John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 713
- 1,245
Wakati macho na masikio ya watanzania wengi ni kusubiri kwa hamu kuhusu Nani na Nani watakuwepo kwenye baraza na watakuwa wapi; mjadala wa MUUNDO umetawaliwa zaidi na kutazama sura. Mjadala wa watu, MODS napendekeza uendelee katika ile thread ya uchambuzi kuhusu baraza la mawaziri; hii iachwe pekee kwa lengo la kujadili masuala ya ukubwa wa baraza lenyewe na mpangilio wa wizara. Wakati sura ni suala la muhimu sana la kwanza kabisa kabla ya mfumo mzima, ni muhimu pia tujadili muundo wa baraza kwa maana ya mpangilio wa wizara na idadi ya wizara. Sauti ya umma kupitia kwa wapinzani, asasi za kiraia, wasomi nk wakati wote zimekuwa ni tunataka baraza dogo la mawaziri lakini lenye ufanisi. Swali la kujiuliza- ni baraza dogo kiasi gani? Mwaka 2005 war room ya CHADEMA tuliwahi kukaa chini na kuanza kutafakari- kama tungeshinda nchi na kuongoza dola- tungetekeleza vipi sera yetu ya kuwa na mfumo mpya wa utawala ambao pamoja na mambo mengine ungekuwa na small but yet accountable and effective government? Wakati huo tulitengeneza Muundo wa Baraza Dogo ambalo mawaziri walikuwa takribani 15 tu. Huku nilipo, nimeshindwa kuipata ile nyaraka ya ndani ya mapendekezo ya wakati huo. Lakini nimeona bado ni vyema nikachokoza mjadala huu kwa mawazo yangu binafsi.
Naanzia na dhana kwamba sikubaliani na muundo wetu wa sasa wa Baraza lenye Mawaziri takribani 29- hili ni kubwa sana. Hata Uingereza ambao wana idadi kubwa ya watu na fedha nyingi na ndio ambao wanachangia bajeti yetu kwa kiasi kikubwa ikiwemo bajeti ya mishahara tunayowalipa mawaziri wetu- wamejipangia kabisa wizara zisizidi 20. Kama Waziri mkuu anataka kuongeza ya 21 inabidi aombe kibali maalumu. Na wizara yoyote zaidi ya hapo basi waziri mkuu anaigharamia mwenyewe kwa fedha zake. Sisi sasa tunazo 29 na Jeshi la manaibu kibao. Kwa kauli ya Waziri Mkuu Pinda inaelekea JK atakubaliana na wazo la wapinzani na wananchi kwa ujumla la kupunguza baraza la mawaziri. Je, apunguze kwa kiasi gani? Huu ndio mjadala wa hapa-
Kwa maoni yangu- atoke toka Wizara 29 mpaka Wizara zisizozidi 10; kwa maneno mengine apunguze wizara takribani 10 katika hatua ya sasa. Afanye namna gani?
Kwanza aamue kabisa kwamba Yeye asiwe Waziri wa Wizara yoyote- huu muundo wa baadhi ya Wizara kuwa Ofisi ya Rais unamfanya Rais ajiingize katika kazi za Uwaziri bila sababu yoyote ya msingi. Rais yeye awe Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri tu na mwongozaji mkuu wa Wizara zote. Nakumbuka wakati wa Rais Mkapa alikuwa pia Waziri wa TAMISEMI, matokeo yake ilikuwa ni aibu ya moja kwa moja kwa Rais kwa kuwa alikuwa ndiye msimamizi mkuu wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2004! Sasa TAMISEMI ilikuwa kwa waziri mkuu lakini bado, kuna mawaziri waliokuwa katika ofisi ya Rais.
Pili, nashauri baadhi ya wizara ziunganishwe kama nitakavyopendekeza na baadhi ya Wizara kwa kweli zilikuwa hazistahili kuwa Wizara kabisa; labda ziwe idara tu katika wizara Fulani Fulani. Kwa ujumla sitapendekeza wizara ziitwejwe, lakini nitaunganisha zaidi yale majukumu ili kujua ni yapi waziri anayependekezwa atahusika nayo. Baada ya kukubaliana MAJUKUMU- ndio suala la JINA LA WIZARA linafuata halafu ndio JINA LA WAZIRI:
Mapendekezo yangu ya Wizara 19:
1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano
2. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Afrika Mashariki( ingekuwa vyema masuala ya Afrika ya Mashariki yakawa kwenye mahusiano ya Kimataifa- hata hivyo, kuna azimio nakumbuka liliwahi kupitishwa na EAC kwamba kila nchi inapaswa kuwa na Wizara mahususi ya Afrika Mashariki).
3. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma
4. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)- chini ya D&D, wizara hii ni kiungo muhimu katika ya serikali kuu na serikali za mitaa.
5. Wizara ya Mambo ya Nje(na Mahusiano ya Kimataifa)
6. Wizara ya Ulinzi( Na jeshi la Kujenga Taifa)
7. Wizara ya Uchumi na Fedha(na mipango)- hapa napendekeza wizara mbili ziunganishwe
8. Wizara ya Mambo ya Ndani( Na usalama wa Raia)- hapa napendekeza wizara mbili ziunganishwe
9. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Ushirika( na Chakula)- Hapa napendekeza Wizara mbili ziunganishwe.
10. Wizara ya Maliasili na Utalii( pamoja na kuwa ni rahisi kushawishika kuunganisha mazingira hapa, lakini kwa unyeti wa sekta ya utalii katika uchumi wa taifa siku za usoni ni vyema majukumu yakaishia hapo tu).
11. Wizara ya Miundo Mbinu- hii itajumuisha pia masuala yote ya ujenzi wa barabara na mawasiliano, unaweza kushawishika kuingiza hapa pia nyumba na makazi lakini mzigo utakuwa mkubwa sana.
12. Wizara ya Maji, Nishati na Madini- hapa wizara mbili zimeunganishwa. Maji ni sekta ambayo ingeweza kuingia katika wizara kadhaa nyingine mathalani kilimo, maliasili ama ardhi lakini hapa inaweza kukaa vizuri zaidi.
13. Elimu na Teknolojia- hapa imeunganisha wizara mbili, ya elimu na ufundi stadi na ile ya elimu ya juu; ni vyema masuala yote ya elimu yakakaa mahali pamoja.
14. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Vijana na Watoto- hapa nimeunganisha Wizara moja pamoja na sekta ya vijana ambayo awali ilikuwa Wizara ya Kazi na ajira.
15. Wizara ya Afya(na ustawi wa jamii)- ni vyema kutakakari kuurudisha ustawi wa jamii kwenye wizara ya maendeleo ya jamii.
16. Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko
17. Wizara ya Ardhi, Makazi(Nyumba) na Mazingira- hapa nimeunganisha Wizara na Waziri mwingine ambaye alikuwa ofisi ya Makamu wa Rais.
18. Habari, Utamaduni na Michezo- Kuna hoja kwamba utamaduni ukae kwenye elimu; na habari iwe kitengo tu kama MAELEZO au IKULU na michezo iwekwe karibu na wizara yenye Vijana. Hata hivyo, kwa umuhimu wa Utamaduni kwa Taifa; na fursa ya Michezo kuwa sekta ya muhimu katika uchumi- haya mambo ni vyema yakapewa uzito unaostahili. Na ukishakuwa na wizara hiyo, ni rahisi kuunganisha na habari hapo hapo.
19. Kazi, (Ajira na Uwezeshaji)- ni rahisi kuiacha hii wizara ikawa ya masuala ya Kazi(Labour pekee) na masuala ya ajira(employment) ukayepeleka kwenye uchumi au ukayaacha kuwa mtambuka(cross cutting katika kila wizara). Lakini kwa hali ya uchumi wetu wa sasa wa kutegemea wageni na kuwaweka mstari wa mbele wageni- tunahaja ya kuwa na wizara ambao inalinga maslahi na kuendeleza maslahi. Kama Afrika Kusini walivyokuwa na sera/sheria ya black empowerment, hapa napo tunahitaji kwa muda kulipa kipaumbele suala la UWEZESHAJI. Wizara hii inaweza kuondolewa masuala ya uwezeshaji baadaye ikabaki na KAZI pekee.
Kwa mapendekezo haya:
Wizara ya Sheria na Katiba inafutwa badala yake majukumu yake ya kiutendaji yanapelekwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni sehemu ya Baraza la Mawaziri. Na majukumu ya Usimamizi wa Sheria yanabaki kwa Mahakama. Majukumu ya kusimamia HAKI, yanabaki chini ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Waziri wa Nchi-Utawala Bora anafutwa- Majukumu ya kusimamia utawala bora kwa maana ya uongozi yanabaki wa Rais Mwenyewe. Kwa maana ya Kulinda utawala bora, yabaki kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Sekretariati ya Maadili ya Watumishi wa Umma; Masuala ya Usalama wa Taifa yanabaki kwa Rais Mwenyewe. Masuala ya TAKUKURU inabidi kubadili sheria kukifanya kuwa chombo huru zaidi baada ya kusimamiwa na Waziri kwa maelekezo ya Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Bunge, anafutwa; masuala ya Bunge ashughulikie Waziri Mkuu mwenyewe ili kuongeza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Siasa na Uhusiano wa Jamii anafutwa- Wizara hii haikuwa na sababu yoyoye ya kuwepo, ilianzishwa kisiasa kwa lengo la kumpa nafasi Kingunge kuwa karibu na Rais, kuuingiza kwenye Baraza la Mawaziri na kupata fursa ya kuropoka hadharani masuala ya kisiasa na uhusiano wa kijamii. Kazi ambayo hata yenyewe ameshindwa kuifanya! Hivyo, anapaswa kuondoka yeye na wizara iliyoazishwa kwa ajili yake. Majukumu haya ya siasa na uhusiano na jamii ni mambo ya kawaida ya ofisi ya Rais hayahitaji kuundiwa Wizara.
Huu ndio muundo wa Baraza Jipya la Mawaziri 19 tu ninalopendekeza lijadiliwe. Katika hali hii, manaibu nao wanapaswa kupungua kabisa, na ikiwezekana baadhi ya Wizara zisiewe kabisa na manaibu. Kama Manaibu sio wajumbe wenye kura wa Baraza la Mawaziri, wanafanya nini? Kwa nini wasiwe under secretaries tu?
Haya ni maoni yangu binafsi, tujadili- tunataka Baraza la Mawaziri dogo na lenye ufanisi kiasi gani?