Sanda Matuta
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 949
- 134
Wakulu nimeiona hii ikizagaa za gaa kule kwa JayDee, naona kama watu wameogopa kuileta huku kwa haraka kama wafanyavyo kwa zengine. Labda kwa sababu ya history.
Hapa ni kwake mahara muafaka kwani ninaamini watu wengi wanasoma JF (nadhani) hata mushemiwa rais.
Pia (siku moja kwenye taarifa ya habari ya TBC niliona akisoma habari furani kwenye page ya jf wakisisitiza habari kutoka kwenye chombo cha habari).
Sasa muheshimiwa kabla haijaja rasmi mezani kwako hii hapa barua.
Hapa ni kwake mahara muafaka kwani ninaamini watu wengi wanasoma JF (nadhani) hata mushemiwa rais.
Pia (siku moja kwenye taarifa ya habari ya TBC niliona akisoma habari furani kwenye page ya jf wakisisitiza habari kutoka kwenye chombo cha habari).
Sasa muheshimiwa kabla haijaja rasmi mezani kwako hii hapa barua.
MF/NA: 836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam
Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania
YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.
Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga.
Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais. Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais
Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.
Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.
Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi.
Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu
Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.
Mungu akubariki!
Wako mtiifu
NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)
Tahadhari:
Inaruhusiwa kuinakili hii story kama ilivyo ( i wont mind), ila sio vibaya pia mkitoa credit na sio kusema eti ni kutokana na vyanzo vyenu vya habari.
Walengwa mnajijua sio lazima nitaje majina (jaydee)