Hili swala la kitoto sana. Hivi ikitokea kikao ambacho yeye Zitto ndiyo mwenyekiti na imeandikwa katika ripoti na mwisho Zitto hakuweka sahihi kwenye kitabu cha waliohudhuria kwenye kikao, utasemaje kuwa Zitto hakuhudhuria kikao?
Ikiwa bungeni Zitto atafika na kuuliza maswali na mwisho wanaweza ripoti kuwa Zitto, siku fulani saa hii aliuliza hili swali bungeni na mwisho wa siku haweki sahihi ya mahudhurio, bado watalazimisha kusema kuwa Zitto hakufika kwenye kikao?
Mbona hili jambo la kitoto sana sana? Au ndiyo wanataka tena kumpa Zitto umaarufu?
Naona kuna haja hili swala liwe la Chadema wote na tuone wanavyowafukuza Chadema nzima, NCCR na baadhi ya CUF maana Hamad atakuwa mbongo kuhoma kuchukua hela huku mamaa wawili wanasubiri ulaji.