Barua ya Papii Kocha kwa JK

Barua ya Papii Kocha kwa JK

Naona anajaribu kulinganisha haya maneno!
Msaada na msamaha!

Msamaha kwa kosa gani?
Na kama unakiri kosa ni wazi kwa kosa hili unalo kiri kulifanya halistahili msamaha!

Hakika tafsiri ya kuomba msamaha inaweza ikawa njia ya kuendelea kuwatia hatiani kabisa!
 
Salimaaaa! Uliniacha mimi...........Wimbo huu ulichangia s
ana kwani huyo salimaa ni yupi? Au ni salma jk. Hapo ndo maana tunasema mahakama zetu zinatumiwa na wakuu
 
Hii laana ndo inamtafuna jk kila siku matatizo na bado!
 
Huyu na babake si nilisikia walifungwa kwa kusingiziwa na aliyetaka wafungwe ndie huyo huyo wanamuomba msamaha! hapo chacha mi sidhani kama itawezekana hii kitu kwani jamaa alijiapiza lazima waozee jela sidhani kilipizo chake mwenyewe anaweza kukivunja manake kinaweza kikamrudia yeye akimaliza utawla wake anaweza zamishwa....!

Walisingiziwa? Ushahidi wa picha mpaka za video ulitolewa mahakamani, walikuwa wanawala na kuwalawiti watoto wadogo wa shule za msingi. Hao ilikuwa wauliwe tu. Si wakuhurumiwa hata kidogo, fikiria wale watoto sasa hivi wanaojiita hizi nyuzi na waneshakuwa watu wazima. Roho zao zinawauma vipi wakikumbuka unyama waliofanyiwa kwa kudanganywa kwa chipsi na biskuti!
 
haa! Jamaa kafafanua kuwa hakutenda kosa hvyo wenye mamlaka walitumia mamlaka yao kuwafunga yeye pamoja na watoto wake wote. Kwn we haujui km demu wa mjomba ndo aliyesababisha haya?

Hujajibu swali.

Kuomba msamaha ni kukubali kukosea.

Huwezi kukubali kukosea, kuomba msamaha, halafu kusema hujakosea.

Ama unasema "naomba msamaha nimekosea" unakubali umekosea na kuomba msamaha, au unasema "sikukosea nimefungwa kwa makosa, nataka kuachiwa".

Huwezi kuomba msamaha halafu ukasema hukufanya kosa.

Msamaha wa nini na wewe hukufanya kosa?
 
Nikifikaka hapa ndo huwa naamini Walioko magerezani sio wote wanamakosa!! Why hii issue watu wanaikomalia sana??? By the way hakuna kisichokuwa na mwisho n I hope siku moja haya yatafika Mwisho
 
Hizi NGOZI kweli ni tamu! Yani unamtesa mwenzako hivyo kwa sababu ya haya makitu!! Nukuu ya msiba toka kwa Jk, Kifo kilikuwa kinatafuta sababu!! Kweli haya makitu ni matamu Lulu yuko nje kwa dhamana
 
Ili watoke jela waombe cdm ichukuwe nchi 2015.maana watanzania wanajua kuwa walifungwa kwa hujuma na hila mbaya ya m/magogoni. Mungu awalinde ili msipate maradhi. Iko siku mtatoka
 
Laana ni wewe unaeshadidia ushenzi walioufanya hawa wakongo kwa watoto na wajukuu zetu.

Hakika Zomba huwa nikisoma comments zako, huwa najuta kabisa kuzaliwa mtanzania na kuwa na watu wanalamba miguu viongozi na huku taifa halijulikani liendako. Ila naamini kitu kimoja Bendera hufuata upepo na kila mtu anaakili zake. Iz better kama hii kesi inamkono wake angewahukumu kifo. Niliamini sana katika huyu Rais JK. Nilishinda barabarani namsubilia 2004 ili japo nimuone my next presidend! Baada ya kukata tamaa na Mh. Benja, Lakini sijiraumu ila huwa najiuliza why Nyerere alimkataa JK na Lowa????Na kwa nini Nyerere alikufa na kifo chake kilikuwa na utata sana?? Kwa haya huwa najifariji kwa kauli ya yule mh aliyesema Wabunge wa Dar wanafikiri kwa kutumia makalio na watu wakaubatiza msemo huu nakuwa wanafiki kwa kutumia Masabuli??? Masabuli ni nani na ni nini!!
 
Mbona nilisikia kesi ya hawa jamaa ilitengenezwa............ni kweli?
 
Haeka Mangi nimegonga LIKE; hapo umemalisa ubishi mangi... haingii akilini eti mtu na watoto kushea demu tena kwa kubaka.waiiih meku!!!
 
Laana ni wewe unaeshadidia ushenzi walioufanya hawa wakongo kwa watoto na wajukuu zetu.

Siku hizi kuna teknolojia watu wanatengeneza vidio za ushaidi! Ni mambo ya mademu tu hamna lingine hapo!
 
Hii tabia ya kutetea watu maarufu tu wakati kuna maelfu ya maskini na watu wengine wa chini walioonewa na mamlaka mbalimbali hakuna apazaye sauti yake.....CHANGE!!!
 
Siku hizi kuna teknolojia watu wanatengeneza vidio za ushaidi! Ni mambo ya mademu tu hamna lingine hapo!

Na wale mahakimu na mawakili wote unafikiri wana ujinga kiasi unachokionesha hapa? na wale watoto wote na waalimu na wazee wao waliokwenda kutowa ushahidi mahakamani nao wote wakutengenezwa?

Mambo mengine mnakuwa kama misukule hamuamini mahakama wala hata raia wenzenu basi hata watoto wadogo wasio na hatia nao hamuwaamini? tafadhali.
 
Back
Top Bottom