Baraza la Mawaziri: Nani atoke, Nani abaki, Nani aingie?


kaka.wanatangaza saaa ngapi baraza
 
Mh. Ndungulile, unaweza kufafanua kidogo juu ya suala hili muhimu la 'mfumo", hasa kuliweka vyema katika muktadha wake? Mfumo wa chama tawala au mfumo wa utawala wa nchi?



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi swali lako hili kwa DK,, binafsi naungana nae kwa kilio cha mfumo [tumezoe SYSTEM].Nitajibu kwa upande wangu mimi kama ifuatavyo.
1: Je unaamini katika MFUMO kama ndio engine halisi ya kujenga ama kubomoa Nchi?
2: Nchi yetu Watanzania Tunaiendesha katika aina ipi ya MFUMO.Je ni mfumo wa KITAIFA kwanza ndio unaoendesha Taifa au MFUMO wa CHAMA tawala Kwanza ndio unaoendesha Nchi.Kati ya aina hizo mbili mfumo upi ndio mfumo mama wa jamii yetu watanzania.

Naamini kwa uwezo wako siitaji kufafanua mfumo ni nini kwako?

Madhara ya mfumo wa uendeshaji Taifa ulipoguswa na kada ya wafanyabishara ndipo itilafu ilipoingia ndani ya engine.
Mfano unazungumzia uteuzi.Ni kweli ni jambo jema tu,lakini wateule ni aina gani ya watu kwenye society yetu.Historia ya wateule wetu ni POSITIVE au NEGATIVE kwenye jamii anayotoka mteule, manake Charity Begins At Home.Je viongozi wetu ni aina hiyo ya watu?

3: Je vetting zinafanyika na kufuata historia za kizazi cha mteule kwa maana uongozi na maadili uanzia nyumbani.

4: Je mwenendo mzima wa wajibu na kanuni za utendaji wa mteule zinapimwa kwa vigezo kubalika na hasa jamii, inapotokea mteule kushindwa matarajio ya WANANCHI ambao ndio waajili wakuu. mteule je awajibike kwa kwa nani
(a) Awajibike kwa WANANCHI waliowaajili wakuu kikatiba wasio na uwezo wa kumtoa au kumwajili kiutendaji wa mfumo?
(b) Ama awajibike kwa Mteuzi aliyemteua ambae kapewa dhamana na Wananchi kupitia sanduku la kura au ajira ya Serikali?

Mfano tumeshuhudia mawaziri wanne[4] wakitimuliwa.Lakini ndani ya hao mawaziri wanne,ni mmoja tu Kagasheki aliyeonyesha kutambua MWAJILI wake mkuu ni nani!!Na akamuomba Mwajili mwenye dhamana ya KIKATIBA yani mteuzi wake kuachia ngazi kwa kuwa WANANCHI wameongea.Je ndio mfumo wetu unaanda Viongozi walioko madarakani au watalajiwa kuwa na mindset za Kagasheki au Rais Mstaafu Ally H Mwinyi?
5: Mfumo wetu huko tayari kupokea na kufanya kazi na watu wasio na ITIKADI ZA VYAMA VYA SIASA.Je engine watendaji wetu wakuu ambao kwa ujumla wao tunaita mfumo wanaitikadi ipi ndani ya mioyo yao, yani wana mlengo upi kimawazo, kimtizamo, kifikra, kimausiano, kiuwajibikaji, kiutekelezaji.nk,?
(a) Je Ni Taifa Kwanza ?
(b) Ama ni Chama Cha Kisiasa Kwanza na Taifa Baadae linakuja baada ya msambaratiko?

Ebu nakuja Mkuu
 
Katika yote unasoma upepo wa LOWASSA tu wewe, yaaani na akili zetu watu sie LOWASSA arejee? mnadhani watanzania wanasahau haraka kiasi hicho au?
 
Kuna kijana amemaliza UDOM anaitwa Saul Mwaisenye nasikia anatajwa tajwa kushika nafasi ya Amosi Makalla hadi hivi sasa inasemekana ameisha itwa Dsm kwenda kumalizia Logistics za mwisho za ubunge wa kuteuliwa. All the best kijana wa kitanzania
 
Reactions: DSN

Mimi kwa upande wangu namuona BALOZI KHAMISI KAGASHEKI anafaa kuwa WAZIRI MKUU!
Nimependezwa na utendaji kasi wake, ni mchapakazi mwenye kujiamini.
 
Natokea mkoa wa Kagera na kwa sababu hiyo Prof Tibaijuka ni home girl wangu kwa ufupi dada yangu. Na kiukweli nilikuwa na imani naye kweli kabla hajateuliwa katika nafasi aliyonayo. Lakini ni dhahiri dada yangu huyu ameniangusha kweli. Hizi hapa ni sababu zangu:-

- Kupanda kwa gharama za kulipia viwanja

- Migogoro ya ardhi imeongezeka hadi kusababisha mauaji (Kilombero Kiteto na Mwanza)

- Mipanagilio ya miji yetu inaendelea kuwa hovyo na haonyeshi hata matumaini ya kuwa na majibu

- Uchafu wa miji yetu, hili linamgusa maana wizara yake inahusika na makazi

Dada yangu huyu ni member wa Jf labda anaweza kuja kujitetea, lakini najiuliza kama David Mathayo alitimuliwa kwa sababu ng'ombe wanazurura, kwanini Prof Tibaijuka aendelee kuwa waziri wakati wananchi wanakufa kwa magonvi ya ardhi? Na mbaya zaidi hawezi hata kwenda eneo la tukio?
 
Nimekutana na kitu cha aina hii Mchambuzi nisaidie kujua kupitia taarifa hii hapa mfumo wa Watendaji na Viongozi wetu ni upi kupitia MINDSET ZAO. Je NI TAIFA KWANZA vyama baadae au ni VYAMA KWANZA TAIFA NNTONDO AU IGOLO.!!!Samaahani kwa kutumia msamiati nimeutumia kuweka msisitizo.

Haya chini kwangu binafsi ndio majanga!!Kinaconiuma hatuna organ ya kumonitor viongoz na watendaji wetu mind set zao na matendo yao ni yepi na kuwalekebisha tena ikibid kwa kutmia ukali pale inapobidi tukizingatia MASLAHI YA TAIFA NA WANANCHI WAKE KWANZA NA SIO MASLAHI YA VYAMA NA BINAFSI.

 
Cabinet ijayo ni timu ushindi. Pindi Chana hawezi kabisa kuletwa, anajifanya tuu strictly mguu upande haweki!. Alipaswa awe waziri zamani tatizo sio mnyenyekevu!.
Pasco
Hapa I was dam wrong!, kumbe kupata uwaziri siku hizi, mtu sio lazima mpaka ukae mguu upande!. Uteuzi wa Mhe. Pindi Chana ni uthibitisho wa hili.
Hongera zake!.
Pasco.
 
Mkuu Salary Slip, angalau ulituandaa tusijeshangaa!, huvyo hatushangai!.
Pasco.

Mkuu Pasco ,hapa ninachokiona kwa siku za usoni ni kuwa endapo baraza hili litavurunda,basi wabunge na wananchi kwa ujumla wata-demand raisi mwenyewe ajiuzulu.

Kwa maneno mengine,Kikwete kawabeba hawa mawaziri akiwemo waziri mkuu kwa gharama za uraisi wake kwa siku zijazo.

Mkuu,usitarajie tena watu watalia na Pinda au mawaziri bali Kikwete himself will be the next target for resignation.

Tusubiri,time will tell.
 
Last edited by a moderator:
summon
Atakayeingizwa ni Deo Filikunjombe ili kumcontain, Dr. Mwaki pia atahamishwa to save his face na madudu ya Bandari na ATCL
Pasco
ni Deo Filikunjombe ili kumcontain....
at last...contained!....
RIP Deo Filikunjombe!.
Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…