodi ni nini? wanajua wenyewe. Basi bora hiyo Kodi wasiite pay as you earn (PAYE) kwa sababu, wale wanapata kikubwa hawalipi kodi. Nashauri waiite Kodi ya mlala hoi. Ili tujue kuwa Sisi akiana Kajamba nani ndo tunapaswa kulipa kodi. Hao viongozi alio wataja Bashe kuanzia Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri et al wote wanapata fringe benefits nyingi na kubwa lakini bado hawalipi kodi. Huku ni kugawa watu katika Matabaka. Kama ni kulipa kodi basi tulipe tu wote.
 
Huyu bashe bado ni mfuasi wa Lowasa mpaka sasa hivi..Magufuli akipewa uenyekiti aanze nae huyu mamluki kumshughulikia
Umamluki wake kutupigania inaonekana wewe ndo unataka kumbukumbu ya push-ups
 
Back
Top Bottom