Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,769
- 2,544
Kwa mujibu wa vyanzo vyangu vya taarifa, Bashe amepata ule wasaa aliokuwa akiutamani na ambao ulimponyoka bila yeye kutarajia-kuingia mjengoni. Vyanzo vinasema kuwa Rostam anahakikisha kuwa jimbo lile linarudi 'kwake' kupitia mtu wake wa karibu na ambaye kwa sasa ni ceo wa habari corporation. Mwenye masikio na akae mkao wa kula
Mod. UPDATE:
Response by the aforementioned:
Mod. UPDATE:
Response by the aforementioned:
Wana Jf naomba nitumie nafasi hii kusema sina NIA,UTASHI WA KISIASA,kugombea jimbo la Igunga wala Jimbo lingine lolote Tanzania zaidi ya Jimbo la Nzega mungu akinifikisha salama 2015, reason nitakua nimesaliti wana nzega,nitakua nimeenda kinyume na dhamira yangu.Kwahiyo nisema hizi tetesi si za kweli na mwisho ni mwana siasa gani ambae atafanya kosa kama HILO? Kwetu nzega nitabaki nzega nitagombea nzega nitawatumikia wana nzega.Ninawatakia Heri wote watakaoenda kugombea Igunga.Mwisho nitoe angalizo kwa wana jamvi hapa hizi lugha za kikaburu,za kubaguana kwa rangi,dini nadhani si njema sana kwa Taifa letu inawezekana aneziandika hapa jamvini haoni madhara leo basi ipo siku italitafuna Taifa letu zimeanza kujitokeza naziona hapa jamvini,nazisikia midomoni mwa wana siasa na sasa zimeanza kwenda ktk nyumba za dini,nilizoea kwetu kijijini kabila hutajwa wakati wa utani lakini sasa naona miongoni mwa wasomi na viongozi zikitajwa kwa nia ya kutugawa nadhani TUNAPOTOKA.ipo siku tutawajibishwa. Nasisitiza SIGOMBEI IGUNGA.