Barua: Zitto akataa posho za vikao

Barua: Zitto akataa posho za vikao

Hii habari iko one sided sana, nilitegemea CDM wangeulizwa kuhusu hili. Hata Zitto hakukataa posho alichotaka ni kubadilishwa matumizi yake kwa kuingizwa kwenye A/C ya KDF. Kwa namna moja ama nyingine, Bunge likaleta mizwenge, jambo hilo likashindikana. CDM walifungwa mikono hapa, of course Zitto anaweza kuacha kusaini kwa sasa lakini itafika kipindi itabidi akubali tu. Then CDM hawakatai Posho zote, ni hii "sitting allowance" ndo inakataliwa, kikao kijacho waweke, kitabu cha mahudhurio na cha "sitting allowance" tofauti so that we can separate black from white swans.

"Katika ilani ya uchaguzi ya chadema ya mwaka 2010,chadema kilikataa posho.Kikawaelekeza wabunge wake wazipinge bungeni.Hatuwezi kuungana na wenzetu wanoziunga mkono".Alisema Marando.

Hata hivyo taarifa kutoka ofisi za bunge hadi jana zionasema ni Zito Kabwe pekee ndiye mbunge wa chadema ambayea aliacha kusaini posho huku wengine wote wakitia kibindoni. source Mwananchi.-29/08/2011 page 4

UTAWATAMBUA KWA MATENDOOOO..MATENDOO
Ni ujinga kuwalaumu CHADEMA kwa kupokea posho waliyoijengea hoja ya nguvu kuifuta lakini mliwashinda kwa uwingi wenu wa kishetani. Kanuni za Bunge ni za "wengi wape" kwa mantiki hiyo kupokea posho zile si hiyari tena bali ni lazima kutokana na hoja yao kushindwa na wabunge wachumia tumbo wa CCM. Isitoshe, kwa jinsi tunavyouelewa utendaji wa serikali hii inayonuka rushwa na wizi, hata kama wangeziacha posho hizo kamwe zisingerudi hazina bali zingeishia mifukoni mwa wezi na vibaka waliosheheni katika kila nyanja za serikali hii iliyokubuhu kwa kuwahujumu watanzania. Ziko wapi hela za EPA mlizoiba na tukaambiwa "Mmezirudisha"?
Tukutane Igunga mwezi ujao na 2015 inshallah kama mola atawafikisha. Wezi na wahujumu wa usitawi wa watanzania msio na haya nyie ambao licha ya kujitahidi kuwavumilia, mmeendelea kutusukumizia upinzani sisi tuliokuwa wana CCM wachache wenye roho ngumu tuliokuwa tumebaki.

"Katika ilani ya uchaguzi ya chadema ya mwaka 2010,chadema kilikataa posho.Kikawaelekeza wabunge wake wazipinge bungeni.Hatuwezi kuungana na wenzetu wanoziunga mkono".Alisema Marando.

Hata hivyo taarifa kutoka ofisi za bunge hadi jana zionasema ni Zito Kabwe pekee ndiye mbunge wa chadema ambayea aliacha kusaini posho huku wengine wote wakitia kibindoni. source Mwananchi.-29/08/2011 page 4

UTAWATAMBUA KWA MATENDOOOO..MATENDOO

Tumieni akili Zitto anatafuta umaarufu wa kisiasa na anajaribu kujiweka tofauti na wenzake wa Chadema anataka uraisi 2015,ni ujinga kuzira pesa kama hoja mliopeleka haijakubalika kwanza ndio anaona leo kakaa muda gani bungeni ndio azire leo asitudanganye huko!big up kwa wabunge wa CDM waliochukua mshiko

sasa we ndo unaspin,kwanini zito asisign na bado ni mbunge na yeye ni chadema? Tuwe wakweli na tutende tunachosema..kigeugeu.

Mangi, Zitto ha-sign mahudhurio na mwanzoni kulikuwa na malumbano kidogo kati ya ofisi ya spika na zitto maana kanuni zinasema kama mbunge hatohudhuria vikao vitatu mfululizo bila idhini ya Spika basi aweza kupewa adhabu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa. Shida imekuwa kwenye tafsiri ya neno 'vikao', je vikao kwa maana ya jumatatu, jumanne n.k? au vikao kwa maana ya msimu e.g kikao jun, jan or nov? Hapa ndio issu huku watu wakivuta pumzi.

Na hapa ndio nasema inawekezekana kabisa kama wabunge wote kwa ujumla wao hawaku-sign mahudhurio kwa kanuni za sasa kukawa na madhara, hasa ukizangatia CHADEMA ndio wanaunda kami rasmi ya ubunge na Mbowe ndio kiongozi wa kambi ya upinzani buneni. Hata hivyo mara kadhaa wamekuwa wanasisitiza kuwepo kwa vitabu viwili vya mahudhurio kimoja kwa wale wanaokubaliana na posho na kingine kwa wale wanaokataa posho. Ofcourse hii imekataliwa. Kwa ujumla hii issue bado kuna vizingiti wanatakiwa wavuke.

John Mnyika ni msomaji mzuri hapa jamvini, ningependa niamini atatolea ufafanuzi zaidi na complications zilizopo kwa sasa.

"Katika ilani ya uchaguzi ya chadema ya mwaka 2010,chadema kilikataa posho.Kikawaelekeza wabunge wake wazipinge bungeni.Hatuwezi kuungana na wenzetu wanoziunga mkono".Alisema Marando.

Hata hivyo taarifa kutoka ofisi za bunge hadi jana zionasema ni Zito Kabwe pekee ndiye mbunge wa chadema ambayea aliacha kusaini posho huku wengine wote wakitia kibindoni. source Mwananchi.-29/08/2011 page 4

UTAWATAMBUA KWA MATENDOOOO..MATENDOO
Ok, wewe si unatafuta makosa ya CDM ili uwa disqualify kushika dola?hongera umefanikiwa!wape hao ccm wako ili uibiwe zaidi, hivi mtu mwenye uelewa wake mzuri anaweza kulinganisha usafi wa CDM na CCM? hao wabunge wa CDM si walipinga hizo posho bungeni mkawalazimisha kuzichukua watake wasitake? si ninyi ccm mliokataa mpango huo kwa vyovyote vile?walipotaka itungwe sera ya kuondoa posho kwa wabunge na maafisa wa serikali mliwaambiaje?nina mashaka na akili yako, bado uko tayari kuibiwa kwa kuwaonyesha wakombozi wa kweli kuwa ni wabaya!ama kweli mkataa pema pabaya panamngoja!

Wanasiasa wote ni wasanii 2,si CCM wala CHADEMA,ctakuwa ladhi kufa kwa ajiri ya mwanasiasa bali nitakuwa tayari kufa kwa ajiri ya wananchi.

MWANANCHI inahitaji kutufafanulia zaidi kuhusu hili.

Tunakumbuka mjadala wa posho ulichukuliwa ni wa kitaifa. Ni mjadala ambao umeacha makovu ndani CHADEMA hasa ukimtaja Shibuda. Lakini vilevile ulitikisa hata nje ya CHADEMA, taja jina la January Makamba.

Suala hilo lilipamba magazeti kwa kuwa habari iliyojaza kurasa mbili au zaidi.

Nimeisoma habari yote a MWANANCHI leo.

Kwanza kuna utata wa kujaza fomu na kuchukua posho. Pendekezo la CHADEMA lilikuwa ili kuepuka mtego wa kubambikiziwa kwamba mbunge amechukua posho basi zitenganishwe fomu za mahudhurio na za kupokea posho. Je, fomu za kupokea posho zimeshatenengezwa?

Kama fomu hazijatangenezwa basi ndiko kulekule kwa masuala a mahudhuriao ambayo hatuna haja ya kuyarudia maana nchi nzima iliyajadili labda kama humu JF kuna wasinziaji kama wale wabunge wachapa usingizi.

Mambo ya kusema habari za kuaminika toka mahala fulani ndiyo Nape Nnauye anapigana nayo kuhusu kukataa mwandishi aliyemuuliza kuhusu barua ya Tendwa kuitwa kwa masuala ya muafaka na CHADEMA

Hivyo, MWANANCHI itafute mbinu za kupata wasomaji kuliko kukimbilia kupachika sentensi moja kujibu mjadala wa posho uliochukua wiki kadhaa na kujaza kurasa za magazeti yote East Africa.

Na ukiangalia kwa makini utaona inasema "taarifa toka ofisi ya Bunge". Ninavyowajua MWANANCHI wameandika habari nyingi wakisisitiza neno "Barua ambayo MWANANCHI imeiona". Hapa wanasema ni taarifa. Hawasemi kama wameona signed document ambao CHADEMA wamepokea posho hizo.

Hivyo gazeti kama hili litambu kuwa umakini wa wasomaji umeongezeka na si rahisi kuwapata vipofu wa kuishia kusoma juujuu. Ni hali hii ya uandishi inayofanya gazeti moja leo lilalamike kuwa mitandao imesababisha magazeti yapungue soko.

Mh.Mbunge usilaumu bure mwanachi,cha msingi we tuambie posho mmechukua ama la,na kwa nini zito asisign nyie msaini.Je hizo implication za kutokusign zinamexcude Zito?NA KAMA HIZO FOMU HAZIKUANDALIWA KWA NINI HAMKUANDAMANA ZIANDALIWE?

Jamani ninavyokumbuka mama kiroboto alisema si sheria posho ya mbunge ibaki kwenyemamlaka ya bunge ,nakama mbunge anataka ikasaidie kwenye jimbolake aichukue apeleke na si kaziya bunge

For some reason I just think Zitto is not serious or sincere with this and he is just trying to score some political popularity points.

Nyaningabu kumbuka ule msemo kuwa MUUNGWANA NI VITENDO!

Mnafiki zaidi ni nani kati ya Chadema ambapo kunatoka Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (alirudisha shangingi), na naibu wake (amekataa posho) au wabunge wa CCM walalao bungeni na kuunga hoja asilimia mia moja? Katibu mkuu Jairo anatoka Chadema? Kahonga wabunge wapitishe bajeti ya wizi.
CCM unafiki mtupu!

