Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 322
- 645
MH RAIS WAPE MUDA WATANZANIA, TATIZO NI NIDA.
Na Elius Ndabila
0768239284
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema aliyenipa afya njema na nguvu ili niweze kukuandikia barua hii ya wazi Mh Rais. Pia nitumie wasaa huu kuwatakia heri ya mwaka mpya Watanzania wote ambao Mungu ameendelea kuwalinda na kuwavusha mwaka mpya wa 2020. Hongereni sana. Na mwaka huu uwe mwaka wa kutimiza ndoto ya kila mmoja kwa kadili Mungu alivyokusudia.
Pili nikupongeze Mh Rais kwa kuendelea kuisimamia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Nikupongeze pia kwa kazi kubwa unayofanya ili kuliletea Taifa hili maendeleo. Wewe na timu yako munaendelea kuandika historia kubwa katika Taifa hili. Kamwe msiyumbishwe na kelele za baadhi ya Watanzania wenzetu ambao hawaini jema lolote kwenu.
Wapo wachache waliokuwa wanufaika wakuu wa mifumo ya zamani ambayo iliruhusu gepu kubwa Kati ya wanyonyaji na wanyonywaji. Waliokuwa wamezoea kunyonya baada ya mirija kuzibwa ni lazima walalamike na taratibu wataanza kuzoea. Kazi kubwa ya miaka minne inaonekana kwa macho na si kazi yangu kuielezea kwa leo.
Mh Rais mwishoni mwa mwezi Desemba ulipoenda kusajili laini yako ya Airtel ulinukuliwa na vyombo vya habari ukiongeza siku 20 za usajili wa laini za simu ambapo zoezi hili ilitakiwa likamilike Disemba 31 mwaka 2019. Baada ya kauli yako inaonyesha sasa zoezi hili litaendelea hadi January 20, 2020. Ninaungana na WATANZANIA wote waliokupongeza kwa moyo wako wa huruma kwa kusikia kilio chao. Lakini Mh Rais pamoja na kuongoza siku bado kuna changamoto kubwa ambayo ninakuomba uitazame tena kwa jicho la uzazi na ulezi kwa Watanzania hawa.
Kabla sijazungumza changamoto hii ni lazima nikili wazi kwamba kusajili laini za simu ni jambo la mhimu sana. Mimi ni sehemu ya wahanga ambao tumekoswa koswa na wahuni waliokuwa wanatumia vibaya simu zao. Na mara nyingi hawa wahalifu ilikuwa ni ngumu kuwakamata kwa kuwa simu zao hazikuwa katika mifumo mizuri ya kuweza kuzibaini ziliko na kuwajua wanaozitumia kwani walitumia majina yasiyo ya kwao. Baada ya kila mtu kusajili laini ya simu yake sasa uhalifu wa kutumia simu utapungua na kila mtu atamiliki simu ambayo inatumia jina lake halisi na si majina ya kughushi.
Mh Rais pamoja na nia yako njema ya kuongeza siku 20, Mimi ninakuomba uongeze siku nyingi zaidi ili kila mtanzania mwenye simu aweze kupata haki yake. Wapo Watanzania wengi ambao wanatamani kutii agizo la serikali ambayo ni matokeo ya sheria iliyotungwa na Bunge letu, lakini kumekuwa na changamoto ya watu wa NIDA. Mh Rais wapo wananchi ambao taarifa zao zilichukuliwa na NIDA lakini hadi sasa hawana vitambulisho wala namba zao hazipo.
Wapo wanaojaribu ku request namba zao NIDA lakini hawajapata, lakini wapo ambao hadi leo hawajafanikiwa kuchukuliwa alama zao na watu wa NIDA. Mh Rais hawa watu pamoja na nia njema ya kuhakikisha tunaliweka taifa katika usalama, lakini pia hili litaathiri uchumi wa Taifa kwani tutakosa kodi kwa laini zitakazofungiwa kwa sababu tu watu wa NIDA wamewacheleweshea watu kadi/ namba zao.
Mh Rais, ombi langu kwako kwa niaba ya Watanzania hasa ndugu zangu wa Ileje ni ku kuomba Mh Rais tena Rais wa wanyonge kuongeza muda na kuwaagiza watu wa NIDA waende vijijini. Ninawaomba NIDA wafanye process ili watu wote waliokusimamisha chukuliwa alama wapewe namba zao na wasajiliwe. Ninaamini Mh Rais ukiongeza siku na ukatoa maagizo kwa watu wanaohusika kutoa vitambulisho utakuwa umewasaidia wananchi wengi.
Mh Rais ninatambua upendo na adhima yako kwa Taifa hili, lakini ninatambua moyo wako wa huruma kwa Watanzania hawa. Ni matumaini yangu utalegeza mashariti ili Watanzania hawa waweze kupata haki yao ya kusajili laini zao za simu.
Mwisho ninakutakia kazi njema na Mungu aendelee kukulinda na kukupa nguvu ili kufikia Tanzania ya viwanda na yenye Uchumi wa kati.