Baraza Dogo la Mawaziri na Muundo wa Wizara

Unaleta unazi hata kwenye serious issues ?John ame suggest na wewe unaweza kusema yako hajakulazimisha wala JK hajapewa amri.Why jump to conclude ?

HUYU PUNDAMILIA NAYE NA MAMBO YAKE YA VYAMA!

Wakuu Lunyungu na jmushi1
Najua ninyi ni wepesi wa kujibu lakini ninawashauri pia muwe wepesi wa kuelewa mambo.
Swali langu ambalo nilikuwa ninahitaji ufafanuzi nililielekeza mahususi kwa John na amelitolea majibu mazuri kabisa.
Next time mjitahidi kusoma na kuelewa.
 
Nakubaliana kabisa na nia za kuwepo kwa baraza dogo la mawaziri. Kwa kweli JK alichemsha alipounda baraza na kuongeza ukubwa. Kwa hiyo tuki rudi kwenye muundo unaopendekezwa na JMnyika, bado nina matatizo na wizara kadhaa
Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma! Huyu waziri hana kazi, kwani hakuna siasa kwenye utumishi wa umma. Hotuma yake ya bajeti ni mishahara ya watumishiwa umma! Ilichofanikiwa kufanya ni kuua nguvu za vyama vya wafanyakazi. Hii irudi iwe Idara chini ya ofisi ya Rais.

Wizara za maji, mazingira, maliasili na ardhi. Hakuna sababu zozote za kufanya ziwe tofauti. Shughuli nyingi za wizara ya ardhi zinafanywa na halmashauri wizara inaongeza urasimu na kupeleka huduma mbali na wananchi. Wizara hizi zote zina jihusisha na menejimenti ya ardhi na kunaoverlap na migongano mingi. Wazuri mmoja ataweza kuweka muelekeo na haswa kupeleka shughuli nyingi za wizara halmashauri
 
Aisee Mnyika,pongezi nyingi zikufikie kwakua umesema kitu ambacho hata mimi nilikifikiria.Utitiri wa mawaziri sio uwezo suala ni uwezo wa hao walioteuliwa kutatua matatizo ya watanzania. CHONDE JK,PUNGUZA HILO BARAZA LIJALO.
 
Nakubaliana kabisa na nia za kuwepo kwa baraza dogo la mawaziri. Kwa kweli JK alichemsha alipounda baraza na kuongeza ukubwa. Kwa hiyo tuki rudi kwenye muundo unaopendekezwa na JMnyika, bado nina matatizo na wizara kadhaa
Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma! Huyu waziri hana kazi, kwani hakuna siasa kwenye utumishi wa umma. Hotuma yake ya bajeti ni mishahara ya watumishiwa umma! Ilichofanikiwa kufanya ni kuua nguvu za vyama vya wafanyakazi. Hii irudi iwe Idara chini ya ofisi ya Rais.

Wizara za maji, mazingira, maliasili na ardhi. Hakuna sababu zozote za kufanya ziwe tofauti. Shughuli nyingi za wizara ya ardhi zinafanywa na halmashauri wizara inaongeza urasimu na kupeleka huduma mbali na wananchi. Wizara hizi zote zina jihusisha na menejimenti ya ardhi na kunaoverlap na migongano mingi. Wazuri mmoja ataweza kuweka muelekeo na haswa kupeleka shughuli nyingi za wizara halmashauri na sekta binafsi
 
Mh Ukweliii, unajua hata huyu aliyekua waziri wa ajira,kazi na maendeleo ya vijana hatakiwi kurudi kwani alichowafanyia wafanyakazi Tz sio kizuri.
 
Yohana wa Mnyika,

Je umeridhika na muundo huu mpya? Je kipaumbele kwa 80% walioko vijijini kwa kuwa na wizara takribani tatu kuangalia maswala yao ni bora?

Binafsi kuweka msukumo kwenye Kilimo na Chakula, Mifugo na Uvuvi na Maji na Umwagiliaji ni ishara kuwa JK anaweza kuwa anabadilisha mwelekeo na kurudi kwenye Uchumi asili wa Uzalishaji mazao ambao Watanzania wengi watachangia uazalishaji mali na kunufaika.

In fact kupelekwa Mwandosya, Magufuli na hata Msolla, kunania tumaini!
 
Nakubaliana kabisa na nia za kuwepo kwa baraza dogo la mawaziri. Kwa kweli JK alichemsha alipounda baraza na kuongeza ukubwa. Kwa hiyo tuki rudi kwenye muundo unaopendekezwa na JMnyika, bado nina matatizo na wizara kadhaa
Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma! Huyu waziri hana kazi, kwani hakuna siasa kwenye utumishi wa umma. Hotuma yake ya bajeti ni mishahara ya watumishiwa umma! Ilichofanikiwa kufanya ni kuua nguvu za vyama vya wafanyakazi. Hii irudi iwe Idara chini ya ofisi ya Rais.

Wizara za maji, mazingira, maliasili na ardhi. Hakuna sababu zozote za kufanya ziwe tofauti. Shughuli nyingi za wizara ya ardhi zinafanywa na halmashauri wizara inaongeza urasimu na kupeleka huduma mbali na wananchi. Wizara hizi zote zina jihusisha na menejimenti ya ardhi na kunaoverlap na migongano mingi. Wazuri mmoja ataweza kuweka muelekeo na haswa kupeleka shughuli nyingi za wizara halmashauri na sekta binafsi



kwa kweli kazi ya kugawa wizara kwa nchi maskini na zenye diversity kibao ni kazi ngumu sana!!!hata hiyo classification ya Yohana haiwezi kukidhi mahitaji ya watu kama mnavyo isisifu. kwa nchi kama yetu ugawaji wa wizara hauzingatii majukumu ya serikali peke yake, ila sababu zingine nyingi na muhimu kama uwakilishi wakigeographia, makundi pamoja na misukumo ya kisiasa iliyopo. jaribuni kupitia kitabu cha Richard, Scott huyu ni classical writter wa public administration na amejishughulisha sana na structure of governmnet.

kwa kifupi bidii hii ya kutaka kuwa na wizara fixed ni nzuri ila kwa watanzania naona muda bado. ....... we have a long way to go before comparing our bureaucracy with the old bureaucracies of the developed world. sisi public administration yetu bado iko mbali kutoka ile ya weberian ambayo kwa kiasi kikubwa ndio iliyoshamiri kwenye nchi zilizo endelea.
 
Hapa tunakumbuka shuka wakati tayari kumekucha, kwani JK kasheamua kugagana vyeo na kuendelea kutupa mzigo mzito sana .

Nafikiri hapa jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa tunalijadili baraza hili na mafisadi wote wawekwe hadaharani na wawajibike ama wawajibishwe na nguvu ya ummma .
 
Msingi wa utendaji bora wapasa kuwa kwenye kurugenzi imara ambazo huundwa kuzingatia umuhimu wake na vigezo maalum. HIzi lazima zijengewe hoja bungeni na kupitishwa kisheria kama tukiwa na bunge makini. Kadhalika wizara zipi zisimamie kurugenzi zipi lazima zipendekezwe, zijadiliwe na kupitishwa bungeni. Waziri ana kazi ndogo sana kama mshauri wa kabibu wa raisi katika maswala ye sekta husika kama kurugenzi imara zipo na zinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa kisheria. Ufisadi wooote tunaoshuhudia ni matokeo ya mawaziri kujigeuza wakurugenzi kila wanavyojisikia kwa maslahi binafsi. Tukiwa na kurugenzi makini idadi ya wizara twahitaji ndogo sana. 15 ni nyingi.

Ikumbukwe mfumo wetu wa utawala huwapa mawaziri maslahi ya juu na kupita watendaji wote na pia mamlaka na nguvu kisheria ya kuingilia na kuvuruga utendaji wa kurugenzi. Baraza likiwa dogo inapunguza idadi ya wavurugaji.

Kama kweli mawaziri ni washauri wa raisi wa karibu basi wanapaswa kuwa wachache ili aweze kushauriana nao kikamilifu. Wakiwa wengi raisi anakuwa na mawaziri ambao hushauriana nao na wengine humuona tu kwenye vikao na wengine wanaanza hata kuingilia utendaji wa wizara nyingine. Matokeo ni ufisadi kutukuzwa.

Kila muundo mpya wa baraza hufuatwa na kipindi kirefu cha kujipanga na matumizi hovyo ya pesa kujenga au kukarabati majengo na ununuzi wa samani ambavyo hutoa mwanya wa ufujaji na utapeli. Mara nyingi wizara zimeundwa kwa sura ya kumpatia mtu wadhifa na ulaji badala ya utoaji huduma. Hii inaletapelekea wizra moja kuwa na manaibu waziri kadhaa(mzigo usio lazima)Mfano unakuwa na wizara za kilimo lakini na chakula, mifugo, umwagiliaji badala ya moja tu yenye kurugenzi imara zinazosimamia utendaji kitaaluma. Kilimo wanahimiza matumizi ya samadi na kutumia wanyama kazi bila kuwa na wataalamu wa aina ya wanyama na matunzo yake. Tuanjenga tu mivutano. Kilimo anataka kumwagilia lakini mifugo wanataka njia kwenda malishoni na wa umwagiliaji wanasema sasa hivi tunashughulikia ukanda fulani tu kitaifa. Baada ya muda mfupi tunapangua na kuanza tena moja. Hapna tuache. Raisi abaki na uhuru wa kuteua mawaziri lakini idadi ya wa aina ya wizara ziamulike Bungeni kwa kuzingatia usharui wa wataalamu husika kisheria.
Kisingov
 
Rev Kishoka,
In fact kupelekwa Mwandosya, Magufuli na hata Msolla, kunania tumaini

Hata mimi nilifikiria hivyo mwanzoni lakini nikajirudi baada ya kugundua kwamba watu hawa hawa walishindwa kukamilisha waliyopewa mwanzo kwa sababu pakacha letu linavuta sehemu muhimu zaidi.. Wizara ya fedha, Benki kuu, TRA, Bandari, Utalii, Madini na kadhalika. Hizi ni sehemu zinazotuingizia fedha sana na ndizo pekee zinazo weza kutupa mtaji wa kufufua KILIMO...
Sasa basi ikiwa utawaweka wataalam ama watu unaowaamini ktk sehemu zinazotegemea zaidi uimara wa wizara na Taasisi zinazoendesha mtaji wetu sidhani kama dhana yake itamfikisha popote!..
.
Kuwaachisha kazi viongozi kina Lowassa, Mama Meghji na kadhalika sio somo kabisa kwa hawa waliopo leo madarakani isipokuwa inatia moyo zaidi wa CHUKUA CHAKO MAPEMA...
Hawa pia watachukua chao na kufungua Biashara kabla ya miaka mitatu ijayo wakiwa na hofu ndogo ya kujiuzuru ama kuwekwa pembeni 2010...
Kwa hiyo swali kubwa la viongozi (from CCM) ni, umeweza chukua nini ktk wakati uliopewa?...Hapa hakuna cha kilimo wala mjomba wake.
 
Marekebisho kidogo ktk usemi wangu uliotangulia..
Naposema CHUKUA CHAKO MAPEMA sina maana ya viongozi wazuri kama kinndosya na Magufuli ila nina maana ya kuwa wale waliopewa nafasi za wizara ama Taasisi ambazo ndizo zinaingiza fedha zaidi... Ni hatari kubwa sana kwa viongozi kuendelea kufanya biashara chini ya kivuli cha Azimio kwani ni wachache watakao kuwa na moyo wa Uzalendo hasa pale wanapoona kina Lowassa na wengineo wamepita salama na sasa hivi wamejituliza Beach huko Zenj wakitumbuizwa na Sauti za Busara.
Kwa raha zao..
 
Rev Kishoka,


Hata mimi nilifikiria hivyo mwanzoni lakini nikajirudi baada ya kugundua kwamba watu hawa hawa walishindwa kukamilisha waliyopewa mwanzo kwa sababu pakacha letu linavuta sehemu muhimu zaidi.. Wizara ya fedha, Benki kuu, TRA, Bandari, Utalii, Madini na kadhalika. Hizi ni sehemu zinazotuingizia fedha sana na ndizo pekee zinazo weza kutupa mtaji wa kufufua KILIMO...
Sasa basi ikiwa utawaweka wataalam ama watu unaowaamini ktk sehemu zinazotegemea zaidi uimara wa wizara na Taasisi zinazoendesha mtaji wetu sidhani kama dhana yake itamfikisha popote!..
.
Kuwaachisha kazi viongozi kina Lowassa, Mama Meghji na kadhalika sio somo kabisa kwa hawa waliopo leo madarakani isipokuwa inatia moyo zaidi wa CHUKUA CHAKO MAPEMA...
Hawa pia watachukua chao na kufungua Biashara kabla ya miaka mitatu ijayo wakiwa na hofu ndogo ya kujiuzuru ama kuwekwa pembeni 2010...
Kwa hiyo swali kubwa la viongozi (from CCM) ni, umeweza chukua nini ktk wakati uliopewa?...Hapa hakuna cha kilimo wala mjomba wake.

Bob Mkandara,

Mara nyingine, inabidi tujiulize viranja wanaweza kufanya kazi vizuri zinazoonekana kuwa njema ikiwa Kiranja Mkuu ni mbabe na kila siku kufukia sauti za viranja wengine kwa Mwalimu Mkuu?

Mwandosya na Magufuli, ni wachapa kazi. Sina uhakika sana na Msolla kutokana na kushindwa kuongoza Wizara iliyopita. Swali ni hivi, ukiondoa utashi wa siasa na woga wa kuvuma kwa hawa jamaa kisiasa na utendaji, Wizara walizopewa ni muhimu sana kwa Taifa letu na nashukuru Mungu kuwa wamepewa hawa jamaa na si wababaishaji wengine.

Uvuvi na Mifugo, Maji na Umwagiliaji na Kilimo na Chakula. Hizi ni wizara nyeti sana kwa maendeleo ya Taifa na nina matumaini makubwa kuwa in long term, tutaona mafanikio ya utendaji na uongozi wa hawa jamaa kwa hizi wizara.
 
Nakusikia mkuu wangu na nakubaliana na maneno yako isipokuwa labda sikueleza vizuri hapo mwanzo...
Chukulia hili sakata la Richmond na BoT yote yamewahusisha viongozi MAWAZIRI... ambao baada ya kuiba pengine kila mmoja wao ni Millionea leo hii kwa kuhujumu uchumi wa nchi..Tazama adhabu zao basi?... Wamestaafishwa kazi!...lakini watakula ruzuku zao kama kawaida.
Kwa hiyo, hawa wote waliochaguliwa sasa hivi watakuwa na funzo moja kubwa sana nalo ni chukua chako mapema kisha ukikamatwa utastaafishwa kazi bila kufika mahakama wala kupoteza mamillioni uliyopoteza..
Hivyo basi kila mmoja wao atajaribu kuchuma mapema kabla ya 2010, na hao mawaziri wazuri kama Magufuli na huyo Mwandosya watapata wapi fedha za kuendeleza miradi hiyo unayoisema?...
Bila kuwaadhibu viongozi waliotuibia badala yake JK kawatetea kuwa walikuwa ni viongozi wazuri sana maneno mazito na tofauti kabisa na ilani ya chama chake wala ya Kitaifa... Hapo uncle bado una tegemeo na hawa watu wawili sijui watatu ambao wamewekwa kama kichombezo?
 
Wakati macho na masikio ya watanzania wengi ni kusubiri kwa hamu kuhusu “Nani na Nani’ watakuwepo kwenye baraza na watakuwa ‘wapi’; mjadala wa MUUNDO umetawaliwa zaidi na kutazama “sura”. Mjadala wa “watu’, MODS napendekeza uendelee katika ile thread ya “uchambuzi kuhusu baraza la mawaziri”; hii iachwe pekee kwa lengo la kujadili ‘masuala’ ya ukubwa wa baraza lenyewe na mpangilio wa wizara. Wakati “sura” ni suala la muhimu sana la kwanza kabisa kabla ya ‘mfumo’ mzima, ni muhimu pia tujadili muundo wa baraza kwa maana ya mpangilio wa wizara na idadi ya wizara. Sauti ya umma kupitia kwa wapinzani, asasi za kiraia, wasomi nk wakati wote zimekuwa ni ‘tunataka baraza dogo la mawaziri lakini lenye ufanisi’. Swali la kujiuliza- ni baraza dogo kiasi gani? Mwaka 2005 ‘war room’ ya CHADEMA tuliwahi kukaa chini na kuanza kutafakari- kama tungeshinda nchi na kuongoza dola- tungetekeleza vipi sera yetu ya kuwa na “mfumo mpya wa utawala” ambao pamoja na mambo mengine ungekuwa na ‘small but yet accountable and effective government’? Wakati huo tulitengeneza Muundo wa Baraza Dogo ambalo mawaziri walikuwa takribani 15 tu. Huku nilipo, nimeshindwa kuipata ile nyaraka ya ndani ya mapendekezo ya wakati huo. Lakini nimeona bado ni vyema nikachokoza mjadala huu kwa mawazo yangu binafsi.

Naanzia na dhana kwamba sikubaliani na muundo wetu wa sasa wa Baraza lenye Mawaziri takribani 29- hili ni kubwa sana. Hata Uingereza ambao wana idadi kubwa ya watu na fedha nyingi na ndio ambao wanachangia bajeti yetu kwa kiasi kikubwa ikiwemo bajeti ya mishahara tunayowalipa mawaziri wetu- wamejipangia kabisa wizara zisizidi 20. Kama Waziri mkuu anataka kuongeza ya 21 inabidi aombe kibali maalumu. Na wizara yoyote zaidi ya hapo basi waziri mkuu anaigharamia mwenyewe kwa fedha zake. Sisi sasa tunazo 29 na Jeshi la manaibu kibao. Kwa kauli ya Waziri Mkuu Pinda inaelekea JK atakubaliana na wazo la wapinzani na wananchi kwa ujumla la kupunguza baraza la mawaziri. Je, apunguze kwa kiasi gani? Huu ndio mjadala wa hapa-

Kwa maoni yangu- atoke toka Wizara 29 mpaka Wizara zisizozidi 10; kwa maneno mengine apunguze wizara takribani 10 katika hatua ya sasa. Afanye namna gani?

Kwanza aamue kabisa kwamba Yeye asiwe Waziri wa Wizara yoyote- huu muundo wa baadhi ya Wizara kuwa Ofisi ya Rais unamfanya Rais ajiingize katika kazi za Uwaziri bila sababu yoyote ya msingi. Rais yeye awe Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri tu na mwongozaji mkuu wa Wizara zote. Nakumbuka wakati wa Rais Mkapa alikuwa pia Waziri wa TAMISEMI, matokeo yake ilikuwa ni aibu ya moja kwa moja kwa Rais kwa kuwa alikuwa ndiye msimamizi mkuu wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2004! Sasa TAMISEMI ilikuwa kwa waziri mkuu lakini bado, kuna mawaziri waliokuwa katika ofisi ya Rais.

Pili, nashauri baadhi ya wizara ziunganishwe kama nitakavyopendekeza na baadhi ya Wizara kwa kweli zilikuwa hazistahili kuwa Wizara kabisa; labda ziwe idara tu katika wizara Fulani Fulani. Kwa ujumla sitapendekeza wizara ziitwejwe, lakini nitaunganisha zaidi yale majukumu ili kujua ni yapi waziri anayependekezwa atahusika nayo. Baada ya kukubaliana MAJUKUMU- ndio suala la JINA LA WIZARA linafuata halafu ndio JINA LA WAZIRI:

Mapendekezo yangu ya Wizara 19:

1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano
2. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Afrika Mashariki( ingekuwa vyema masuala ya Afrika ya Mashariki yakawa kwenye mahusiano ya Kimataifa- hata hivyo, kuna azimio nakumbuka liliwahi kupitishwa na EAC kwamba kila nchi inapaswa kuwa na Wizara mahususi ya Afrika Mashariki).
3. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma
4. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)- chini ya D&D, wizara hii ni kiungo muhimu katika ya serikali kuu na serikali za mitaa.
5. Wizara ya Mambo ya Nje(na Mahusiano ya Kimataifa)
6. Wizara ya Ulinzi( Na jeshi la Kujenga Taifa)
7. Wizara ya Uchumi na Fedha(na mipango)- hapa napendekeza wizara mbili ziunganishwe
8. Wizara ya Mambo ya Ndani( Na usalama wa Raia)- hapa napendekeza wizara mbili ziunganishwe
9. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Ushirika( na Chakula)- Hapa napendekeza Wizara mbili ziunganishwe.
10. Wizara ya Maliasili na Utalii( pamoja na kuwa ni rahisi kushawishika kuunganisha mazingira hapa, lakini kwa unyeti wa sekta ya utalii katika uchumi wa taifa siku za usoni ni vyema majukumu yakaishia hapo tu).
11. Wizara ya Miundo Mbinu- hii itajumuisha pia masuala yote ya ujenzi wa barabara na mawasiliano, unaweza kushawishika kuingiza hapa pia nyumba na makazi lakini mzigo utakuwa mkubwa sana.
12. Wizara ya Maji, Nishati na Madini- hapa wizara mbili zimeunganishwa. Maji ni sekta ambayo ingeweza kuingia katika wizara kadhaa nyingine mathalani kilimo, maliasili ama ardhi lakini hapa inaweza kukaa vizuri zaidi.
13. Elimu na Teknolojia- hapa imeunganisha wizara mbili, ya elimu na ufundi stadi na ile ya elimu ya juu; ni vyema masuala yote ya elimu yakakaa mahali pamoja.
14. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Vijana na Watoto- hapa nimeunganisha Wizara moja pamoja na sekta ya vijana ambayo awali ilikuwa Wizara ya Kazi na ajira.
15. Wizara ya Afya(na ustawi wa jamii)- ni vyema kutakakari kuurudisha ustawi wa jamii kwenye wizara ya maendeleo ya jamii.
16. Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko
17. Wizara ya Ardhi, Makazi(Nyumba) na Mazingira- hapa nimeunganisha Wizara na Waziri mwingine ambaye alikuwa ofisi ya Makamu wa Rais.
18. Habari, Utamaduni na Michezo- Kuna hoja kwamba utamaduni ukae kwenye elimu; na habari iwe kitengo tu kama MAELEZO au IKULU na michezo iwekwe karibu na wizara yenye Vijana. Hata hivyo, kwa umuhimu wa Utamaduni kwa Taifa; na fursa ya Michezo kuwa sekta ya muhimu katika uchumi- haya mambo ni vyema yakapewa uzito unaostahili. Na ukishakuwa na wizara hiyo, ni rahisi kuunganisha na habari hapo hapo.
19. Kazi, (Ajira na Uwezeshaji)- ni rahisi kuiacha hii wizara ikawa ya masuala ya Kazi(Labour pekee) na masuala ya ajira(employment) ukayepeleka kwenye uchumi au ukayaacha kuwa mtambuka(cross cutting katika kila wizara). Lakini kwa hali ya uchumi wetu wa sasa wa kutegemea wageni na kuwaweka mstari wa mbele wageni- tunahaja ya kuwa na wizara ambao inalinga maslahi na kuendeleza maslahi. Kama Afrika Kusini walivyokuwa na sera/sheria ya ‘black empowerment”, hapa napo tunahitaji kwa muda kulipa kipaumbele suala la UWEZESHAJI. Wizara hii inaweza kuondolewa masuala ya uwezeshaji baadaye ikabaki na KAZI pekee.

Kwa mapendekezo haya:

Wizara ya Sheria na Katiba inafutwa badala yake majukumu yake ya kiutendaji yanapelekwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni sehemu ya Baraza la Mawaziri. Na majukumu ya Usimamizi wa Sheria yanabaki kwa Mahakama. Majukumu ya kusimamia HAKI, yanabaki chini ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Waziri wa Nchi-Utawala Bora anafutwa- Majukumu ya kusimamia utawala bora kwa maana ya uongozi yanabaki wa Rais Mwenyewe. Kwa maana ya Kulinda utawala bora, yabaki kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Sekretariati ya Maadili ya Watumishi wa Umma; Masuala ya Usalama wa Taifa yanabaki kwa Rais Mwenyewe. Masuala ya TAKUKURU inabidi kubadili sheria kukifanya kuwa chombo huru zaidi baada ya kusimamiwa na Waziri kwa maelekezo ya Rais.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Bunge, anafutwa; masuala ya Bunge ashughulikie Waziri Mkuu mwenyewe ili kuongeza uwajibikaji.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Siasa na Uhusiano wa Jamii anafutwa- Wizara hii haikuwa na sababu yoyoye ya kuwepo, ilianzishwa kisiasa kwa lengo la kumpa nafasi Kingunge kuwa karibu na Rais, kuuingiza kwenye Baraza la Mawaziri na kupata fursa ya kuropoka hadharani masuala ya kisiasa na uhusiano wa kijamii. Kazi ambayo hata yenyewe ameshindwa kuifanya! Hivyo, anapaswa kuondoka yeye na wizara iliyoazishwa kwa ajili yake. Majukumu haya ya siasa na uhusiano na jamii ni mambo ya kawaida ya ofisi ya Rais hayahitaji kuundiwa Wizara.

Huu ndio muundo wa Baraza Jipya la Mawaziri 19 tu ninalopendekeza lijadiliwe. Katika hali hii, manaibu nao wanapaswa kupungua kabisa, na ikiwezekana baadhi ya Wizara zisiewe kabisa na manaibu. Kama Manaibu sio wajumbe wenye kura wa Baraza la Mawaziri, wanafanya nini? Kwa nini wasiwe under secretaries tu?

Haya ni maoni yangu binafsi, tujadili- tunataka Baraza la Mawaziri dogo na lenye ufanisi kiasi gani?

Mnyika wasalaam

Kwanza nakupongeza kwa kujaribu kuibua mjadala huu kwani ndo wakati wenyewe.Tunapokua na mawaziri wengi automatically gharama za kuendesha wizara hizo ni kubwa na cha kusikitisha hapa kwetu haziendani na matunda ya wizara husika.Naunga mkono tuwe na wizara chache makini na mawaziri wenye wito kweli wa kutumikia wananchi.Unaweza pia kuwa na wizara chache but mambo yasiende kama mawaziri hawatakua commited vya kutosha.
 
John Mnyika,

Mulifanya kazi nzuri, nakubaliana na wewe kwa asilimia kama 70%, lakini asilimia 30% hapa...nitaijibu kwa kuweka mbadala wake....

Mapendekezo yangu ni Haya

ORGANIZATION OF THE GOVERNMENT OF THE REPUBLIC OF TANZANIA

-Ofisi ya Rais
-Ofisi ya Makamu wa Rais
-Ofisi ya Waziri Mkuu

-Wizara ya TAMISEMI ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu
-Wizara ya Fedha
-Wizara ya Mipango na Uwezeshaji [Planning and National Development]
-Wizara ya Afya
-Wizara ya Uchukuzi, barabara na Ujenzi
-Wizara ya Elimu na Ufundi
-Wizara ya Elimu ya Juu, Science na Technologia
-Wizara ya Kilimo
-Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi (Livestock and fisheries development)
-Wizara ya Mambo ya Nje
-Wizara ya Regional Affairs (East Africa and SADC)
-Wizara ya Justice and Constitutional Affairs (ikumbukwe uendeshaji wa mahakama administratively uko hapa)
-Wizara ya Jinsia, Michezo, Utamaduni na Ustawi wa Jamii
-Wizara ya Habari na Mawasiliano (Information anc Communications)
-Wizara ya Nishati na Madini
-Wizara ya Utalii na Wanyama Pori
-Wizara ya Maji na Umwagiliaji (Water and Irigation)
-Wizara ya Ushirika, Biashara na Masoko (co-operatives, industry and trade)
-Wizara ya Mali asili na Mazingira (Natural resource and Environment)
-Wizara ya Ardhi na Nyumba
-Wizara ya Kazi na Ajira (Labour and Human Resources Development)​
-Mwanasheria Mkuu [State Law Office)
-Mahakama (Judiciary)
-Tume ya Uchaguzi [National Electrol Commission]
-Tume ya Haki za Binadamu
-Tume ya maadili ya viongozi na utawala bora [commission for national ethics and good governance]
-Tume ya Utumishi [comming soon to Tanzania]
-Mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali [National Audit General Office]
-Bunge la Jamhuri [National Assembly]
-Taasisi ya PCCB


Maelezo ya Ziada
-Ustawi wa Jamii umepelekwa kwenye gender, sports, cultural and social affairs
-Mawasiliano imeondolewa kwenye miundo mbinu kwa kuwa kwa mfumo wa sasa haitendewi haki, information [maelezo] imeunganishwa na mawasiliano kuunda wizara.
-Hakuna waziri utawala bora, bali kuna tume ya maadili na utawala bora
-Hakuna waziri anayehusika na Utumishi, kwani kutaundwa tume ya utumishi wa umma.
-Wizara ya Maji, imewekewe na Umwagiliaji
-Wizara ya Kilimo ni wizara likubwa mno limebaki lenyewe
-Mifugo imeongezewa Uvuvi kwa ajili ya ku-take advantage ya mali asili hii tunayoichezea.
-Utalii na Wanyama Pori [Tourism and Wildlife Development], Mali asili sio mahali pake.. Utalii ili upate msukumo... ukiangalia vizuri uvuvi umeondolewa hapa.
-Mali asili sasa iko na Mazingira... in short... unatakiwa kumtoa Mh. Mark Mwandosya kutoka kwenye makamu wa raisi umpe mazingira na mali asili.

Niko tayari sasa kuchukua maswali yenu.


Wizara ya Mambo ya ndani na usala wa raia hujaitaja au macho yangu??????????
 
Wooote mna mawazo madogo baada kusema kurekebisha mawaziri kwanza huyu hafai huyu anafaaa matokeo yake mnapanga wizara hii kazi siyo yenu ni ya waziri mkuu na mkuu wa nchi.
 
Kama watu wanaofanya kazi za umma wengi wangekuwa proactive katika kutimiza wajibu wao, basi idadi ya mawaziri ingeweza kuwa ndogo bila tatizo lolote.Isipokuwa pia ni lazima tukumbuke kuwa wengine wapo ndani ya nafasi ambazo zimetengenezwa ili baadhi ya waliohadiwa hafasi hizo wapate kazi
 
Hoja ni nzuri sana ila naelewa kwamba baraza la mawaziri siku zote litaendana na ilani ya uchaguzi ya chama kilichoshinda uchaguzi.serikali ipo kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama kilichochaguliwa na wananchi.
 
mimi ninapendekeza wizara kumi na tano za msingi na majina yake.
wizara zenyewe ziwe kama hivi ifuatavyo:

1-wizara ya uchumi na mapato ya taifa
2-wizara ya rasilimali na maliasili
3-wizara ya demokrasia na muungano
4-wizara ya sheria na haki

5-wizara ya ulinzi
6-wizara ya miundo mbinu
7-wizara ya uwezeshaji na uwekezaji
8-wizara ya chakula na afya
9-wizara ya mambo ya kimataifa
10-wizara ya mafuta na umeme
11-wizara ya elimu na tekinolojia
12-wizara ya utamaduni na michezo
13-wizara ya kazi na maendeleo ya vijana
14-wizara ya jamii na watoto
15-wizara ya mambo ya ndani


Hii nimeikubali mkuu. Sasa tuangalie vichwa vitakavyopewa ulaji kwenye hizi wizara zako

1-wizara ya uchumi na mapato ya taifa-Waziri Kihiyo Mkulo
2-wizara ya rasilimali na maliasili-Anaweza kupewa Makamba
3-wizara ya demokrasia na muungano-Nasikia Tambwe atagombea ubunge anaweza kuzawadiwa hii nafasi

4-wizara ya sheria na haki- Rosti hamu Aziiiiiiii-ziiiii

5-wizara ya ulinzi-Serukamba
6-wizara ya miundo mbinu-Stella Manyanya
7-wizara ya uwezeshaji na uwekezaji- Sofia Simba
8-wizara ya chakula na afya- Aisha Kigoda
9-wizara ya mambo ya kimataifa-Membe
10-wizara ya mafuta na umeme-Mwangunga
11-wizara ya elimu na tekinolojia-Lau Masha
12-wizara ya utamaduni na michezo-Kama kawaida Nchimbi
13-wizara ya kazi na maendeleo ya vijana-Zitto Kabwe (Endapo mpango wake wa kuhamia CCM utakamilika mapema)
14-wizara ya jamii na watoto-Kweygir
15-wizara ya mambo ya ndani-Adam Malima

Manaibu mtanisaidia.............
 
Kazi nzuri sana Kaka yangu Mnyika na pia itakuwa ni vizuri kama mapendekezo kama haya ungeandika kwa rais ay barua kwake ile mwakani mtu yoyote yule anaweza kufanya mambo kama haya kuliko na kuwa baraza au yote haya yaingie kwenye katiba ya Taifa ya nchi maana kila mwaka tumeona kuwa mambo yanabadika kila siku na kufanya au kupoteza resources za taifa la Tanzania
 
Back
Top Bottom