Barack Obama kawaangusha watu weusi wa Marekani na Waafrika

Mar 10, 2021
35
125
Barack Obama aliingia madarakani akibeba matumaini makubwa sana ya watu weusi wa Marekani na waafrika wengi kwa ujumla. Watu walifurahi sana na nyimbo nyingi zikaimbwa kusherehekea ujio wa nabii na shujaa huyu mweusi.

Huku kwa mataifa yetu tulitembea kifua mbele tukijua we have a Big brother. "What a proud moment to live" ilikua kama bahati kumshuhudia Rais wa kwanza wa Marekani kutoka kwa jamii ya watu weusi.

Alitukumbusha ndoto Maarufu ya Mwanaharakati Martin Luther King.

Ila sasa muhula wake wa kwanza ukapita muhula wa pili nao ukafuatia ukapita, akamaliza kipindi chake cha urais hata huko uraiani kama Rais mstaafu hatujaona kile ambacho tulikitegemea.

Mtu mweusi wa Marekani amebakia kua mtumwa, akiendelea kubaguliwa na kunyimwa haki nyingi kama raia wa Marekani.

Huku Afrika tumebaki tukipigana vita vyetu wenyewe kama ilivyokuwa kabla.

Juzi tu kama Tanzania, ilipopata msiba mkubwa, tulipata salamu za rambirambi kutoka kwa Malkia kwanza ila za Jirani yetu na ndugu yetu mjaluo Obama sikuziona. Kuna nukuu moja ya mpambanaji Samora Machel kama ntaikumbuka vizuri inasema "siku mtakayoona nikisifiwa na watu weupe msinipe siri zenu tena hata nikiwauliza maana nitakua nimeshawasaliti".

Nenda katembelee kwenye page zake za kijamii ni Rais anayependwa sana na kusifiwa na watu weupe. Kwa nafasi yake hakuna mtu mweusi anayeweza kuifikia kirahisi kwa miaka ya hivi karibuni ila mchango wake huwezi kuulinganisha na watu kama kina Malcom X, Martin Luther, Jesse Jackson pamoja na Mashujaa wetu wa Afrika kina Nyerere, Lumumba na wengine wengi waliopambana kutetea haki na utu wa mtu mweusi wa Marekani na Afrika. Anapoondoka anatuachia alama gani? Wamarekani weusi watamkumbuka kwa lipi sisi Waafrika tumkumbukeje?
 
blogger

JF-Expert Member
Mar 13, 2012
5,196
2,000
Shida yako nini sasa?
Barack Obama aliingia madarakani akibeba matumaini makubwa sana ya watu weusi wa Marekani na waafrika wengi kwa ujumla. Watu walifurahi sana na nyimbo nyingi zikaimbwa kusherehekea ujio wa nabii na shujaa huyu mweusi...
 
babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
7,374
2,000
Miafrika ndivyo mlivyo,mnamlaumu Magufuli hajawahi hata kusafiri siku 1 kwenda nje.

Mnalaumu

Obama ni Mulatta yule wala hawajui nyie muacheni Ndo mana alilia alipokatazwa kwenda kula ugali kwa shangazi yake.
 
Maulaga59

Senior Member
Feb 1, 2021
184
250
Barack Obama aliingia madarakani akibeba matumaini makubwa sana ya watu weusi wa Marekani na waafrika wengi kwa ujumla. Watu walifurahi sana na nyimbo nyingi zikaimbwa kusherehekea ujio wa nabii na shujaa huyu mweusi.
Yeye pale ni Rais wa Marekani na wala si mwanaharakati, na urais ni taasisi siyo mtu, kwa hiyo alipngoza kulingana na katiba ya Marekani siyo kama Obama mweusi! Unatakiwa kuelewa hilo, full stop! Hakuna cha huyu ni wa kwetu hapo! Yeye ni Mmatekani na atakufa kama Mmatekani na wala siyo Mkenya au Mwafrika!
 
Kwa watu wanaofuatilia mwenendo wa vuguvugu la BLM utagundua wengi bado wanalalamikia sheria nyingi kandamizi dhidi ya mtu Mweusi wa Marekani.

Hata kama huku kwetu Afrika tutakua tukimtwisha mzigo mzito sisi tutajipambania wenyewe.

Ila swali la msingi linabaki kuwa amewafanyia nini wamarekani weusi ambao bado wanaendelea kuumia?
 
Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
3,592
2,000
Kwani Obama baada ya kutoka Tanzania kwenye ziara yake ya kitalii mwaka 2018 akiwa kwenye Nelson Mandela Annual Lecture huko South Africa alisemaje kuhusu demokrasia ya Africa? Fuatilia alichokisema kuhusu strongman politics utaona kama alikuwa akimkubali mwendazake au la hasa kuhusu hiyo demokrasia.
 
Mar 10, 2021
35
125
A

Ntafuatilia hiyo speech ila what is his legacy kwa upande wa kutetea haki za mtu mweusi wa Marekani?
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,968
2,000
TANZIA: BARRACK OBAMA AMEFIWA NA BIBI YAKE HUKO KENYA, MAZIKO YATAFANYIKA LEO 30/03/2021 ADHUHURI.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,968
2,000
Barack Obama aliingia madarakani akibeba matumaini makubwa sana ya watu weusi wa Marekani na waafrika wengi kwa ujumla. Watu walifurahi sana na nyimbo nyingi zikaimbwa kusherehekea ujio wa nabii na shujaa huyu mweusi.

Huku kwa mataifa yetu tulitembea kifua mbele tukijua we have a Big brother. "What a proud moment to live" ilikua kama bahati kumshuhudia Rais wa kwanza wa Marekani kutoka kwa jamii ya watu weusi.

Alitukumbusha ndoto Maarufu ya Mwanaharakati Martin Luther King.

Ila sasa muhula wake wa kwanza ukapita muhula wa pili nao ukafuatia ukapita, akamaliza kipindi chake cha urais hata huko uraiani kama Rais mstaafu hatujaona kile ambacho tulikitegemea.

Mtu mweusi wa Marekani amebakia kua mtumwa, akiendelea kubaguliwa na kunyimwa haki nyingi kama raia wa Marekani.

Huku Afrika tumebaki tukipigana vita vyetu wenyewe kama ilivyokuwa kabla.

Juzi tu kama Tanzania, ilipopata msiba mkubwa, tulipata salamu za rambirambi kutoka kwa Malkia kwanza ila za Jirani yetu na ndugu yetu mjaluo Obama sikuziona. Kuna nukuu moja ya mpambanaji Samora Machel kama ntaikumbuka vizuri inasema "siku mtakayoona nikisifiwa na watu weupe msinipe siri zenu tena hata nikiwauliza maana nitakua nimeshawasaliti"
Nenda katembelee kwenye page zake za kijamii ni Rais anayependwa sana na kusifiwa na watu weupe.
Kwa nafasi yake hakuna mtu mweusi anayeweza kuifikia kirahisi kwa miaka ya hivi karibuni ila mchango wake huwezi kuulinganisha na watu kama kina Malcom X, Martin Luther, Jesse Jackson pamoja na Mashujaa wetu wa Afrika kina Nyerere, Lumumba na wengine wengi waliopambana kutetea haki na utu wa mtu mweusi wa Marekani na Afrika. Anapoondoka anatuachia alama gani? Wamarekani weusi watamkumbuka kwa lipi sisi Waafrika tumkumbukeje?
Watanzania! Barrack Obama angekuwa mtanzania wakenya tungewasimanga na kuwanyanyasa wasimsogelee kipenzi chetu! Na angekuwa mtanzania na mkenya angeandika Post hii angekoma, angeipata habari yake.
Sisi ni wabinafsi sana ndiyo maana Mungu aliifunga miguu ya mbwana Samatta kutokana na midomo yetu iliyomfanya aonekane kuwa ni mchezaji wakwanza toka Afrika.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom