Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.
Masatu!

Mhh wewe mwisho! utakuwa ama kada CCM au ni M-NEC, hii ya Sitta V Kapuya ni mpya kwangu na niko hoi!. Anyway good analysis bro
Unaona Nchi isivyokuwa na uwajibikaji watu wanaoneshana ufahari kwa fedha ya walipa kodi wewe ukiagiza kingora cha polisi mwenzako anaagiza Ndege la kijeshi na MP.........................Kweli mbombo ngafuuuuuu!
 
Kwa sababu chama tawala hawatapenda kuumbuana bungeni,
kwa kuzingatia kuwa Mmasai ameguswa na tuhuma za Ndesa,
kwa kuhofia kuwa Mzee VI anaweza kumwanika Mmasai,
Mhe Malima ameandika barua ku-pre-empt hiyo move, kwani sasa itabidi chama tawala kimwambie Six atulize boli...funika kombe mwanaharamu apite!
 
mwanagenzi.. so.. katika hii drama u think Mhe. Sitta ataibuka kidedea? I think we need to put up a bet... can we put a poll on this.. of what action chama cha mapinduzi kitachukua..!!?
 
Nilisema toka jana Masatu kichwa sana ni product ya Mzumbe university hoja zake Fikiraduni hawezi hata kidogo kugusa.
na anatoka kabila la professor Warioba.
Mwanasiasa kimya? mmeona kazi za Mzumbe?

MWANAKIJIJI.

Umejitahidi kuweka vitu sawa kuna mtu alisema huyo Mbunge alifanya kazi kwa Manji ni nani alisema hivyo? Tuache Chuki Adam katulia na anajua anafanya nini?
 
Malima amehukumiwa na bunge kuwa ana makosa, wabunge wawili wamtaka awajibishwe katika maoni yao, Spika amepeleka kesi kwa PCB, Malima ameamua kwenda CCM,

Malima kuiandikia CCM, hakubadili ukweli kuwa kesi ipo PCB, na haibadili ukweli kuwa baso Spika anazo all the rights za kumuadhibu atakapoamua, Kwenda kwa Malima CCM, hakuizuiii PCB, chombo cha serikali kufanya kazi yake, na Spika kufanya kazi yake, CCM haiwezi kuitoa kesi kutoka PCB!

Whatever comes out of CCM, haiwezi kuzuia PCB, na Mengi na Ndesamburoi, ambao ni wahusika muhimu hawaweezi kuhusika huko CCM, hilo ni tatizo la CCM na Malima, na wabunge wa CCM akiwemo Spika,

Sasa Why all this speculations?
 
Mzee ES, heshima yako mkuu,

Nadhani utakuwa umechanganya habari hapo ama kwa makusudi au kwa slip of keyboard tu.

Kesi za msingi zilizopelekwa kwenye kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya bunge ilikuwa ni Mengi Vs Malima na Malima Vs Mengi. Ndani ya kesi hizo 2 ndio ikazaliwa kesi nyingine ya Mh Ndesamburo na suala la rushwa kwa wabunge/kamati (bado kuna utata kutoka kwa mtoa madai waliohongwa ni kamati au ni wabunge wote, presumably wa ccm)

Kesi ya Mh Ndesamburo ipo PCB wao watachunguza na kutoa maamuzi kulingana na sheria na taratibu zao.

Kesi mama zimeshatolewa uamuzi na spika na ndio hichi kimbembe tunachokijadili zaidi hapa (ile ya Ndesamburo tuwape muda PCB) Maamuzi ya kesi za msingi ndio yaliyopingwa na Mh Malima na ameamua kupitia mkondo wa chamani kwake huko Mh Mengi hakumuhusu kwani sio kiongozi au Mbunge ndani ya CCM.

Kama wataayamaliza wenyewe huko well and good, lakini kama itashindikana na ikaamuliwa suala lirudi bungeni tena hapo ndio shughuli sasa. Itabidi vifungu na kanuni zichambuliwe.

Kama alivyokiri Mh Spika kuwa kuna utata wa tafsiri ya ibara ya 100 ya katiba “100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge, na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama au mahali penginepo
nje ya Bunge.

Mh Sitta katika rulling yake kajaribu sana kupiga piga chenga hapo kutafuta namna ya kuchopoka. Nadhani kwenye mjadala mpana wa bunge lote ambao sisi waumini wa demokrasia tunausubiri tutanufaika kujua kama kweli Mh Malima halindwi na kinga hiyo au la.

Pia sina uhakika kama wataamua kumuita Mh Mengi bungeni kwa overrule kanuni aingie bungeni kama inavyofanywa marais wa kigeni ambao sio wabunge wanapokuja kulihutubia bunge. Kwa kawaida spika huwa anatoa azimio la ku over rule kanuni ili asiekuwa Mbunge aingie bungeni. Au wataamua kulijadili kavukavu hivyo hivyo bila Mh Mengi kuwepo.

Nadhani kwa maelezo haya mzee ES utata utakuwa umetoka.
 
Mzee Masatu,

Ndesamburo alipeleka kesi yake, na Spika alipeleka kesi yake, ninacho kitabu maalum kilichotolewa na bunge hivi karibuni kuhusu hii kesi, ninaweza kukutumia ukitaka at anytime nitakufanyia kopi, na yote ninayoyasema yamo,

baaada ya kutoa uamuzi ndani ya kamati ya bunge, Spika aliipeleka kesi hiyo PCB, kuhusu wabunge waliokula rushwa, na kesi nzima kwa ujumla,

kwangu the big question ni kwa nini Spika hakumwajibisha Malima, baada ya kukubalika kuwa alikuwa amelidanganya bunge la taifa?

Sasa ninaomba niseme, kuwa mimi binafsi mimi nilifikiri wa-Tanzania na hasa wasomi tutaiangalia hii kesi kwa mapana na marefu, na ku-appreciate kuwa at least Tanzania tunaanza kwenda mbali, nani alitegemea kuwa ingekuja siku wa-Tanzania tungeyaona haya? Sasa mambo kama haya ndio yanaweka historia kwa ajili ya taifa letu huko kesho, na hasa katika nyanja ya sheria za bunge, kesho na keshokutwa itakapotokea kesi ya namna nyingine inayofanana na hii hakutakuwa na tatizo,

I do not see the problem ya Malima kwenda CCM, yeye ni mbunge wa CCM, na mwanachama wa CCM, kuna mapungufu ya hiyo kesi ambayo kwake yanahitaji kupelekwa ndani ya chama chake, kwa kuwahusisha wabunge wa chama chake, na hapa ndipo hasa hisia za Mwalimu kutaka mwenyekiti wa CCM awe ndio rais zinapoonekana, kama Malima hawezi kuchukuliwa hatua kama mbunge, basi mwenyekiti wa CCM anaweza kumchukulia hatua Malima, kama mwanachama wa CCM, na ndio njia iliyotumika kuwaondoa Mbilinyi na Simba, toka kwenye uwaziri ilikuwa ni chama baada ya njia zote za serikali kushindikana, Mwalimu aliwaondoa Jumbe na Seif kupitia hicho hicho chama CCM, sasa kwa nini leo Malima kwenda huko iwe tatizo?

what is wrong with that? Mpaka ku-create all this fuss? I mean mzee Clean, heshima mbele kwa clear and cut on the ishu, Mbunge Malima analindwa na sheria ya kutomuhukumu kutokana na maneno atakayoyamka akiwa ndani ya bunge, unless akisema nje kwenye viwanja vya bunge hapo kisheria hana kinga, hiyo ni kwa sheria ya jamhuri, but Spika anao wajibu kisheria za bunge kumuwajibisha mbunge aliyepatikana kuvunja kanuni za bunge na kamati inayohusika ya bunge,

Sasa nilifikiri the fuss ingekuwa kwa nini Mbunge Malima hakuwajibishwa, na mapungufu ya sheria yetu ya bunge na uimara wake, lakini hasa tungelenga kwenye mapungufu ili kuwasaidia wananchi wa taifa la kesho,

Haya ni mawazo yangu tu!
 
Mzee Es;28598]

Sasa nilifikiri the fuss ingekuwa kwa nini Mbunge Malima hakuwajibishwa, au?

Hii tulisema toka awali kwenye Manji VS Mengi Kwamba Mh. Spika alipindisha kanuni ktk kutoa Hukumu au Maamuzi ikiwa yeye na kamati walioiunda wanakubali Malima alilidanganya Bunge Hapa ni kwamba wamemtia hatiani na Kama wamemtia hatiani nini kilitakiwa kufanywa?

Ni kumuadhibu kwa mujibu wa kanuni zilizopo kama tulivyoshuhudia watu waliongea ndani ya Bunge hilo hilo na kuadhibiwa tena yeye ilitakiwa Kwanza Afute kauli yake aliyeitoa,pili amuombe msamaha aliyemsingizia yaani mengi, Kama ilivyoamuliwa kwenye swala Mh. Cheyo Na Mh. Shibuda kutokana na kauli ya cheyo aliyeitoa kwa shibuda kuhusiana na fedha zilizotumika ktk ujenzi wa shule huko Shinyanga.

Sasa kwanini hili halikufanyika hii ni Tabia ile ile ambayo tumejionea kwa Mh.Spika kuwa mwepesi kufuata sheria zinapowahusu Wapinzani na Hapa kilichomponza ni Huo Umwamba na kuacha kufuata kanuni husika tena kwa huyu kijana Mh. Adam isingeishia hapo kama mimi ningekuwa spika ningempa Adhabu ya kulipa na Fedha za walipa kodi alipokuwa Anadanganya na kuombwa toka awali afute kauli yake aligoma na kufikia hadi kuundwa kwa tume iliyotugharimu walipa kodi.

Sasa Mh. amembeba mtu asiyebebeka pamoja na kutopenda kumuadhibu kijana amemgeuka na kumuona hajui kazi yake kama alivyoonyesha ,Sasa hivi Mh.Spika analalamika nini kwamba kachafuliwa Jina kwani alikuwa hajui alichokifanya kilikiuka kanuni kwa kutomuadhibu mtu ambaye ushahidi unaonyesha kwamba ana kosa.

Halafu Kosa jingine Kwanini ile ripoti hakuiwakilisha Bungeni na wabunge wakaichambua pamoja na matokeo yake Lakini kwa UBABE ULEULE ALISEMA TUME ILIKUWA YAKE NA RIPOTI NI YAKE, Sasa anapotaka kulipeleka tena swala Bungeni Kwani hiyo tume kwasasa imegeuka kuwa ya wabunge na si ya spika tena. Anyway, Anavuna alichopanda................Ajifunze sheria na kanuni zipo kwa wote ndani ya ukumbi wa bunge na Yeye ni msimamizi wa kuhakisha zinachukua mkondo wake kwa wote wanaongozwa nazo ndani ya bunge hilo Tukufu. Hapa labda kuna Ambacho kimejificha ambacho Mh. Adam anakijua sisi hatukijui na ndiyo maana anaendeleza chokochoko Lakini Kama si Leo basi masiku ya usoni tutalielewa!
 
Mzee Es
Nimeona hoja zako nami nimeona nikuulize tu swali moja kwamba una hakika kwamba CCM hawawezi kutengua shauri ama tuhuma ambazo ziko PCB ? Una hakika kwamba PCB ni chombo huru ambacho kinaweza kufanya maamuzi bila ya kuingiliwa ? Ukisha nijibu haya Mzee nitasema nini nia yanu ya kuuliza , lakini bado naamini Malima was wroong and he is still wrong kwenda CCM badala ya kurudi Bungeni.

Kwa mtizamo wangu Malima is joining Zitto kusema kwamba Ama Sitta hajui ama anaunja kanuni makusudi ndiyo maana hana imani naye kama alivyo onyesha kakimbilia kwenye Chama lakini shauri lenyewe halina uhusiano na Chama .
 
Nimezungumza na Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Makamba na amehakikisha kuwa barua ameipokea na bado hajaitolewa uamuzi. Kwa mtazamo wake amesema kuwa Bw. Malima amefanya jambo sahihi la kuleta suala hilo chamani na yeye kama Katibu Mkuu ataamua hatua za kufuata kama ni kulipeleka jambo hilo kwenye Kamati ya Wabunge wa CCM kujadiliwa au kulileta kwenye vikao vingine vya chama.


mzee ES said:
I do not see the problem ya Malima kwenda CCM, yeye ni mbunge wa CCM, na mwanachama wa CCM, kuna mapungufu ya hiyo kesi ambayo kwake yanahitaji kupelekwa ndani ya chama chake, kwa kuwahusisha wabunge wa chama chake, na hapa ndipo hasa hisia za Mwalimu kutaka mwenyekiti wa CCM awe ndio rais zinapoonekana, kama Malima hawezi kuchukuliwa hatua kama mbunge, basi mwenyekiti wa CCM anaweza kumchukulia hatua Malima, kama mwanachama wa CCM, na ndio njia iliyotumika kuwaondoa Mbilinyi na Simba, toka kwenye uwaziri ilikuwa ni chama baada ya njia zote za serikali kushindikana, Mwalimu aliwaondoa Jumbe na Seif kupitia hicho hicho chama CCM, sasa kwa nini leo Malima kwenda huko iwe tatizo?

Mimi nadhani kuwa ni makosa sana kwa viongozi wa CCM kutumia madaraka yao ya CCM kuingilia shughuli za Bunge. Standing orders za bunge zinaonyesha wazi kabisa utaratibu wa kupitia iwapo mbunge hakuridhishwa na uamuzi wa spika; kwa nini Mheshimiwa Malima hakupitia utaratibu huo na badala yake kwenda kwa Makamba ambaye kuna watu wameshaainisha uhusiano wao usio wa kikazi unaoweza kuathiri maamuzi yake.


Kuhusu CCM kuwachukulia hatua za kichama wabunge wake ili kuwaondolea madaraka yao ya ubunge pia ni makosa ambayo yalifanyika bila kufuata Katiba ya nchi; najua kuwa NCCR-Magezu chini ya Mrema, na UDP nao walishawahi kufanya makosa hayo hayo. Shukurani zaidi kwa Mzee Mtikila na Mahakama iliyotoa bayana kuwa mtu kuwa mbunge siyo lazima awe mwanachama wa chama chochote. Kwa hiyo kama mbunge akifukuzwa unachama wa chama chake bado ana haki ya kuendelea kuwa mbunge huru.



masatu said:
Mh Sitta katika rulling yake kajaribu sana kupiga piga chenga hapo kutafuta namna ya kuchopoka. Nadhani kwenye mjadala mpana wa bunge lote ambao sisi waumini wa demokrasia tunausubiri tutanufaika kujua kama kweli Mh Malima halindwi na kinga hiyo au la.

Kanuni za Bunge la Tanzania linampa madaraka makubwa sana spika kuamua ni nini kijadiliwe bungeni na kipi kisijadiliwe. Hii ni unfortunate lakini ndivyo ilivyo pamoja na kuwa inapingana na katiba. Kile kifungu alichotumia Mzee 6 kutolea umuzi wake katika kesi hii ni halali kwa vile ndicho kinachompa nguvu ya kuamua ni mada gani zijadiliwe bungeni na zipi zitupwe kapuni. Kuna haja ya bunge kupitia tena kanuni zake na kudhibiti madaraka ya spika dhidi ya wabunge kwa kukiandika kifungu hiki tena kuwa na specific limits dhidi ya haya madaraka makubwa ya spika.
 
Uhuru wa vyombo vya serikali yetu vinavyoongozwa kwa sera za CCM, hilo ni a million question, lakini tunaweza kuangalia historia kidogo, Blaza Dito anashitakiwa na chombo cha sheria ya serikali, Balozi Mahalu anashitakiwa na serikali hiyo hiyo, kesi hii ya Malima imaeamuliwa na chombo cha serikali, je PCB itafanya tofauti kwenye kesi ya Malima/Mengi? Ninasema lazima tuviamini vyombo vyetu kwani si mahakama ya serikali ya CCM ndiyo iliyompa ushindi Mtikila kwenye kesi ya wagombea huru? au? Sasa kwa nini tuwe na wasi wasi kwenye hili la Malima?

Mbunge Zitto, alishaomba radhi na akasamehewa kuwa alimkosea Spika kwa kanuni za bunge, na Spika hakumuadhibu ila alimsamehe kiungwana kwa hiyo sidhani kwamba kuna any mahusiano na kesi hii ya Malima,

Ninasema kwamba Spika ana swali la kujibu kutoka kwa wananchi kwamba kwa nini hakumuwajibisha Mbunge Malima, baada ya kumuona ana makosa kwa kanuni za bunge letu la taifa?
 
Mzee Kichuguuu,

Heshima mbele, ila for some reason unaonekana kufanana sana na Mwanakijiji anyway,

madaraka ya Spika, katika kila nchi huwa ni yale yale na katika nchi yetu mimi ninasema kuwa tunahitaji Spika strong kama Sitta ambaye bila ya kuwa alivyo angeburuzwa sana na mawaziri na waziri mkuu,

Now sisemi kuwa Spika wetu ni malaika, ila binafsi ninaheshima naye sana, sio kama aliyepita ambapo kila wakati ilibidi waziri mkuu kumuita rais kuwatisha wabunge, this time arround ni waziri mkuu na Spika, face to face, el kazi ni kulia lia huko pembeni lakini usoni kwa Spika haoni ndani,

Sheria tuliyonayo sidhani kama ina matatizo on Spika, tatizo ni Spika mwenyewe na affiliations zake na chama chake cha siasa, labda tuwe na Spika ambaye sio kutoka chama chochote cha siasa!
 
Mwanakijiji.

Umekimbilia kumuhoji Mh Malima kule TRA huna muda.

anyway nimefurahi kuona mtoto wa kiswahili Malima alivyoshusha issue imenipa mwangaza. ulikuja na agenda yako ya udini na chuki kwa Mh Malima lakini umekoma.

kijana yuko fit hakuna six wala seven na wala si Mengi,Ndesamburo,Mushi.Massawe au Mbowe.

Nashangaa kuna wazushi wanahoji elimu ya Malima na jinsi alivyopata kazi B.OT? huyu ni graduate na mbowe alikuwa four form failure still alipata kazi B.O.T kama upendeleo basi ni kwa Mbowe alikuwa hana sifa.

na baada ya kutoka benki kuu akawa D.J anaruka majoka Mbowe club. huwezi kutoka B.O.T na then kuwa D.J. unless uwe huna qualification.

kifupi malima mtamchukia sababu tu mtoto wa kiswahili.

Malima kashusha vitu hadi Mwanakjj akabaki NDIYO NDIYO.
Tunaomba interview TRA.
 
Mzee Kichuguuu,

Heshima mbele, ila for some reason unaonekana kufanana sana na Mwanakijiji anyway,

madaraka ya Spika, katika kila nchi huwa ni yale yale na katika nchi yetu mimi ninasema kuwa tunahitaji Spika strong kama Sitta ambaye bila ya kuwa alivyo angeburuzwa sana na mawaziri na waziri mkuu,

Now sisemi kuwa Spika wetu ni malaika, ila binafsi ninaheshima naye sana, sio kama aliyepita ambapo kila wakati ilibidi waziri mkuu kumuita rais kuwatisha wabunge, this time arround ni waziri mkuu na Spika, face to face, el kazi ni kulia lia huko pembeni lakini usoni kwa Spika haoni ndani,

Sheria tuliyonayo sidhani kama ina matatizo on Spika, tatizo ni Spika mwenyewe na affiliations zake na chama chake cha siasa, labda tuwe na Spika ambaye sio kutoka chama chochote cha siasa!


Unajua kuwa watu wanakiona kile kifungu 4(2) kijuu juu tu. Kile ni kifungu kikubwa sana katika madaraka ya Spika kwa vile kinamruhusu kuseti agenda ya Bunge, na anaweza kukitumia kifungu hiki kuamua ni jambo gani lijadiliwe bungeni. Ndiyo maana nikasema Mheshimiwa Malima anafanya mcehzo na madaraka ya Spika. Ni kwa kuutumia kifungu hicho hicho Spika anaweza kupokea ripoti ya kamati na asiruhusu ripoti kujadiliwa bungeni. Nilichokuwa nishauri ni kuwa Bunge liandike upya kifungu hicho kwa makini na kuweka bayana kuwa Spika ana uhuru wa kufanya hili na lile isipokuwa katika mazingira haya na yale, badala ya kukiacha wazi kama ilivyo sasa.
 
Mwanakijiji.

Umekimbilia kumuhoji Mh Malima kule TRA huna muda.

anyway nimefurahi kuona mtoto wa kiswahili Malima alivyoshusha issue imenipa mwangaza. ulikuja na agenda yako ya udini na chuki kwa Mh Malima lakini umekoma.

kijana yuko fit hakuna six wala seven na wala si Mengi,Ndesamburo,Mushi.Massawe au Mbowe.

Nashangaa kuna wazushi wanahoji elimu ya Malima na jinsi alivyopata kazi B.OT? huyu ni graduate na mbowe alikuwa four form failure still alipata kazi B.O.T kama upendeleo basi ni kwa Mbowe alikuwa hana sifa.

na baada ya kutoka benki kuu akawa D.J anaruka majoka Mbowe club. huwezi kutoka B.O.T na then kuwa D.J. unless uwe huna qualification.

kifupi malima mtamchukia sababu tu mtoto wa kiswahili.

Malima kashusha vitu hadi Mwanakjj akabaki NDIYO NDIYO.
Tunaomba interview TRA.


Mchango wako ungeweza kuwa mzuri zaidi ya hapa ila tu naona umetaka iwe hivyo.
 
duh.. mwaka huu nina kazi.. !! nisimhoji mtu bila kurushiwa TRA... na sijui nilileta udini vipi tena!! Wakati mwingine napenda kukujibu Mswahili lakini wakati mwingine huwa najiuliza maswali 101..!

Mzee ES natumaini humaanishi au kuashiria japo kwa mbali kuwa mimi na Kichuguu ni mtu mmoja (kuna watu waliojaribu kunipa majina mengine hapa). Siingii humu kwa zaidi ya jina hili, sihitaji kuficha hoja zangu au mitazamo yangu kwa kujibadilisha badilisha kama kinyonga! Hoja zangu kama ni dhaifu, pumba au zenye msingi nazitoa kwa jina hili hili. Nina udhaifu mwingi, lakini wa kuogopa kuzungumza na watu wakajua ni mimi nimezungumza udhaifu huo sina, wengine hata hivyo ndio udhaifu wao na siwalaumu, kwani kila shetani na mbuyu wake!!
 
mswahili
njoo na hoja za kumkoma nyani giladi baaabaake na wacha mchezo mchafu wa kung'ang'ania mambo ya ukabila kila wakati, au hapa pia ukabila umepita? au spika ni mchaggga?(jokes)
 
Unaona Nchi isivyokuwa na uwajibikaji watu wanaoneshana ufahari kwa fedha ya walipa kodi wewe ukiagiza kingora cha polisi mwenzako anaagiza Ndege la kijeshi na MP.........................Kweli mbombo ngafuuuuuu!

Lakini kapuya kama waziri wa ulinzi si yuko entitled kutumia ndege ya jeshi ama?
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom