Barua ya wazi kwa wizara ya afya, tamisemi na wahusika wengine

pombe kali

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
225
447
Salamu ziwafikie nyote,
Naandika kwa wino unaovuja damu pia nitajitahidi kukosoa kwa staha, baada ya hosipitali ya amana kupewa hadhi ya rufaa, kuna hosipitali ilijengwa huku kivule ambayo inajulikana kama hosipitali ya wilaya ya kivule, mgonjwa anatakiwa aanzie hapo ndipo apewe rufaa ya kwenda Amana cha kusikitisha hosipitali hii imekuwa ni gofu linalotisha hata kupita usiku unaogopa, hakuna usafiri wa uma unaofika hapo usafiri pekee uliopo ni pikipiki na ukifika umechoka kama vile umepigwa ukifanikiwa kufika hakuna huduma madaktari hawapo ukienda moja kwa moja amana ambayo ni safari ya nusu siku kutokana na ubovu wa barabara wanakurudisha kule kule kivule kwa madai kuwa huwezi kuanzia hosipitali ya rufaa..kuna mtoto hapa jirani amevunjika mkono nimejitolea kumpeleka hosipitali yamenikuta hayo madhira mwishowe wazazi wake wakaamua kumpeka kwa mtaalamu wa tiba asilia, inaumiza watu na kutufanya tuwe na chuki kubwa sana na serikali yetu, kuna mtoto mwingine alibakwa alienda kuchukua pf3 kisha wakaenda hosipitali akakosa huduma na alipofika amana alipewa huduma ila kwa masimango makubwa na kuulizwa kwa nini mmekuja hosipitali ya rufaa na huku mlikotoka kuna hosipitali. Mheshiwa waziri uelewa wangu mdogo najua mambo ya serikali ni mchakato mrefu ili yatimie lakini wewe ni mwanamama liangalie hili kama mzazi jitahidi uje utembee tu huku hosipitali uone wananchi wanavyoteseka na barabara hii ya kuelekea hosipitali ya wilaya isiyo na huduma..
 
Back
Top Bottom