Barua ya Papii Kocha kwa JK

Barua ya Papii Kocha kwa JK

Mangi na penda kukupa pongezi sana kwa maelezo yako mafupi lakini yenye maana sana, ukweli kuwa wengi humu ndani wanakurupuka tuu kuhukumu watu bila sababu za msingi.

Lakini Tanzania kila jambo lina wezekana kwani siku mbili tumesikia Lema alivyo shinda kesi hivyo sina imani sana na watoa hukumu kwani hoja iliyo mfanya lema ashinde ilikuwa ndogo sana hata mimi ningeweza kuona kuwa hakupaswa kuvuliwa ubunge wake.

Ila ndio ilivyo tokea, turudi kwenye kesi ya Nguza na vijana wake, kuna wale wawili waliwekwa ndani pia kwa hukumu hiyo hiyo ila ilipo kwenda huku na kule ikaonekana hawakuhusika ni mahakama hizi hizi za tanzania zilifanya jambo hili. ukweli ni kwamba ningekuwa ni wale watoto ningeweza kufunga mashitaka kwa walio nizushia na kwa serekali pia kunifunga bila kosa.

Hivyo na imani kuwa hawa jamaa wameonewa sana hivyo kijana kama ameandika barua hiyo hakuna haja ya kumshambulia amesha sema mara nyingi hakuhusika sifahamu hao wanaotaka kwanza akiri kama alifanya au hakufanya wanataka kujua nini?
 
sio wote wlio jela wamekosa wengine wamesingiziwa. pole sana papii
 
Sidhani kama anaulazima wa kukiri, dhumuni kuu la barua ni kuomba msamaha
 
Only GOD knows, kama ni kweli walifanya hilo kosa au la!
- Ila kama ni kweli JK anahusika na hukumu hiyo, basi anayo nafasi pia ya kuwasamehe na kuwatoa.
- Na kama ni kweli walihusika na sheria kweli ilfata mkondo wake, basi wao Watubu tu na kumuomba sana mungu awasamehe madhambi yao na awape wepesi ktk mustakbali wa maisha yao ya duniani na ya akhera.
 
KAMA HUKUWAHI KUISOMA BARUA YA PAPII KOCHA KWENDA KWA RAIS JAKAYA KIKWETE, KUPITIA KWA LADY JAY DEE HII HAPA >>>MF/NA: 836'04|Johnson Nguza (Papii Kocha)Gereza Kuu UkongaS.L.P 9091Dar es Salaam Mh. Rais Jamuhuriya MuunganoTanzania YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU. Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga. Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais.Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu. Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi. Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.Mungu akubariki Wako mtiifuNO:836'04 JOHNSON NGUZA(PAPII KOCHA)
 
Anataka kusema amefungwa kwa matakwa ya Rais? Kama ni kwa mujibu wa sheria Rais hayuko juu ya Sheria
 
inatia huruma sana lakini kwa kuwa ni nchi ya wasioelewa itakuwa ngumu kufahamu shida ulizonazo ndugu yangu papii mpaka leo tunakukumbuka
 
inatia huruma saana, kwani barua ilitumwa lini?
hawa jamaa huwa nnawaonea huruma, nnasikia wale waliotoa ushahidi kwenye ile kesi yao wamekufa kufa hovyo, hela mbaya saana.
 
Atakaye jaaliwa kwenda kumuona Papii kule gerezan mwambien asife moyo duniani ni mapito na la zaidi asiache sala.

Maisha ni yaleyale na zaidi labda angelikuwepo huku uswahiln labda angekuwa tayar marehemu. Avumilie na kukubali yote hasa yeye ni mwanaume haiitaji kukimbia tatizo au kulia ingawa saa nyingine machozi hayazuiliki.

Sisi raia hatujui kama ni kweli au si kweli juu ya maelezo ya hukumu yake ila kama binadam mwenzetu tunakuombea kwa mungu uwe imara muda wote hadi pale yeye maulana atakapoamua kukuchukua.

Keep ot UP nguza n ur dingi one day brother..
 
Uache kushea mademu na wakubwa!!!
Kaka kwani we hushei? Dem wako au bwana wako umemkuta bikra? Mwenzetu anatatizo sio style kama hizi unazoleta. Usije kumlaumu mungu yakikutokea wewe kaka hii dunia tunapita tu.
 
Hadi nimeamua kusikiliza nyimbo ya Sea. Usihofu Papii ipo siku utatoka kwa amri ya Muumba na tukapata kusikiliza nyimbo yako nyingine.
 
Papii Vumilia tu utatoka! Hata aliyekutendea unyama Nchi nayo imemshinda.....Kila mtu kamgeuka! malipo ni duniani,Lazima kufanya mabadiliko ili mambo mengine yawezekane!
 
Back
Top Bottom