Barua ya Malcom X: Huko Makka Saudi Arabia

Barua ya Malcom X: Huko Makka Saudi Arabia

zaburi
Taurati
injili
Qur'an

ukielewa huo mtiririko wa hivyo vitabu (kama umevisoma). uje ureview ulichokiandika kama kina make sense...
NO OFFENCE
Ndy haya niliyosema mm,,

Wafia dini..
Wenyewe hayo mambo hawana nafasi nayo.

Nimekwambiya huku ni saudia,,, kuna Chanel hata za kikristo ktk kipindi vyao..
Wala hawabaguani kwa dini zao.

Unataka uniletee kusoma maandiko gani?
 
hujanielewa na hatutoelewana nadhani... let's cut this story...
Nilikuelewa sana mkuu,,

Lakini ile point yako uliposema mwisho ni review kama kina make sense,,

Maana yake niliyoandika haya make sense..

Unajuwa ktk sentence yeyeto,,neno moja linaweza likaharibu maana nzima..

Hapo kama una make sense ndy tatizo lilipoanzia.
 
Malcolm X au (Al-Hajj Malik El-Shabazz) huyu wengi wetu tunamjua wengineo wakimwiga na kufata matendo yake, na itikadi zake. Huyu mmarekani mweusi ambaye Alisiliimu na kuitwa jina maliki el shaabaz

Baada ya kufika MAKKA kama ilivyo amri hii kwenye vitabu vya dini ya kiislamu ni nguzo moja kati ya nguzo zinazojenga uislamu kuhiji makka , kwa mwenye uwezo.

Naye alilitimiza hili na ndani ya ibada hii akapata kuandika aliyojifunza na kuyapata huko 1964, huko alipata kuandika Barua juu ya aliyojifunza na kushuhudia huko

Barua yake aliyoiandika kutoka kwa Makka alipokuwa Hija Makkah, al-Hajj Malik El-Shabazz aliandika barua kwa wasaidizi wake waaminifu wa Harlem ...
View attachment 1711213

Na haya ni baadhi ya yaliyoandikwa katika

Barua ipo kama ifuatavyo

"Kamwe sikuwahi kushuhudia, Ukarimu wa dhati wa namna ile Na roho ya ukweli ya undugu ambao umefanywa na watu wa Rangi zote, Katika mji huu mkongwe na mtakatifu, Nyumbani kwa Ibrahim ,Muhammad na mitume wote , waliotajwa katika maandiko matukufu.

"Kwa wiki iliyopita nimekuwa kimya kutafakari , huku nikishuhudia neema ambayo nimeioona imeonyeshwa kila mahali na watu wa rangi zote"

"Nimepata bahati ya kutembelea mji mtukufu wa makka, nmekamilisha mizunguko yangu saba kuizunguka Al kaaba, nikiongozwa na kijana mdogo aitwaye Muhammad, Nmekunywa Maji kutoka katika visima vya ZamZam"

Nilikimbia mara saba nyuma kwenye vilima vya Safa na Marwah. Nikaswali na kuomba katika mji mtukufu wa kale wa Mina, na nikaswali juu ya Mlima Arafat.

" Kulikuwa na makumi na maelfu ya mahujaji, kutoka duniani kote. Walikuwa wa rangi zote, weupe kwa Waafrika wenye rangi nyeusi.
Lakini sisi wote tulishiriki katika ibada hiyo hiyo, tukiwa na roho ya umoja na udugu

kwamba katika uzoefu wangu wote nlipoishi huko Amerika uliniongoza kuamini haiwezekanii kuwepo mchanganyiko kati ya nyeupe na isiyo nyeupe.

" Amerika inahitaji kuuelewa Uislamu, kwa sababu hii ni dini ambayo inapinga na kuondoa katika jamii yake tatizo la utaifa. Katika safari zangu katika ulimwengu wa Kiislamu, nimekutana, nimezungumza na hata kula pamoja na watu ambao huko Amerika wangechukuliwa kama ni weupe lakini mtazamo wa rangi uliondolewa kwenye mawazo yao na dini ya Uislam"

"Sijawahi kuona udugu wa kweli uliofanywa na rangi zote pamoja, bila kujali rangi yao. "

Unaweza kushangazwa na maneno haya yanayotoka kwangu. Lakini juu ya safari hii, yale niliyoyaona, na uzoefu wangu, vimenifanya tena niweke upya mawazo yangu iyokuwa nayo hapo awali, na kutupa kando baadhi ya fikra za awali.

Hii haikuwa vigumu sana kwangu. Licha ya imani yangu imara, sikuzote nimekuwa mtu ambaye anajaribu kukabiliana na ukweli, na kukubali ukweli wa maisha kwa kupokea mafunzo mapya na ujuzi mpya unaomfumbua mtu.

Nimekuwa na akili ya wazi, ambayo ni muhimu inapaswa kwenda nayo pamoja ili kutafuta kubadilika.

"Katika siku kumi na moja hapa katika ulimwengu wa Kiislam, nimekula kwenye sahani , na kunywa katika kikombe kimoja, na kulala katika sakafu moja, huku tukimuabudu Mungu mmoja na waislamu wenzangu Weupe,
Nilihisi kuwa na uaminifu nilihisi kati ya Waislamu wa Afrika wa Nigeria, Sudan na hata Ghana. "

Tulikuwa ndugu kwa sababu imani yao katika Mungu mmoja iliondoa matabaka ya Rangi.


Niliweza kuona kutokana na hili, labda Wamarekani wazungu wanaweza kukubali Mungu mmoja basi labda, pia, wangeweza kukubali kwa kweli umoja katika Ubinadamu - na kusitisha ubaguzi, na kuzuia, na kuwadhuru wengine kwa suala la 'tofauti' zao katika rangi

Kwa ubaguzi , marekani ni sawa na Cancer isiyoponyeka, waamerika weupe wanapaswa kuopokea suluhisho

Labda inaweza kuokoa Amerika kutokana na maafa ya karibu ,uharibifu kama huo uliiletea Ujerumani Shida juu ya ubaguzi wa rangi ambao hatimaye ukawaangamiza Wajerumani wenyewe.

"Kila saa hapa katika Nchi Takatifu inaniwezesha kuwa na ufahamu mkubwa wa kiroho katika kile kinachotokea Amerika kati ya weusi na weupe.

Negro wa Marekani hawezi kuhukumiwa kwa chuki za kibaguzi- anajaribu kupinga miaka mia nne ya ubaguzi wa rangi wa wazungu wa Marekani. Lakini kama ubaguzi wa rangi unaongoza Amerika juu ya njia ya kujidhuru

Naamini, kutokana na uzoefu ambao nimekuwa nao, wazungu hawa kizazi cha vijana, katika vyuo vikuu na mashuleni wataona maandiko juu ya kuta na wengi wao watageuka njia ya kiroho na kufuata haki ya kweli

Kamwe sijawahi kuheshimiwa sana namna hii

Kamwe sijawahi kufanywa kujisikia mnyenyekevu zaidi.

Nani angeamini baraka ambazo zimefanywa juu ya mtu mweusi wa Amerika?

Siku chache zilizopita, mtu ambaye huko marekani angeitwa mzungu au mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa, balozi, au rafiki wa wafalme,yeye alinipa hoteli yake, na kitanda chake.

Kamwe nisingeweza hata kufikiria au kuota kwamba ningewahi kuwa mpokeaji wa heshima kama hizo - heshima ambazo huko Amerika zitapewa Mfalme , mtu mweupe na- sio mtu mweusi"

Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.







(kutoka kwa Autobiography ya Malcolm X kwa msaada kutoka kwa Alex Haley, mwandishi wa ROOTS)

Malcolm X alifundisha mengi na kuona Mengi

Nyuzi hii ni baadhi ya yaliyoandikwa kwenye barua hio

UKIACHANA NA UDINI KUNA LA KUJIFUNZA hapa






DA VINCI XV
Waarabu nao pia ni wabaguzi tu...hz n propaganda tu. Ni ndugu zetu wangapi hasa wadada wanaokwenda huko kufanya kazi za ndan kisha wakaanza kunyanyaswa kingono ? Hv kwann sisi ngozi nyeusi tunapenda kuwatukuza ngozi nyeupe
 
Malcolm X ni miongoni mwa viongozi wapuuzi na wabaguzi wa kale.

Hili jamaa lilienda kwenye uislamu kutoka kuwa Atheist na sababu kuu ni eti America kuna Makanisa kwa ajili ya wazungu, busses kwa ajili ya wazungu, na mengineyo ila sio watu weusi PUNGUANI KABISA HILI this was before 70's!

Mbona Martin hakubadili? Ndio maana halijaacha legacy kwa wengi.
Kwa hiyo upumbavu wake ni kuingia kwenye uislam au unataka kumasanisha nn?
Au una maanisha wanao fuata dini ya uislam ni wapuuzi ila wanaofiata ukirsto ni werevu? Ebu fafanua kosa lake ni lipi mpaka uamue kumvunjia heshima kiasi hicho.
 
Waarabu nao pia ni wabaguzi hv n propaganda tu. Ni ndugu zetu wangapi hasa wadada wanaokwenda huko kufanya kazi za ndan kisha wakaanza kunyanyaswa kingono ? Hv kwann sisi ngozi nyeusi tunapenda kuwatukuza ngozi nyeupe
Nadhani hujaelewa makala mkuu
 
Kwa hiyo upumbavu wake ni kuingia kwenye uislam au unataka kumasanisha nn?
Au una maanisha wanao fuata dini ya uislam ni wapuuzi ila wanaofiata ukirsto ni werevu? Ebu fafanua kosa lake ni lipi mpaka uamue kumvunjia heshima kiasi hicho.
Bora uulize wew mkuu
 
Watumwa kutoka Africa waliopelekwa uarabuni waliishia wapi? Mbona katika mataifa ya kiarabu hakuna kizazi cha watu weusi ambacho kinatokana na watumwa waliopelekwa huko enzi za biashara ya utumwa?
hivi nyie mlisoma historia ya wapi sasa mtumwa aende uarabuni akalime nn? watumwa walienda America, Uingereza na Ufaranasa na ndio maana hadi leo athari ya rangi za watumwa zipo acheni kilujitoa ufaham
 
Tangu karne ya 15 mpaka leo watumwa wanapelekwa uarabuni.
hivi nyie mlisoma historia ya wapi sasa mtumwa aende uarabuni akalime nn? watumwa walienda America, Uingereza na Ufaranasa na ndio maana hadi leo athari ya rangi za watumwa zipo acheni kilujitoa ufaham
 
Muslim slavery was not just economic

Unlike the Western slave trade, slavery in Islam was not wholly motivated by economics.
Although some Muslim slaves were used as productive labour it was not generally on the same mass scale as in the West but in smaller agricultural enterprises, workshops, building, mining and transport.
Slaves were also taken for military service, some serving in elite corps essential to the ruler's control of the state, while others joined the equivalent of the civil service.
Another category of slavery was sexual slavery in which young women were made concubines, either on a small scale or in large harems of the powerful. Some of these women were able to achieve wealth and power.
These harems might be guarded by eunuchs, men who had been enslaved and castrated.

Where did the slaves come from?

Muslim traders took their slaves from three main areas:

Non-Muslim Africa, in particular the Horn

Central and Eastern Europe

Central Asia

hivi nyie mlisoma historia ya wapi sasa mtumwa aende uarabuni akalime nn? watumwa walienda America, Uingereza na Ufaranasa na ndio maana hadi leo athari ya rangi za watumwa zipo acheni kilujitoa ufaham
 
Aisee! kweli jf imejaa majitu ambayo ni broke sana, mtu kashasema ameleta uzi sio kwa ajili ya majibizano yenye mlengo wa kidini lakini kuna mangedere tayari yameanza kukuru kakara za kuharibu malengo ya mleta mada.
 
Hujasoma Trans Saharan slave trade au Indian Ocean/Arab slave trade?
Mnaikumbuka Trans Atlantic slave trade tu.
Kuna hizo nyingine mbili na hizo ndio nauliza watumwa wake waliishia wapi?
hivi nyie mlisoma historia ya wapi sasa mtumwa aende uarabuni akalime nn? watumwa walienda America, Uingereza na Ufaranasa na ndio maana hadi leo athari ya rangi za watumwa zipo acheni kilujitoa ufaham
 
Katika kusafir kwangu hakuna watu mashetan kama waarabu. Na hakuna watu wanajiona cku zote wao wako juu kwa kila kitu kama wazungu. na hakuna watu wanaotafute hela kwa namna yoyote kama muasia. Waafrica cc sio watu wa kujifunza. Ni wazee wa lawama. Ni kama vile hawatak kukubali walishawahiwa so wajipange ili wajikomboe hilo hawalitak kila cku ni kulaumu tu mwanzo mwisho. Tumeshindwa kujifunza kwa japan. Maana baada ya kichapo walijipanga sasa hiv wako juu.
 
Back
Top Bottom