Bashe upo kwenye kilele cha mafanikio

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,330
21,422
Amani iwe kwenu.

Tunafurahi kumpata mpambanaji mpya bungeni kijana Husseini Bashe mbunge wa Nzega

Lakini labda tumkumbushe Bashe yale yote anayoyapigania kwa kupaza sauti ni maslahi yake binafsi si chama wala wananchi wake waliomtuma wa nzega.

Bashe amesahau kuwa yupo pale kwa tiketi ya CCM si vinginevyo hata anaposema afukuzwe mwenyewe ana uhakika kuwa chumba chake kipya ameshakisafisha kinamsubiri yeye.

Bashe amesahau kama kuna mtu anaitwa Kafulila alitetea maslahi ya taifa kweli bungeni lakini leo hii hata alipo potelea hatui sembuse yeye mwenye kutafuta kiki,
wanafiki waliokuzunguuka na wewe ni mmoja wa wanafiki hupenda kuanzisha migogoro nina kumbukumbu ulikuwa na mgogoro na kigwangwala usio na kichwa wala miguu.

Tunajua huna hasira na usalama wa taifa ila una hasira na John Magufuli baada ya kumshinda Lowassa na hasira zaidi ni pale kampuni yenye maslahi na nyinyi ilipolazimishwa kujiunga kwenye soko la hisa,kwani unapoitisha CCM ikufukuze wewe ni nani na una historia gani kama alifukuzwa Sophia Simba,akaondoka Kingunge, Lowassa, Seif bado CCM ipo wewe ni nani, ili nikuone shujaa anza kuondoka mwenyewe kuliko kungoja kufukuzwa ili tukusifie kua ni mpiganaji wa haki,usalama walikukamata baada ya kuwa ulitaka kuvuruga mkutano mkuu kwani uongo.

Kumbuka wanaokuchochea sasa watakukana baadae.

Kama unataka kuishambulia sana serikali rudi kule new habari kafanye kazi ya uhariri.

Tanzania ndio kwanza inaanza zama mpya za utawala wa awamu ya tano tunataka hoja zenye tija na taifa.

Hao unaowalalamikia sasa umesahau kipindi cha utawala wa rostam na lowassa uliwatumia kufanya na kuficha madhambi yenu sasa wanadai chao kwa kazi waliokufanyia walipe sasa.

kijana usiongee sana mwisho utaongea pumba!

Kamua baba Magufuli hapa kazi tu.

Tumeshaanza kuwaona sungura na ndezi!
 
Hakiii mtu kuna watu pombe imewalevya aiseeeee kweliii hivi kuna mtu na akili zake timamu anadiriki kuongeaa upuuzi wa kuitetea pombeee haoni madhara yakee??basi kama hayajakupata wewe madhara yake angalia basi hata wenzio yaliyowakutaaa
 
Msimshutumu sana bashe wakati anamwaga ukweli,mgodi wa resolute unafungwa unaondoka na mabilioni na kutuachia shimo nusu ya ngorongoro,sasa tanzania yetu tunataka domo bomu wala sio fataki.
 
Siwezi kushangaa nikisikia mleta uzi nae amewahi kupata degree ya chuo kikuu. Ajira kwasasa ni tatizo kubwa mno nchini; sometimes inabidi uongee usio yaamini ili tumbo lipate kitu. TABU sana.
 
Hata mbunge wa CCM atakayelalamika juu ya utekelezaji mbovu wa bajeti ya maendeleo (34% ) bado mtaendelea kumuona hafai na mchochezi. Hivi nyinyi maCCM mpo kwa ajili ya maslahi ya Taifa (watanzania wote) ama ni kwa maslahi ya chama chenu? Bashe anawasemea watanzania wote, then unakuja hapa na kutuaminisha kwamba anafanya vile kwa maslahi yake binafsi, au unafikiri sisi watanzania hatuoni hicho akifanyacho Bashe. Go, Go, Hussein Mohamed Bashe, watanzania tuko nyuma yako.
 
Hata mbunge wa CCM atakayelalamika juu ya utekelezaji mbovu wa bajeti ya maendeleo (34% ) bado mtaendelea kumuona hafai na mchochezi. Hivi nyinyi maCCM mpo kwa ajili ya maslahi ya Taifa (watanzania wote) ama ni kwa maslahi ya chama chenu? Bashe anawasemea watanzania wote, then unakuja hapa na kutuaminisha kwamba anafanya vile kwa maslahi yake binafsi, au unafikiri sisi watanzania hatuoni hicho akifanyacho Bashe. Go, Go, Hussein Mohamed Bashe, watanzania tuko nyuma yako.
Itakuwa ni mara ya kwanza bashe kupigania maslahi ya taifa kama si tumbo lake una hakika kabsaa anakupigania wewe!
 
Huyu akitumiwa na kina lowassa rostam aziz walihakikisha kwa gharama zote wabunge wengi hawarudi bungeni baada ya kuwa na misimamo ya kitaifa zaidi akiwemo Lucas selelii aliyekuwa mbunge wa nzega jimbo ambalo yeye ni kama amelishikilia kwa sababu ya fedha na soon mwenye jimbo selelii atarudishiwa jimbo lake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom