Barua kwa Dr. Slaa: Mageuzi/Mapinduzi ni kubwa kuliko agenda ya Ufisadi

TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,306
2,000
Hivi hawa wanaomshabikia Lowassa na kumwona mkombozi mpya wa siasa za upinzani wamewahi kujiuliza kwanini wafuasi wa Lowassa bado wanashiriki ktk zoezi la kura za maoni ndani ya CCM?Hiyo inamaanisha bado kuna strong bond kati ya Lowassa na wafuasi wake kwa CCM na si rahisi uhusiano wao huu kuvunjika,to be honest Lowassa ataleta utaratibu wa KiCCM ndani ya CHADEMA, huo ndio ukweli.
 

PROPHET POLY

JF-Expert Member
Oct 15, 2012
469
195
Hata Musa hakutoka Mtu au mpambe mwingine.awaye yeyote kulioko Taifa lake...pia Nyiae ndio.mnatulete UKOO WA PANYA...BABA MAMA MTOTO...MALENGO UPEWE WEWE THEN UNAWAKARIBISHA WATU??
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,568
2,000
Mageuzi ya kweli yanayotokana na dhamira safi kabisa kwa Tanzania
1. namba moja kukomesha ufisadi.
2. namba mbili kukomesha ufisadi.
3. namba tatu kukomesha ufisadi.

Ufisadi/Rushwa ndo adui wa haki. Adui wa haki ndo anajifungua mambo yote dhalimu ambayo kwayo ndo yanayomwelemea common mwananchi.
Adui wa haki sio CCM wala CHADEMA adui wa haki ni wale jamaa wanaotumia mulungalu kufinyanga haki za common mwananchi. Mkimuona kokote mtu wa aina hiyo mahala popote aliye tu na character za namna hiyo mpigeni li-rungu.

Msidanganywe eti adui wa haki ni CCM ama System. Adui wa haki ni mtoa na mpokea rushwa, na System inatengenezwa kwa kuunganisha watu wa namna hiyo yani watoa rushwa na wapokea rushwa na mafisadi.
Hiyo teamLowasa tayari ni System. Sasa mnataka kutoa System ipi?
Acha kuleta propaganda zako uchwara hapa wewe. Kuna mafisadi wa hatari kuliko Lowassa mara milioni moja na wote wana vyeo vya juu serikalini na bado watachaguliwa tena. Angalia hii listi ya mafisadi na wauza unga iliyoshinda kwa kishindo kwenye kura za maoni za CCM kwenye udiwani na ubunge: Chenge, Tibaijuka, Riziwani, Manji, Azani, Makamba, Nyalandu, etc.. Hii inatufundisha nini? 1. Lowassa hakuondolewa kwenye mbio za urais kwasababu ya ufisadi ila ni ugomvi binafsi wa kudhulumiana fedha na mkuu wa nchi. 2. Wananchi wa Tanzania hawachaguu viongozi waadilifu bali mafisadi.
 

nuruyamnyonge

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
4,201
2,000
Kuna kitu hamjakijua tu..Mungu amenionesha:
1. Udini.(sio sana )
2.Udhehebu unataka kulitafina Taifa hili kwa mara nyingine.
Nb:
1. Dr.Umetumwa ukomboe Taifa la Tanzania sio kueneza udhehebu.
2. Unaona bora Umsapoti Magufuli coz ya kutokea zizi moja kiaina?
3.Mungu atawadhibuni nyote kwani Amesikia kilio Cha watanzania wengi..Acheni Mzaha.

4. Kumkataa E.l si tu Ufisadi..Kwani wako wangapi ccm?
Ni zaidi ya Ufisadi Na.agenda hii ya siri..
ONYO.
utawala wenye Baraka..watoka kwa Mungu.
NOTE....
1.MUSA ALIUA KULE MISRI NA BADO MUNGU AKAMTUMA KULIKOMBOA TAIFA LAKE...SEMBUSE UFISADI AMBAO HAU.A UHAKIKA KWA E.L?
2.MNAMWAMINI MUNGU YUPI?Aliyesema samehe mara saba sabini?
ACHENI MZAHA..

Mmmhh!! Taifa lilipofika hapa ni Dr Slaa pekee atalikomboa taifa, kwa kumuunga mkono Lowassa, tutafika mbali sana kumbe siasa ni hatari nimeogopa sana. Dr Slaa chondochonde baba, njoo Taifa litabomoka rudi chadema tutabaki yatima naona hatari hukoooo.......
 

Gor

JF-Expert Member
May 27, 2014
2,793
1,195
Woote wanamageuzi lengo letu kuu ni kuiondoa CCM madarakani basi....nguvu nyingi zielekezwe huko.Baada ya lengo kuu kutimizwa tutatasonga mbele sasa.Njoo na ungana nasi kutimiza hilo.Hakuna fisadi upinzani.Fisadi anataka kulindwa.
 

m2me

Member
Jul 23, 2012
55
95
Nikiwa kama mtanzania mpenda mabadiliko sina budi nami kutia neno katika uhamuzi wa Dr.Wilbrod Slaa kususa siasa za CHADEMA tena katika kipindi ambacho “mwali ameishaingia chumbani na tena kavua nguo zote”

Nakili kuwa ni haki yako kabisa kuchukua uhamuzi aliouchukua lakini pia nikili kuwa ulipaswa kutafakari kwa kina na kama kiongozi uliyetazamiwa kupewa nchi haukupaswa kujifungia muda mrefu kutafakari bali siku moja au mbili zingekutosha kuueleza umma maamuzi yako badala ya ‘kuzira’ kimyakimya!

Taswira uliyoijenga kama kiongozi shupavu na jasiri na hata kutuaminisha kuwa ulifaa kupewa nchi sasa inatufanya tuwaze vinginevyo. Kumbe siku moja ukiwa rais ungeweza kususia kushirikiana na viongozi wenzako wa mataifa ya Afrika, America, Ulaya na hata Asia kisa rais Kagema amepinga au amekusema vibaya..au Nkurunzinza kalazimisha kugombea mhura wa tatu kinyume na makubaliano ya Arusha! Ungekuwa rais wa ajabu kwelikweli.

Siku za nyuma kidogo, niliandika nikipongeza hotuba ya Mwenyekiti Mbowe nikidiliki kusema kuwa itachukua miaka mingi kusikia tena hotuba kama hiyo. Katika hotuba yake mbowe aligusia umuhimu wa kutokaa na ‘madonge’ moyoni ambayo hayawezi kutusogeza mbele kimaendeleo bali kusahau ya nyuma na kusonga mbele akisisitiza kuwa katika siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu.
Aliongeza kuwa jamii yote ingemshangaa kama mwenyekiti wa chama kumkataa Lowasa, mtu mwenye mtaji mkubwa wa wapiga kura kisa hisia tu zilizojengwa juu yake kuwa utajiri wake ni wakifisadi. Siku zote adui wa adui yako ni rafiki…CCM tayari wameweka uadui na Lowasa kwa kumkata jina bila sababu za msingi kama alivyothibitisha Prof. Mwandosa, Kingunge, Nchimbi na wengineo.

Wakati huu ambao CHADEMA imeunganisha nguvu na vyama vya CUF, NLD na NCCR Mageuzi ni wakati ambao haujawahi kutokea katika historia ya vyama vyingi vya siasa hapa nchini. Kwa tabia hii ya Slaa inaonesha si tu kumkataa Lowasa bali pia hata kama Prof. Lipumba angepitishwa kupeperusha bendera ya UKAWA angesusa au anatuma salamu kwa wagombea wa chadema wa majimbo na udiwani kuwa kwa kuwa wameshiriki kukijenga chama basi kama wakikatwa na nafasi zao kupewa wagombea wengine wa UKAWA basi nao wasuse!

Katika hotuba yake ya kumkaribisha Lowasa, Mbowe alisema kuwa “hatuwezi kujenga chama cha viongozi, aliyejiunga leo, jana ana haki sawa na mwasisi wa chama hicho…tusiwakatae wageni kisa nafasi zetu, CHADEMA siyo chama cha kugawana vyeo bali majukumu’’ na hiyo ndiyo demokrasia. Tusijiwekee hati miliki kwenye vyama ambavyo tunadai ni vya wananchi, amabao waamefanya vyama mali yao binafsi kama akina mzee Cheyo, Mrema, Mtikila na wengineo tunaona uimara wa vyama hivyo.

Dr. Slaa kubali kuwa siasa ndivyo zilivyo… tuwe na mtizamo mpana wan chi badala ya maslahi binafsi, nafasi yoyote inayolenga kuongeza nguvu katika mapambano itumie. Siyo kwamba CUF na wenzao ni wajinga bali wameweka mbele maslahi taifa kwanza badala ya ruzuku, viti maalum, uimara wa vyama vyao badala ya uchaguzi ili kwanza lengo la kuiondoa CCM madarakani litimie na mengine yatajadilika daadae.

Kama Dr. Slaa anaamini ndugu Edward ni mwizi/fisadi basi apeleke ushahidi huo mahakamani na kama hana ushahidi basi arudi washirikiane kuondoa mfumo unaowawezesha watu kufanya ufisadi. Lazima tukubali, kama mfumo unatoa ‘magepu ya kupiga’ hata mimi nikiingia lazima nipige coz opportunity ipo!

Kinachonishangaza kwa Dr. Slaa; kapiga chenga uwanja mzima..kabaki na kipa …kipa amekaba upande wake na kuacha goli wazi na kwa bahati nzuri anatokea mchezaji mwenzake anaomba pasi amalizie anashindwa kumpasia kisa mchezaji huyo hampendi.

Mwisho nakuomba Dr. piga moyo konde..rudi jeshini tumalizie mapambano, kumkomboa mtanzania siyo mpaka wewe uwe rais. Fanya kama walivyofanya wanamapinduzi wengine akina Che Guevara n.k

Abiiiingeeee...
 

mwanadome

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
4,138
2,000
Binadamu hamna jema,bado hata kukaa kimya kwa dr slaa imekua nongwaa?,mnataka aseme.muanga kumuita msaliti?,jaribuni kuheshimu maamuzi yake,kiherehere cha nn?
 
Jun 14, 2014
73
125
Jambo Jema ni kwamba kundi
linalotak mabadiliko haliongozw na
mtu wala halimfuat mtu.....Linaong
ozwa na ukomavu wa akil na
uzalendo wa nchi yao ...linaongozwa
na namna ambavyo CCM imechoka
Ccm mtafany nn kugeuza huu
upepo ??? Hata wakiondoka viongozi
wote mkafany fitina bado tuko tyar
kumpa hat mtikila kura zetu....
Mliyemtesa Kakua na kajiandikisha na
kuimiliki silaha.. TUFUNGAMANE KWA
PAMOJA WAPENDA MABADILIKO WE
LEAD BY NO ONE....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom