Barua kwa Dr. Slaa: Mageuzi/Mapinduzi ni kubwa kuliko agenda ya Ufisadi

KATASAN'KAZA

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
3,098
1,345
Ndugu!

Nakusalimu katika jina la MAGEUZI.

Ni takribani wiki sasa kukiwa na hali ya sintofahamu juu ya kiongozi wetu mpendwa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndg. Dr. Wilbroad Peter Slaa. Ni dhahiri kuwa kwa watanzania tulio wengi hasa wapenda mageuzi ambao haturidhiki na kasi ya uongozi wa watawala (CCM) na serikali yote kwa ujumla katika suala zima la kutuletea maendeleo na kupambana na changamoto kama Umasikini ulio kithiri (extreme poverty), ujinga(illiteracy) na maradhi (diseases). Lengo/malengo ya bandiko hili lenye maadhi ya barua, ni mambo mawili;-

Kwanza kabisa kumsihi baba yangu Dr. Slaa aelewe agenda ya mabadiriko(changes) kwenye mkitadha wa utawala/uongozi(system) katika nchi yetu (Tanzania). Staki kuhukumu kuwa hajui anachokifanya ila naomba nieleweke kuwa yanayosemwa kwenye mitandao ya jamii na baadhi ya vyombo vya habari juu ya maisha yake ya kisiasa hasa kuhusishwa na kuachana na siasa za vuguvugu la mageuzi (movement politics) kama yasemwayo yatakuwa ni kweli au yakaja kutimia kuwa kweli binafsi nitakuona baba yangu Dr.Slaa kama MSALITI wa wanamageuzi/wanamapinduzi wa Tanzania na pia msaliti wa wanyonge wote waliishio katika dimbwi zito la umasikini, mardahi na ujinga usio na ndoto za kusita katika taifa hili isipokuwa kwa kufanya mapinduzi/mageuzi ya mfumo wa uongozi (the leadership system).

Niliyosema hapo juu yamejengwa juu ya msingi mmoja tu, nao ni MAGEUZI YA KWELI pasipo kujua yatakujaje ila kwa kuangalia kila fursa iliyopo mbele yetu na kuitumia kikamilifu ili kufanikisha dhana nzima ya UKOMBOZI wa wanyonge kwa kuleta mageuzi katika nyanja za uchumi(economic reform), uongozi bora (leadership reform) na fikra (mind set) za watu(watanzania).

Ni ukweli usiyo na chembe ya shaka kuwa sasa hivi (kipindi cha uchaguzi) ni muda wa sisi wanamapinduzi/wanamageuzi (changes championes) tukiongozwa na viongozi wa vyama vya wanamaguzi watu kama Dr. slaa, Limpumba, Mbowe, Mnyika, Mbatia, Lissu, Mdee, S.Lyimo, kwa kutaja tu wachache ila na wengine kwa uchache wao ambao ni wanazuoni wetu wanaotuongoza katika kuendesha mapambano haya, nikishawishika kumtaja Prof. Baregu, Prof. Safari, Wakili msomi Mabere Marando. Wengine sikwamba sitambui mchango wenu na mimi pia nikiwa mstari wa mbele ingawa sionekani ila labda kwasababu ya ufupi wangu( umhimu mdogo) kwa jinsi waonavyo walio warefu( wenye nyazifa) hii haiwezi kuwa sababu ya kujipuuza na kujitisha tamaa katika safari hii ya kutafuta mageuzi ya kweli (real changes) kwangu mimi lililo la msingi ni kuyatia mkononi magauzi ya sekta/nyanja nilizotaja hapo juu.

Kidogo nitoe historia yangu kusupport mageuzi iliko anzia, ni mwaka 2007 nikiwa nimemaliza kidato cha sita, nilipata daraja la tatu kwangu ulikuwa ufaulu mkubwa sana nikilinganisha mazingira niliyosomea(shule za serikali) nilinyimwa mkopo na Bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Mwaka 2008 nilifanya mtihani tena kam amtahiniwa binafsi, nikapata point 10(dvsn3) sababu ya kutorudia somo la GS, niliomba vyuo nikachaguliwa chuo pendwa (UDOM) katika masomo humanities, shida ikalrudi ileile nikinyimwa mkopo sababu ya penalty a GS, hii haikuwa sababu ya msingi ila tu mfumo dhaifu wa usimamizi wa elimu ulipelekea watu tulikuwa na matatizo kama haya kuhangaika sana.

Nilipambana mpaka kwa mkurugenzi wa elimu ya juu, wengi wa wanafunzi wenzangu walifukuzwa chuo, kiukweli nilivumilia matatizo kwa mwaka na nusu nikisoma bila mkopo hatimaye ule msemo wa HAKI HAIPOTEI ILA INAWEZA CHELEWESHWA TU, ulitimia ingwa pia wanasema HAKI ILIYOCHELEWESHWA NI SAWA NA HAKI ILIYOPOTEA. Sikukata tama mwisho nilipata hati yangu ya kulipiwa na serikali kama watanzania wengine. Kwangu ilikuwa ni funzo kubwa sana, na kuanzia hapo niliamua kujiunga na wanamapinduzi na ilikuwa mwanzo wa kujua kuwa kuna haja kufanya mageuzi. Nisiwachoshe sana.

Nikirudi kuelezea msimamo wangu juu ya ujio wa Lowasa katika siasa za Mageuzi, ni kweli usiopingika kuwa kilichombele yetu kama kizuizi cha mabadiriko ya uchumi, siasa(uongozi), kijamii na mambo ya maendeleo kwa ujumla ni mfumo(CCM) na bila chenga ya aibu naomba niwaeleweshw watanzania wapi tumekwama kwenye kujikomboa kwenye umasikini na ujinga vitu ambavyo ni kikwanzo kwa kila binadamu duniani katika kujieletea maendeleo.

Moja, Siasa za kuandaana katika kubadirishana madaraka; hii kati ya changamoto kubwa inayotupelekea kuishi jinsi tunavyoishi leo, si vibaya kiongozi yeyote kuwaandaa watu wake ili katika kutokuwepo kwake awepo mtu mwingine atakayechukua nafasi ya kuwaongoza au kuwatawala. Shida inayojitokeza ni kuwa hapa nchini hawaandaliwi watu badala yake anaandaliwa mtu( kibaraka) katika haya kumekuwa na juhudu nyingi za watu wenye nyazifa wamekuwa wakitumia nafasi zao katika kutafuta ridhaa ya kuwaongoza watnazania. Haya ni kati ya makosa makubwa katika mstabari mzima wa uongozi wa Tanzania.

Nimalize tena na tena kwa kumuumba Dr. slaa. Chondechonde hakikisha unatambua kuwa agenda ya MAGEUZI/MAPINDUZI ni kubwa kuliko agenda ya UFISADI twajua umetukuka kwa kupinga ufisadi ila katika hili la ujio wa LOWASA kukufanya uonekane kupoteza uelekeo katika agenda ya kutafuta mabadiriko(changes) haitakuwa sawa. Umma wa watanzania wanatambua mchango wako katika kuleta na kupigania mabadiriko tadhali na unaombwa kwa niaba ya WAPENDA MABADILIKO tunakusihi sana tubaki kitu kimoja huku agenda ya ujio wa Lowasa ikituongoza kama sime ya kuchinjia mfumo mfu wa SSM katika nchi yetu. MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKA TANZANIA. Mageuzi yabaki agenda kubwa kuliko zote!

Nimeandika makala haya kwa niaba nzuri ya Taifa letu.
 
Mbona mnaweweseka Mmecomprimise Principles mnataka D Slaa naye awe rahisi rahisi kama nyinyi?. Hamuwezi kuwatumia watu kama Ngazi.
Dr Slaa kwa msimamo wake huu anaweza kuusaidia sana Upinzani Ujitafakari na hivyo kusaidia kujenga upinzani Imara utakaouiondoa CCM kwa hoja, sera, ubora na Usafi, Siyo kuiondoa CCM for the sake of kuiondoa then What?
 
Dr Slaa na usomi wake alitakiwa kujua siasa ni mchezo wa kucompromise. you can't have it all.
 
Mbona mnaweweseka Mmecomprimise Principles mnataka D Slaa naye awe rahisi rahisi kama nyinyi?. Hamuwezi kuwatumia watu kama Ngazi.
Dr Slaa kwa msimamo wake huu anaweza kuusaidia sana Upinzani Ujitafakari na hivyo kusaidia kujenga upinzani Imara utakaouiondoa CCM kwa hoja, sera, ubora na Usafi, Siyo kuiondoa CCM for the sake of kuiondoa then What?

Mbona unalialia, kwani wewe umejipangaje?

Unataka upinzani uendelee kusubiri mana kutoka mbiguni kuiondoa ccm? Cha msingi ccm b kwanza iondoke tuko tayari kuanza upya!
 
Ndugu!

Nakusalimu katika jina la MAGEUZI.

Ni takribani wiki sasa kukiwa na hali ya sintofahamu juu ya kiongozi wetu mpendwa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndg. Dr. Wilbroad Peter Slaa. Ni dhahiri kuwa kwa watanzania tulio wengi hasa wapenda mageuzi ambao haturidhiki na kasi ya uongozi wa watawala (CCM) na serikali yote kwa ujumla katika suala zima la kutuletea maendeleo na kupambana na changamoto kama Umasikini ulio kithiri (extreme poverty), ujinga(illiteracy) na maradhi (diseases). Lengo/malengo ya bandiko hili lenye maadhi ya barua, ni mambo mawili;-

Kwanza kabisa kumsihi baba yangu Dr. Slaa aelewe agenda ya mabadiriko(changes) kwenye mkitadha wa utawala/uongozi(system) katika nchi yetu (Tanzania). Staki kuhukumu kuwa hajui anachokifanya ila naomba nieleweke kuwa yanayosemwa kwenye mitandao ya jamii na baadhi ya vyombo vya habari juu ya maisha yake ya kisiasa hasa kuhusishwa na kuachana na siasa za vuguvugu la mageuzi (movement politics) kama yasemwayo yatakuwa ni kweli au yakaja kutimia kuwa kweli binafsi nitakuona baba yangu Dr.Slaa kama MSALITI wa wanamageuzi/wanamapinduzi wa Tanzania na pia msaliti wa wanyonge wote waliishio katika dimbwi zito la umasikini, mardahi na ujinga usio na ndoto za kusita katika taifa hili isipokuwa kwa kufanya mapinduzi/mageuzi ya mfumo wa uongozi (the leadership system).

Niliyosema hapo juu yamejengwa juu ya msingi mmoja tu, nao ni MAGEUZI YA KWELI pasipo kujua yatakujaje ila kwa kuangalia kila fursa iliyopo mbele yetu na kuitumia kikamilifu ili kufanikisha dhana nzima ya UKOMBOZI wa wanyonge kwa kuleta mageuzi katika nyanja za uchumi(economic reform), uongozi bora (leadership reform) na fikra (mind set) za watu(watanzania).

Ni ukweli usiyo na chembe ya shaka kuwa sasa hivi (kipindi cha uchaguzi) ni muda wa sisi wanamapinduzi/wanamageuzi (changes championes) tukiongozwa na viongozi wa vyama vya wanamaguzi watu kama Dr. slaa, Limpumba, Mbowe, Mnyika, Mbatia, Lissu, Mdee, S.Lyimo, kwa kutaja tu wachache ila na wengine kwa uchache wao ambao ni wanazuoni wetu wanaotuongoza katika kuendesha mapambano haya, nikishawishika kumtaja Prof. Baregu, Prof. Safari, Wakili msomi Mabere Marando. Wengine sikwamba sitambui mchango wenu na mimi pia nikiwa mstari wa mbele ingawa sionekani ila labda kwasababu ya ufupi wangu( umhimu mdogo) kwa jinsi waonavyo walio warefu( wenye nyazifa) hii haiwezi kuwa sababu ya kujipuuza na kujitisha tamaa katika safari hii ya kutafuta mageuzi ya kweli (real changes) kwangu mimi lililo la msingi ni kuyatia mkononi magauzi ya sekta/nyanja nilizotaja hapo juu.

Kidogo nitoe historia yangu kusupport mageuzi iliko anzia, ni mwaka 2007 nikiwa nimemaliza kidato cha sita, nilipata daraja la tatu kwangu ulikuwa ufaulu mkubwa sana nikilinganisha mazingira niliyosomea(shule za serikali) nilinyimwa mkopo na Bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Mwaka 2008 nilifanya mtihani tena kam amtahiniwa binafsi, nikapata point 10(dvsn3) sababu ya kutorudia somo la GS, niliomba vyuo nikachaguliwa chuo pendwa (UDOM) katika masomo humanities, shida ikalrudi ileile nikinyimwa mkopo sababu ya penalty a GS, hii haikuwa sababu ya msingi ila tu mfumo dhaifu wa usimamizi wa elimu ulipelekea watu tulikuwa na matatizo kama haya kuhangaika sana.

Nilipambana mpaka kwa mkurugenzi wa elimu ya juu, wengi wa wanafunzi wenzangu walifukuzwa chuo, kiukweli nilivumilia matatizo kwa mwaka na nusu nikisoma bila mkopo hatimaye ule msemo wa HAKI HAIPOTEI ILA INAWEZA CHELEWESHWA TU, ulitimia ingwa pia wanasema HAKI ILIYOCHELEWESHWA NI SAWA NA HAKI ILIYOPOTEA. Sikukata tama mwisho nilipata hati yangu ya kulipiwa na serikali kama watanzania wengine. Kwangu ilikuwa ni funzo kubwa sana, na kuanzia hapo niliamua kujiunga na wanamapinduzi na ilikuwa mwanzo wa kujua kuwa kuna haja kufanya mageuzi. Nisiwachoshe sana.

Nikirudi kuelezea msimamo wangu juu ya ujio wa Lowasa katika siasa za Mageuzi, ni kweli usiopingika kuwa kilichombele yetu kama kizuizi cha mabadiriko ya uchumi, siasa(uongozi), kijamii na mambo ya maendeleo kwa ujumla ni mfumo(CCM) na bila chenga ya aibu naomba niwaeleweshw watanzania wapi tumekwama kwenye kujikomboa kwenye umasikini na ujinga vitu ambavyo ni kikwanzo kwa kila binadamu duniani katika kujieletea maendeleo.

Moja, Siasa za kuandaana katika kubadirishana madaraka; hii kati ya changamoto kubwa inayotupelekea kuishi jinsi tunavyoishi leo, si vibaya kiongozi yeyote kuwaandaa watu wake ili katika kutokuwepo kwake awepo mtu mwingine atakayechukua nafasi ya kuwaongoza au kuwatawala. Shida inayojitokeza ni kuwa hapa nchini hawaandaliwi watu badala yake anaandaliwa mtu( kibaraka) katika haya kumekuwa na juhudu nyingi za watu wenye nyazifa wamekuwa wakitumia nafasi zao katika kutafuta ridhaa ya kuwaongoza watnazania. Haya ni kati ya makosa makubwa katika mstabari mzima wa uongozi wa Tanzania.

Nimalize tena na tena kwa kumuumba Dr. slaa. Chondechonde hakikisha unatambua kuwa agenda ya MAGEUZI/MAPINDUZI ni kubwa kuliko agenda ya UFISADI twajua umetukuka kwa kupinga ufisadi ila katika hili la ujio wa LOWASA kukufanya uonekane kupoteza uelekeo katika agenda ya kutafuta mabadiriko(changes) haitakuwa sawa. Umma wa watanzania wanatambua mchango wako katika kuleta na kupigania mabadiriko tadhali na unaombwa kwa niaba ya WAPENDA MABADILIKO tunakusihi sana tubaki kitu kimoja huku agenda ya ujio wa Lowasa ikituongoza kama sime ya kuchinjia mfumo mfu wa SSM katika nchi yetu. MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKA TANZANIA. Mageuzi yabaki agenda kubwa kuliko zote!

Nimeandika makala haya kwa niaba nzuri ya Taifa letu.

​mkuu nakupongeza sana kwa barua yako nzuri sana. nadhani ataelewa.
 
Adui wa Tanzania ni CCM kwa attribute ya ufisadi tu. Ufisadi ndo uliotufikisha hapa tulipo kwa mashua ikiwa ni CCM kwa sababu ya ufisadi. Lakini manahodha walioifikisha hapa CCM kwa sababu ya ufisadi wamekitekeleza chombo cha mashua CCM, na kutimukia ktk mashua CHADEMA, ili kuwafikisha CHADEMA walipowaacha CCM. Very interesting.

Na ukiiondoa attribute ya ufisadi ndani ya CCM, hivi adui wa Tanzania anakuwa ni nani? Kwi kwi kwi kwi
 
Mageuzi ya kweli yanayotokana na dhamira safi kabisa kwa Tanzania
1. namba moja kukomesha ufisadi.
2. namba mbili kukomesha ufisadi.
3. namba tatu kukomesha ufisadi.

Ufisadi/Rushwa ndo adui wa haki. Adui wa haki ndo anajifungua mambo yote dhalimu ambayo kwayo ndo yanayomwelemea common mwananchi.
Adui wa haki sio CCM wala CHADEMA adui wa haki ni wale jamaa wanaotumia mulungalu kufinyanga haki za common mwananchi. Mkimuona kokote mtu wa aina hiyo mahala popote aliye tu na character za namna hiyo mpigeni li-rungu.

Msidanganywe eti adui wa haki ni CCM ama System. Adui wa haki ni mtoa na mpokea rushwa, na System inatengenezwa kwa kuunganisha watu wa namna hiyo yani watoa rushwa na wapokea rushwa na mafisadi.
Hiyo teamLowasa tayari ni System. Sasa mnataka kutoa System ipi?
 
Pini hii Lowasa aliitumia kwa ccm....alipiga kimya watu wakamsemea weee!..
..sasa Dr Slaa sasa naye kachukua pini hiyo hiyo anaitumia kwa pipoz,people full network search! nataman slaa ahamie ACT ili ZZK naye awachunie kina mwigamba kama wiki mbili hivi naye tumsemee.
 
Mageuzi ya kweli yanayotokana na dhamira safi kabisa kwa Tanzania
1. namba moja kukomesha ufisadi.
2. namba mbili kukomesha ufisadi.
3. namba tatu kukomesha ufisadi.

Ufisadi/Rushwa ndo adui wa haki. Adui wa haki ndo anajifungua mambo yote dhalimu ambayo kwayo ndo yanayomwelemea common mwananchi.
Adui wa haki sio CCM wala CHADEMA adui wa haki ni wale jamaa wanaotumia mulungalu kufinyanga haki za common mwananchi. Mkimuona kokote mtu wa aina hiyo mahala popote aliye tu na character za namna hiyo mpigeni li-rungu.

Msidanganywe eti adui wa haki ni CCM ama System. Adui wa haki ni mtoa na mpokea rushwa, na System inatengenezwa kwa kuunganisha watu wa namna hiyo yani watoa rushwa na wapokea rushwa na mafisadi.
Hiyo teamLowasa tayari ni System. Sasa mnataka kutoa System ipi?
mbona unaongea mambo ya ajabu! hujui system ndiyo inawafanya watu kuwa fisadi, maskini, matajiri etc. unafikiri wachina hawapendi kufisidi mali za umma!?
 
System inaundwa na watu, ndugu. Hakuna kitu System.
Na hiyo System kwa kiwango kikubwa ndo imehamia upande wa pili. Sasa ni system gani mnayotaka kuungusha?
 
Tafadhali Dr.W Slaa hembu legeza shingo kidogo, huoni hata vijana wadogo kabisa kiumri kama hawa wanakuhitajinkatika chama?

Kama kweli ni mkristo na unajua nguvu ya kusamehe sitarajii kujiondoa kwako karika chama.
 
Last edited by a moderator:
Kweli kabisa Agenda ya mageUzi ni kubwa mno baba yetu Dr.slaa hebu iangamize kwanza ccm ufusadi in rahisi sana tunakuomba she wana chadema unganisheni nguvu
 
System inaundwa na watu, ndugu. Hakuna kitu System.
Na hiyo System kwa kiwango kikubwa ndo imehamia upande wa pili. Sasa ni system gani mnayotaka kuungusha?

MkamaP najua unatoka sehemu ya wale watu wenye akili wanaokula aina ya samaki wa kutoka ziwani na mitoni. Hawa unaowahabarisha hawatakuelewa kwa sababu uelewa wao mdogo, wao hawali samaki, wanakula nyama kwa wingi , wezi wengi wanatoka kwao shida tupu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom