Barack Obama kawaangusha watu weusi wa Marekani na Waafrika

Hoja gani unataka wakati nimekwambia JIONGEZE kabla ya KUKURUPUKA na kuandika kile usichokijua kuhusu Obama kutowafanyia chochote Weusi na Waafrika!? Kama unaonyesha ujuha hadharani mie sijui kuremba. Wapuuzi kama wewe ndiyo mnakaa vijiweni na kuanza kupotosha ukweli kuhusu mambo ambayo hamna ufahamu nayo. Kama hujui uliza.
Leta hoja mkubwa, kama huna hoja sit back n learn, U can't win an argument by matusi. Hawa ndo wanajiona wajanja huko vijiweni jenga hoja jombii, wewe uliyesoma unashindwa kujenga hoja unaishia kutukana.. shame on u
 
Yani Matatizo ya watu weusi huku afrika sababu ni viongozi wa afrika ila huko Marekani weusi matatizo yao sababu ni weusi wao kwamba watu weusi ndio wenye matatizo huko Marekani.
 
Hoja gani unataka wakati nimekwambia JIONGEZE kabla ya KUKURUPUKA na kuandika kile usichokijua kuhusu Obama kutowafanyia chochote Weusi na Waafrika!? Kama unaonyesha ujuha hadharani mie sijui kuremba. Wapuuzi kama wewe ndiyo mnakaa vijiweni na kuanza kupotosha ukweli kuhusu mambo ambayo hamna ufahamu nayo. Kama hujui uliza.
SIJAKURUPUKA kila mmoja anapimwa kutokana na nafasi aliyoipata kwenye jamii, waliokuja kumtetea Obama wamezungumzia Obamacare ambayo naona ndicho hicho tu atakachokumbukwa.

Sasa kama Obamacare is his only legacy huoni kama amefanya chini ya matarajio ya wengi.
 
Yani Matatizo ya watu weusi huku afrika sababu ni viongozi wa afrika ila huko Marekani weusi matatizo yao sababu ni weusi wao kwamba watu weusi ndio wenye matatizo huko Marekani.
Ni kweli kwa kiasi flani ila takwimu zinafikirisha na kuonesha kuwa wanalengwa na system. Kuna idadi kubwa wanaouwawa bila hata kuwa na silaha, vijana wengi weusi wamekua wakipikiwa kesi na mahakama kuendelea na kesi za hizo zisizo na mashiko na mengine mengi
 
Narudia tena hujui unachokizungumza. Obama ameingia madarakani wakati uchumi wa Marekani na dunia ukiwa umeyumba sana. Marekani ilikuwa inapoteza ajira laki nane na ushee kwa mwezi lakini baada ya miezi michache madarakani aliweza kuja na policies ambazo zilisaidia katika kurescue uchumi wa Marekani na hivyo kucreate ajira 11.5 millions ambazo watu weusi wengi walifaidika nazo na mishahara pia iliongezeka.

Hujui gharama kubwa za matibabu za US ndiyo sababu unabeza mafanikio makubwa ya Obama care hasa kwa watu wenye kipato cha chini na kati na ndiyo sababu hadi hii leo bado Ina umaarufu mkubwa na Biden kairudisha tena baada ya Trump kutaka kuifuta bila mafanikio. Mafanikio ya Obama si Obamacare tu pekee yake ndiyo sababu bado ana umaarufu mkubwa kwa Wamarekani wengi ikiwemo weusi na ndiyo sababu Biden alimtumia sana kwenye Kampeni zake 2020.

Sasa hayo uliyoyasema yakitokea Afrika basi Mamlaka zinalaumiwa ila yakitokea huko kwa weusi wa Marekani utasikia wamarekani weusi ni watukutu hivyo hayo wanayofanyiwa huko ni kwa sababu ya huo utukutu wao watu weusi.
 
Narudia tena hujui unachokizungumza. Obama ameingia madarakani wakati uchumi wa Marekani na dunia ukiwa umeyumba sana. Marekani ilikuwa inapoteza ajira laki nane na ushee kwa mwezi lakini baada ya miezi michache madarakani aliweza kuja na policies ambazo zilisaidia katika kurescue uchumi wa Marekani na hivyo kucreate ajira 11.5 millions ambazo watu weusi wengi walifaidika nazo na mishahara pia iliongezeka.

Hujui gharama kubwa za matibabu za US ndiyo sababu unabeza mafanikio makubwa ya Obama care hasa kwa watu wenye kipato cha chini na kati na ndiyo sababu hadi hii leo bado Ina umaarufu mkubwa na Biden kairudisha tena baada ya Trump kutaka kuifuta bila mafanikio. Mafanikio ya Obama si Obamacare tu pekee yake ndiyo sababu bado ana umaarufu mkubwa kwa Wamarekani wengi ikiwemo weusi na ndiyo sababu Biden alimtumia sana kwenye Kampeni zake 2020.
Hukunielewa sibishani na kazi kubwa alizofanya kama Rais wa Marekani.

Obama anaondoka kama Rais kipenzi cha wamarekani wengi, mwanasiasa na mwanadiplomasia mzuri.

Ila kwa upande wa kutetea haki za watu weusi wa Marekani na ndugu zake wa Africa huku tunatafuta legacy yake kwa tochi.
 
Angekuwa hakufanya chochote kuhusu Weusi basi asingekuwa na umaarufu mkubwa aliokuwa nao kwa watu weusi na narudia tena ungeujua utawala wa US wa mihimili mitatu Rais, Senate na Congress unavyofanya kazi basi usingeandika ulichoandika.
Hukunielewa sibishani na kazi kubwa alizofanya kama Rais wa Marekani.

Obama anaondoka kama Rais kipenzi cha wamarekani wengi, mwanasiasa na mwanadiplomasia mzuri.

Ila kwa upande wa kutetea haki za watu weusi wa Marekani na ndugu zake wa Africa huku tunatafuta legacy yake kwa tochi.
 
"siku mtakayoona nikisifiwa na watu weupe msinipe siri zenu tena hata nikiwauliza maana nitakua nimeshawasaliti".

HII NUKUU YAKO IMEPITWA NA WAKATI ILIKUA NI WA KIPINDI CHA UKOLONI NADHANI BADO UMEJIFUNIKA SHUKA LA MAREHEMU ZINDUKA
 
Ndugu ukoloni haukuishia tulipopewa bendera ila tuna njia ndefu mpaka kufikia Uhuru wa kiuchumi.

Tulitawaliwa kisiasa na Kiuchumi kisiasa tuliachiwa kupandisha bendera zetu ila bado wanacontrol kila kitu bado tumejiingiza kwenye mikataba ya kimataifa ambapo inatubidi kufuata wanavyotaka.

Kiuchumi ndo kabisa wachanga.

Waafrika bado tuna akili kama za Kuku anayefugwa anapopewa chakula na mfugaji anajenga na urafiki kabisa na mfugaji akijisahau kua mfugaji anataka nyama tu mwisho wa siku.
 
Barack Obama aliingia madarakani akibeba matumaini makubwa sana ya watu weusi wa Marekani na waafrika wengi kwa ujumla. Watu walifurahi sana na nyimbo nyingi zikaimbwa kusherehekea ujio wa nabii na shujaa huyu mweusi.

Huku kwa mataifa yetu tulitembea kifua mbele tukijua we have a Big brother. "What a proud moment to live" ilikua kama bahati kumshuhudia Rais wa kwanza wa Marekani kutoka kwa jamii ya watu weusi.

Alitukumbusha ndoto Maarufu ya Mwanaharakati Martin Luther King.

Ila sasa muhula wake wa kwanza ukapita muhula wa pili nao ukafuatia ukapita, akamaliza kipindi chake cha urais hata huko uraiani kama Rais mstaafu hatujaona kile ambacho tulikitegemea.

Mtu mweusi wa Marekani amebakia kua mtumwa, akiendelea kubaguliwa na kunyimwa haki nyingi kama raia wa Marekani.

Huku Afrika tumebaki tukipigana vita vyetu wenyewe kama ilivyokuwa kabla.

Juzi tu kama Tanzania, ilipopata msiba mkubwa, tulipata salamu za rambirambi kutoka kwa Malkia kwanza ila za Jirani yetu na ndugu yetu mjaluo Obama sikuziona. Kuna nukuu moja ya mpambanaji Samora Machel kama ntaikumbuka vizuri inasema "siku mtakayoona nikisifiwa na watu weupe msinipe siri zenu tena hata nikiwauliza maana nitakua nimeshawasaliti".

Nenda katembelee kwenye page zake za kijamii ni Rais anayependwa sana na kusifiwa na watu weupe. Kwa nafasi yake hakuna mtu mweusi anayeweza kuifikia kirahisi kwa miaka ya hivi karibuni ila mchango wake huwezi kuulinganisha na watu kama kina Malcom X, Martin Luther, Jesse Jackson pamoja na Mashujaa wetu wa Afrika kina Nyerere, Lumumba na wengine wengi waliopambana kutetea haki na utu wa mtu mweusi wa Marekani na Afrika. Anapoondoka anatuachia alama gani? Wamarekani weusi watamkumbuka kwa lipi sisi Waafrika tumkumbukeje?
mashujaa wa Afrika kina Nyerere, Lumumba na Magufuli.
 
Napenda hoja kama hizi sio porojo..natake note Obama Care lete kingine
HAYA NI BAADHI YA MACHACHE MENGINE:

1.Soko la ajira kwa Weusi liliongezeka maradufu kulinganisha na kabla ya yeye Obama kuingia madarakani.

2.Obama alipigania na kufanikiwa kupitishwa kwa Mswaada/Sheria ya kudumu ya kupunguza mzigo wa Kodi ya Mapato,
Yaani Income tax credit and Child tax credit, ambapo inakadiriwa kuwa hadi sasa wastani wa Wamarekani weusi 2Million wanafaidika na nafuu ya wastani/upungufu wa Kodi ya $1000 katika kodi ya Mapato.

3.Elimu ndio usiseme, watoto Waswahili walikuwa wanasoma wachache, wanafaulu wachache na waliokuwa wanaendelea na masomo wachache sana lakini jamaa alibailisha vyote hivyo na kuweka Historia mpya.

4. Kuporomoka kwa Uhalifu,
Utakubaliana nami kuwa umasikini huchangia uhalifu kuanzia wizi,ukabaji,uasherati, kwa wao wenzetu silaha,madawa n.k.
Waafrika wanasifika na hayo yote kwakuwa wengi ndio wa hali ya chini lakini,
-Kihistoria hakuna kipindi takwimu za uhalifu zimesoma chini Tangia kuundwa kwa Amerika kama 2014 wakati Usukani kaushikilia Obama.

5.Katika Historia haijawahi kutokea kwa Marais wa Marekani kutoa nafasi kwa Majaji Weusi kiasi alichotoa Obama.
-Obama alichagua jumla ya Majaji 53 WEUSI ambapo 9 kati yao walikuwa Majaji/ Wakuu wa Mabaraza.
Hiyo ni asilimia 19, ya Majaji wote aliowahi kuwachagua.
Kumbuka Clinton yeye hadi anamaliza ngwe yake aliweza kutoa Majaji asilimia 16 tu kwa Watu Weusi,
Akifuatiwa kwa karibu na Bush mkubwa ambae aliteua asilimia 7 tu Weusi kati ya jumla yote ya Majaji aliowahi kuteua..
Wengine wote wa nyuma walitoa idadi ndogo zaidi kwa Weusi.

Hivyo Obama anabaki kuwa kinara wa kihistoria.

Niendelee mkuu?

-
 
Santee niko nazipitia hoja zako mkuu.
 
Yani Matatizo ya watu weusi huku afrika sababu ni viongozi wa afrika ila huko Marekani weusi matatizo yao sababu ni weusi wao kwamba watu weusi ndio wenye matatizo huko Marekani.
True that, imagine Congo hapo wana laumu wazungu wakati washika mitutu ni weusi against weusi
 
Back
Top Bottom