Barack Obama kawaangusha watu weusi wa Marekani na Waafrika

Barack Obama aliingia madarakani akibeba matumaini makubwa sana ya watu weusi wa Marekani na waafrika wengi kwa ujumla. Watu walifurahi sana na nyimbo nyingi zikaimbwa kusherehekea ujio wa nabii na shujaa huyu mweusi.

Huku kwa mataifa yetu tulitembea kifua mbele tukijua we have a Big brother. "What a proud moment to live" ilikua kama bahati kumshuhudia Rais wa kwanza wa Marekani kutoka kwa jamii ya watu weusi.

Alitukumbusha ndoto Maarufu ya Mwanaharakati Martin Luther King.

Ila sasa muhula wake wa kwanza ukapita muhula wa pili nao ukafuatia ukapita, akamaliza kipindi chake cha urais hata huko uraiani kama Rais mstaafu hatujaona kile ambacho tulikitegemea.

Mtu mweusi wa Marekani amebakia kua mtumwa, akiendelea kubaguliwa na kunyimwa haki nyingi kama raia wa Marekani.

Huku Afrika tumebaki tukipigana vita vyetu wenyewe kama ilivyokuwa kabla.

Juzi tu kama Tanzania, ilipopata msiba mkubwa, tulipata salamu za rambirambi kutoka kwa Malkia kwanza ila za Jirani yetu na ndugu yetu mjaluo Obama sikuziona. Kuna nukuu moja ya mpambanaji Samora Machel kama ntaikumbuka vizuri inasema "siku mtakayoona nikisifiwa na watu weupe msinipe siri zenu tena hata nikiwauliza maana nitakua nimeshawasaliti"
Nenda katembelee kwenye page zake za kijamii ni Rais anayependwa sana na kusifiwa na watu weupe.
Kwa nafasi yake hakuna mtu mweusi anayeweza kuifikia kirahisi kwa miaka ya hivi karibuni ila mchango wake huwezi kuulinganisha na watu kama kina Malcom X, Martin Luther, Jesse Jackson pamoja na Mashujaa wetu wa Afrika kina Nyerere, Lumumba na wengine wengi waliopambana kutetea haki na utu wa mtu mweusi wa Marekani na Afrika. Anapoondoka anatuachia alama gani? Wamarekani weusi watamkumbuka kwa lipi sisi Waafrika tumkumbukeje?
Yani Obama apoteze muda kutuma salamu za rambirambi za dikteta uchwara Magu? Nadhani haupo vizuri kichwani..
 
we are one.. io ndo kitu ambacho nakumbuka barack alikisema, kuhusu sheria kandamizi sio rahisi kukiondoa hasa kwa mataifa au watu ambao bado tunatawaliwa (Afrika) sababu vingi tunategemea kutoka kwao hata kwenye swala la maamuzi ndio mana mtu mweusi hana nafasi kubwa
 
Mkuu,

Nina mashaka kama kweli unajua na kufuatilia kwa maana ya kuelewa aliyoyafanya huyo muungwana.
Hapo palipokolezwa pahusike;
Swali moja tu. Je, unajua ni nini? au umewahi kusikia kitu inaitwa OBAMACARE?
Iliwahi kuwepo kabla ya Obama kuingia Madarakani?
Kwa faida yako tu ingawa haibagui Raia ila wafaidika wakubwa ni 'Waswahili' kama ulivyopenda kujua.

Yule 'Mwehu' alieondoka juzi alikuwa hataki hata kuisikia hiyo OBAMACARE lakini ameshindwa kuifuta kwakuwa ipo Kisheria na Akijua inamfaidisha nani zaidi.

Hicho ni kimojawapo ya vitu muhimu sana ambavyo 'Waswahili' wale hawawezi kumsahau Bw. Obama kwacho,
Nikutajie kingine?
Napenda hoja kama hizi sio porojo..natake note Obama Care lete kingine
 
Waafrica tunajipendekeza sana kwa wamarekani weusi,sisi tunaona kama n ndugu zetu ila czan kama wao wanatuchukulia hvyo
Obama keshakuwa mmarekan usimkumbushe mambo ya kiafrika, kama tu kwenye msiba wa bibi yake hajafika anaanza vp kumkumbuka mtu ambaye hawana mahusiano
Pia usiisahau OBAMACARE
 
Hahahaha
Dah inashangaza yaan una lilia POLE ? Hii sio sawa mtoa UZI.

Kumbuka mchuma janga hulia na nduguze sasa tambuaa Obama sio ndugu zako ile ni rangi tu ngozi ila moyon mwake ni mtu mweupe
Nadhani uzi umejikita zaidi kwenye matatizo ya mtu mweusi..
 
Waafrica tunajipendekeza sana kwa wamarekani weusi,sisi tunaona kama n ndugu zetu ila czan kama wao wanatuchukulia hvyo
Obama keshakuwa mmarekan usimkumbushe mambo ya kiafrika, kama tu kwenye msiba wa bibi yake hajafika anaanza vp kumkumbuka mtu ambaye hawana mahusiano
Pia usiisahau OBAMACARE
Mugabe alipowagusa settlers kule Zimbabwe alipigwa vikwazo mpaka leo hii wakati mpaka sasa wengi wa wale masettlers ni wazaliwa wa Zimbabwe... kama hatutaangaliana kama ndugu tutashindwa kwenye hii vita
 
Waafrica tunajipendekeza sana kwa wamarekani weusi,sisi tunaona kama n ndugu zetu ila czan kama wao wanatuchukulia hvyo
Obama keshakuwa mmarekan usimkumbushe mambo ya kiafrika, kama tu kwenye msiba wa bibi yake hajafika anaanza vp kumkumbuka mtu ambaye hawana mahusiano
Pia usiisahau OBAMACARE
Mnamlaumu Obama bure. Msiba yule Bibi anazikwa kiislamu . Mambo ya haraka haraka na Corona nayo imepamba moto .

Obama amefanya makubwa kwenye hiyo family . Unalalamika bure

Odhis *
 
Nami narudia . Wewe ni mpuuzi. America si kama Tanzania kwamba Rais akiingia anaweza kufanya apendavyo. No kule taasisi zao zina nguvu kuliko mtu binafsi . Ndiyo maana umeona kichaa cha Trump kimetulizwa. Ingekuwa Africa Trump angelifia madarakani .

So Obama asingeweza kufanya makubwa juu ya wa Africa na watu weusi duniani . Ni kwa sababu hatujitambui. Nakumbuka alipoingia madarakani alifanya ziara mara kadhaa Africa . Na moja alifanyia Adis aababa kwenye mkutano wa AU aliwashauri viongozi wetu kutengeneza taasisi imara badala ya viongozi imara. Alipoondoka tu Marais watatu walibadili katiba zao ili wajiongezee mihula madarakani (Mseveni, Kagame & Nagsimbe). So alijaribu kuweka kitu lakini aina ya viongozi tulionao ndiyo kama hawa waTz . Waliodai apende asipende anabaki madarakani eg Ndugai & co

Odhis *
Kwahiyo Rais wa Marekani hawezi kushughulikia matatizo ya wamarekani weusi huko Marekani kwa sababu taasisi zao zina nguvu zinazuia hilo? watu walitegemea kwamba Obama angewaza kutatua changamoto za wamarekani weusi(sio kuwapendelea) lakini haikuwa hivyo,Obama(mweusi mwenzao) kaingia madarakani na kutoka ila matatizo ya wamarekani weusi yamebaki hivyo hivyo.
 
Wa America weusi wana matatizo huwezi kuyatatua kwa mpigo.

Kwanza genge la wahuni ni pamoja African Americans na Latinos. Pili uchumi, elimu , huduma za jamii kwao ni daraja la chini sana ukilinganisha na wenzao European American's .

Kikubwa Obama aliwasaidia ktk Obama care . Na hii Trump hakuitaka hata kidogo. Mengine ni maswala na bidii ya mtu binafsi

Odhis *
 
Kwa watu wanaofuatilia mwenendo wa vuguvugu la BLM utagundua wengi bado wanalalamikia sheria nyingi kandamizi dhidi ya mtu Mweusi wa Marekani.
Hata kama huku kwetu Afrika tutakua tukimtwisha mzigo mzito sisi tutajipambania wenyewe.

Ila swali la msingi linabaki kuwa amewafanyia nini wamarekani weusi ambao bado wanaendelea kuumia?
Aliwekwa mahsusi kwa ajili ya kuutetea na ku legalize ushoga na transgenders marekani na duniani..Nothing more nothing less. Hana Legacy nyingine..
 
... the only thing Obama performed perfectly during his presidency is PROMOTION OF HOMOSEXUALITY.
 
UPUUZI MTUPU!!!
Barack Obama aliingia madarakani akibeba matumaini makubwa sana ya watu weusi wa Marekani na waafrika wengi kwa ujumla. Watu walifurahi sana na nyimbo nyingi zikaimbwa kusherehekea ujio wa nabii na shujaa huyu mweusi.

Huku kwa mataifa yetu tulitembea kifua mbele tukijua we have a Big brother. "What a proud moment to live" ilikua kama bahati kumshuhudia Rais wa kwanza wa Marekani kutoka kwa jamii ya watu weusi.

Alitukumbusha ndoto Maarufu ya Mwanaharakati Martin Luther King.

Ila sasa muhula wake wa kwanza ukapita muhula wa pili nao ukafuatia ukapita, akamaliza kipindi chake cha urais hata huko uraiani kama Rais mstaafu hatujaona kile ambacho tulikitegemea.

Mtu mweusi wa Marekani amebakia kua mtumwa, akiendelea kubaguliwa na kunyimwa haki nyingi kama raia wa Marekani.

Huku Afrika tumebaki tukipigana vita vyetu wenyewe kama ilivyokuwa kabla.

Juzi tu kama Tanzania, ilipopata msiba mkubwa, tulipata salamu za rambirambi kutoka kwa Malkia kwanza ila za Jirani yetu na ndugu yetu mjaluo Obama sikuziona. Kuna nukuu moja ya mpambanaji Samora Machel kama ntaikumbuka vizuri inasema "siku mtakayoona nikisifiwa na watu weupe msinipe siri zenu tena hata nikiwauliza maana nitakua nimeshawasaliti".

Nenda katembelee kwenye page zake za kijamii ni Rais anayependwa sana na kusifiwa na watu weupe. Kwa nafasi yake hakuna mtu mweusi anayeweza kuifikia kirahisi kwa miaka ya hivi karibuni ila mchango wake huwezi kuulinganisha na watu kama kina Malcom X, Martin Luther, Jesse Jackson pamoja na Mashujaa wetu wa Afrika kina Nyerere, Lumumba na wengine wengi waliopambana kutetea haki na utu wa mtu mweusi wa Marekani na Afrika. Anapoondoka anatuachia alama gani? Wamarekani weusi watamkumbuka kwa lipi sisi Waafrika tumkumbukeje?
 
Kwahiyo Rais wa Marekani hawezi kushughulikia matatizo ya wamarekani weusi huko Marekani kwa sababu taasisi zao zina nguvu zinazuia hilo? watu walitegemea kwamba Obama angewaza kutatua changamoto za wamarekani weusi(sio kuwapendelea) lakini haikuwa hivyo,Obama(mweusi mwenzao) kaingia madarakani na kutoka ila matatizo ya wamarekani weusi yamebaki hivyo hivyo.
Matatizo yapi? Unaongea general sana
 
Ungekuwa unajua system ya utawala wa Marekani kuanzia Rais, Senate na Congress inavyofanya kazi usingeandika huu upumbavu wako eti Obama aliwafanyia nini watu weusi. JIONGEZE kabla ya KUKURUPUKA na kuonyesha ujuha wako hadharani.
Kwa watu wanaofuatilia mwenendo wa vuguvugu la BLM utagundua wengi bado wanalalamikia sheria nyingi kandamizi dhidi ya mtu Mweusi wa Marekani.
Hata kama huku kwetu Afrika tutakua tukimtwisha mzigo mzito sisi tutajipambania wenyewe.

Ila swali la msingi linabaki kuwa amewafanyia nini wamarekani weusi ambao bado wanaendelea kuumia?
 
Ungekuwa unajua system ya utawala wa Marekani kuanzia Rais, Senate na Congress inavyofanya kazi usingeandika huu upumbavu wako eti Obama aliwafanyia nini watu weusi. JIONGEZE kabla ya KUKURUPUKA na kuonyesha ujuha wako hadharani.
Kwa hyo wewe na Barack mnaojua system mnakaa kimya mnavuta popcorns na kuangalia kwenye tv mambo yaende yenyewe.
 
Sasa jiwe nani yaani huko Duniani mpaka obama atoe pole ... Acha ubwege
 
Back
Top Bottom