Barua kwa Mke Wangu...

Barua kwa Mke Wangu...

Nice story Mentor!!ni somo zuri kwa watu wanaoendekeza uzinzi na kutoka nje ya ndoa hata kwa sisi ambao hatujaingia kwenye ndoa,majaribu na misukosuko wanayopitia wanandoa ni foundation nzuri ya kujenga uhusiano madhubuti na imara kwasababu unachallenge subira na uvumilivu wao,pamoja na kujiifunza mapungufu ya wenza hao!
  • Ustahamilivu na kusameheana ni mambo muhimu sana kwenye mahusiano yoyote. mwallu has a big heart and true love it takes a lot of courage to go through what she did and still hold on and stay strong...ijapokuwa Mentor alinogewa na kusahau hata kwanini alimuoa yule alomuoa na si huyo mlimbwende mwengine!TAMAA MBELE MAUTI NYUMA!!Ni vyema tukajifunza jinsi ya kudhibiti tamaa zetu za kimwili!
  • Ndugu sio watu wakutegemea 100% ukiwa na matatizo ndio unaona utu wa watu.. Ndio maana wazungu wanasema familiy ni wife,husband and children hao wengine ni relatives.
  • Ulifanya jambo la maana kuandika ile barua ya wosia..cause you can never predict the future so we should always be prepared for anything..like having enough savings now while we flourishh..
  • Felix is a true friend,sio sifa kuwa na marafiki chungu nzima,binafsi bora niwe na rafiki mmoja tu ambae namuamini na najua ni rafiki wa kweli AKUFAAYE KWA DHIKI NDIO RAFIKI

Thanks mimi49 ....am humbled!!!

Thank you so much kwa kuwa mkweli . Wanawake ni viumbe tofauti sana Eeee Mungu wabariki wanawake wote na uwaongezee moyo wa kusamehe na uvumilivu zaidi.

Na infii wote wakiongozwa na Mtambuzi na Dark City waseme amen.

Thanks kwa ku appreciate who we are (Women)..we tend to forgive so easily

Heveni is such a bad girl....am sure she will fix it by tomorrow...

Ngoja nimalizie ushindi wetu Yanga wil kam bak to u!!!
 
Last edited by a moderator:
hii story inafanana na wimbo mmoja huwa nausikisikia kaimba mwanamke sijui anaitwa nani....wimbo mrefu sana,kwenye AUDI yule dada aliimba VOGUE....

Bahati Bukuku - Dunia haina huruma.

...Very true Mkuu Mentor halafu penzi likakolea kupita kiasi...Ukiwaambia watu nilikutana na mupenzi wangu wa moyo Bar wanakuangalia kama hawakuelewi vile.....Chezeya Penzi weye!!!! Una kipaji kikubwa sana Mkuu cha uandishi, usinisahau kunipatia copy utakapoamua kuandika kitabu chako cha kwanza.








Weww wajua mkuu BAK...one day ntawaambia nilivyokutana na mwallu that is if she lets me...
Abt kitabu...kip praying for my wife n good things will come. You know what they say, "..behind every man's success (and ofcoz failure) there is a woman."

Story inafanana kabisa na wimbo wa bahati bukuku usikilize utaskia yote hayo aliyesema anaenda nje ya nchi alikuwa anaenda kuangalia mpira ila hongera mtoa mada kwa kuweza kuielezea vizuri

It is right mkuu ningependa na yeye aisome hadithi hii. Mimi na mke wangu mwallu hatukuipenda solution aliyoitoa kuhusu Mkristo ujaribiwapo. Kwa wimbo wa dini tuliona una walakini nyingi na mkono wa Mungu si mdogo kiasi kile hata ashindwe kumpa mlango wa kutokea.
Isitoshe, kosa halitengui kosa.

Siku ya kufa nyani miti yote haikubali idandiwe

Heheheh kwel mkuu. Na ujanja wangu wote kwa mkurya yule nilishindwa kufurukuta kabisa.
 
Last edited by a moderator:
nimeipenda
Mwisho imedhihirisha kuwa kimfaacho mtu chake

Thanks BADILI TABIA. Kweli chako chako aisee...

Mentor you are so strategic like PK!!mwallu sijui kama atakataa tena hapo ,kwa sababu kapata bonge la bwana!!
mwekundu ssssshhhhhhh.... #kimyakimya

Ngoja kuna NDOA mpya hapa ya Hamidini na Madame B inatakiwa iige mfano wa penzi la mfano la Mentor na Mwallu

Naam mkuu waite wote wenye ndoa zao wajifunze kwetu.
I love you so much mwallu.

Mentor hii Kweli ni story na kwa Kweli ina kila sababu ya kuwa kwenye hili jukwaa na sitakuwa na la kuongeza maana AshaDii kashamaliza yote
Ndoa na iheshimiwe na watu wote na kumpata mke mwema na atakayekupenda haswa katika kipindi kigumu na cha shida ni jambo jema sana
Naona unapredict kitu kitakachotokea baada ya miaka miwili ya ndoa yako ila angalia yasikupate Kama haya uliyoyaandika mkuu Mentor

Mkuu Mr Rocky dada AshaDii yupo deep mno mpaka anatisha..hiyo analysis.
Ila tia neno jiweke kwenye upande wa mwanaume useme jambo...

Hapo mwisho panipitie mbali mm uhuni nshaacha...
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu Mentor sitaki kuwa biased na sitaki kuonekana napendelea upande wowote ila ningekuwa sina hiyo ningesema sisi wanaume tuna sijui kimdudu kinatekenya mara kwa mara. Maana unaweza ukawa na mwanamke amekamilika kila idara na anakupenda sana na anakupa kila unachokihitaji ila bado macho yetu yanatambaa kuangalia kila ndege arukaye twamtaka
Haijalishi tuko kwenye ndoa wala single au bachelor mzoefu ila hatuishi tamaa. Hatujali maumivu wanayopata wenzetu wakati wanapogundua kuwa tunacheat tena na vitu ambavyo havina Hata uzuri wa wake zetu. Hatuoni Kama tunawaumiza wenzetu ila huwa tunajifikiria wenyewe na tamaa zetu. Na mwanaume mwenzako akiwa na kitu kizuri bado tunakionea wivu natamani ningekuwa nacho mimi na sio yule yaani BAK akiwa na kitu kizuri Mr Rocky roho inadunda kwa nini nisingekuwa nacho mimi. Nitatafuta kila njia nikipate au Hata kuwa nacho one night stand ndo hayo ya Mtambuzi na mke wa mjeda
Muhimu ni kuwa heshimu ndoa yako na heshimu hisia za mwenzako jiweke kwenye moyo wake anavyoumia atakaposikia au kujua kuwa unamsaliti
Mentor ulikuwa na kila kitu Kutoka kwa mwallu ila tamaa zikakufanya utamani vya nje na kukumbushia vya zamani ambavyo ushaviacha tangu umetoa kiapo cha kuwa na huyu peke yake. Kumbe kiapo kile ulikuwa ni upepo tuu upite hukumaanisha ni mbaya sana.
 
Last edited by a moderator:
Mleta uzi uache tabia za KDF wa westgate ...kwa ufupi story ni kutoka kwenye wimbo wa Bahati Bukuku ...
 
Uko serious kabisa mkuu?

Hebu fanya haraka kuomba radhi kabla hayajakukuta...

Babu DC!!

Ulisha-retire kwani babu Dark City? ngoja nimuulize Kaizer...

Mleta uzi uache tabia za KDF wa westgate ...kwa ufupi story ni kutoka kwenye wimbo wa Bahati Bukuku ...

Ahaha...read the ending to my story. And besides I do not deny the fact kwamba idea ya hadithi hii ilitokana na wimbo huo. Read my previous comments sir!
 
Last edited by a moderator:
Ablessed umenena kweli
kwa hali ya kawaida tu hakuna mwanaume anaeweza kumsamehe mke wake kwa jambo la aibu kama hilo,na hata kama anampenda kiasi gani,bado atafikiria watu wa nje watakavomchukulia incase akisamehe,watamuona ni mwanaume wa aina gani? heshima yake kwa jamii inayomzunguka na nduguze itakuwaje? lakini sisi wanawake huwa hatujali,Mungu katupa mioyo yenye kuhimili mikiki mikiki kutoka upande wa pili
Jamani haya mambo mengine kama utani vile lkn kwenye jamii yamekuwepo sana. Hili ni fundisho kwa wanaume wasio waaminifu kwenye ndoa zao na pia thamani ya mke ni kubwa mno yaweza shinda hata thamani ya ndugu. Lakini nani anajali alarm za aina hii kila mara zinagonga hakuna anaetaka kusikia. Pia najiuliza hivi Mentor ungekuta mwallu kafanya hayo je ungemsaidia kweli. Mwanamke ana role kubwa sana kwenye familia. Halafu jamani mahusiano ya kale haifai kuyachokoza kwani bond zingine huwa ni ngumu kuziharibu cha msingi ni kukaa mbali nazo na ikiwezekana kuacha kabisa mawasiliano wala kujua kinachojili ulikotoka wewe songa mbele usitazame nyuma.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Mr Rocky,kwanza hongera kwa kuukubali ukweli kua wanaume ni viumbe wabinafsi sana..hasa linapokuja suala la hisia
natumaini na wanaume wengine wote watakua wameelewa ulichoongelea hapa
Mkuu Mentor sitaki kuwa biased na sitaki kuonekana napendelea upande wowote ila ningekuwa sina hiyo ningesema sisi wanaume tuna sijui kimdudu kinatekenya mara kwa mara. Maana unaweza ukawa na mwanamke amekamilika kila idara na anakupenda sana na anakupa kila unachokihitaji ila bado macho yetu yanatambaa kuangalia kila ndege arukaye twamtaka
Haijalishi tuko kwenye ndoa wala single au bachelor mzoefu ila hatuishi tamaa. Hatujali maumivu wanayopata wenzetu wakati wanapogundua kuwa tunacheat tena na vitu ambavyo havina Hata uzuri wa wake zetu. Hatuoni Kama tunawaumiza wenzetu ila huwa tunajifikiria wenyewe na tamaa zetu. Na mwanaume mwenzako akiwa na kitu kizuri bado tunakionea wivu natamani ningekuwa nacho mimi na sio yule yaani BAK akiwa na kitu kizuri Mr Rocky roho inadunda kwa nini nisingekuwa nacho mimi. Nitatafuta kila njia nikipate au Hata kuwa nacho one night stand ndo hayo ya Mtambuzi na mke wa mjeda
Muhimu ni kuwa heshimu ndoa yako na heshimu hisia za mwenzako jiweke kwenye moyo wake anavyoumia atakaposikia au kujua kuwa unamsaliti
Mentor ulikuwa na kila kitu Kutoka kwa mwallu ila tamaa zikakufanya utamani vya nje na kukumbushia vya zamani ambavyo ushaviacha tangu umetoa kiapo cha kuwa na huyu peke yake. Kumbe kiapo kile ulikuwa ni upepo tuu upite hukumaanisha ni mbaya sana.
 
Last edited by a moderator:
Yani we Mentor wewe. Yani mi na wewe tunahitaji kuwa na serıous talks.

