Bashe ajipanga kugombea Igunga

Dk. Peter Kafumu nae ni GAMBA tu madudu yote yanayotokea huko wizara ya Nishati na Madini anahusika! kwahio sioni kama ataleta mabadiliko yoyote katika maendeleo ya nchi hii. NI MWIZI KAMA MWENZAKE RA.
 
Nilitegemea CCM itaelekeza nguvu nyingi kwenye kutekeleza ahadi zake (ambazo ni nyingi sana), lakini nahisi kukata tamaa kwa kuwa wameanza kwa kuchoshana nguvu wenyewe kwa wenyewe mapema kwa mambo yao ya ndani badala ya kazi. Wasiwasi wangu ni kuwa vita vyao havitaisha kabla ya 2015, halafu kwenye uchaguzi watakuja na ahadi nyingine. Naihurumia nchi yangu.
 
hivi kwanini mods wanamlea lea huyu shoga?
Pro-CDM-Jf, wakisema CUF wameolewa na CCM ni sawa, mimi kusema CDM wameolewa na CCM kosa la jinai, unanitolea matusi unanishataki kwa mods, sijui nimefanya kosa gani! Pro-CDM-JF, lazima mkubali kuwa Breadth kutoka kwa watu wengine, mpaka mnatia huzuni JF, sio ya CDM
 
Moyoni RA atataka hilo jimbo sasa lichukuliwe na Upinzani ndio maana hawezi kukubali kijana wake bashe agombee.

Jinsi politics za bongo zilivo hata EL na chenge nao lazima ni jumbe watataka kuwapa kina nape uwa mkifanya mchezo kwa manufaa ya taifa maana yake mnawapa nchi wapinzani.

Movie ya magamba inaendelea sasa io scene ya RA
 
Mkuu tunashukuru kusikia msimamo wako na kuwa muwazi hapa JF, lakini inanishangaza sana kuona wewe kama mmoja wa vijana tunaokutegemea, imekuwaje kuwa mstari wa mbele kushikamana na Rostam hasa wakati anajiuzuru kama sii kujenga majungu zaidi! Na hizi habari za rangi na Ukabila yamekukuta ukigombea Ubunge, leo bila kujifunza unakuwa mbele wakati chama chako kimekwisha amua kujivua magamba na Rostam ambaye hakubaliki unamtandikia red carpet!..

Huoni kama unazidi kujipotezea nafasi ya kuaminiwa na wananchi, pamoja na yote ndani ya CCM watakuona wewe mnafiki? Mkuu Siasa ni mchezo mchafu inatakiwa uwe makini sana na sii kuonyesha emotions zako mahala ambapo viongozi wako wamefikia maamuzi ya kumwondoa. Rostam kaondolewa madarakani, alipewa barua na makamu mwenyekiti mzee Msekwa, hizi habari za kujiuzuru ni staha tu alopewa lakini lugha ilikuwa wazi kwamba asipojiuzuru chama kitamwondoa! haya wewe ndio kwanza huelewi!
Mkuu Mkandara tumtendee haki Bashe, hivi wewe binafsi unaweza kwenda kinyume na mtu aliekuajili tena amekupa cheo cha mkurugenzi mtendaji wa kampuni yake?
CCM waseme kwanza Kagoda ni dudu gani ili ndio ujuwe ccm hakuna mtu safi ila wanazidiana tuhuma tu. Rais JK leo anaweza kutoa maelezo jinsi mwanae alivyokuwa millionea wakati amemaliza chuo kikuu juzi juzi tu? hivi ni vita vya kimakundi ndani ya chama chao kilichooza.
 
kwa mwanasiasa makini uamuzi wa bashe nauunga mkono.. kama lengo lake ni kuwatumikia wana nzega basi hana budi kusubiri 2015!

mbunge anayewakilisha nzega kwa sasa anapiga siasa za kulinda chama badala ya kutetea wananchi.. sidhani kama wananchi walimchagua kwa shughuli hiyo
 
RA anaweza anzisha bifu na ccm washindwe ili ionekane yeye alikuwa kidume cha igunga!

Nakuhakikishia hawezi anaijuwa CCM na serikaliyake, siku zote tunasema ukiendekeza hujuma ujue kuna siku itakuwa zamu yako na husilie kwasababu wewe mwenyewe ulipokuwa Madarakani huliendekeza hilo.

Kama akijaribu nakwambia utasikia yupo Mahakamani na hata swala lake la uraia unaweza kulisikia linaibuliwa chini ya meza, we subiri uone mwisho wa maigizo ya CCM yeye ndiye atakaye kuwa team meneja wa kampeni ya mgombea wa CCM, analijuwa hilo na hawezi kufanya kosa.

CCM watu wenye ubavu na kifua cha kutunisha ni wale ambao wanajuwa fika kuwa hawana cha kupoteza mbele ya CCM, na ndio maana Bashe anakwambia ataendelea kuwa CCM si kwasababu ya kuipenda ni kwasababu anajuwa ndio njia pekee ya kuishi salama hakiwa humu Tanzania, kama baada ya ule uchaguzi wa Nzega angejifanya kuahama chama ungesikia ambavyo CCM ingekuwa serious juu ya uraia wake.

Wao wamekuwa sehemu ya siasa ya aina hiyo leo wanalalamika nini? RA alikuwa msatari wambele katika kampeni ya 2005 ya kuahadaa wananchni na kufanya siasa za maji taka dhiki ya SAS hasilalamike ameze dawa kimia kimia eti anajifanya yeye hapendi siasa chafu! kuna siasa chafu kama waliyofanya 2005 yeye na EL.
 
Kijana mbona unaleta mambo ya Kitchen Party! Bashe kakukana na umbea wako, saizi umeamia kwa Selelii, JF, sio sehemu ya porojo
sikushangai maana hata sura yako inaonyesha wewe ni ZOMBIE. unajua hiyo post ni ya ngapi?
 
Back
Top Bottom