Nani kakwambia amerudisha? Yupo anatesa nalo tu. Sasa ndo uwajue vizuri viongozi wako.
Maslai kwanza mengine bla bla tu.
Ni basi tu hawajapata nafasi ya kutawala nchi hii lakini kwa matendo yao utawatambua nia zao.

viongozi wetu wenyewe wanaingia humu kwa kubeep tofauti na zamani kidogo,wamekomaa na twitter na facebook zao! Haya!

tuache kum discuss Zitto,tujadili na mtihani mdogo kwa wenzangu mwenye maelezo mepesi kumsaidia Kashaija kuleee Mabira karagwe,nini msimamo wa cdm na hatua gani wamechukua kama chama kuhusu posho?

CDM ni wasanii sana hawana dhamira ya dhati ya kuwaongoza wananchi wa Tanzania.
Mpaka leo bunge limemaliza vikao vyake, ofisi katibu wa bunge haijapokea barua yoyote kutoka CDM kupinga kupokea posho, zile porojo za kina Mbowe na Lissu, kumbe ilikuwa usanii mtupu Magamba bana

Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi ni kwamba CHADEMA walishatoa maelezo ya kile wanachopinga. Ni mfumo sio particular transation. Na ilivyo sasa, uki-sign daftari la mahudhurio basi hela zinalipwa moja kwa moja kwenye account yako. Pia nadhani kuna madhara kama wabunge wote wa CHADEMA wangegomea kuto-sign mahudhurio (mwenye uelewa zaidi asaidie hapa tafadhali). Kwa hiyo ili kuondoa tatizo lote walishauri KUNG'OA MTI NA SIO KUKATA MATAWI. Na bunge ndio chombo sahihi cha kutunga sheria.Nadhani ccm wanaweza kujaribu ku-spin hii lakini kwa kumbukumbu zangu CHADEMA walijaribu sana kupaza sauti za kubalisha hii sheria inayoruhusu posho lakini hawakufanikiwa. Wasiwasi wangu ccm wanaweza kupoteza umuhimu wa huu mjadala kwa kusema kuwa hawa CHADEMA nao wamepokea lakini cha msingi hapa tukumbuke kama hatutajikita kwenye kujadilikubalisha mfumo tutapotea tatizo la msingi.
Si mchezo mbona unatufanya sisi sote hatuna akili bwana.sasa unataka kuniambia Mh Zitto hachukui hizo hela kwa sababu ha-sign hilo daftari la mahudhurio?kama ni kweli Mh Zitto ki kanuni alikuwa ni absentee!!! na sifikirii kama Mh Zitto ha-sign na kama ana sign kutokana na maelezo yako hela zinaenda moja kwa moja kwenye account yake.. na sasa kwa nini office za bunge ziseme Mh zitto hachuki posho....Bora hao CCM hawajaonesha unafiki lakini CHADEMA walitaka kutumia populist politics na matokeo yake wakashindwa na ndiyo maana mpaka leo hawajamchukulia hatua Shibuda kwani wabunge wote wa chadema isopokuwa Zitto ni sawa na shibuda..... hatari kweli kweli.... Unafiki bwana!???

Hata mkiichafua CDM mimi sing'oki waliposema posho zifutwe,mlifikiri zinafutwa siku hiyo hiyo?na anayeng'ang'ania posho ni nani kama sio ccm? WADANGANYIKA BADO TUNASAFARI NDEFU SANA KUHUSU KUPAMBANUA MAMBO,mimi binafsi naona hiyo hoja haina mashiko,MSIWE LEGE LEGE KAMA SERIKALI YA sisi M.

Hii taarifa imenishtua sana!!!!sijui tunaelekea wapi.who iz cleannnnnn.imenidiscourage kisiasa.
Imekushtua sana kuliko habari kuwa watanzania lukuki wanakufa kwa magonjwa yanayotibika wakati viongozi wao wanakwenda kutibu funza za miguuni mwao huko India?

Mh.Mbunge usilaumu bure mwanachi,cha msingi we tuambie posho mmechukua ama la,na kwa nini zito asisign nyie msaini.Je hizo implication za kutokusign zinamexcude Zito?NA KAMA HIZO FOMU HAZIKUANDALIWA KWA NINI HAMKUANDAMANA ZIANDALIWE?

Umechanganyikiwa kama serikali yako ambayo haijagutuka kutoka kwenye usingizi wa kudhani kila aliye informed au analytical basi ama ni mbunge, au yuko kwenya taasisi za serikali anatoa siri za ofisi.

Habari ya taarifa ya bunge kuhusu posho kama ilivyoripotiwa na MWANANCHI ni wazi kwamba hata gazeti lenyewe lilipuuza kwani ni ki-sentensi kimoja kati ya half page ya gazeti hilo.

Tatizo lako ni la ufahamu kwamba jinsi ilivyoandikwa MWANANCHI wanakubali na wameiweka katika hali a tetesi, lakini kwa uelewa wako mdogo hukutumia humu neno tetesi na ukajimwaga mzimamzima ukidhani wote tumepitia shule za kata au zile za Kana ka nsungu umwelu.

Back
Top Bottom