Barua ya wazi kwa Mh Rais Dkt Magufuli, Wape muda watanzania, tatizo ni NIDA

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
MH RAIS WAPE MUDA WATANZANIA, TATIZO NI NIDA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema aliyenipa afya njema na nguvu ili niweze kukuandikia barua hii ya wazi Mh Rais. Pia nitumie wasaa huu kuwatakia heri ya mwaka mpya Watanzania wote ambao Mungu ameendelea kuwalinda na kuwavusha mwaka mpya wa 2020. Hongereni sana. Na mwaka huu uwe mwaka wa kutimiza ndoto ya kila mmoja kwa kadili Mungu alivyokusudia.

Pili nikupongeze Mh Rais kwa kuendelea kuisimamia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Nikupongeze pia kwa kazi kubwa unayofanya ili kuliletea Taifa hili maendeleo. Wewe na timu yako munaendelea kuandika historia kubwa katika Taifa hili. Kamwe msiyumbishwe na kelele za baadhi ya Watanzania wenzetu ambao hawaini jema lolote kwenu.

Wapo wachache waliokuwa wanufaika wakuu wa mifumo ya zamani ambayo iliruhusu gepu kubwa Kati ya wanyonyaji na wanyonywaji. Waliokuwa wamezoea kunyonya baada ya mirija kuzibwa ni lazima walalamike na taratibu wataanza kuzoea. Kazi kubwa ya miaka minne inaonekana kwa macho na si kazi yangu kuielezea kwa leo.

Mh Rais mwishoni mwa mwezi Desemba ulipoenda kusajili laini yako ya Airtel ulinukuliwa na vyombo vya habari ukiongeza siku 20 za usajili wa laini za simu ambapo zoezi hili ilitakiwa likamilike Disemba 31 mwaka 2019. Baada ya kauli yako inaonyesha sasa zoezi hili litaendelea hadi January 20, 2020. Ninaungana na WATANZANIA wote waliokupongeza kwa moyo wako wa huruma kwa kusikia kilio chao. Lakini Mh Rais pamoja na kuongoza siku bado kuna changamoto kubwa ambayo ninakuomba uitazame tena kwa jicho la uzazi na ulezi kwa Watanzania hawa.

Kabla sijazungumza changamoto hii ni lazima nikili wazi kwamba kusajili laini za simu ni jambo la mhimu sana. Mimi ni sehemu ya wahanga ambao tumekoswa koswa na wahuni waliokuwa wanatumia vibaya simu zao. Na mara nyingi hawa wahalifu ilikuwa ni ngumu kuwakamata kwa kuwa simu zao hazikuwa katika mifumo mizuri ya kuweza kuzibaini ziliko na kuwajua wanaozitumia kwani walitumia majina yasiyo ya kwao. Baada ya kila mtu kusajili laini ya simu yake sasa uhalifu wa kutumia simu utapungua na kila mtu atamiliki simu ambayo inatumia jina lake halisi na si majina ya kughushi.

Mh Rais pamoja na nia yako njema ya kuongeza siku 20, Mimi ninakuomba uongeze siku nyingi zaidi ili kila mtanzania mwenye simu aweze kupata haki yake. Wapo Watanzania wengi ambao wanatamani kutii agizo la serikali ambayo ni matokeo ya sheria iliyotungwa na Bunge letu, lakini kumekuwa na changamoto ya watu wa NIDA. Mh Rais wapo wananchi ambao taarifa zao zilichukuliwa na NIDA lakini hadi sasa hawana vitambulisho wala namba zao hazipo.

Wapo wanaojaribu ku request namba zao NIDA lakini hawajapata, lakini wapo ambao hadi leo hawajafanikiwa kuchukuliwa alama zao na watu wa NIDA. Mh Rais hawa watu pamoja na nia njema ya kuhakikisha tunaliweka taifa katika usalama, lakini pia hili litaathiri uchumi wa Taifa kwani tutakosa kodi kwa laini zitakazofungiwa kwa sababu tu watu wa NIDA wamewacheleweshea watu kadi/ namba zao.

Mh Rais, ombi langu kwako kwa niaba ya Watanzania hasa ndugu zangu wa Ileje ni ku kuomba Mh Rais tena Rais wa wanyonge kuongeza muda na kuwaagiza watu wa NIDA waende vijijini. Ninawaomba NIDA wafanye process ili watu wote waliokusimamisha chukuliwa alama wapewe namba zao na wasajiliwe. Ninaamini Mh Rais ukiongeza siku na ukatoa maagizo kwa watu wanaohusika kutoa vitambulisho utakuwa umewasaidia wananchi wengi.

Mh Rais ninatambua upendo na adhima yako kwa Taifa hili, lakini ninatambua moyo wako wa huruma kwa Watanzania hawa. Ni matumaini yangu utalegeza mashariti ili Watanzania hawa waweze kupata haki yao ya kusajili laini zao za simu.

Mwisho ninakutakia kazi njema na Mungu aendelee kukulinda na kukupa nguvu ili kufikia Tanzania ya viwanda na yenye Uchumi wa kati.
 
Maneno ya busara sana, sema tu utangulizi mrefu unaweza kumchosha Rais asipate hoja msingi maana hoja msingi ipo karibia na mwisho, ila kwa kuwa ni msikivu ataongeza spidi ya NIDA
 
Unahangaika bure.. .Rais ana vyombo vya kutosha kumweleza ukweli, hili la kulazimisha fingerprints na namba za NIDA untimely ni ubabe tu .....
Usilojua ni kwamba kuna watu ID zao zita expire kabla ya wengine kupata za kwanza... hii ndio bongo...
Acha watu waendeshe mambo wanavyotaka nchi ni yao..
Kujiita mnyonge kwenye issues za systems failure kama hizi ni kujidharaulisha tu...
 
MH RAIS WAPE MUDA WATANZANIA, TATIZO NI NIDA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema aliyenipa afya njema na nguvu ili niweze kukuandikia barua hii ya wazi Mh Rais. Pia nitumie wasaa huu kuwatakia heri ya mwaka mpya Watanzania wote ambao Mungu ameendelea kuwalinda na kuwavusha mwaka mpya wa 2020. Hongereni sana. Na mwaka huu uwe mwaka wa kutimiza ndoto ya kila mmoja kwa kadili Mungu alivyokusudia.

Pili nikupongeze Mh Rais kwa kuendelea kuisimamia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Nikupongeze pia kwa kazi kubwa unayofanya ili kuliletea Taifa hili maendeleo. Wewe na timu yako munaendelea kuandika historia kubwa katika Taifa hili. Kamwe msiyumbishwe na kelele za baadhi ya Watanzania wenzetu ambao hawaini jema lolote kwenu.

Wapo wachache waliokuwa wanufaika wakuu wa mifumo ya zamani ambayo iliruhusu gepu kubwa Kati ya wanyonyaji na wanyonywaji. Waliokuwa wamezoea kunyonya baada ya mirija kuzibwa ni lazima walalamike na taratibu wataanza kuzoea. Kazi kubwa ya miaka minne inaonekana kwa macho na si kazi yangu kuielezea kwa leo.

Mh Rais mwishoni mwa mwezi Desemba ulipoenda kusajili laini yako ya Airtel ulinukuliwa na vyombo vya habari ukiongeza siku 20 za usajili wa laini za simu ambapo zoezi hili ilitakiwa likamilike Disemba 31 mwaka 2019. Baada ya kauli yako inaonyesha sasa zoezi hili litaendelea hadi January 20, 2020. Ninaungana na WATANZANIA wote waliokupongeza kwa moyo wako wa huruma kwa kusikia kilio chao. Lakini Mh Rais pamoja na kuongoza siku bado kuna changamoto kubwa ambayo ninakuomba uitazame tena kwa jicho la uzazi na ulezi kwa Watanzania hawa.

Kabla sijazungumza changamoto hii ni lazima nikili wazi kwamba kusajili laini za simu ni jambo la mhimu sana. Mimi ni sehemu ya wahanga ambao tumekoswa koswa na wahuni waliokuwa wanatumia vibaya simu zao. Na mara nyingi hawa wahalifu ilikuwa ni ngumu kuwakamata kwa kuwa simu zao hazikuwa katika mifumo mizuri ya kuweza kuzibaini ziliko na kuwajua wanaozitumia kwani walitumia majina yasiyo ya kwao. Baada ya kila mtu kusajili laini ya simu yake sasa uhalifu wa kutumia simu utapungua na kila mtu atamiliki simu ambayo inatumia jina lake halisi na si majina ya kughushi.

Mh Rais pamoja na nia yako njema ya kuongeza siku 20, Mimi ninakuomba uongeze siku nyingi zaidi ili kila mtanzania mwenye simu aweze kupata haki yake. Wapo Watanzania wengi ambao wanatamani kutii agizo la serikali ambayo ni matokeo ya sheria iliyotungwa na Bunge letu, lakini kumekuwa na changamoto ya watu wa NIDA. Mh Rais wapo wananchi ambao taarifa zao zilichukuliwa na NIDA lakini hadi sasa hawana vitambulisho wala namba zao hazipo.

Wapo wanaojaribu ku request namba zao NIDA lakini hawajapata, lakini wapo ambao hadi leo hawajafanikiwa kuchukuliwa alama zao na watu wa NIDA. Mh Rais hawa watu pamoja na nia njema ya kuhakikisha tunaliweka taifa katika usalama, lakini pia hili litaathiri uchumi wa Taifa kwani tutakosa kodi kwa laini zitakazofungiwa kwa sababu tu watu wa NIDA wamewacheleweshea watu kadi/ namba zao.

Mh Rais, ombi langu kwako kwa niaba ya Watanzania hasa ndugu zangu wa Ileje ni ku kuomba Mh Rais tena Rais wa wanyonge kuongeza muda na kuwaagiza watu wa NIDA waende vijijini. Ninawaomba NIDA wafanye process ili watu wote waliokusimamisha chukuliwa alama wapewe namba zao na wasajiliwe. Ninaamini Mh Rais ukiongeza siku na ukatoa maagizo kwa watu wanaohusika kutoa vitambulisho utakuwa umewasaidia wananchi wengi.

Mh Rais ninatambua upendo na adhima yako kwa Taifa hili, lakini ninatambua moyo wako wa huruma kwa Watanzania hawa. Ni matumaini yangu utalegeza mashariti ili Watanzania hawa waweze kupata haki yao ya kusajili laini zao za simu.

Mwisho ninakutakia kazi njema na Mungu aendelee kukulinda na kukupa nguvu ili kufikia Tanzania ya viwanda na yenye Uchumi wa kati.
Shida ipo kwetu watanzania. Mtu anajiandikisha, ukifika muda wa kuchukua namba, unakuta kasahau majina aliyojiandikisha, kasahau majina ya wazazi hata tarehe ya kuzaliwa. Inabidi apige picha mara ya pili, matokeo system inakataa kwani anakuwa 'Duplicate'.

Mtu Kama huyu hata aende wapi hawezi kusajiliwa kwani finger print zake tayari zipo kwenye mfumo. Tujifunze kutunza kumbukumbu na kusema ukweli, sio kuwalaumu watenda kazi wa NIDA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja, kwanza inabidi NIDA wafanye kazi masaa 24.
Pili wahakikishe zoezi la uchukuaji taarifa na kuzichakata linafanyika kwa haraka.
 
Watu si mnasema Magufuli kaleta nidhamu na uwajibikaji serikalini? Sasa NIDA inakuwaje tatizo? au NIDA si sehemu ya Serikali hii?
 
Kwa kweli shida in NIDA, ila pia viambanisho in shida kwa baadhi ya watu haswa wazee. Busara inatakiwa itumike barua ya mtendaji iliyosainiwa pamoja na mjumbe in utambulisho tosha sana
 
Afisa Uhamiaji Aliandika CQ kwenye Form yangu na kuniambia ipo poa niwape nida mwaka Jana Machi.. nimeenda NIDA December hii baada ya kuona sipati namba kwa mfumo waliouweka ndo wananiambia fimu Ina shida niende Uhamiaji!

Sasa kama yule afisa alikuwa na mashaka si angenijulisha tuu mapema mwezi Machi mwaka Jana?
 
Shida ipo kwetu watanzania. Mtu anajiandikisha, ukifika muda wa kuchukua namba, unakuta kasahau majina aliyojiandikisha, kasahau majina ya wazazi hata tarehe ya kuzaliwa. Inabidi apige picha mara ya pili, matokeo system inakataa kwani anakuwa 'Duplicate'.

Mtu Kama huyu hata aende wapi hawezi kusajiliwa kwani finger print zake tayari zipo kwenye mfumo. Tujifunze kutunza kumbukumbu na kusema ukweli, sio kuwalaumu watenda kazi wa NIDA

Sent using Jamii Forums mobile app
AAAAAAH,weweeeeee,namba za simu tu zinatosha kumpa mtu kitambulisho chake cha NIDA,au labda tuseme kila mahali wana maswali yao,lakini wengine tumeenda kuchukua namba kwa kutaja namba ya simu,tu,sasa hayo maswali mengine ya nini,na ina maana mfumo wao ni mdhaifu kiasi hicho cha kuhifadhi kumbukumbu kidogo tu ?
 
Shida ipo kwetu watanzania. Mtu anajiandikisha, ukifika muda wa kuchukua namba, unakuta kasahau majina aliyojiandikisha, kasahau majina ya wazazi hata tarehe ya kuzaliwa. Inabidi apige picha mara ya pili, matokeo system inakataa kwani anakuwa 'Duplicate'.

Mtu Kama huyu hata aende wapi hawezi kusajiliwa kwani finger print zake tayari zipo kwenye mfumo. Tujifunze kutunza kumbukumbu na kusema ukweli, sio kuwalaumu watenda kazi wa NIDA

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nini hao maofisa wa NIDA wasiwaambie watu wakaandika hayo majina yao ili siku wakienda kuchukua namba wasikosee,mimi hapa ni mmoja ya hao waliosahau majina yao😂😂😂
 
Ngoja kwanza niwaseme hawa jamaa wa NIDA KIBAHA
1. Hawa vijana wanaenda kwa kujuana sana yaani watu wapo kwenye foleni wanakuja watu wanaojuana nao hao hawakai foleni form zao zinachukuliwa wanaenda ndani wanaandikishwa wanapiga picha wanatoka wanakuacha upo kwenye foleni hapo.

2.Kama hujuani nao ili ufanyiwe haraka lazima utoe rushwa kwanza wanachukua form yako unaenda ndani moja kwa moja.

3.Hawa jamaa sijui mkubwa wao ni nani pale maana mda wrote wanajizungusha zungusha mara watoke nje waende dukani mara wanatoka wanaenda kukaa kwenye benchi huku umati wa watu wamekaa tu kwenye foleni.

NIDA KIBAHA NI JIPU LILILOIVA KABISA
Lakini mweshimiwa hawa viongozi wa mkoa wa Pwani anawachekea sana mfano.
Wametujengea kastendi kadogo kweli halafu hakana ubora kabisa kila siku kanatitia ukarabati unaanza upya.
 
Mh Rais hayo maneno yaliyoandikwa na huyu mwenzetu ni ya kweli kabisa. Hadi sasa kuna watu majina yao yapo katika mtandao tangu awamu ya kwanza kabisa lakini kuna ukiritimba NIRA ambao imesababisha MAMILIONI YA WATANZANIA KUSHINDWA KUPATA VITAMBULISHO VYAO. NIDA wamekuwa na sababu za ajabu sana kwamba mtu anaambiwa akalete cheti cha kuzaliwa cha marehemu Baba yake. Baba mwenyewe alizaliwa miaka ya 1920's hicho cheti halikuwepo, unatengeneza Afidavit wanakula zimeisha ipeleke cheti au Passport ya Mzazi wako. Milolongo ya namna hii imetengeneza mianya ya rushwa kwa hawa watendaji wa NIDA

Mh Rais kwa kweli ikiwezekana badili uongozi wa NIDA ili wajifunze jinsi nyingine ya kutufaa badala ya kufanya kazi kwa mazoea. Miaka imepita tunafuatilia kitambulisho cha NIDA bila mafanikio. Tutashukuru sana ikiwa Mh Rais utaongeza muda wa kutosha na kufanya mabadiliko hapo NIDA. Asante sana Mh Rais.
 
Shida ipo kwetu watanzania. Mtu anajiandikisha, ukifika muda wa kuchukua namba, unakuta kasahau majina aliyojiandikisha, kasahau majina ya wazazi hata tarehe ya kuzaliwa. Inabidi apige picha mara ya pili, matokeo system inakataa kwani anakuwa 'Duplicate'.

Mtu Kama huyu hata aende wapi hawezi kusajiliwa kwani finger print zake tayari zipo kwenye mfumo. Tujifunze kutunza kumbukumbu na kusema ukweli, sio kuwalaumu watenda kazi wa NIDA

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo siyo hilo....

Tatizo ninaloliona hasa kwenye hili la vitambulisho vya NIDA baada tu ya kujiandikisha inamchukua mtu tena takribani miezi kibao ili aje apate kitambulisho,

je system au technology inayotumika na TUME YA UCHAGUZI zinautofauti gani mpaka zinachelewesha hilo nafikiri wangepewa Tume ya Uchaguzi watumie system na technology yao ili utakapo enda kujiandikisha upate kila kitu kwasababu kitambulisho ni haki kwa kila mwanachi japo changu kinakaribia kuexpire

Jambo jingine hili la muda kuongezwa au kuto kuongezwa mimi naamini vitambulisho si kwaajili ya kutuwezesha tuweze kuwasiliana na tuwapendao Tu bali hata kuonyesha uraia wetu na utaifa kwa ujumla

Mwisho

Nawaomba msiweke ukomo wa kufungia hizo line za simu maana watu wanahangaika tu wapate vitambulisho au namba kwaajili ya kusajili simu kadi zao, je hii ndio maana ya kuwa na kitambulisho cha Taifa?

Taasisi ijikite kuelimisha umuhimu wa vitambulisho vya Utaifa hapo tutafikia lengo na lolote litakalotokea linalohusu kitambulisho cha Taifa kama wananchi wote wamepata elimu na maarifa zaidi, hatutoweza kushuhudia mahangaiko wanayoyapata wabibi, wababu,mama zetu hapo siku za usoni

Ni mtazamo wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom