Barua ya wazi kwa dada Halima Mdee

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,446
6,311
Dada halima najua uko poa kabisa

Madhumuni ya barua hii ya wazi ni kutaka kukufikishia ujumbe ufuatao

Kuna taarifa nimezipata chini ya kapeti zikisema kuwa asilimia kubwa ya Wabunge wanaume ambao wamekosa ubunge ndio wanapambana nyie wakina mama msiende viti maalum

Napenda kukwambia kuwa hao wabunge wanasema nyie msiende ni kwa sababu ya ubinafsi wao tu. Hii fursa ingekuwa ya wao wanaume wasingewasikiliza nyie kabisa ingekuwa wameshaenda long time

Wewe ndio kiongozi wa wanawake CHADEMA please acha kusikiliza hao wabinafsi, peleka majina ya akina mama wenzako ili mkatetee Chama

Miaka yote CHADEMA huwa hairidhiki na matokeo ila huwa wanaenda Bungeni hiyo ni kwa sababu wanaume wengi walikuwa wanachaguliwa

Najua una changamoto sana juu ya suala hili but be strong and peleka majina tume. Mwanaume ambae anakwambia msiende bungeni then mwambie avae sketi aende yeye.
 
Ni kweli Dada Halima, jifunze kufanya positive decision ili kujiweka in positive side kila wakati. Uchaguzi wa maisha mabaya ya kisiasa ni mtu mwenyewe huchagua. Lakini all in all siasa za kujiumiza binafsi sioni kama zina tija kipindi hiki. Peleka majina
 
Ni kweli Dada Halima, jifunze kufanya positive decision ili kujiweka in positive side kila wakati. Uchaguzi wa maisha ya mabaya ya kisiasa ni mtu mwenyewe huchagua. Lakini all in all siasa za kujiumiza binafsi sioni kama zina tija kipindi hiki. Peleka majina

Absolutely uko sahihi
 
Akili kama za Ndugai hizi. Unajua kuwa kama kura zingeheshimiwa pengine ushindi wa Chadema ungesababisha ipate viti maalumu sio chini ya 80?

Sasa kwa nini hao 19 wakubali wakati wenzao zaidi ya 60 wamedhulumiwa?
Kukubali jambo hilo sio ujinga ulio vuka mipaka?

Na je unadhani hao 19 wanalazimishwa waende kwa manufaa ya demokrasia na CHADEMA au kwa manufaa ya CCM kutambulika ina bunge la vyama vingi?
 
Akili kama za Ndugai hizi. Unajua kuwa kama kura zingeheshimiwa pengine ushindi wa Chadema ungesababisha ipate viti maalumu sio chini ya 80?
Sasa kwa nini hao 19 wakubali wakati wenzao zaidi ya 60 wamezulumiwa?
Kukubali jambo hilo sio ujinga ulio vuka mipaka?
Na jee unadhani hao 19 wanalazimishwa waende kwa manufaa ya demokrasia na Chadema au kwa manufaa ya ccm kutambulika ina bunge LA vyama vingi?

Sasa basi jambo la msingi ni kufuta chama na kila mtu akafanye biashara yake

Chadema kuwa nje ya platform ya kuongea kwa miaka mitano ujui 2025 itakuwa ni kazi kubwa sana kishawishi watu?

But pia nikuulize swali je ni lini uchaguzi wa Tanzania ulikuwa huru na haki? Mbona hakuna chaguzi ambayo mligomea?

Tuache mfumo dume na ubinafsi wa kijinga
 
Akili kama za Ndugai hizi. Unajua kuwa kama kura zingeheshimiwa pengine ushindi wa Chadema ungesababisha ipate viti maalumu sio chini ya 80?
Sasa kwa nini hao 19 wakubali wakati wenzao zaidi ya 60 wamezulumiwa?
Kukubali jambo hilo sio ujinga ulio vuka mipaka?
Na jee unadhani hao 19 wanalazimishwa waende kwa manufaa ya demokrasia na Chadema au kwa manufaa ya ccm kutambulika ina bunge LA vyama vingi?
Serikali za mitaa walilizwa nafasi zote na bado mwaka huu wakaingia kwenye uchaguzi kwa kuwa zilikuwa ni nafasi yao, wakaamini watapita. Ubinafsi wa viongozi unaponza chama. Wanapoona ni nafasi zao wanaingia uchaguzini, sasa ngoja nao wasikilizie joto ya jiwe!
 
Back
Top Bottom