Sanda Matuta
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 949
- 142
- Thread starter
-
- #41
Unajua blogu ya JD ni ya habari nilichouliza mimi kuna maelezo yoyote kwenye blogu yake yanayoeleza jinsi anavyopokea habari na kuziweka kwenye blogu yake na jinsi watu wanavyoweza kutumia kazi za blogu hiyo ? najua kwamba ni blog spot kwahiyo watu wafuate maelezo ya blogger ambayo ni mali ya google lakini kulitakiwa kuwe na maelezo ya ziada haswa yanayoendana na sheria za nchi husika kama tanzania blogu na tovuti nyingi hazina hivyo hata jf haina terms of use ambayo inaendana na na mazingira ya tanzania
Barua iko too simple lakini kuna mambo mawili yamejificha hapa.
kwanza
Huyu nguza inawezekana kabisa hakutaka kuweka mambo hadhani, Kwa mfano hakutaka kuzungumzia kama alisingiziwa au la! Nafikiri ingekuwa si busara kama angesema kwamba "Mheshimiwa nisaheme kwa sababu nilisingiziwa ".
Vile vile issue hii ina muhusu Nguza na Muheshimiwa kwa hiyo chochote atakachoandika lzm kiandikwe kwa umakini.
...
...ni ukweli 99.9%!
Kwenye mila na desturi hizi za kibantu, ukishaanza kusema 'lakini' maana yake unamuweka pabaya 'mzee wa busara.' Heri hivyo hivyo 'alivyoandika' bila kusema lolote kuhusiana na kesi au hukumu yake.
Mie barua hii nahisi kama vile ni ya kizushi.,na kama ni ya kweli basi Lady JD amechemka kuiweka kwenye Blog yake kabla haijamfikia mkuu.,mchana wa leo nimesikia katika kipindi cha XXL Clouds FM kuwa JD alipewa barua hiyo aifikishe kwa mkuu, lakini kwa kuwa si rahisi yeye kuonana nae akaamua aipost kwanza kwenye Blog yake wakati juhudi za kuiwasilisha kwa mlengwa zinaendelea ili wananchi wasikie kilio cha Papii na labda mkuu mwenyewe anaweza kukutana nayo kwenye hiyo Blog.
Naamini hii barua ilikuwa ni ya Rais personal.,sasa imekuwaje huyu JD akaisoma tena na kuiweka kwenye mtandao kabla aliyeandikiwa hajaipokea?
Hawezi kuzungumzia kesi kwa sababu kuna uwezekano wa ku file kesi mbele zaidi kwa hiyo kuongelea kesi na kusema alifungwa kimakosa sio sasa,anachomuomba Mh. ni msamaha haijarishi ametenda ama la.Hivi huyu jamaa ni kweli alitenda hayo makosa? Mbona hazungumzii lolote kuhusu hilo?
Hivi kesi ya kubaka watoto huwa inahitaji msamaha wa Raisi??? naomba kuelimishwaaa
Ninavyojua barua kama hiyo lazima ingegusia ni nini kimetokea na kwanini yeye anaona anastahili kusamehewa. Sasa unaomba tu msamaha kwa kigezo cha umri wakati pale kuna kosa la jinai, sidhani kama ni njia nzuri ya kuomba huo msamaha. Yeye ali appeal kwa vigezo fulani fulani vya kisheria. Atumie namna kama ile kuomba msamaha badala ya kuomba general tu kama vile alienda enda tu kuhukumiwa bila makosa.
Aombe msamaha kwa wale watoto zaidi y kumi (10) waliowaharibu damn!
Una uwakika na unachosema??Unajuwa saa zingine tukae tufikiria kama watu wazima na tunajuwa nini tunachokiandika,eti kabaka watoto 10 acheni kushabikia vitu ambavyo vipo open na vinaonekana vya uongo!!
Sipendi justice ya kuangalia upande moja? hivi wale wazazi wa wale watoto mmewahi kuwauliza walivyo na hasira na huyu firauni? agh!
Mkuu fikiria kwanza hilo swala??Hivi mtu anaweza kuwabaka watoto 10 wote hao inawezekana kweli?
Hawezi kuzungumzia kesi kwa sababu kuna uwezekano wa ku file kesi mbele zaidi kwa hiyo kuongelea kesi na kusema alifungwa kimakosa sio sasa,anachomuomba Mh. ni msamaha haijarishi ametenda ama la.
ANATAKIWA AKIRI KWANZA KUTENDA KOSA LILILO MPELEKA JELA. Hiki kipande cha barua kinaonyesha kuomba msamahe bila kukiri kwa kinywa chake kwamba ALIWACHEZEA KINGONO WATOTO WADOGO. VINGINEVYO JELA NI SIZE YAKELakini mbona hiyo barua ni very simpo one ..mie nimeisoma naona kama barua ya kawaida saaana ,,mheshimiwa anaweza kuisoma na kuweka pembeni ..hebu aandike nyingine yenye kuonyesha msisitizo ....
Kufungua kesi mbele zaidi...?, mbona haiingii akilini, watafungua kesi wapi tena na imeshatoka mahakama ya rufaa ambayo ndio mahakama ya juu kabisa katika ngazi za mahakama ya Tanzania.,hata kama wakisamehewa leo hawawezi kufungua hata kesi ya kudai fidia kwani msamaha huo hautamaanisha kuwa hawana hatia wala hautawafutia hatia walionayo.,wangeweza tu kufanya hivyo kama wangeachiwa na mahakama tena kwa kuonekana kwamba hawana hatia.,so labda barua hii ifanye miujiza otherwise imeshakula kwao.
Mhh! hapo atajiingiza mtegoniMbona hajaongelea lolote kuhusu hukumu yake/
angemwomba rais akisema kwamba amehukumiwa kwa hila nadhani ingekuwa nzuri zaidi.