Baraza la Maaskofu Katoliki kuhamia Dodoma

Baraza la Maaskofu Katoliki kuhamia Dodoma

Kwani kuna shida gani kanisa kuhamishia makao makuu yake dodoma? Pesa za ujenzi serikali haitatoa bali wakatoliki pekee yao. Kwanini wahamishe inaweza kuwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika mchakato wa kuhamia dodoma, kuweka shughuli za kanisa katikati ya nchi nk. Udini hadi kwenye mambo yasiyowahusu ,mbona shida sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna pahala umenisoma nimesema "kuna shida"?
 
Usiwe mweprsi wa kusahau pia. Mwaka 1960s Nyerere aliweka jiwe la Msingi ujrnzi wa Chuo kikuu cha waislam chini ya Usimamizi wa EAMWS na ufadhili wa Gamel Nasser wa Misri.. matokeo yake Tewa Said Tewa aliyekuwa mratibu wa zoezi hilo akahamishiwa kuwa Balozi wa China. Na hatimaye serikali kuiua EAMWS na kuianzisha BAKWATA. Uongozi wote wa BAKWATA ukawekwa na Serikali. Katiba ya Bakwata ikawa Copyright ya katiba ya TANU.. Mali zote za EAMWS zikawekwa chini ya BAKWATA. BAKWATA ndio hawa wakawa wauza mali za Waislam. Sbb ni taasis iliyoanzishwa na Serikali kuwa watchdog wa waislam and not Waratibu wa maendeleo ya Waislam. Tunapoijad8lk historia tuwe wakweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo mnataka maaskofu katoliki wawasaidie AMA? Wenzenu wamepewa ardhi nyie bado mko usingizini na EAMWS, mkiamka wenzenu wanafungua vyuo vikuu,mnabakia kulaumu serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusaidia lingewezesha serikali kuwa na hivyo vitu. Sio wao kanisa kuwa navyo halifu wakavifanya biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pugu Secondary(Catholic School)
Minaki Secondary(Catholic School)
Tosa Maganga Sec(Catholic School)
Weruweru Sec(Catholic School)
Lyamungo Sec(Catholic School)
Ilboru Sec
Ndanda Sec........(Catholic School)



Una wazimu...?
 
Kusaidia lingewezesha serikali kuwa na hivyo vitu. Sio wao kanisa kuwa navyo halifu wakavifanya biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pugu Secondary(Catholic School)
Minaki Secondary(Catholic School)
Tosa Maganga Sec(Catholic School)
Weruweru Sec(Catholic School)
Lyamungo Sec(Catholic School)
Ilboru Sec
Ndanda Sec........(Catholic School)



Una wazimu...?
 
BARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limethibitisha kuwa lina mpango wa kuhamisha makao yake makuu kutoka Kurasini jijini Dar es salaam kwenda Dodoma. Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais wa TEC ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya, wakati wa Misa Takatifu ya kilele cha jubilei ya miaka 100 ya upadri Tanzania, iliyofanyika katika kituo cha hija cha Mbwanga, Dodoma.

Akitoa salamu za TEC katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya waamini, Askofu Kinyaiya amesema kuwa baraza lina mpango wa kuhamisha makao yake makuu yaende Dodoma na mchakato huo utaanza baada ya kufanya mazungumzo na serikali ya kupata ardhi itakayotumiwa na shughuli za TEC.

“Tuna mpango wa kuhamisha makao yetu makuu yaje Dodoma. Bado tunaongea na serikali ili tupate kipande cha ardhi, ambapo leo pia tumebariki jiwe la msingi la kikanisa kitakachojengwa mahali hapo” ameeleza Askofu Kinyaiya.

Kwa upande wake mwakilishi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe hizo, ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene, ametoa agizo kwa serikali ya Mkoa wa Dodoma ihakikishe inafanya mazungumzo na TEC ili ndani ya siku 10 kiwanja kiwe kimepatikana kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Makao Makuu ya TEC.
“Maamuzi ya kubariki jiwe la msingi la kikanisa cha TEC kama ishara ya kuhamia Dodoma ni ujumbe mzito sana kwa serikali ya awamu ya tano na serikali ya Dodoma. Ninaagiza ndani ya siku kumi zoezi la upatikanaji wa kiwanja sehemu wanapohitaji liwe limekamilika. Sisi tutawapa kila aina ya msaada kwa haraka, nasi wana Dodoma tutoe ushirikiano” ameeleza.
Awali akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Mkoa huo Jordan Rugimbana amesema kuwa TEC imebariki wazo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli la kuhamishia Makao Makuu ya nchi mkoani Dodoma.
Aidha Rugimbana amesema kuwa serikali ya mkoa huo itatoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu hayo mapya ya TEC.
Hivi Kanisa Katoliki linamiliki ardhi kiasi gani hapa nchini?
 
Kwa hiyo mnataka maaskofu katoliki wawasaidie AMA? Wenzenu wamepewa ardhi nyie bado mko usingizini na EAMWS, mkiamka wenzenu wanafungua vyuo vikuu,mnabakia kulaumu serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu jifunze kusoma between the lines. Mimi nimeeleza fact ya historia. Hakuna anayelaumu hapa and im not a Muslim. Lakini muhimu ujue hapa maendeleo yeyote yanatokana na uratibu wa Uongozi. taasis ya waislam ndio hiyo bakwata ambayo ni mkono wa serikali. Taasis zingine zinapopigania masuala hayo ndio unaona mara kesi ya ponda n.k. Kimsingi hao jamaa wameshapigwa kabali kitambo ambayo kujinasua ni issue..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanisa katoliki mna kesi ya kujibu na misalaba minene shingoni isiyokuwa na manufaa kwa watu! Mko kimya kama mmebwi maji mdomoni! Kila kitu kipo sawa na utawala huu, hamna pa kukemea? mbona JK mlimsakama sana au kwa vile ni dini ingine?
Kwani Kanisa wanazuiwa kuhamia Dodoma
 
mimi kama mkatotiki sitachanga hata sumuni. lissu haya mambo ameyakemea. tatizovoa waromz ni kumuona kiongozi mu rc kama hakosei
 
Kanisa katoliki mna kesi ya kujibu na misalaba minene shingoni isiyokuwa na manufaa kwa watu! Mko kimya kama mmebwi maji mdomoni! Kila kitu kipo sawa na utawala huu, hamna pa kukemea? mbona JK mlimsakama sana au kwa vile ni dini ingine?
Zamani nilikuwa najivunia kuwa Mkatoliki, siku hizi navumilia kuwa Mkatoliki. Muda si mrefu nitakuwa Mkatakona.
 
Sasa huu mfano wa waislam kupewa chuo cha Tanesco utatolewa mara ngapi? Huu mfano umesha-expire. Kutuletea mambo yaliyofanyika miaka 15 iliyopita wakat kuna ishu za motomoto za mwaka 2017 ni kutuchezea akili.

Mood swings za kanisa katoliki, kila baada ya miaka 10 lazima zichunguzwe kimakini sana.
xx kuwa 15 miak iliyopita inaondoa ukweli?
uchunguze kanisa wewe km nan,kanisa ni dini pia ni dola uelewe!
usione km unaongea na kina kipozea o ponda!
 
Wasipasuke tu msamba kwa kuiga kunya kwa tembo
Watu hawawezi kuogopa kujaribu kisa wanaogopa kupasuka msamba. La sivyo humu JF kungejaa mabikira, lakin ndo hivyo tena😛.
 
Back
Top Bottom