Baraza Jipya la Mawaziri hili hapa...

Baraza Jipya la Mawaziri hili hapa...

Baraza la zawadi, yaani post zimetengenezwa ili kuwaridhisha watu wachache!! hakukua na haja ya kua na mawaziri wa nchi kibao, ni uvivu, kutokuwajibika na urafiki!! sasa fikiria posho, mashangingi, wakurugenzi, makatibu wakuu, na nyumba ndogo!!! at whose cost? tuna utajiri gani huo wa kugharamia yote haya!!!
 
JK katangaza baraza lake na kumrudisha Sitta kuwa waziri wa Afrika Mashariki na kwatosa Prof Msola, Kapuya na Mwakyusa, pia amemrudisha Pombe Magufuli ujenzi(barabara) na naibu wake kuwa Mwakyembe, cha kushangaza kampa Kombani(Sheria),Ghasia(utumishi) na Shangazi Sofia karudishwa(ustawi na wanawake), kwa mtazamo wangu hapa kachemka, hizi ni wizara nyeti sana hasa sheria na utumishi.

KUNA SIRI GANI KATI YA JK NA SOPHIA SIMBA, MBONA HANA AFANYALO HALAFU KAMRUDISHA? NIMECHUKIA!!!:A S-cry:
 
Kwa hesabu za haraka mawaziri kamili 29 na manaibu 8
 
Mh! HUyo Nchimbi eti kapewa wizara ya habari na michezo, anajua nini kuhusu habari yule jamaa?

unaonekana una chuki za ajabu sana na huyo Nchimbi.............pole bwana usijali ndio maisha muda mwingine usiempenda si mara zote anapata unacopenda wewe apate
 
ujenzi- barabara na viwanja vya ndege.... hakika kipele kimepata mkunaji--- mwakyembe na magufuli ni majembe!
 
Ndugu wadau,

hivi huyu jamaa ana maana gani kumuweka makanga kwenye uwaziri huku anakesi mahakamani? Tena hata yeye mwenyewe anajua hali yake ni mbaya. Ndiyo maana hana ujasiri wowote. Tena kuna uwezekano mkubwa wa uchaguzi kurudiwa. Hii ni kuwaona wananchi wajinga.
 
kuna mtu mwenye simu ya lowasa hapa, au r. Aziz ?tuulizie maoni yao

pamoja na kuwa simpendi mkwere kwa kila jambo analofanya ila kwa hili la wizara ya ujenzi natarajia mabadiliko makubwa sana kwenye mstakabari wa nchi yetu, na kwa mama tibaijuka pia natarajia kuonana maendeleo kwa speed nzuri sana, sijui nani kamshauri kwani nahisi kama siyo yeye aliyefanya hivi.
 
Unmaana baraza tayari limetangazwa , tujuze; source pls!!
 
Kwa hii ya Magufuli na Mwakyembe nategemea kuona flyovers pale dar es salaam
 
Wanabodi,

Hatimaye Baraza jipya la Mawaziri ndio lianza kutangazwa sasa live kupitia TBC!
Endelea kufuatilia...

UPDATES:

  • Wizara ya maji imeunganishwa na Kilimo - Itakuwa Wizara ya Kilimo na umwagiliaji!
  • Kazi ajira na vijana - kitengo cha vijana kimehamishiwa michezo na utamaduni
  • Uwezeshaji wa wananchi (Baraza la uwezeshaji) - Ilikuwa wizara ya fedha, imebidi kuipunguzia Hazina mzigo huu na kulielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Waziri wa TAMISEMI atakuwa na manaibu wawili
  • Wizara ya Miundo Mbinu imepunguzwa, imegawanyika kuwa na Wizara ya Ujenzi (barabara na viwanja vya ndege) & Wizara ya Uchukuzi - Reli, bandari na usafiri wa majini
  • Magufuli atachukua wizara ya Ujenzi na msaidizi wake ni Mwakyembe
  • Sitta atakuwa waziri wa Wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki
  • Membe ataendelea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje
  • Ngeleja ataendelea kubaki wizara ya Nishati na Madini
  • Wizara ya Mambo ya Ndani atakuwepo Nahodha akishirikiana na Kagasheki
  • Anna Tibaijuka atakuwa waziri wa Wizara ya Ardhi na Makazi
  • Hakuna jina la Januari Makamba wala Lowassa kama wengi walivyokuwa wakishuku
WIZARA NA MAWAZIRI WAKE:
) Wizara ya ofisi ya utawala bora chikala
2) Wizara ya Mahusiano wassira
3) Wizara ya manegement – hawa ghasia
4) Wizara ya makamu wa rais – samia suluhu hassan
5) Wizara ya mazingira - therezia
6) Wizara ya waziri mkuu – william lukuvi
7) Wizara ya uwezeshaji nagu
8) Wizara ya tawala za mkoa mkuchika
9) Wizara ya fedha mkula, teu, amisilima
10) Wizara ya mambo ya ndani nahoza, kagasheki
11) Wizara ya katiba na sheria Kombani
12) Wizara ya nje membe
13) Wizara ya ulizi mwingi
14) Wizara ya mifugo mathayo d. Athayo
15) Wizara ya mawasiliano science makame, kitwanga(mawe matatu)
16) Wizara ya ardhi prof. Tibaijuka
17) Wizara ya maliasili maige
18) Wizara ya nishati ngeleja, malima
19) Wizara ya ujenzi Magufuli, Mwakyembe
20) Wizara ya uchukuzi Omary N
21) Wizara ya Viwanda na Biashara Chami-
22) Wizara ya Elimu Dk Kawambwa
23) Wizara ya Afya Hadji H Mpanda
24) Wizara ya Kazi Ajira Kabaka, Mahanga
25) Wizara ya Maendeleo ya jamii Sophia SImba
26) Wizara ya Elimu habari vijana na michezo Nchimbi
27) Wizara ya Ushirikiano EAC Sitta
28) Wizara ya Kilimo Magheme, Chiiza
29) Wizara ya Maji Prof Mwandozya

Inaelekea ulikuwa na haraka ya kutafuta sifa ya kuwa the 1st to post, jamani wizara ya makamu wa Rais, na wizara ya waziri mkuu?????? Hapana hizo hazipo na wala kikwete hajazitangaza. Samia ni waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa rais, muungano, Na Lukuvi ni waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia masuala ya Bunge.
 
Zitto tena? mwacheni zitto wetu na chadema yetu akiingia humo unafikiri pinda atakula wapi?unafikiri akiingia ccm si ajira za wengi zitakuwa matatani? je watamfanya nini?
 
Back
Top Bottom