Bashe anataka kumfanya nini Nape?

Hapa Bashe amenichekesha sana...

...Eti Bashe akawaondoa Waandishi wake ili wasisikie yale atakayoongea na Nape...
...Ghafla eti habari ya mazungumzo yale(ambayo Bashe aliwatimua waandishi wake) ikafika Mwanahalisi...
...Eti Mwanahalisi wakampigia Bashe kumuuliza ukweli wa habari hizo...
...Ikajengwa taswira ya Bashe kushangaa jinsi habari hizo zilivyofika Mwanahalisii?...??
...Mwanahalisi wakamwambia wamezipata kwenye "chumba chake cha habari"...??
...Ikajengwa taswira ya Bashe kushangaa sana...??
...Ikajengwa taswira tena ya Bashe kuwaomba sana wasizitoe hewani,kwani CCM ina matatizo mengi na wanapoelekea kama chama ni kugumu sana...??
...........................................................................
...Ukurasa unaofuata kuna habari nyingine ya Posho..ndani yake Shujaa Bashe tena, mmmh..??
 
CCM haipaswi kujiingiza ktk siasa ktk staili ya Bomoa tutajenga kesho..., Hussein yuko sahihi sana lakini pia namuona Nape akiwa na dhamira safi ila anakosa maarifa sahihi na hekima ya kuinusuru CCM.
Kidumu chama cha Mapinduzi..
 
Jf niwatu makini.umeanza kwa kukurupuka sana tafura habarikamili Kwanza ndipo u comment. naona unahamu sana yakuanzisha Chama, ccj imetokawapi hapo?
Sio lazima uwe bookish ndo uweze kuchangia hata ktk mazingira ya mambo yanayohitaji plain common sense ,mm nimejadili scenario kwa ujumla wake kama ilivyokuwa presented na mwana jamvi.Linkage ninayoizungumzia mm ni kwamba,kwa kuwa na.pe alituhumiwa kushiriki kikamilifu ktk uanzishwaji wa ccj na yy akakubali kwa kutokanusha,na limejitokeza hili la kumtaka mkuu wake ajivue gamba,huku akimsifia majukwaani=UNAFIKI,sawa mkuu?
 
tatizo la nchi ambazo freedom of expression una mipaka. kama bosi wako hawezi kazi au ni kikwazo cha kufikia ufanisi unaotegemewa unatakiwa uweze kumwambia free from fear. lkn kwa vile sisi ni watu wa kujipendekeza na kutotaka bosi ajue kuwa nae hufanya makosa au hafai tena pale alipo, ndo maana hii inakuwa issue ya uchokozi. whether nape alisema ay hakusema, lkn neno la msingi ni la kweli kuwa mkuu wao ndio tatizo kubwa zaidi kuliko wengineo wote watwajao chini yake
 
Kikwete mbunifu sana wa mbinu za kugonganisha vichwa halafu yeye anakaa kando akichekelea mambo yanavyoenda. Alijua fika kilichoendelea ndani ya CCM wakati Sitta, Nape na Mpendazone wakihaha kuanzisha CCJ, yeye akawatibua kwa kumpa cheo Nape kuwa mkuu wa wilaya na hivyo kuwa bizu na shughuli za serikali na papo hapo akiwa chini ya usimamizi wa vyombo vya usalama kama mkuu wa wilaya. alishinda kwa hilo. Pamoja na kukwamba kumtoa Sitta kwa vile ndani ya vikao alikuwamo basi vita vikaishia kumwengua kwenye uspika na kumweka kilaza atakayefanya kila anachotaka bungeni.

Lengo la kikwete kumnyanyua Nape kwenye nafasi nyeti Chamani ilikuwa kumthibiti, lakini undani wa Nape na Kikwete wanatofautiana kwa kiasi kikubwa, ingawa kikwete kamnyanyua Nape ili kumthibiti lakini kiitikadi wanatofautiana. Matokeo yake ndio haya vijembe vya Nape kwa mwenyekiti wake vimeanza. Na kinachomlinda Kikwete ni kinga ya Urais vinginevyo yangeshampata mambo zaidi ya hawa mapacha watatu.

Kujiengua kwa Rostam Aziz madhara yake ni makubwa ndani ya CCM maana huyu anajua siri nyingi na udhaifu mwingi wa viongozi wengi wa CCM kuanzia ngazi ya juu. Sitashangaa CCM sasa kutengeneza maadui wengi ndani ya chama chao wenyewe kutokana na itikadi za makundi, na makundi ndiyo yanayozidi kukidhoofisha chama.

Yanayotokea kujivua magamba kwa kunyoosheana vidole majukwaani na kwenye vyombo vya habari ni dalili za wazi mmommonyoko wa hekima na busara ndani ya CCM iliyojengeka miaka mingi. Ububu wa mwenyekiti wa chama nao ndio umesababisha ufa mkubwa ambao kuzibika kwake ni ziada isiyofikirika kwa urahisi. Uadui ndani ya CCM pamoja na uroho wa vyoe ambao umeonyesha dhahiri kuwepo na cheo ni njia rahisi ya kujichotea mapesa ya wavuja jasho sasa vinapelekesha CCM mchakamchaka ambao hauonyesha dalili za lini wataweka kituo cha kurushiana makonde.

Biashara na Siasa haviendani, na kama Rostam alivyoamua kuachia yote kwa ajili ya biashara zake nampongea ni uamuzi mgumu unaotakiwa kwa manufaa yake binafsi, familia yake na taifa kwajumla. Maana kwa mazingira yaliyokuwepo kila lililofanywa na ye yote Rostam alionekana kama ndiye mbunifu. Tusubiri mengine yaja. Na kosa kubwa la CCM kuweka vuvuzela lisilotumia hekima na busara, na afadhali Mkama angekuwepo vinginevyo mambo yangezidi kuharibika na huyu kijana motomoto Nauye Nape.
 
ANC waliamua kufanya uamuzi mgumu katika historia ya Afrika kusini tangu weusi washike madaraka. CCM inapaswa kujifunza kwa ANC kufanya uamuzi mgumu vinginevyo mambo yanazidi kuharibika. Kukata matawi hali shina lililina gonjwa linaloozesha matawi linaachwa sana na hekaya za abunuwasi kukata tawi wakati umelikalia.
 
Si huyu huyu nape ambaye juzi tu alijiumauma eti hajasema kuwachukulia hatua kama wahusika hawatajiuzuru baada ya siku 90?
Ni sawa na kinyonga, hachelewi kubadilika huyu!
 
Yes he has said it all, the problem is Kikwete himself and should bear all the blames!!!!!!!!

Tiba
 
kwani ni nani asiejua kua mtu namba moja aliyesababisha ccm kufikia hapo ilipo ni Jk? K

uchelewa kwake kutoa maamuzi kumesababisha wanachama wa kawaida kukamatana baraaa bara huku kila upande wa kundi linalokinzana na jingine kudhania kuwa Jk yuko upande wao. Mwisho wa siku huangalia upepo umeelemea wapi na ndipo anajiunga upande wa washindi.

Style hii imekigharimu sana chama chake. Lakini tusisahau kwamba udhaifu wa Jk umeleta neema kwa taifa kwani wezi wote ndani ya ccm wametajana wenyewe.
 
JK anataka kila mtanzania aweke fikra zake katika mambo yanayotukabili badala ya kusubiria fikra za mwenyekiti. Safi sana Kikwete, tukiendelea hivi hakuna atakaeingia madarakani na kujifanya mungu mtu tukabaki vichwa chini kama kipindi kile cha zamani.

Narudia Tena Hongera Kikwete tutakukumbuka kwa hili, tena nakushauri usimame hadharani na utuambie waTz suala la Umeme halikuhusu, maji halikuhusu, hata mishahara haikuhusu kwani kuna watu wanalipwa mishahara kwa kazi ya kubuni na kuratibu mambo hayo, why raisi?.

Hongera Nnape Nnauye kwa kutumia nafasi yako kufanya maamuzi badala ya kulialia na kuogopa nadhani hata JK atafurahi kusikia ukimkosoa.
 
Kikwete mbunifu sana wa mbinu za kugonganisha vichwa halafu yeye anakaa kando akichekelea mambo yanavyoenda. Alijua fika kilichoendelea ndani ya CCM wakati Sitta, Nape na Mpendazone wakihaha kuanzisha CCJ, yeye akawatibua kwa kumpa cheo Nape kuwa mkuu wa wilaya na hivyo kuwa bizu na shughuli za serikali na papo hapo akiwa chini ya usimamizi wa vyombo vya usalama kama mkuu wa wilaya. alishinda kwa hilo. Pamoja na kukwamba kumtoa Sitta kwa vile ndani ya vikao alikuwamo basi vita vikaishia kumwengua kwenye uspika na kumweka kilaza atakayefanya kila anachotaka bungeni.

