Barua: Zitto akataa posho za vikao

Barua: Zitto akataa posho za vikao

Inabidi na wabunge wengine waige kwa mheshimiwa Zitto..
 
Mbona mbowe hakwenda mahakamani lakini wenzake slaaa na Ndesamburo na Lema walikwenda. Kwa nini hawakufanya maamuzi ya pamoja kwenye hili . Punguzeni conspiracy theory zenu

Mambo ya posho ni kitu binafsi wakiona inafaa ila mtu ataamua naye afanyie posho zake jamabo analoona linafaa jimboni kwake au wenye chama chake

Suala la mtu binafsi vipi wakati ni msimamo wa Chama? Kwenye msimamo wa Chama suala binafsi linatoka wapi? Au ndio tuseme hawana msimamo mmoja? Walikuwa wanataka kuwadanganya watu na sasa Zitto anafanya kweli wengine wanarudi nyuma?
 
Jamani, sio nyinyi mliokuwa wa kwanza kumtaka aziache hizo posho? Kaziacha imekuwa maneno!
Hata nyinyi acheni unafiki

Tunataka afanye marekebisho aziachie bila masharti yoyote, ndio tutampa Big Up. Haiwezekani ukakataa mali haramu, halafu ukatoa maagizo ikanunue kitoweo nyumbani. Zitto nan maslahi mapana na KDI na jimbo lake , hivyo kitendo chochote cha fedha hizo harama kupelekewa huko tena kwa maagizo yake hakiwezi kuchagia kuondoa mfumo huo mbovu wa kifisadi. At least he gets 50% credit.
 
Sioni mantiki yoyote kwa hili. Posho ni haki yake. Jimbo kwake kuna matatizo kibao ya huduma za wananchi. Angeweza kutangaza kuwa anaelekeza posho hizo kwenye huduma za jamii jimboni kwake. Hivi kumgekuwa na ubaya gani kama angeeleza posho hizo hospitali ya jimbo lake? Asilewe sifa ingawa ana ubora.

Ndivyo alivyoelekeza malipo yake yaelekezwe kwa shughuli za maendeleo kigoma KDI
 
Hiki ndicho kilikuwa kinakosekana kwa wanasiasa wetu. Maneno bila vitendo. Zitto ametupeleka hatua 100 mbele katika mustkabali wa siasa zetu-tunampongeza. Asirudi nyuma. Mwanasiasa hapaswi kufanya jambo ambalo haliamini. Hata kama wengine wataendelea kupokea waendelee, lakini usikubali kusaliti utashi wako.

Mkuu ina maana wabunge wengine wote wa CHADEMA ambao wataendelea kupkea posho watakuwa wanafanya jambo ambalo hawaliamini? Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Budget Mubadala ya CHADEMA posho zinatakiwa zifutwe na hivyo walikubaliana kwamba hiyo ndio imani yao hadi wakaiweka kwenye badget kivuli. Wakiendelea kupokea tuamini kuwa wanafanya jambo ambalo hawaliamini?
 
Safi sana Zitto....wengine inabidi waige hapa!!!
 
Tunataka afanye marekebisho aziachie bila masharti yoyote, ndio tutampa Big Up. Haiwezekani ukakataa mali haramu, halafu ukatoa maagizo ikanunue kitoweo nyumbani. Zitto nan maslahi mapana na KDI na jimbo lake , hivyo kitendo chochote cha fedha hizo harama kupelekewa huko tena kwa maagizo yake hakiwezi kuchagia kuondoa mfumo huo mbovu wa kifisadi. At least he gets 50% credit.

Kuziacha bila maelekezo ni kuwaachia wajanja wale, Ztto Mhe. anaakili sana. Ndo maana anazielekeza kwenye kazi za maendeleo KDI amabpo anaweza nkuziona wazi kazi zinazofanya.
 
Zitto aache janja yake! Anatupiga tu wananchi changa la macho. Hii Kigoma Development Initiative(KDI) ni NGO yake mwenyewe! So hizo allowance zinamrudia yeye mwenyewe!
Sasa hiyo NGO Kama ni yake na ipo kwa ajili ya kuwasaidia wengine pana tatizo gani hapa!!?au umeamua tu kuchafua hali ya hewa.Mimi na wewe tuwe na mawazo mazuri ili tulijenge hili taifa la Tanzania lisilokamilika kila siku matatizo
 
Tunataka afanye marekebisho aziachie bila masharti yoyote, ndio tutampa Big Up. Haiwezekani ukakataa mali haramu, halafu ukatoa maagizo ikanunue kitoweo nyumbani. Zitto nan maslahi mapana na KDI na jimbo lake , hivyo kitendo chochote cha fedha hizo harama kupelekewa huko tena kwa maagizo yake hakiwezi kuchagia kuondoa mfumo huo mbovu wa kifisadi. At least he gets 50% credit.

Akiziachia zitaliwa hazina je nikuulize kipi kati ya hicho bora zitafunwe na mafisadi hazina au zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo jimboni mwake? Acha kuwa na ukungu kichwani.....
 
Tena unafiki wa kutaka kuoneka mzuri machoni pa watanzania,,leo kuna familia ngapi, huko jimboni mwako maskini wa kutupwa
kwa nini usingepeleka hizo posho moja kwa moja kwenye familia maskini kabisa, ili ziweze kuwasaidia kwa sababu ni pesa zao?

Narudia huo ni unafiki wa kutaka kuoneka mzuri machoni pa Watanzania.

UNA TATIZO LA AKILI ,HUJASOMA VIZURI NA KUELEWA ,ZITTO AMEANDIKA KWA BUNGE KUOMBA WAPELEKE POSHO ZAKE KWENYE MFUKO WA MAENDELEO WA KIGOMA KASKAZINI

sasa ulitaka aziache bungeni ziliwe na CCM au ulitaka awapelekee maskini gani ???na kazi ya CCM ninini??

HONGERA ZITTO KWA UAMUZI W BUSARA ,UTATAWALA KIGOMA KASKAZINI DAIMA
 
Mkuu ina maana wabunge wengine wote wa CHADEMA ambao wataendelea kupkea posho watakuwa wanafanya jambo ambalo hawaliamini? Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Budget Mubadala ya CHADEMA posho zinatakiwa zifutwe na hivyo walikubaliana kwamba hiyo ndio imani yao hadi wakaiweka kwenye badget kivuli. Wakiendelea kupokea tuamini kuwa wanafanya jambo ambalo hawaliamini?

Fahamu kuwa kusema ni jambo moja lakini kutenda ni jambo lingine kabisa, tunahitaji vitendo na sio maneno matupu, Zitto kaonyesha mfano na wabunge wengine watembee kwenye maneno yao na sio kupiga domo tu...
 
Hongera sana mh. Zitto, ninaamini kabisa kama mwenyezi mungu atakujalia kuja kuiongoza hii nchi mambo mengi yatakwenda pasi na kupinda pinda, mh. Zitto yuko mjengoni hii ni term yake ya pili tu, tukitaka tujuwe ni kiasi gani cha feza za umma ambazo zimeokolewa, aweke hapa toka kawa mbunge ni milioni ngapi za posho alichopokea, kisha angalia wale wabunge wanaowakilisha majimbo miaka 20, ni pesa nyingi sana zinaweza okolewa zikafanyiwa mambo mengi tu ya maana, sehemu kibao hakuna zahanati, kwenye zahanati hata panadol hakuna.
 
Mkuu ina maana wabunge wengine wote wa CHADEMA ambao wataendelea kupkea posho watakuwa wanafanya jambo ambalo hawaliamini? Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa Budget Mubadala ya CHADEMA posho zinatakiwa zifutwe na hivyo walikubaliana kwamba hiyo ndio imani yao hadi wakaiweka kwenye badget kivuli. Wakiendelea kupokea tuamini kuwa wanafanya jambo ambalo hawaliamini?

Kwani hiyo bajeti yao kivuli ndio itakayojadiliwa na kupitishwa?
 
Mimi yangu mawili:
1. Zitto amekuwa Bungeni kwa kipindi cha pili sasa?Je ubaya wa posh hizi anakuja sasa?
2. Kwanini asiseme kuwa posh hizi zirudishwe serikalini? Nani mmiliki wa KDI? Tutathibishaje kuwa posho hizo hazitakuwa kwa matumizi binafsi?
Mwisho huu ni msimamo wa CHADEMA au kujitafutia umaarufu? Mkumbusheni kurudisha na fedha za gari.
 
Mkuu, katika lugha yetu ya kiswahili hakuna kitu kama "kwa niaba yake binafsi".

Lakini jambo la msingi nililotaka kusema, mbona huelweki?? mara useme zitto kapeleka pesa kwenye NGO yake hapo hapo unasema hujui hiyo KDI ni ya nani. Mara useme NGO za bongo ni usanii mtu, kwahiyo unataka tuamini kwamba hapa bongo hakuna NGO iliyo serious? hapa dude hebu kuwa mkweli.

Ghafla tena unaanza kuhamisha mada kutoka kwa KDI na kuielekeza kwa chadema, mbona unaruka ruka? hebu jielekeze kwenye hoja ya msingi, zitto kaamua posho yake ielekezwe kwenye shughuli za maendeleo ya wananchi wake wa kigoma, wao ni sehemu ya watanzania wanaohitaji maendeleo, kwani kila kitu anachofanya zito lazima uwe msimamo wa chama?mambo mengine ni yake yeye na wapiga kura wake.

Kwanza tambua kama mbunge sisi wananchi tunamlipa mshahara, hivyo kazi aliyofanya na kutoa taarifa kwa wananchi kama mbunge sio ya kweke binafsi ni yetu hivyo inatuhusu kwa kiwango kikubwa sana.

Pia fedha zinzotumika vibaya ambazo yeye kama Waziri Kivuli wa Fedha anazizungumzia ni kodi za watanzania wote. Hivyo sio busara mapato yatokanayo na wizi akayatumia kunufaisha watu wa jimbo lake, tena kwa kututamkia hadharani.

Ni heri wale wanaotuibia lakini hawasemi wanatuibia, kuliko yule aliyetuambia mnaibiwa, halafu wezi wenzie walipokataa kuacha wizi akawataka wampelekee mzigo wake wa wizi nyumbani.
 
Kuziacha bila maelekezo ni kuwaachia wajanja wale, Ztto Mhe. anaakili sana. Ndo maana anazielekeza kwenye kazi za maendeleo KDI amabpo anaweza nkuziona wazi kazi zinazofanya.
Yaani fedha wizi ziklete maendeleo Kigoma?
 
BINAFSI NATOA PONGEZI ZANGU STAHILI.......(ANGALIZO) KAMA ALIPOELEKEZA ZIPELEKWE KWELI IKAWA NI NGO YAKE BINAFSI (hiyo ni sarkasi katuchezea) SI SAHIHI SANA.....! BALI NINGEMWELEWA ANGEPELEKA KATIKA TAASISI AMBAZO HANA MKONO WAKE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE!TUHESHIMU MCHANGO WAKE NA PIA LOLOTE AMBALO AENDA KINYUME TUWE KINYUME NALO
Mi nadhani inatupasa tupongeze hatua aloipiga Zitto ni ajabu kukuta eti mtu anadhihaki kwa kua KDI ipo chini ya uongozi wa zitto. Hvi tulitarajia apeleke fedha za posho yake jimboni kwa chiligati, Nyambari,January au kwa Majaliwa na wengineo wa CCM? Kila mbunge ana watu anawawakilisha ambao anawajibika kwao. Zitto kaonyesha njia apongezwe na si kukatishwa tamaa.
 
zitto huyu jamaa anafaa kuwa rais wetu 2015

Acha mbwembwe wewe. Juzi tu ametaka kuishitaki CDM TAKUKURU kwa sababu ya uchaguzi wa BAVICHA, leo katoka hivi tayari umemuona kuwa anafaa kuwa raisi wako. Kweli watanzania wengi wanasahau baada ya dakika moja tu na wala hawana backup ya information zao.
Swali ni kwamba, kwa nini Zitto ameamua kufanya hivyo? Je pato lake ni kiasi gani?

Je hiyo pesa amelenga kufanya nini?
Kujenga barabara, hospitali, shule au kuwa kwenye mfuko wa maendelo kwa ajili ya kunenepesha watu wengi tofauti na Zitto?

Mbona tuna mifuko mingi tu ya maendeleo amabayo haileti maendeleo zaidi ya ugomvi na chuki tu baina ya viongozi?
Mimi nahitaji kuona utendaji na wala siyo hizi vurugu za kisiasa ambazo hazina maana zaidi ya public popularity.
 
naona ingekuwa vizuri kama wabunge wote wa chadema
wangekataa posho cos nimoja ya mapendekezo yao
kwenye bajeti watakayo isoma jumatano
 
Back
Top Bottom