Barua: Zitto akataa posho za vikao

Barua: Zitto akataa posho za vikao

Kweli uamzi mzito sana huu, hii inastahili wabunge wote waseme hivyo kuwa posho zao sije majimboni kufanya maendeleo... lakini hili ni swala gumu pia kwa wabunge ambao ni wapya bungeni kama kina Lema, coz baso wajaupata utamu wa allowance vizuri wm jiweke wewe kwenye hiyo position uone kama kirahisirahisi utakubali, najua zito amekuwepo bungeni mda mrefu na kwenye kamati kibao yupo sasa nikama ameshiba, so ninampongeza zito kwa kushiba maana kuna wazee huko hawashibi na hata kuongea bungeni huwa hawaongei kabisa, mfano mzuri Lowasa, chenge, na wenzao..!
 
Safi sana. Rachel Mashishanga, mbunge wa shinyanga mjini, fuata nyayo. Hizo posho zako zielekeze kwenye chama mkoa wa shy. Hatuna sound systems na hivyo shughuli za uenezi zinakuwa ngumu. Na wambunge wengine wa chama wazitumie posho hizo kukiimarisha chama. Hii itakuwa ni njia moja wapo ya kushinikiza zifutwe kabisa.
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuiomba isimamishe kumlipa posho zake zinazotokana na vikao vya Bunge kuanzia juzi. Zitto ametoa ombi hilo kwa barua rasmi aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah Juni 7 mwaka huu.

Barua yenyewe hii hapo chini

View attachment 31767

Big challenge ever to CCM MP’s
 
Safi sana ZITTO unauchungu na watanzania najua malimbukeni CCM hawajapenda wazo lako kuwakilisha upinzani,VIVA CHADEMA,ANGUKO LA CCM LIMETIMIA
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Thursday, 09 June 2011 23:25 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

Exuper Kachenje
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuiomba isimamishe kumlipa posho zake zinazotokana na vikao vya Bunge kuanzia juzi.Zitto ametoa ombi hilo kwa barua rasmi aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah Juni 7 mwaka huu.
Katika barua hiyo, ambayo gazeti hili limefanikiwa kuiona, Zitto alisema anaamini kuwa watumishi wa Serikali na wabunge, hawastahili kulipwa posho wanapohudhuria vikao rasmi vya uwajibikaji wao wa kawaida.
Zitto alisema kuwa posho hiyo haistahili kulipwa kwake, wabunge wengine wala watumishi wa umma kwa kuwa kuhudhuria vikao ni sehemu ya kazi zao.

"Kwa mujibu wa Sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly Act of 2008) na kwa mujibu wa Masharti ya Kazi za Mbunge niliyokabidhiwa, ninastahili kupata posho za vikao, (sitting allowances) kila ninapohudhuria vikao vya Bunge na Kamati zake,"alisema Zitto na kuongeza:
"Ni imani yangu kuwa posho ya kikao haistahili kulipwa kwa mbunge na mtumishi mwingine yeyote wa Serikali kwani kuhudhuria kikao ni sehemu ya kazi yangu,".

Kupitia barua hiyo, Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha, alieleza kwamba amekuwa akipendekeza posho za vikao hivyo ifutwe, jambo ambalo pia limo katika mapendekezo ya chama chake (Chadema) katika Bajeti ya 2011/2012.
"Nimekuwa nikipendekeza kuwa posho hii ifutwe. Chama changu cha Chadema pia kimependekeza jambo hili katika mapendekezo yake ya Bajeti 2011/2012," alisema Zitto na kuendelea:
"Mpaka hapo mfumo wa kulipana posho za vikao utakapofutwa, ninaelekeza kwamba stahili zangu zote za posho zielekezwe katika Taasisi ya Kigoma Development Initiative (KDI).., utaratibu huu uanze kuanzia tarehe 8/6/2011."


Katibu wa Bunge agoma kuizungumzia
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alipoulizwa jana kama amepokea barua hiyo ya Zitto, alisema kuwa, yeye kama mtendaji wa mhimili huo wa Dola, anapokea barua nyingi, hivyo si rahisi kukumbuka kama barua hiyo imefika ofisini kwake.

Lakini akasema, hata kama barua hiyo itakuwa imemfikia ofisini, kanuni na taratibu haziruhusu Bunge kutangaza habari za mtu binafsi.Alisema ofisi yake hairuhusiwi kuandika masuala binafsi ya wabunge yanayofikishwa ofisini na kwamba hilo linawezekana ikiwa mhusika (Zitto), ameruhusu lifanyike kwa maandishi.
"...Haturuhusiwi kuandika habari za mtu. Nikiwa Katibu wa Bunge, napokea barua nyingi 'personal' (binafsi), lakini kama yeye mwenyewe amewaambieni kuwa kaleta barua hiyo, basi mwambieni pia atuandikie barua kuturuhusu na sisi ili tulitangaze hilo," alisema Dk Kashililah.
Bajeti ya posho kulipa walimu laki moja
Uamuzi huo wa Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, umekuja huku taarifa za utafiti wa taasisi ya Policy Forum inayojihusisha na tafiti mbalimbali za sera zikionyesha kuwa, katika mwaka 2008/2009, Serikali katika bajeti yake ilitenga Sh506 bilioni kwa ajili ya malipo ya posho.

Kwa mujibu wa utafiti huo, ambao taarifa yake ilitolewa mwaka uliopita, fedha hizo ni sawa na mishahara ya mwaka mzima kwa walimu 109,000 ambao ni robo tatu ya walimu wote nchini.
Kwa mujibu wa utafiti huo mwaka 2009/10 kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya posho za watumishi wa umma kilikuwa sawa na asilimia 59 ya malipo ya wafanyakazi wa ngazi ya chini .

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Good start lets move na kwenye hiyo mishahara minono nayo ipigwe panga anagalau kidogo tu...
 
Soma uelewe alichosema, malipo yafanyike to Kigoma Development Initiative(KDI) mpaka hapo posho zitakapositishwa.
Zitto aache janja yake! Anatupiga tu wananchi changa la macho. Hii Kigoma Development Initiative(KDI) ni NGO yake mwenyewe! So hizo allowance zinamrudia yeye mwenyewe!
 
Mh. Zitto angeweza kupeleka mwenyewe kule kwenye NGO yake lakini naona alitaka kufikisha ujumbe kwa viongozi wa Bunge. Swali langu hapa; nani ameleta hii nakala JF wakati KAtibu wa Bunge anadai kutoijua barua hii?
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuiomba isimamishe kumlipa posho zake zinazotokana na vikao vya Bunge kuanzia juzi. Zitto ametoa ombi hilo kwa barua rasmi aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah Juni 7 mwaka huu.

Barua yenyewe hii hapo chini

View attachment 31767


Zito si mtu wa kwanza, wengine wanapeleka Halmashauri mfano Mzee Ndesamburo na Mbowe tangu miaka ya 2000. Kajitahidi kwa kuwaiga. Good.
 
CDM kama chama wameipendekeza hoja hii kwenye bajeti, kwa hiyo ZITTO ametekeleza pendekezo la chama chake ''ie hana makosa kwa chama, pia amejijenga kisiasa. Ikiwa hoja ya CDM ya kufuta posho ililenga kwa dhati kuleta maendeleo kwa wananchi, hawana budi kumuunga mkono ZITTO, na hilo litawaongezea credibility kwa wapiga kura na kuendelea kuwaamini zaidi. Ikiwa wanatafuta umaarufu wa kisiasa, huu wa ZITTO ni mtego mkubwa and they need an intelligent consultant.
 
kiongozi ni kama huyu maslahi binafsi badaye kazi nzuri
 
Mabadiliko daima huletwa na waliotayari ku-sacrifice. Zitto, umeweka "precedent", umeonesha mfano ambao uigwe. Wa-tz tunasubiri kwa hamu kuona nani atakuwa jasiri kufuata!
 
mkuu kukataa posho ni msimamo wa chama siyo msimamo wa mtu binafsi. Huo msimamo umetoka wapi kama ni mbunge mmoja tu natekeleza msimamo wa chama? Chadema kama insititution inatakiwa iwe na misimamo ya ki insititution na siyo msimamo wa mtu mmoja mmoja. Kama ni msimamo wa mtu mmoja mmoja basi hakuna maana ya kuwa na msimamo wa chama katika mambo mbalimbali.

Hapa nakumbuka msimamo wa chama wa kutoka nje wakati jk anahutubia bunge, zzk akaja na msimamo wake wa kupingana na chama. Mbona chama hakina misimamo?

wewe ni mnafki na umetumwa na nepi inatosha. Nyie ndio kama akina chief mangungo waliouza nchi. Sisi tuna akili timamu mtausikia mziki mzito na bado unakuja.
 
..naona hii ni move ya Zitto peke yake.

..CDM wanapaswa kuja na tamko lao kama chama kuhusu suala hili.

..mapendekezo yangu wabunge wote wa CDM ambao wamekuwa bungeni more than one term wafuate utaratibu aliochukua Zitto.

..wale wanao-serve term yao ya kwanza wakatwe 50% ya posho zao kupeleka kwenye miradi ya maendeleo majimboni mwao.
 
ANAESTAHILI SIFA ASIFIWE SINA BUDI KUMPONGEZA MUHESHIMIWA ZITO KWA UWAMUZI WAKE (M/MUNGU AKUZIDISHIE)Bajeti ya posho kulipa walimu laki moja
"... taarifa za utafiti wa taasisi ya Policy Forum inayojihusisha na tafiti mbalimbali za sera zikionyesha kuwa, katika mwaka 2008/2009, Serikali katika bajeti yake ilitenga Sh506 bilioni kwa ajili ya malipo ya posho..., fedha hizo ni sawa na mishahara ya mwaka mzima kwa walimu 109,000 ambao ni robo tatu ya walimu wote nchini.

Kwa mujibu wa utafiti huo mwaka 2009/10 kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya posho za watumishi wa umma kilikuwa sawa na asilimia 59 ya malipo ya wafanyakazi wa ngazi ya chini .

Kwa mtindo huu, anaesema hii serikali ya CCM ni makini na alaaniwe mbinguni na Duniani! Huu ni ufujaji wa mapato ya Taifa huku wananchi wakikabiliwa na umasikini wa kupindukia! Umeme hakuna, hospitali hazina dawa, wa mama wajawazito hawana vitanda na wana ambiwa waende na gloves na nyembe wakati wa kujifungua! Shule hazina madawati watoto wanaburuza ****** kwenye vumbi! Barabara mbovu kila mahali. Huu ni uwenda wazimu wa kujitakia.

Hongera Zitto kwa kufanya vitu kwa vitendo! Hongera CHADEMA kwa sera za ukweli na wengine wafuate nyayo!
 
..naona hii ni move ya Zitto peke yake.

..CDM wanapaswa kuja na tamko lao kama chama kuhusu suala hili.

..mapendekezo yangu wabunge wote wa CDM ambao wamekuwa bungeni more than one term wafuate utaratibu aliochukua Zitto.

..wale wanao-serve term yao ya kwanza wakatwe 50% ya posho zao kupeleka kwenye miradi ya maendeleo majimboni mwao.

Sema posho zote za wabunge zifutwe siyo kwa CDM pekee, wote hasa za magamba ndo wajue uchungu wa kutumikia wananchi siyo chama,
 
wewe ni mnafki na umetumwa na nepi inatosha. Nyie ndio kama akina chief mangungo waliouza nchi. Sisi tuna akili timamu mtausikia mziki mzito na bado unakuja.

Achana na huyo kimbunga kibarua wa Nepi, kwa kazi hiyo anayoifanya anaingiza siku japo ukweli anaufahamu. Mwenda wazimu kakimbia na nguo zako-achana naye-fanya maalifa mengine.
 
Mh. Zitto angeweza kupeleka mwenyewe kule kwenye NGO yake lakini naona alitaka kufikisha ujumbe kwa viongozi wa Bunge. Swali langu hapa; nani ameleta hii nakala JF wakati KAtibu wa Bunge anadai kutoijua barua hii?

Katibu wa Bunge ana-element za magamba ndo maana anarusha mistari!
 
Back
Top Bottom