Lengo la kikwete kumnyanyua Nape kwenye nafasi nyeti Chamani ilikuwa kumthibiti, lakini undani wa Nape na Kikwete wanatofautiana kwa kiasi kikubwa, ingawa kikwete kamnyanyua Nape ili kumthibiti lakini kiitikadi wanatofautiana. Matokeo yake ndio haya vijembe vya Nape kwa mwenyekiti wake vimeanza. Na kinachomlinda Kikwete ni kinga ya Urais vinginevyo yangeshampata mambo zaidi ya hawa mapacha watatu.

Kujiengua kwa Rostam Aziz madhara yake ni makubwa ndani ya CCM maana huyu anajua siri nyingi na udhaifu mwingi wa viongozi wengi wa CCM kuanzia ngazi ya juu. Sitashangaa CCM sasa kutengeneza maadui wengi ndani ya chama chao wenyewe kutokana na itikadi za makundi, na makundi ndiyo yanayozidi kukidhoofisha chama.

Yanayotokea kujivua magamba kwa kunyoosheana vidole majukwaani na kwenye vyombo vya habari ni dalili za wazi mmommonyoko wa hekima na busara ndani ya CCM iliyojengeka miaka mingi. Ububu wa mwenyekiti wa chama nao ndio umesababisha ufa mkubwa ambao kuzibika kwake ni ziada isiyofikirika kwa urahisi. Uadui ndani ya CCM pamoja na uroho wa vyoe ambao umeonyesha dhahiri kuwepo na cheo ni njia rahisi ya kujichotea mapesa ya wavuja jasho sasa vinapelekesha CCM mchakamchaka ambao hauonyesha dalili za lini wataweka kituo cha kurushiana makonde.

Biashara na Siasa haviendani, na kama Rostam alivyoamua kuachia yote kwa ajili ya biashara zake nampongea ni uamuzi mgumu unaotakiwa kwa manufaa yake binafsi, familia yake na taifa kwajumla. Maana kwa mazingira yaliyokuwepo kila lililofanywa na ye yote Rostam alionekana kama ndiye mbunifu. Tusubiri mengine yaja. Na kosa kubwa la CCM kuweka vuvuzela lisilotumia hekima na busara, na afadhali Mkama angekuwepo vinginevyo mambo yangezidi kuharibika na huyu kijana motomoto Nauye Nape.
JK mjanja sana sijui kama Nape analijua hilo na sijui kama Nape anafanya yale anayoyafanya kwa makusudi.

Jk hapendi lawama anataka aonekane mzuri kwa pande zote wakiwemo wananchi, kama hakutaki hawezi kuja moja kwa moja kukuambia wazi atatumia njia ya mzunguko, mfano kuondolewa kwa Makamba lilikuwa dili la Kikwete lakini katumia mbinu ya kuivunja sekretariate nzima ili ampate mtu mmoja wakiwemo target zake kina RA EL na CH wasirudi tena. Hata hili la kuwavua kina RACHEL ni dili lake lakini anawatumia kina Nape kutimiza matakwa yake.

Nape awe careful sana ndiyo maana nikauliza kama anafanya yale anayoyafanya kwa kujua kuwa kuna siku moja atabaki peke yake, siku atakapotakiwa kujiuzuru na NEC/CC sidhani kama JK atamsaidia zaidi ya kuambiwa ni maamuzi ya NEC.
 
Nape- Mikakati ya mafisadi hainitishi
Imeandikwa na Maulid Ahmed, Dodoma; Tarehe: 13th July 2011 @ 23:57

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema mkakati wa mafisadi wa kumchafua na kumgombanisha na Rais Jakaya Kikwete kutokana na msimamo wake wa kuwapinga, hautamfanya arudi nyuma katika vita dhidi ya ufisadi.

Alitoa msimamo wake wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kukanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti moja la kila wiki jana yenye kichwa cha habari ‘Nape amgeukia Kikwete' ambayo ilieleza Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho ameshiriki kukivuruga kwa kuwakumbatia waliomuingiza madarakani na kusababisha kufanya vibaya katika uchaguzi uliopita.

"Habari imenisikitisha kwa sababu si maneno ya kweli na waliponihoji nilieleza, lakini walipuuza. Ninatambua ni mwendelezo wa harakati za kujaribu kunichafua, kunigombanisha na mtakumbuka harakati hizi zimeanza mara baada ya mimi kuonesha msimamo wangu dhidi ya vita ya ufisadi na rushwa nchini.

"Ninaamini msimamo wangu umekuwa mwiba mkali kwa watu wengi ambao wanadhani wanaweza kutumia nafasi zao, pesa zao kufanya wanavyotaka na msimamo huu bahati mbaya kwao hautayumbishwa na harakati zao, nitaendelea kusimama imara kutetea matumizi mazuri ya rasilimali za nchi yangu," alisema Nape katika utetezi wake jana.

Alisema, anaamini kuna kampeni kubwa imeandaliwa kumchafua, kuwagawa na kutaja kulishwa maneno kwenye gazeti hilo ni sehemu ndogo ya kampeni ya kumchafua na kufafanua; "kwenye ukweli uongo hujitenga, juhudi zao zina mwisho wake kwa sababu Watanzania wataujua ukweli baada ya muda kidogo".

Bila kuwataja majina watu hao, alisema wameanza kumchafua baada ya kuona wanaCCM na Watanzania kwa ujumla wameanza kurudisha imani kwa chama na Serikali yao hivyo wanataka kuwarudisha nyuma katika vita hiyo ya ufisadi na wana taarifa za harakati za kuendelea kuwachafua zitaendelea.

"Walidhani tutaishia njiani, nguvu yetu ya soda sasa wanaona tunaendelea mbele na wanashindwa kuturudisha nyuma, wanaamua kupika maneno nawaomba wanaCCM wapuuzeni," alisema.

Licha ya habari hiyo kutoandikwa na gazeti ambalo amelitembelea na kudaiwa kutoa maneno hayo, alisema hana ugomvi na chombo chochote cha habari wala mwandishi wa gazeti lililoandika habari hiyo.

Hata hivyo, alisema kwa sasa anatafakari hatua za kuchukua dhidi ya chombo kilichopika habari hiyo na kukataa kutaja lini atakuwa amefikia uamuzi wa hatua hiyo.

Alipoulizwa kama chombo hicho kitakuwa na ushahidi wa aliyozungumza, atachukua hatua gani alisema "nimeshatembelea vyombo kama nane au tisa na kila nilipokwenda nimeweka rekodi ndo maana nikasema nina hakika na nilichozungumza. Habari yao wameitunga".
 
Nimesoma Gazeti la Mwanahalisi la tarehe 13-19 Julai 2010 kwenye kichwa cha habari kisemacho Nape Amgeukia Kikwete na kukutana na kauli zifuatazo ambazo inasemekana zimetolewa na kada wa CCM ndg. Husein Bashe:

"Siku zote tumekuwa tukitetea kwamba ndani ya chama chetu hakuna mafisadi. Sasa tumetangaza tunao mafisadi. Tukimaliza hili, wananchi watatuuliza, je , mafisadi ni hawa watatu tu?"

Mimi naamini hili ni swali ambalo litaitesa CCM hadi inakufa. Wananchi watauliza kwamba mbona mafisadi waliotajwa ni kumi na moja sasa mbona tumewashughulikia watatu tu wanane wengine vipi?
 
Lina mantiki kubwa tu, na ndio fimbo italayoendelea kuwatesa magamba mpaka 2011!
Tuache ushabiki, Bashe ni kichwa l like his critical way of thinking yuko more objective than most of Magamba!
 
kwani ni nani asiejua kua mtu namba moja aliyesababisha ccm kufikia hapo ilipo ni Jk? Kuchelewa kwake kutoa maamuzi kumesababisha wanachama wa kawaida kukamatana baraaa bara huku kila upande wa kundi linalokinzana na jingine kudhania kuwa Jk yuko upande wao. Mwisho wa siku huangalia upepo umeelemea wapi na ndipo anajiunga upande wa washindi. Style hii imekigharimu sana chama chake. Lakini tusisahau kwamba udhaifu wa Jk umeleta neema kwa taifa kwani wezi wote ndani ya ccm wametajana wenyewe.
.
Nakubaliana na wewe hasa sentensi yako ya mwisho, Mungu anajua jinsi ya kurudisha uhai kwa watu wake kwa hiyo kwa kutupa
Kikwete na serikali legelege angalau tumejua wapi tulikosea na nani adui wakubwa wa taifa. Nani alitegemea gwiji na nguli la kisiasa
kama Rostam siku moja litaondoka ni nani aliyekuwa na ubavu wa kumshinda kwenye jimbo lake naamina hata angetaka kugombea
tena kwa miaka 20 zaidi angeshinda tu. Kile kitendo cha kutajana wao kwa wao na kuanza kufukuzana kwa njia yeyote ile waite
kujivua gamba whatever imetokana kwa njia moja ama nyingine na udhaifu wa Kikwete its like an accidental of hope .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom