Barabara ya 4-8 na eneo lote la Ngamiani jijini Tanga kwanini serikali hailitendei haki kwa kuhimiza ujenzi wa nyumba za kisasa na kuondoa uchafu?

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,039
3,486
Wakuu,

Wagosi wa kaya wamo vibarazani huku jiji lao limetelekezwa kurejeshewa hadhi yake ya zamani. Reli waliboreshewa na hayati JPM mpaka stesheni ilikarabatiwa ikabaki kidogo treni ianze safari kwenda huko lakini mipango ikaenda hali jojo hadi leo.

Swali kwa serikali, kwanini jiji hilo pendwa lenye watu wenye ukarimu, amani na upendo kwa wageni pamoja na rasilimali zake za utalii, kilimo, viwanda nk mmetelekeza kuwekeza na kuhimiza wawekezaji wengine walinawirishe kwa maendeleo ya taifa na watu wake?
 
Iliwezekana vipi Tanga kuwa jiji?
 
wagosi ni wavivu sn
 
Iliwezekana vipi Tanga kuwa jiji?
Zamani Tanga ndio ilikuwa mji wenye maendeleo ya juu sana ukiufuatia Dar Es Salaam. Kipindi hicho viwanda vingi vilikuwa ni Tanga ila watumishi wa umma na srikali ndio waliochangia kudidimia kiuchumi kwa jiji hilo na viongozi wa kuirejeshea hadhi hawapo kwa sasa. Wanaubaguzi sana wenyewe kwa wenyewe ambapo wenyeji wa mji Wabondei hawathaminiki na biashara zimetawaliwa na watu kutoka Lushoto na Korogwe
 
Umekosea sana. Wenyeji wa Mji wa Tanga ni Wadigo ba sio wa Bondei. Afterall..wote hao kutoka Korogwe na Lushoto Tanga kwa maana ya Makao Makuu ya Mkoa ni nyumbani kwao na wana nasaba sana na mji huo.
Tatizo Wabondei,Wadigo na Wasegeju ni wavivu sana suo wa chapakazi hivyo Wasambaa wameonyesha umahiri kwenye utafutaji.
 
Wakuu,

Wagosi wa kaya wamo vibarazani huku jiji lao limetelekezwa kurejeshewa hadhi yake ya zamani. Reli waliboreshewa na hayati JPM mpaka stesheni ilikarabatiwa ikabaki kidogo treni ianze safari kwenda huko lakini mipango ikaenda hali jojo hadi leo.

Swali kwa serikali, kwanini jiji hilo pendwa lenye watu wenye ukarimu, amani na upendo kwa wageni pamoja na rasilimali zake za utalii, kilimo, viwanda nk mmetelekeza kuwekeza na kuhimiza wawekezaji wengine walinawirishe kwa maendeleo ya taifa na watu wake?
Halafu hiyo ni ngome ya CCM wacha wafanyiziwe tu wakome kuiunga mkono CCM
 
Umekosea sana. Wenyeji wa Mji wa Tanga ni Wadigo ba sio wa Bondei. Afterall..wote hao kutoka Korogwe na Lushoto Tanga kwa maana ya Makao Makuu ya Mkoa ni nyumbani kwao na wana nasaba sana na mji huo.
Tatizo Wabondei,Wadigo na Wasegeju ni wavivu sana suo wa chapakazi hivyo Wasambaa wameonyesha umahiri kwenye utafutaji.
Uko sahihi kabila la Wadigo wametamalaki hapo mjini Tanga ambapo asili ya jina la kabila hilo ni mzee mmoja aliyewahi kuwa maarufu sana akiitwa 'Digo'. Kabila hili pia wanapatikana nchini Kenya hasa Ukanda wa Mombasa kusini. Kabila la Wadigo ni watani wakubwa wa kabila la Wanyamwezi na Wasukuma kutokana na mwingiliano kwa kukutana kwenye mashamba ya mkonge ndio maana utakuta Mdigo, Mzigua, Mbondei, Mkilindi au Mluvu anaitwa Maghembe, Lugendo, Shigella, Mazuli, Walwa nk kimsingi chimbuko la majina hayo ni mwingiliano wa kuoana baada ya maisha ya manamba kwenye mashamba ya mkonge na viwanda vilivyokuwepo miaka hiyo.
1694099545787.png
 
Umekosea sana. Wenyeji wa Mji wa Tanga ni Wadigo ba sio wa Bondei. Afterall..wote hao kutoka Korogwe na Lushoto Tanga kwa maana ya Makao Makuu ya Mkoa ni nyumbani kwao na wana nasaba sana na mji huo.
Tatizo Wabondei,Wadigo na Wasegeju ni wavivu sana suo wa chapakazi hivyo Wasambaa wameonyesha umahiri kwenye utafutaji.
Wenyeji halisi wa Tanga ni wabondei, na asili yao ni kisiwa kilichopo bandarini. Mji ulipo sasa yalikuwa ni mashamba ya wabondei wakivuka maji. Neno Tanga limetokana na neno la kibondei "ntanga" likimaanisha shamba, likatoholewa hadi kuwa Tanga.
Wadigo wakitokea kusini mwa Kenya, wakawavamia wabondei na kuwafukuza hadi maeneo ya ilipo Muheza, neno lililotokana na neno la kibondei "mheza" likimaanisha kufikia mwisho. Na ndio sababu ya utani wa wabondei na wadigo... Hizo ndio hadithi za zamani.
Mengine wataongezea wengine.
 
Yaani serikali imetelekeza kabisa ule mji mpaka hatari halafu wameupa hadhi ya jiji ,hawajengi vyuo vikubwa wala majengo ya maana ..
Hakika watu wa Tanga hawatomsahau Nyerere kabisa kwa sera yake mbovu .
 
Wenyeji halisi wa Tanga ni wabondei, na asili yao ni kisiwa kilichopo bandarini. Mji ulipo sasa yalikuwa ni mashamba ya wabondei wakivuka maji. Neno Tanga limetokana na neno la kibondei "ntanga" likimaanisha shamba, likatoholewa hadi kuwa Tanga.
Wadigo wakitokea kusini mwa Kenya, wakawavamia wabondei na kuwafukuza hadi maeneo ya ilipo Muheza, neno lililotokana na neno la kibondei "mheza" likimaanisha kufikia mwisho. Na ndio sababu ya utani wa wabondei na wadigo... Hizo ndio hadithi za zamani.
Mengine wataongezea

Maiyanga1 asante kwa kung'amua hilo kuwa Wabondei walifurushwa kuelekea Bonde mpaka walipofika Muheza na vita maarufu kupiganwa maeneo ya Kivindo.
Hivyo tunakubaliana kuwa sasa kabila dorminant Tanga mjini ni Wadigo na sio Wabondei japo baadhi walikimbilia Mnyanjani, Mwarongo na Dargube
. Wale wote ni Wabondei japo hawataki kuitwa hivyo wakishikilia usegeju na ushirazi. Case closed!
By the way Maiyanga unayotoka ni ya Mkuzi au Misozwe!😅
 
Back
Top Bottom