BTW huyo dokta kama mkeo angekuwa Heaven on earth sidhani kama angetoka salama. LOL

Siku zote nlijua mwallu ni sista wa Paroko.... kumbe kijana hatare sana weye
 
Last edited by a moderator:
true that AshaDii...ndoa ni taasisi yenye changamoto sana,na inayohitaji uvumilivu wa hali ya juu..na siku zote wanawake sie ndo tunavumilia mengine makubwa na magumu kama ya mume wangu Mentor..nakubaliana na wewe kwenye no 1-6 ila kwenye no. 7 hapana,ukimuamini mtu nusu nusu unakua hauna amani kabisa
na ukiamini sana napo ndo ivo unakua dissapointed
Mentor, it is a great story, I have enjoyed reading it. Hongera sana, kuna mengi ya kujifunza hapa.

Hii story inafundisha haya:-

1. Ni muhimu sana kupatia kuoa mwanamke ambaye kweli anafaa kuwa mke. Ni mwanamke mwerevu na mwenye busara pekee anaweza pita kwenye mtihani huu kama alivyoweza kufanya Mwallu, ki ukweli; wengine wangeweza kuacha Mentor ujifie after all anakuwa na hasira kuwa umemsaliti.

2. Sijui watu huwa wanatumia vigezo gani kudhania mwanamke na mwanaume ni sawa. Wanaume wanao tembea na wake za watu wana risk kubwa sana, tena hasa kama hayo mahusiano ni long term, kheri hata wale ambao wanakuwa wamegusa siku moja na kupotea kabisa (sina maana kuwa ni acceptable). Mke wa mtu ni sumu jamaniii... Kaka/baba zetu yapaswa muwe waoga katika hilo. Ni hatari!

3. Wazazi wana umuhimu katika maamuzi yetu ya kila siku. Lakini unapokuwa ni mtu mzima inapaswa kuji emancipate kuwa na uwezo wa kuchagua na kusimamia maamuzi yako. Pengine huyo shombe shombe angefanikiwa kuolewa na wewe asingekusaliti kwa mwanaume mwingine maana inaonyesha wazi (tokana na story uliyotoa) alikuwa anakupenda.

4. Wanaume acheni kupenda dezo na kutaka mteremko. Unatoka na mke wa mtu, huoni aibu jamani hata nafsi kukusuta kwenda kulala kitanda alicho nunua mwanaume mwenzio na kwenda kuvitumia vitu vyake hapo nyumbani? Unaridhika na kujiachia kabisa kana kwamba ni kwako? In such cases ni kheri wale wenye uwezo mtoke nje ya mji kabisa (narudia sina mana kuwa na support - naelezea facts).

5. Wanawake ni muhimu kutambua na kujua thamani ya mume. Hata kama humpendi hata kama hakuridhishi si haki kabisa kumdhalilisha kwa kutembea na mwanaume mwingine tena kwenye nyumba ambayo kakujengea/pangia yeye na mnaishi naye.

6. Kwa wanandoa... Ndoa si mteremko. Na ndoa huimarika zaidi tokana hasa na misuko suko muipatayo na mkafaulu kupitia hayo majaribu. Kwa stori kama hii, naamini kwa kiasi kikubwa Mentor ni lazima ashike adabu, awe mpole, aongeze mapenzi na kujikita katika kuhakikisha anamfurahisha mkewe. Maana Mentor kapata bahati ya kuelewa na kuona ni to what length mkewe anampenda, kumthamini na kuwajibika kama mke mwema.

7. Kwa mwanamke yeyote yule katika ndoa ni muhimu akatambua umuhimu wa kuacha walau kanafasi kadogo sana katika imani ya kuwa mumeo anaweza kukuangusha ama kukuumiza kwa namna moja ama nyingine. Hili husaidia pale matatizo kama haya yakitokea unakuwa una nguvu ya maamuzi sahihi wakati wa kutafakari tukio. Mwallu alizimia, kwa mwingine magonjwa kama pressure yanaweza ibukia hapo hapo sababu tu uliweka imani yako yote hapo. Nisinukuliwe vibaya kuwa wanaume hawaaminiki: ila naomba nieleweke kuwa ni rahisi kuumizwa nae hasa kama unampenda na pengine hata kama na yeye pia anakupenda.


Pamoja Saana.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom