unakubali kwamba CHADEMA nao wana mfumo wao? kwanini unaamini lowassa ataibadili CHADEMA na si CHADEMA kumbadili lowassa (japo hana cha kubadilishwa) ukizingatia kubadili mfumo ni kazi kuliko kumbadili mtu.System inaundwa na watu, ndugu. Hakuna kitu System.
Na hiyo System kwa kiwango kikubwa ndo imehamia upande wa pili. Sasa ni system gani mnayotaka kuungusha?
unakubali kwamba CHADEMA nao wana mfumo wao? kwanini unaamini lowassa ataibadili CHADEMA na si CHADEMA kumbadili lowassa (japo hana cha kubadilishwa) ukizingatia kubadili mfumo ni kazi kuliko kumbadili mtu.
Dr. Slaa akilegea hapa tusahau kupata upinzani wa kweli unaochukia uovu ulio ndani ya wanamtandao wa CCM
harafu unajichanganya, uumesema mfumo ni mtandao wa watu. hii inamaana Lowassa akisimama peke yake anakuwa hana mfumo anaowakilisha. iweje sasa aende CHADEMA na kubadisha mfumo?. hata kama wanahama wengi wanatakiwa kuwa kuwa na power huko waendako ili kuinfluence mambo.Taasisi ya urais ni System tofauti na System ya chama. Ningependa ukaelewa hilo kwanza. System ni watu, ama kwa lugha rahisi ni mtandao wa watu (ktk siasa za tz) ndo system. Na huo mtandano wa watu umeshahamia upande wa pili. Sasa ni mtandao wa watu wapi mnaotaka kuungusha? Maana neno system linaweza kuwa msamiati kwa baadhi yetu.
NB: System ya chama inaongozwa na katiba ya chama na System ya urais inaongozwa na katiba ya Jumhuri wa Muungano wa Tanzania.
harafu unajichanganya, uumesema mfumo ni mtandao wa watu. hii inamaana Lowassa akisimama peke yake anakuwa hana mfumo anaowakilisha. iweje sasa aende CHADEMA na kubadisha mfumo?. hata kama wanahama wengi wanatakiwa kuwa kuwa na power huko waendako ili kuinfluence mambo.
pia unavyosema mfumo umehamia upande wa pili unazua maswali. inamaana huo mfumo unaenda kureplace waliokuwa nao CHADEMA au CHADEMA hawakuwa na wao na huo ndiyo watauchukua? pia unavyosema umehama, huko ulikotoka wamebaki na mfumo gani?
Magufuli alipochaguliwa alisema "wazee msiogope nitawalinda". tunataka kutoa huo mfumo wa kulindana.naona unaunderestimate nguvu ya chama kuendesha urais? mtu kama magufuli hata iweje hawezi kwenda tofauti na matakwa ya chama.
KATASAN'KAZA...Ndugu!
Nakusalimu katika jina la MAGEUZI.
Ni takribani wiki sasa kukiwa na hali ya sintofahamu juu ya kiongozi wetu mpendwa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndg. Dr. Wilbroad Peter Slaa. Ni dhahiri kuwa kwa watanzania tulio wengi hasa wapenda mageuzi ambao haturidhiki na kasi ya uongozi wa watawala (CCM) na serikali yote kwa ujumla katika suala zima la kutuletea maendeleo na kupambana na changamoto kama Umasikini ulio kithiri (extreme poverty), ujinga(illiteracy) na maradhi (diseases). Lengo/malengo ya bandiko hili lenye maadhi ya barua, ni mambo mawili;-
Kwanza kabisa kumsihi baba yangu Dr. Slaa aelewe agenda ya mabadiriko(changes) kwenye mkitadha wa utawala/uongozi(system) katika nchi yetu (Tanzania). Staki kuhukumu kuwa hajui anachokifanya ila naomba nieleweke kuwa yanayosemwa kwenye mitandao ya jamii na baadhi ya vyombo vya habari juu ya maisha yake ya kisiasa hasa kuhusishwa na kuachana na siasa za vuguvugu la mageuzi (movement politics) kama yasemwayo yatakuwa ni kweli au yakaja kutimia kuwa kweli binafsi nitakuona baba yangu Dr.Slaa kama MSALITI wa wanamageuzi/wanamapinduzi wa Tanzania na pia msaliti wa wanyonge wote waliishio katika dimbwi zito la umasikini, mardahi na ujinga usio na ndoto za kusita katika taifa hili isipokuwa kwa kufanya mapinduzi/mageuzi ya mfumo wa uongozi (the leadership system).
Niliyosema hapo juu yamejengwa juu ya msingi mmoja tu, nao ni MAGEUZI YA KWELI pasipo kujua yatakujaje ila kwa kuangalia kila fursa iliyopo mbele yetu na kuitumia kikamilifu ili kufanikisha dhana nzima ya UKOMBOZI wa wanyonge kwa kuleta mageuzi katika nyanja za uchumi(economic reform), uongozi bora (leadership reform) na fikra (mind set) za watu(watanzania).
Ni ukweli usiyo na chembe ya shaka kuwa sasa hivi (kipindi cha uchaguzi) ni muda wa sisi wanamapinduzi/wanamageuzi (changes championes) tukiongozwa na viongozi wa vyama vya wanamaguzi watu kama Dr. slaa, Limpumba, Mbowe, Mnyika, Mbatia, Lissu, Mdee, S.Lyimo, kwa kutaja tu wachache ila na wengine kwa uchache wao ambao ni wanazuoni wetu wanaotuongoza katika kuendesha mapambano haya, nikishawishika kumtaja Prof. Baregu, Prof. Safari, Wakili msomi Mabere Marando. Wengine sikwamba sitambui mchango wenu na mimi pia nikiwa mstari wa mbele ingawa sionekani ila labda kwasababu ya ufupi wangu( umhimu mdogo) kwa jinsi waonavyo walio warefu( wenye nyazifa) hii haiwezi kuwa sababu ya kujipuuza na kujitisha tamaa katika safari hii ya kutafuta mageuzi ya kweli (real changes) kwangu mimi lililo la msingi ni kuyatia mkononi magauzi ya sekta/nyanja nilizotaja hapo juu.
Kidogo nitoe historia yangu kusupport mageuzi iliko anzia, ni mwaka 2007 nikiwa nimemaliza kidato cha sita, nilipata daraja la tatu kwangu ulikuwa ufaulu mkubwa sana nikilinganisha mazingira niliyosomea(shule za serikali) nilinyimwa mkopo na Bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Mwaka 2008 nilifanya mtihani tena kam amtahiniwa binafsi, nikapata point 10(dvsn3) sababu ya kutorudia somo la GS, niliomba vyuo nikachaguliwa chuo pendwa (UDOM) katika masomo humanities, shida ikalrudi ileile nikinyimwa mkopo sababu ya penalty a GS, hii haikuwa sababu ya msingi ila tu mfumo dhaifu wa usimamizi wa elimu ulipelekea watu tulikuwa na matatizo kama haya kuhangaika sana.
Nilipambana mpaka kwa mkurugenzi wa elimu ya juu, wengi wa wanafunzi wenzangu walifukuzwa chuo, kiukweli nilivumilia matatizo kwa mwaka na nusu nikisoma bila mkopo hatimaye ule msemo wa HAKI HAIPOTEI ILA INAWEZA CHELEWESHWA TU, ulitimia ingwa pia wanasema HAKI ILIYOCHELEWESHWA NI SAWA NA HAKI ILIYOPOTEA. Sikukata tama mwisho nilipata hati yangu ya kulipiwa na serikali kama watanzania wengine. Kwangu ilikuwa ni funzo kubwa sana, na kuanzia hapo niliamua kujiunga na wanamapinduzi na ilikuwa mwanzo wa kujua kuwa kuna haja kufanya mageuzi. Nisiwachoshe sana.
Nikirudi kuelezea msimamo wangu juu ya ujio wa Lowasa katika siasa za Mageuzi, ni kweli usiopingika kuwa kilichombele yetu kama kizuizi cha mabadiriko ya uchumi, siasa(uongozi), kijamii na mambo ya maendeleo kwa ujumla ni mfumo(CCM) na bila chenga ya aibu naomba niwaeleweshw watanzania wapi tumekwama kwenye kujikomboa kwenye umasikini na ujinga vitu ambavyo ni kikwanzo kwa kila binadamu duniani katika kujieletea maendeleo.
Moja, Siasa za kuandaana katika kubadirishana madaraka; hii kati ya changamoto kubwa inayotupelekea kuishi jinsi tunavyoishi leo, si vibaya kiongozi yeyote kuwaandaa watu wake ili katika kutokuwepo kwake awepo mtu mwingine atakayechukua nafasi ya kuwaongoza au kuwatawala. Shida inayojitokeza ni kuwa hapa nchini hawaandaliwi watu badala yake anaandaliwa mtu( kibaraka) katika haya kumekuwa na juhudu nyingi za watu wenye nyazifa wamekuwa wakitumia nafasi zao katika kutafuta ridhaa ya kuwaongoza watnazania. Haya ni kati ya makosa makubwa katika mstabari mzima wa uongozi wa Tanzania.
Nimalize tena na tena kwa kumuumba Dr. slaa. Chondechonde hakikisha unatambua kuwa agenda ya MAGEUZI/MAPINDUZI ni kubwa kuliko agenda ya UFISADI twajua umetukuka kwa kupinga ufisadi ila katika hili la ujio wa LOWASA kukufanya uonekane kupoteza uelekeo katika agenda ya kutafuta mabadiriko(changes) haitakuwa sawa. Umma wa watanzania wanatambua mchango wako katika kuleta na kupigania mabadiriko tadhali na unaombwa kwa niaba ya WAPENDA MABADILIKO tunakusihi sana tubaki kitu kimoja huku agenda ya ujio wa Lowasa ikituongoza kama sime ya kuchinjia mfumo mfu wa SSM katika nchi yetu. MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKA TANZANIA. Mageuzi yabaki agenda kubwa kuliko zote!
Nimeandika makala haya kwa niaba nzuri ya Taifa letu.
Mimi naona upofu tu na ubinafsi unamsumbua; hivi Lowassa angebakia sisiem na akawa mgombea halafu katiba ikaruhusu Raisi kuteua hata mawaziri toka upinzani akaamua kuchukua UKAWA watupu atawale nao si ingekuwa ujinga kukataa fursa ya kuingia uwanjani kufunga goli? Hata Wamarekani wanashirikiana na Iran kumpiga ISIS. Penye common enemy watu huunganisha nguvu kumtoa baada ya hapo ndio waanze kujichambua ipi pumba ipi mchele lakini si kabla ya hapoDr Slaa na usomi wake alitakiwa kujua siasa ni mchezo wa kucompromise. you can't have it all.
sure mkuu. first thing first. huwezi pata mambo yote kwa wakati mmoja.Mimi naona upofu tu na ubinafsi unamsumbua; hivi Lowassa angebakia sisiem na akawa mgombea halafu katiba ikaruhusu Raisi kuteua hata mawaziri toka upinzani akaamua kuchukua UKAWA watupu atawale nao si ingekuwa ujinga kukataa fursa ya kuingia uwanjani kufunga goli? Hata Wamarekani wanashirikiana na Iran kumpiga ISIS. Penye common enemy watu huunganisha nguvu kumtoa baada ya hapo ndio waanze kujichambua ipi pumba ipi mchele lakini si kabla ya hapo