Barua ya Papii Kocha kwa JK

Unajua blogu ya JD ni ya habari nilichouliza mimi kuna maelezo yoyote kwenye blogu yake yanayoeleza jinsi anavyopokea habari na kuziweka kwenye blogu yake na jinsi watu wanavyoweza kutumia kazi za blogu hiyo ? najua kwamba ni blog spot kwahiyo watu wafuate maelezo ya blogger ambayo ni mali ya google lakini kulitakiwa kuwe na maelezo ya ziada haswa yanayoendana na sheria za nchi husika kama tanzania blogu na tovuti nyingi hazina hivyo hata jf haina terms of use ambayo inaendana na na mazingira ya tanzania

Sawa,sasa what is the bottom line?
Je unahisi chombo kama JF na hiyo Blog haziwezi kutumika kama vyombo vya habari?na kama hivyo ndivyo then umechelawa na hi alert kwani hao waandishi wetu habari nyingi wanazitoa humu humu mitandaoni
 
Barua iko too simple lakini kuna mambo mawili yamejificha hapa.

kwanza

Huyu nguza inawezekana kabisa hakutaka kuweka mambo hadhani, Kwa mfano hakutaka kuzungumzia kama alisingiziwa au la! Nafikiri ingekuwa si busara kama angesema kwamba "Mheshimiwa nisaheme kwa sababu nilisingiziwa ".

Vile vile issue hii ina muhusu Nguza na Muheshimiwa kwa hiyo chochote atakachoandika lzm kiandikwe kwa umakini.

...

...ni ukweli 99.9%!

Kwenye mila na desturi hizi za kibantu, ukishaanza kusema 'lakini' maana yake unamuweka pabaya 'mzee wa busara.' Heri hivyo hivyo 'alivyoandika' bila kusema lolote kuhusiana na kesi au hukumu yake.
 
Je wale watoto wasio na hatia na raisi naye awarudishie utoto wao ulio ibiwa na huyu Nguza na Nduguze? .. ina maan kama ana jua ana hatia hajui uzito wa kosa alilofanya mbaka kuomba msamaha kirahisi tena ki jinga namna hiyo? ...
 
Nasikiliza Clouds FM,Ifrahim Kibonde anasoma barua usika kwenye kipindi cha Jahazi ambacho ana kiendecha Gadner G.Abash ambaye ni mumewe na Jaydee mmh....

SHY,kuwa wazi tafadhali Jaydee yuko kwenye system gani ?
 
...ni ukweli 99.9%!

Kwenye mila na desturi hizi za kibantu, ukishaanza kusema 'lakini' maana yake unamuweka pabaya 'mzee wa busara.' Heri hivyo hivyo 'alivyoandika' bila kusema lolote kuhusiana na kesi au hukumu yake.

Hahahaha Mbu umenichekesha na jibu lako
 
Mie barua hii nahisi kama vile ni ya kizushi.,na kama ni ya kweli basi Lady JD amechemka kuiweka kwenye Blog yake kabla haijamfikia mkuu.,mchana wa leo nimesikia katika kipindi cha XXL Clouds FM kuwa JD alipewa barua hiyo aifikishe kwa mkuu, lakini kwa kuwa si rahisi yeye kuonana nae akaamua aipost kwanza kwenye Blog yake wakati juhudi za kuiwasilisha kwa mlengwa zinaendelea ili wananchi wasikie kilio cha Papii na labda mkuu mwenyewe anaweza kukutana nayo kwenye hiyo Blog.
Naamini hii barua ilikuwa ni ya Rais personal.,sasa imekuwaje huyu JD akaisoma tena na kuiweka kwenye mtandao kabla aliyeandikiwa hajaipokea?

Kuna msemo mpya wa kichina unasema 'JK na watanzania ni kama mama na mtoto wake mchanga'. Jide mjanja, anajua ni bora kilio kipitie kwa watanzania kuliko barua kavu.

Usije ukajiuliza wachina ni kina nani, hao ni watanzania wanaotokea mkoa nisioujua mimi. Sijui ni wenyeji wa mkoa gani.
 
Shee yaaaya alishasema nguza atafunguliwa tu piga ua japo mwanzo hakujua kama kuna Nguza wawili na madhali katoka mmoja aliyebakia naye atatoka tu.Pia waliotoka wanatoa ushuda wa mia kwa mia kuwa walobaki watatoka tu je hatusubiri muda?
 
Aombe msamaha kwa wale watoto zaidi y kumi (10) waliowaharibu damn!

Sipendi justice ya kuangalia upande moja? hivi wale wazazi wa wale watoto mmewahi kuwauliza walivyo na hasira na huyu firauni? agh!
 
Hivi rais anaruhusiwa na itakuwa hekima kuwatoa hata hao wa kifungo cha maisha? Walivomuomba kama mzazi vile ndiye aliyewafunga nini?
 
Mbona barua inaongelea kuachiwa yeye tu...na sio baba yake?Je ni kwa ajiri anajua baba yake kafanya kweli yeye wanamuonea?Utengano..kwenye familia wakati wa majanga umeanza..
 
Hivi huyu jamaa ni kweli alitenda hayo makosa? Mbona hazungumzii lolote kuhusu hilo?
Hawezi kuzungumzia kesi kwa sababu kuna uwezekano wa ku file kesi mbele zaidi kwa hiyo kuongelea kesi na kusema alifungwa kimakosa sio sasa,anachomuomba Mh. ni msamaha haijarishi ametenda ama la.
 
Hili ni suala la kisheria ni lazima itofautishwe wazi kati ya KUOMBA MSAMAHA NA KUOMBA HAKI IFANYIKE.

Anayeomba msamaha hawezi kukana mashtaka. Kwanza anatakiwa kukiri kosa.

Lets be serious, haya mambo hayaendi tu kwa hisia. Hebu tutafakari makosa nyenyewe tunayoyazungumzia kama ni kweli!

Yaani mtu ahukumie kwa makosa ya kubaka, tena watoto si mtoto mmoja halafu amekana makosa na kwa sababu tunazozijua eti za kupitia kuomba msamaha kwenye blogu basi Mh. Rais anamsamehe? Alafu saa hiyo tunarudi hapa JF na kwenye vyombo vyingine vya habari tunaanzisha threads na tahariri zenye vichwa vywa habari:
Mamlaka ya Serikali na Mahakama au Utawala wa Sheria au Maamuzi ya Raisi n.k


Kama kweli walifanya makosa hayo,
Halafu wakakana na hukumu ikapita kulingana na adhabu inayostahili halafu ghafla waachiwe huru; Je wazazi wa wale watoto, watoto wenyewe walioathiriwa na Majaji waliohukumu kesi hiyo, wao waandike kwenye blogu ya nani ili sheria inayohusika na makosa ya namna hii isomwe na pengine kutafsiriwa kwa umma na wakosaji kurudishwa tena kutumikia kifungo?

Kama hawakufanya kosa na wamesingiziwa sasa hili si suala la msamaha bali ni la kisheria kupitia tena hukumu na ushahidi na kutengua hukumu kwa mkondo wa sheria. Wanasheria walioko humu wanaweza kusaidia hapa kama kuna uwezekano wowote wa rufaa au hakuna rufaa kwa hukumu iliyotolewa sasa.

Vinginevyo naona kama tunafanya maigizo hivi!
 
Hivi kesi ya kubaka watoto huwa inahitaji msamaha wa Raisi??? naomba kuelimishwaaa

Mkubwa hapo unasema ni kesi ya kubaka watoto je wewe unakubaliana na hilo swala??

Ninavyojua barua kama hiyo lazima ingegusia ni nini kimetokea na kwanini yeye anaona anastahili kusamehewa. Sasa unaomba tu msamaha kwa kigezo cha umri wakati pale kuna kosa la jinai, sidhani kama ni njia nzuri ya kuomba huo msamaha. Yeye ali appeal kwa vigezo fulani fulani vya kisheria. Atumie namna kama ile kuomba msamaha badala ya kuomba general tu kama vile alienda enda tu kuhukumiwa bila makosa.

Mkuu hao wanajuana wenyewe ndio maana kaandika barua simple tu

Aombe msamaha kwa wale watoto zaidi y kumi (10) waliowaharibu damn!

Una uwakika na unachosema??Unajuwa saa zingine tukae tufikiria kama watu wazima na tunajuwa nini tunachokiandika,eti kabaka watoto 10 acheni kushabikia vitu ambavyo vipo open na vinaonekana vya uongo!!

Sipendi justice ya kuangalia upande moja? hivi wale wazazi wa wale watoto mmewahi kuwauliza walivyo na hasira na huyu firauni? agh!

Mkuu fikiria kwanza hilo swala??Hivi mtu anaweza kuwabaka watoto 10 wote hao inawezekana kweli?
 
Mkuu fikiria kwanza hilo swala??Hivi mtu anaweza kuwabaka watoto 10 wote hao inawezekana kweli?

Kwanini ishindikane kubaka watoto 10?..kama umefuatilia kisa chenyewe vizuri ni kwamba watoto hawa hawakubakwa kwa siku moja bali ni kwa nyakati tofauti.,sasa huoni kama uwezekano wa kubakwa watoto kumi upo?..najua wengi wanajiuliza kwamba inawezekana vipi baba na watoto wake wakafanya hayo tena kwa pamoja.,katika hali ya kawaida kweli inaweza kuwa ngumu lakini katika mazingira kama ya ushirikina inawezekana, so tusishangae wala kujiuliza sana kwani yote yanawezekana na binadamu tumetofautiana sana unaweza ukamuona mtu ni mwema sana lakini upande wake wa pili ni zaidi ya shetani.
 
Hawezi kuzungumzia kesi kwa sababu kuna uwezekano wa ku file kesi mbele zaidi kwa hiyo kuongelea kesi na kusema alifungwa kimakosa sio sasa,anachomuomba Mh. ni msamaha haijarishi ametenda ama la.

Kufungua kesi mbele zaidi...?, mbona haiingii akilini, watafungua kesi wapi tena na imeshatoka mahakama ya rufaa ambayo ndio mahakama ya juu kabisa katika ngazi za mahakama ya Tanzania.,hata kama wakisamehewa leo hawawezi kufungua hata kesi ya kudai fidia kwani msamaha huo hautamaanisha kuwa hawana hatia wala hautawafutia hatia walionayo.,wangeweza tu kufanya hivyo kama wangeachiwa na mahakama tena kwa kuonekana kwamba hawana hatia.,so labda barua hii ifanye miujiza otherwise imeshakula kwao.
 
Lakini mbona hiyo barua ni very simpo one ..mie nimeisoma naona kama barua ya kawaida saaana ,,mheshimiwa anaweza kuisoma na kuweka pembeni ..hebu aandike nyingine yenye kuonyesha msisitizo ....
ANATAKIWA AKIRI KWANZA KUTENDA KOSA LILILO MPELEKA JELA. Hiki kipande cha barua kinaonyesha kuomba msamahe bila kukiri kwa kinywa chake kwamba ALIWACHEZEA KINGONO WATOTO WADOGO. VINGINEVYO JELA NI SIZE YAKE
 
Kufungua kesi mbele zaidi...?, mbona haiingii akilini, watafungua kesi wapi tena na imeshatoka mahakama ya rufaa ambayo ndio mahakama ya juu kabisa katika ngazi za mahakama ya Tanzania.,hata kama wakisamehewa leo hawawezi kufungua hata kesi ya kudai fidia kwani msamaha huo hautamaanisha kuwa hawana hatia wala hautawafutia hatia walionayo.,wangeweza tu kufanya hivyo kama wangeachiwa na mahakama tena kwa kuonekana kwamba hawana hatia.,so labda barua hii ifanye miujiza otherwise imeshakula kwao.

Wakili Marando: Babu Seya aweza kuokolewa tu na msamaha wa Rais
12/02/2010

Baada ya mahakama ya rufaa nchini Tanzania kukataa rufaa ya mwanamuziki mashuhuri nchini humo, Nguza Viking - maarufu kama Babu Seya – ni wazi kuwa mwanamuziki huyo na mwanae mmoja Papii Kocha ambaye pia ni mwanamuziki wa kizazi kipya watamalizia maisha yao gerezani.

Watoto wengine wawili wa Babu Seya - Francis Mbangu na Nguza Mashine – waliachiliwa huru baada ya kuonekana na mahakama ya rufaa hawana makosa yoyote baada ya kukaa gerezani kwa miaka sita. Babu Seya na watoto wake hao watatu wa kiume walihukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka mbali mbali ya ubakaji.


Sauti ya Amerika imezungumza na mwanasheria wa kujitegemea wa Babu Seya, Mabere Marando, ambaye amesema kufuatia hukumu ya mahakama ya rufaa njia pekee iliyobaki ambayo inaweza kuwatoa Babu Seya na Papii Kocha gerezani ni msamaha wa rais tu.
 
KAMA HUKUWAHI KUISOMA BARUA YA PAPII KOCHA KWENDA KWA RAIS JAKAYA KIKWETE, KUPITIA KWA LADY JAY DEE HII HAPA >>>MF/NA: 836'04|Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam Mh. Rais Jamuhuri
ya Muungano

Tanzania YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga. Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais.

Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu. Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.

Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi. Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.

Mungu akubariki Wako mtiifu
NO:836'04 JOHNSON NGUZA
(PAPII KOCHA)



.........navyoona mimi kitu kikubwa kwa huyu jamaa kabla ya kuomba asamehewe ni kukiri kosa au kukanusha harafu ombi ndio lifuate au mnasemaje wana jamvi........
 
Tafadhali husika na siyo husika na kichwa cha habari kama alivyoanza katika barua yake.

Swali langi je ni Papii peke yake anastahili msamaha wa rais??? Kila la kheri katika maombi yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom