Barua kwa Dr. Slaa: Mageuzi/Mapinduzi ni kubwa kuliko agenda ya Ufisadi

Ndugu!

Nakusalimu katika jina la MAGEUZI.

Ni takribani wiki sasa kukiwa na hali ya sintofahamu juu ya kiongozi wetu mpendwa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndg. Dr. Wilbroad Peter Slaa. Ni dhahiri kuwa kwa watanzania tulio wengi hasa wapenda mageuzi ambao haturidhiki na kasi ya uongozi wa watawala (CCM) na serikali yote kwa ujumla katika suala zima la kutuletea maendeleo na kupambana na changamoto kama Umasikini ulio kithiri (extreme poverty), ujinga(illiteracy) na maradhi (diseases). Lengo/malengo ya bandiko hili lenye maadhi ya barua, ni mambo mawili;-

Kwanza kabisa kumsihi baba yangu Dr. Slaa aelewe agenda ya mabadiriko(changes) kwenye mkitadha wa utawala/uongozi(system) katika nchi yetu (Tanzania). Staki kuhukumu kuwa hajui anachokifanya ila naomba nieleweke kuwa yanayosemwa kwenye mitandao ya jamii na baadhi ya vyombo vya habari juu ya maisha yake ya kisiasa hasa kuhusishwa na kuachana na siasa za vuguvugu la mageuzi (movement politics) kama yasemwayo yatakuwa ni kweli au yakaja kutimia kuwa kweli binafsi nitakuona baba yangu Dr.Slaa kama MSALITI wa wanamageuzi/wanamapinduzi wa Tanzania na pia msaliti wa wanyonge wote waliishio katika dimbwi zito la umasikini, mardahi na ujinga usio na ndoto za kusita katika taifa hili isipokuwa kwa kufanya mapinduzi/mageuzi ya mfumo wa uongozi (the leadership system).

Niliyosema hapo juu yamejengwa juu ya msingi mmoja tu, nao ni MAGEUZI YA KWELI pasipo kujua yatakujaje ila kwa kuangalia kila fursa iliyopo mbele yetu na kuitumia kikamilifu ili kufanikisha dhana nzima ya UKOMBOZI wa wanyonge kwa kuleta mageuzi katika nyanja za uchumi(economic reform), uongozi bora (leadership reform) na fikra (mind set) za watu(watanzania).

Ni ukweli usiyo na chembe ya shaka kuwa sasa hivi (kipindi cha uchaguzi) ni muda wa sisi wanamapinduzi/wanamageuzi (changes championes) tukiongozwa na viongozi wa vyama vya wanamaguzi watu kama Dr. slaa, Limpumba, Mbowe, Mnyika, Mbatia, Lissu, Mdee, S.Lyimo, kwa kutaja tu wachache ila na wengine kwa uchache wao ambao ni wanazuoni wetu wanaotuongoza katika kuendesha mapambano haya, nikishawishika kumtaja Prof. Baregu, Prof. Safari, Wakili msomi Mabere Marando. Wengine sikwamba sitambui mchango wenu na mimi pia nikiwa mstari wa mbele ingawa sionekani ila labda kwasababu ya ufupi wangu( umhimu mdogo) kwa jinsi waonavyo walio warefu( wenye nyazifa) hii haiwezi kuwa sababu ya kujipuuza na kujitisha tamaa katika safari hii ya kutafuta mageuzi ya kweli (real changes) kwangu mimi lililo la msingi ni kuyatia mkononi magauzi ya sekta/nyanja nilizotaja hapo juu.

Kidogo nitoe historia yangu kusupport mageuzi iliko anzia, ni mwaka 2007 nikiwa nimemaliza kidato cha sita, nilipata daraja la tatu kwangu ulikuwa ufaulu mkubwa sana nikilinganisha mazingira niliyosomea(shule za serikali) nilinyimwa mkopo na Bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Mwaka 2008 nilifanya mtihani tena kam amtahiniwa binafsi, nikapata point 10(dvsn3) sababu ya kutorudia somo la GS, niliomba vyuo nikachaguliwa chuo pendwa (UDOM) katika masomo humanities, shida ikalrudi ileile nikinyimwa mkopo sababu ya penalty a GS, hii haikuwa sababu ya msingi ila tu mfumo dhaifu wa usimamizi wa elimu ulipelekea watu tulikuwa na matatizo kama haya kuhangaika sana.

Nilipambana mpaka kwa mkurugenzi wa elimu ya juu, wengi wa wanafunzi wenzangu walifukuzwa chuo, kiukweli nilivumilia matatizo kwa mwaka na nusu nikisoma bila mkopo hatimaye ule msemo wa HAKI HAIPOTEI ILA INAWEZA CHELEWESHWA TU, ulitimia ingwa pia wanasema HAKI ILIYOCHELEWESHWA NI SAWA NA HAKI ILIYOPOTEA. Sikukata tama mwisho nilipata hati yangu ya kulipiwa na serikali kama watanzania wengine. Kwangu ilikuwa ni funzo kubwa sana, na kuanzia hapo niliamua kujiunga na wanamapinduzi na ilikuwa mwanzo wa kujua kuwa kuna haja kufanya mageuzi. Nisiwachoshe sana.

Nikirudi kuelezea msimamo wangu juu ya ujio wa Lowasa katika siasa za Mageuzi, ni kweli usiopingika kuwa kilichombele yetu kama kizuizi cha mabadiriko ya uchumi, siasa(uongozi), kijamii na mambo ya maendeleo kwa ujumla ni mfumo(CCM) na bila chenga ya aibu naomba niwaeleweshw watanzania wapi tumekwama kwenye kujikomboa kwenye umasikini na ujinga vitu ambavyo ni kikwanzo kwa kila binadamu duniani katika kujieletea maendeleo.

Moja, Siasa za kuandaana katika kubadirishana madaraka; hii kati ya changamoto kubwa inayotupelekea kuishi jinsi tunavyoishi leo, si vibaya kiongozi yeyote kuwaandaa watu wake ili katika kutokuwepo kwake awepo mtu mwingine atakayechukua nafasi ya kuwaongoza au kuwatawala. Shida inayojitokeza ni kuwa hapa nchini hawaandaliwi watu badala yake anaandaliwa mtu( kibaraka) katika haya kumekuwa na juhudu nyingi za watu wenye nyazifa wamekuwa wakitumia nafasi zao katika kutafuta ridhaa ya kuwaongoza watnazania. Haya ni kati ya makosa makubwa katika mstabari mzima wa uongozi wa Tanzania.

Nimalize tena na tena kwa kumuumba Dr. slaa. Chondechonde hakikisha unatambua kuwa agenda ya MAGEUZI/MAPINDUZI ni kubwa kuliko agenda ya UFISADI twajua umetukuka kwa kupinga ufisadi ila katika hili la ujio wa LOWASA kukufanya uonekane kupoteza uelekeo katika agenda ya kutafuta mabadiriko(changes) haitakuwa sawa. Umma wa watanzania wanatambua mchango wako katika kuleta na kupigania mabadiriko tadhali na unaombwa kwa niaba ya WAPENDA MABADILIKO tunakusihi sana tubaki kitu kimoja huku agenda ya ujio wa Lowasa ikituongoza kama sime ya kuchinjia mfumo mfu wa SSM katika nchi yetu. MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKA TANZANIA. Mageuzi yabaki agenda kubwa kuliko zote!

Nimeandika makala haya kwa niaba nzuri ya Taifa letu.

Mawazo ni mazuri na yanapaswa kufanyiwa kazi vilivyo ili tuweze kuvuka panapotusumbu.
 
Kwa muda wa wiki moja sasa dr Slaa hajashiriki shughuli za chama kwa kile kinachosemwa ni ' kupinga ujio wa Lowassa chadema'.
Ombi langu kwa Dr Slaa na Familia yake ni KUTAMBUA NA KUKUBALI KWA DHATI KABISA KWAMBA ADUI NA KIKWAZO CHA MAENDELEO YA WATU WETU NI CCM.
Tuungane pamoja katika vita hii kwani miongoni mwa orodha ya mafisadi ndiyo rais wetu hadi leo(Kikwete).
cc.Tumaini Makene
 
Haitashangaza tukiambiwa kasusa na tutashangaaa tukiambiwa kahama chama ingawa ikitokea hivyo hayo ni maamuzi yake. Kwa nini?

Haishangazi tukiambiwa kasusa ni ili apate muda wa kufikiria hatma yake kisiasa. Yaliyotokea ndani ya CHADEMA ni kwa Maslahi mapana ya Taifa badala ya mtu mmoja ni Visionary Leaders pekee hufanya kama viongozi wa CHADEMA walivyofanya.

Kitendo cha kukaribishwa Mh Lowassa CHADEMA na kutunukiwa kugombea Urais, yumkini na UKAWA ni faida kwa CHADEMA kama chama, kama UKAWA, kama Taifa ili kusaidia KUONDOWA MFUMO MKONGWE ulioota mizizi wa CCM.
Ni kwa mantiki hiyo UZITO wa LOwassa una nafasi yake katika mezani ya UKAWA/VS CCM naani asiyejuwa?

Dr Slaa ikitokea kasusa ni haki yake(maoni yangu) lakini iwe ni kwa muda tu ili atafakari vizuri.
Kama mwanasiasa anahitaji kujuwa hatma yake kisiasa. Kwa Mfano alimtaja Lowasa kama fisadi leo anakuja kuwa Rais na Slaa kuwa chini yake itakuwaje? jee kuna makubaliano ya kuja kuondowa kiwingu hicho? Nini Dr Slaa afanye ili kulinda Credibility yake kisiasa inategemea upevu wake kisiasa. Ingekuwa ni Maalim Seif huyu ni gwiji nafikiri aige kwake . Maslahi ya taifa Mbele. (Dr nafikiri kokote uliko unanisikia)

Jee Kuhama kuna Uhalisia?
Logic ya kuhama hapa ni ngumu. Kwamba mapambano yote dhidi ya CCM yaje yafifie kwa kukosa nafasi leo wakati kesho ipo? au eti Kuficha AIBU kwa kisingizio cha CREDIBILITY YA KISIASA iwe sababu ya kurejesha nyuma jitihada zote za miongo mitatu ya vuguvugu la mabadiliko? kwamba CCM kama mfumo uliochoka, uliooza kwa ufisadi, uliokwama kuiendeleza Tanzania leo atokee mtu muhimu katika mageuzi awape fursa ya KUVURUGA UPINZANI ulioimarika katika hali ambayo haijapata kutokea afanye hivyo?

Basi itakuwa hakuwa na DHAMIRA na itakuwa sio mwanasiasa aliyepikika.

Ole wetu.


Mungu ibariki UKAWA.
 
Dr Slaa alidhiriki vikao vya kuridhia ujio wa lowassa, picha zilizo vuja zinaonyesha dhaihi.
 
Nashauri dr Slaa role model wangu achana na siasa za akina mbowe. mwywe nimechana kadi ya chadema leo.
 
Hivi watu mnajihakikishaje kwamba Lowasa anaweza kushinda urais? Mimi mbona naona Slaa alikuwa na chances nyingi za kushinda urais kuliko Lowasa? Na si kulikuwa na uzi wa poll humu JF unaowalinganisha Slaa na Lowasa ambapo Slaa alionyesha kumwacha Lowasa mbali tu?
 
Mageuzi ya kweli yanayotokana na dhamira safi kabisa kwa Tanzania
1. namba moja kukomesha ufisadi.
2. namba mbili kukomesha ufisadi.
3. namba tatu kukomesha ufisadi.

Ufisadi/Rushwa ndo adui wa haki. Adui wa haki ndo anajifungua mambo yote dhalimu ambayo kwayo ndo yanayomwelemea common mwananchi.
Adui wa haki sio CCM wala CHADEMA adui wa haki ni wale jamaa wanaotumia mulungalu kufinyanga haki za common mwananchi. Mkimuona kokote mtu wa aina hiyo mahala popote aliye tu na character za namna hiyo mpigeni li-rungu.

Msidanganywe eti adui wa haki ni CCM ama System. Adui wa haki ni mtoa na mpokea rushwa, na System inatengenezwa kwa kuunganisha watu wa namna hiyo yani watoa rushwa na wapokea rushwa na mafisadi.
Hiyo teamLowasa tayari ni System. Sasa mnataka kutoa System ipi?

Salute mkuu
 
Tunahitaji viongozi wazalendo wa kweli. Wanaochukiwa kuwaonewa kwa mtanzania yeyote kwa kukosa haki za msingi. Mageuzi bila kuwa na watu waadalifu ni sawa na bure. Viongozi waadilifu ndio watakaosaidia kubadili mifumo na sheria kandamizi. Tofauti yake ni kutafuta zamu ya kula.
 
Haya Mageuzi unayoyazungumzia hapa hayatakuwa na maana yoyote kama utwatoa CCM waliovaa gwanda za Kijani na kuwaweka CCM B waliovaa gwanda za kaki (CDM) chini ya Lowasa
 
Nashauri dr Slaa role model wangu achana na siasa za akina mbowe. mwywe nimechana kadi ya chadema leo.

Kwa nini uchane? Nani atajua kwamba umechana au umekasirika? Busara ni kurudisha kadi ya chama kwa kiongozi au ofisi ya chama na uwape sababu za kurudisha kadi ili wafanyie kazi mapungufu hayo siku nyingine!
 
Muhimu zaidi ni kuiondoa CCM madarakani kwa kupitia uchaguzi ujao wa Oktoba.
Ujio wa Lowassa unaongeza ushindi wa Ukawa.

Kama Dk Slaa hatambui na kulikubali hili basi tutasema kumbe hakustahili kuwa rais wetu.

Aaaarrrrrggggghhhhh.........

Ukombozi kwanza.
 
siasa hizi jamani! bora ccm itoke madarakani

Ni kweli tunataka CCM iondoke lakini isiondoke upande wa kushoto ikaja upande wa kulia maana Fisadi Lowasa ni mwanaccm na hajarudishi kadi ya ccm na bado ana mapenzi ya ccm hata baraza lake la mawaziri atawajaza wanaccm. N hata ikitokea kashindwa uchaguzi 2015 hata saidia lolote CHADEMA na UKAWA ataondoka zake amekuja CHADEMA kwa ajili ya kutaka kuogmbea Uraisi tu maana sijamuona akisifia s CHADEMA wala UKAWA ina maana jamaa kaja kama mgombea binafsi zaidi ya peoples power hana jingine
 
Kuna kitu hamjakijua tu..Mungu amenionesha:
1. Udini.(sio sana )
2.Udhehebu unataka kulitafina Taifa hili kwa mara nyingine.
Nb:
1. Dr.Umetumwa ukomboe Taifa la Tanzania sio kueneza udhehebu.
2. Unaona bora Umsapoti Magufuli coz ya kutokea zizi moja kiaina?
3.Mungu atawadhibuni nyote kwani Amesikia kilio Cha watanzania wengi..Acheni Mzaha.

4. Kumkataa E.l si tu Ufisadi..Kwani wako wangapi ccm?
Ni zaidi ya Ufisadi Na.agenda hii ya siri..
ONYO.
utawala wenye Baraka..watoka kwa Mungu.
NOTE....
1.MUSA ALIUA KULE MISRI NA BADO MUNGU AKAMTUMA KULIKOMBOA TAIFA LAKE...SEMBUSE UFISADI AMBAO HAU.A UHAKIKA KWA E.L?
2.MNAMWAMINI MUNGU YUPI?Aliyesema samehe mara saba sabini?
ACHENI MZAHA..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom