Barabara nne Chalinze - Segera hadi Tanga

Barabara nne Chalinze - Segera hadi Tanga

Kwani hamjui kuwa viongozi wetu siyo Business oriented? Huwa hawafikirii athari ya miaka 100 ijayo wanajali kura za mwaka ujao. Nchi imeuzwa kila mahala. Mbuga, barabara, mahoteli, madini kila sehemu ni ujinga mtupu. Kama suala ni Bandari ya Tanga bandari yenyewe dhoflihali.

Ni kweli mkuu kwaba mafisadi karibu wote wametoka huko. hushangai kiwanda cha mbolea kujengwa Kilimanjaro kilimo Ruvuma? Upuuzi mtupu na ubinafsi uliokithiri.

Ipo siku atutakamata mashine hapo ndipo watakaposema!

Suluhisho ni moja tu; nalo ni kuwaondoa watu maboga waliokabidhiwa uongozi wa nchi. Tanzania inao watu werevu MNO kiasi ni aibu kubwa kuongozwa tunavyoongozwa. Nasita kukubaliana na wazo la kukamata mashine, lakini lazima huu uozo uondoke madarakani.
 
Kinyambiss,

It is not either or; it is both and. We have to have both roads and ports.
 
Juzi usiku nimeona kwenye kituo kimoja cha TV serikali yetu ikitangaza mpango wa kujenga barabara nyingine ya kiwango cha lami itakayokuwa sambamba na ile iliyopo kutoka Segera hadi Tanga, hivyo basi moja itakuwa ina kwenda nyingine inarudi (double roads).

Serikali imesema inafanya hivyo kuepusha ajali nyingi zinazotokea katika barabara hiyo, na mradi huo utaanza hivi karibuni , utafanywa kwa awamu na utagharimu Tshs bilioni nne.

1.Jamani hizo hela kwanini zisiende kujenga barabara huko madongo kwinama ambako hakuna barabara za lami na hizo za vumbi zinahali mbaya kabisa?

2.Eti wanazuia ajali watu wasife!, mbona huko madongo kwinama watu wanakufa kwa kukosa usafiri wa kuwapeleka mahosipitliani kwa sababu barabara hazipitiki! nani atwasemea wananchi hao wanaoishi kama wakimbizi ktk ncnhi yao?

3. Mbona mazao ya wakulima yanaozea mashambani kwakukosa usafiri kutokana na ubovu wa barabara, hili serikali haliihusu?

4. Yaani wanataka kutuambia hiyo barabara ndiyo chanzo kikuu cha vifo vya watanzania kikiasi kwamba ndiyo inastahili kutengewa fungu hilo kubwa wakati kiukweli haihitaji hilo fungu!?

5 Au kwakuwa pia ni njia ya kwenda kwa Mkulu wa kaya!

Jamani mimi naona nchi yetu ni kweli inahitaji miundo mbinu, lakini ni kwenye maeneo yanayo stahili, hii ikoje? ahh......... nchi yetu "inanajisiwa"! na watu wajinga kabisa ambao ni viongozi wetu.

Ni Upuuzi hatuna maji safi na huduma bora za Afya hizo barabara zitasaidiaje watu ambao wengi hali zao ni duni
 
kwani Tanga wanafata nini? kuna uzalishaji gani kule wamefata? kwasababu kuna maeneo yapa tz watu hata hawajui hata kiswahili watoto wakiona gari wanakimbia, hamna barabara kabisa kuna vijinjia tu. kwanini selikali isiangalie huko ili twende equally?

Maeneo kama ya western tz, tz kusini, nyanda za juu kusini etc, kuna maisha ya ajabu sana. wanachojali ni kwenda huku kuomba kura tu lakini hata hawajali kuwajengea barabara. angalia kule sumbawawanga angalia kule kigoma duuuuu. kaazi kwelikweli
 
DU!!!
Je huku kwetu ni vipi? kutoka Bagamoyo kupitia Pangani hadi Tanga ili iarakishe sisi tunaotoka Kilimanjaro, kwani kabla ya mwanzo barabara ya Segera Chalinze haikuwepo enzi ya mkoloni ilikuwepo hii ya kwetu Bagamoyo kupitia Pangani Mpaka Tanga, sasa iweje zinajengwa barabara nne kwa pamoja?

Huu ni ufisadi uliokomaa. Basi ziende kujenga barabara za Mbezi Malamba mawili, Barabara ya Mbezi mpigi Magohe na kungineko kujenga sio hii ya sasa. Kama wanataka kuepusha ajali waweke Trani ya Segera Chalinze Express.
 
Mimi sijakubaliana na mpango wa upanuzi wa hii barabara toka njia 2 za sasa kwenda njia 4. Hakuna ulazima sana wa hivyo kwa wakti huu ambao tunaona kabisa hali ya uchumi kitaifa na ki-dunia ni tete.Mimi napenda niungane na Mheshimiwa Selelii ambaye ameiambia serikali wazi kabisa kwamba inabidi ilaaniwa kwa ubaguzi inayowafanyia Waed tanzania wa baadhi ya mikoa na kuwapendelea wengine. Ni aibu na kweli Mungu awalaani hawa Mawaziri wenye kufanya upendeleo na ubaguzi wa waziwazi huu. Na kuthibitisha kuwa hoja hii ni nzito mpaka sasa hivi hakuna aliyejitokeza kujibu hoja ya Selelii kuhusu barabara hii kutengenezwa kwa fedha ambayo bado haijwa-approved na Bunge!!!!

Kwa nini hii pesa ya kupanua hii barabara isipelekwe kule ambako bado kabisa hawajawahi kuiona lami?Kuna barabara zinazosuasua kama hii ya Dodoma-Singida-Shinyanga-Mwanza? Tunajua kuwa kuna tatizo kubwa sana la usafiri kwenda katika mikoa hii ya kati mpaka huko kanda ya Ziwa. Hasa ukizingatia kuwa kwa sasa hata Reli ya Wahindi wa TRL haifanyi sawasawa. Barabara ya lami yenye uhakika ingeweza kupunguza kero ya usafiri kati ya mikoa ya Ziwa na mikoa mingine ya Pwani na Nyanda za Kusini.

Kwa hiyo kupanua barabara ya Chalinze kabla ya kukamilisha barabara za kwenda kanda ya Ziwa au kujenga barabara mpya kwenye maeneo ambayo hakuna kabisa barabara za lami ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Kinachofanyika hapa ni kampeni za chinichini za CCM kwa ajili ya Rais Kikwete na ndugu yake wa karibu Waziri wa Miundo mbinu Mheshimiwa Shukuru Kawambwa.

Namaliza kwa kusema hivi: Kama hayati Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere angelikuwa na upendeleo kama wanaofanya viongozi wa CCM sasa basi kule kanda ya Ziwa ingelikuwa ni Ulaya. Nyerere hakuwa na ubaguzi huu wa kipuuzi unaofanywa na CCM kwa sasa, yeye alitaka mgawanyo sawa wa keki ndogo tunayoipata. Ili kwamba kila eneo la Tanzania lisije likawa na maendeleo makubwa sana kuliko eneo jingine.

Angalia huko Musoma,Mwanza,Shinyanga,Bukoba, na wapi vile! Hakuna maendeleo ya miundo mbinu kabisa. Fikiria kuwa Kanda ya Ziwa ni sehemu yenye utajiri mkubwa sana wa karibu vitu vyote;dhahabu na almasi zimetapakaa kila kona. Samaki(minofu) kila siku wanapelekwa ulaya nasikia jamaa wa minofu walishaanza kufunga viwanda maana Ziwa linakauka kwa kuishiwa na samaki. Pamba,Kahawa,ndizi ni vya kumwaga. Kwa upande wa mifugo usiseme kila aina ya mifugo wapo kule ng'ombe,mbuzi,kondoo n.k.

Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba mikoa hii ya Kanda ya Ziwa ndiyo yenye miundo mbinu mibovu kabisa ambayo tunaishuhudia tangu tupate uhuru karibu nusu karne iliyopita. Usawa uko wapi hapa???

Mimi nasubiri kwa hamu kauli ya serikali kuhusu matumizi ya fedha za kupanua hii barabara ya Chalinze,Segera,Tanga ambazo zimeanza kutumika hata kabla Bunge halijapitisha Bajeti ya mwaka 2009/10.CCM wawe wakweli katika hili, fedha wazitoa wapi na nani katoa kibali? Kama wametumia bila kibali cha Bunge wawajibike kwa kujiuzulu.

Nawasilisha.
 
..hivi haiwezekani kujenga hizo njia 4 Segera-Tanga, na vilevile kujenga barabara ya Dodoma-Singida-Mwanza-Shinyanga?
 
Utata wa barabara ya chalinze
Na Leon Bahati, Dodoma

SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amesema kuwa vitabu vya bajeti vilivyopo kwenye maktaba ya Bunge mjini Dodoma vinaonyesha kuwa barabara ya Chalinze-Segera-Tanga haikuwa imepangiwa fedha katika bajeti zilizopita, jambo ambalo limemfanya achelewe kutoa majibu kwa serikali dhidi ya mbunge wa Nzega, Lucas Selelii.

Selelii, mmoja wa wabunge wanaoshikia bango ujenzi wa barabara, alitaka ufafanuzi wa serikali kuhusu kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo kabla ya Bunge kupitisha bajeti ya mwaka 2009/10, kitu ambacho kikibainika kuwa ni kweli, serikali itakuwa imevunja katiba.

Wiki iliyopita Sitta alilieleza Bunge kuwa ameshapata maelezo ya serikali kufafanua kuhusu suala hilo, lakini amekuwa hayatangazi kwa madai kuwa, kuna matatizo katika vielelezo vilivyowasilishwa na Selelii na vilivyotumiwa na serikali.

Jana Sitta ataendelea kuliweka kiporo suala hilo kwa kuwa bado hajajiridhisha na utata ulio kwenye vitabu alivyowasilisha Selelii na nakala ya ukurasa wa kitabu cha mwaka huo kilichowasilishwa na serikali.

"Mheshimiwa Mbunge alikwenda katika maktaba ya Bunge akatafuta vitabu vya makadirio vya 2006/07 na 2007/08 na 2008/09. Serikali kwa upande wake nayo ikanipa nakala vivuli vya miaka hiyo hiyo," alisema Sitta.

"Sasa nakala ya serikali inaonyesha kuwa fedha zilitengwa, vitabu vilivyopo maktaba ya Bunge vya makadirio, hususan kitabu cha nne- maendeleo inaonyesha sifuri kwa miaka hiyo. Ndio maana kumekuwa na utata kwamba tunafanyaje.

"Kwa hiyo leo nimeagiza kwamba, baada ya kuonana na mheshimiwa Waziri wa Miundombinu na katibu wa Bunge waangalie mtiririko mzima wa vitabu. Mtaona kwamba mathalan mwaka huu imebidi marekebisho yafanywe. Kwa yule mtu aliyechukua kitabu cha kamati tulipokutana mwezi Mei, Dar es Salaam, hakina usahihi kwa sababu baadhi ya sehemu zilibadilishwa.

"Kwa hiyo limebaki hilo tu, kulinganisha hivyo vitabu na baada ya hapo nitatoa basi ufafanuzi na uamuzi wangu kuhusu kilichotokea. Hii ndio sababu, lakini watu, wengi wetu wauza magazeti wakasema Spika sijui anapambana na serikali na vitu vya kipuuzi vya namna hiyo."

Spika Sitta aliongeza kusema: "Hii ni serikali yetu, mimi siwezi kupambana na serikali. Nipambane na serikali kwa sababu gani. Ni jambo tu la uhakika kwa sababu linalotamkwa hapa, likija kugundulika kuwa Spika naye alilolisema hakulifanyia utafiti, tunaweka msingi mbaya sana wa utawala wa Bunge. Ndio maana limenichukua muda. Kwa hiyo tuwe na subira, hili litakwisha hivi punde."

Ukarabati wa barabara hiyo iliyojengwa miaka 18 iliyopita ulizinduliwa mwezi Mei na Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein. Ukarabati huo unafadhiliwa na serikali ya Denmark kwa kutumia shirika lake la Danida.

Serikali hiyo imetoa Sh44 bilioni, wakati serikali imetenga Sh18 bilioni katika bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya kukamilisha mkataba wa ukarabati huo kwa mujibu wa makubaliano baina ya nchi hizo mbili.
 
..hivi haiwezekani kujenga hizo njia 4 Segera-Tanga, na vilevile kujenga barabara ya Dodoma-Singida-Mwanza-Shinyanga?
mimi nafikiria priority ingekuwa kumaliza hiyo ya dodoma-singida-mza, then manyoni- kigoma, then arusha-dodoma-mtera, then tunduru-songea-mtwara, ndipo hapo unaweza kufikiria njia nne hizo za challinze-dar etc etc, sio ambazo tayari zina lami zinaombewa tena, then watu wa kigoma wanawekwa kiporo, na hiyo ya Dom-Singida-Mza inachukua muda mrefu zaidi ya ilivyo tarajiwa, yaani inatumika kama chambo tu cha uchaguzi lakini nia ni kama haipo.
 
mimi nafikiria priority ingekuwa kumaliza hiyo ya dodoma-singida-mza, then manyoni- kigoma, then arusha-dodoma-mtera, then tunduru-songea-mtwara, ndipo hapo unaweza kufikiria njia nne hizo za challinze-dar etc etc, sio ambazo tayari zina lami zinaombewa tena, then watu wa kigoma wanawekwa kiporo, na hiyo ya Dom-Singida-Mza inachukua muda mrefu zaidi ya ilivyo tarajiwa, yaani inatumika kama chambo tu cha uchaguzi lakini nia ni kama haipo.

Mzee, uko sahihi pasenti mia!! huo ndiyo mgawanyo wa utu!
lakini hawa wakubwa mbona wao hawaoni!! mbona jambo hilo liko wazi akili zao zikoje? I see mi nakasirika sana......wanawazaje hawa au wanawaza wakiwa "wanajisaidia"!!
 
hapana ujenzi huangalia uchumi na malipo yake! tar road ni uwekezaji pia, upeleke kigoma kuleta chumvi dar au?dagaa?teheee joke!!
 
Juzi usiku nimeona kwenye kituo kimoja cha TV serikali yetu ikitangaza mpango wa kujenga barabara nyingine ya kiwango cha lami itakayokuwa sambamba na ile iliyopo kutoka Segera hadi Tanga, hivyo basi moja itakuwa ina kwenda nyingine inarudi (double roads).

Serikali imesema inafanya hivyo kuepusha ajali nyingi zinazotokea katika barabara hiyo, na mradi huo utaanza hivi karibuni , utafanywa kwa awamu na utagharimu Tshs bilioni nne.

1.Jamani hizo hela kwanini zisiende kujenga barabara huko madongo kwinama ambako hakuna barabara za lami na hizo za vumbi zinahali mbaya kabisa?

2.Eti wanazuia ajali watu wasife!, mbona huko madongo kwinama watu wanakufa kwa kukosa usafiri wa kuwapeleka mahosipitliani kwa sababu barabara hazipitiki! nani atwasemea wananchi hao wanaoishi kama wakimbizi ktk ncnhi yao?

3. Mbona mazao ya wakulima yanaozea mashambani kwakukosa usafiri kutokana na ubovu wa barabara, hili serikali haliihusu?

4. Yaani wanataka kutuambia hiyo barabara ndiyo chanzo kikuu cha vifo vya watanzania kikiasi kwamba ndiyo inastahili kutengewa fungu hilo kubwa wakati kiukweli haihitaji hilo fungu!?

5 Au kwakuwa pia ni njia ya kwenda kwa Mkulu wa kaya!

Jamani mimi naona nchi yetu ni kweli inahitaji miundo mbinu, lakini ni kwenye maeneo yanayo stahili, hii ikoje? ahh......... nchi yetu "inanajisiwa"! na watu wajinga kabisa ambao ni viongozi wetu.
kwani hii barabara si ndio ile ambayo Mh Selelii amedai imeanza kutengenezwa kabla ya bujet kupitisha..???

ila kwa wakati huu tukiwa na tatizo la kiuchumi, ile barabara hauikutakiwa iwe kipaumbele...
 
hapana ujenzi huangalia uchumi na malipo yake! tar road ni uwekezaji pia, upeleke kigoma kuleta chumvi dar au?dagaa?teheee joke!!

uchumi usiuangalie kwa namna hiyo tu, kukuza potential zingine nako ni kukuza uchumi kama elimu itapitikana kwenye miundo mbinu mizuri most probably itakuwa nzuri and at a lower cost kupeleka wafanyakazi wenye ujuzi, nako ni kuongeza tija, na wafanyakazi wazuri hawawezi kwenda mahali pasipo na huduma nzuri, na ukiwapata si wengi au wanalazimika kutokana na kutokuwa jinsi, Pia Kigoma kuna Bandari, kuna biashara kubwa tu na nchi jirani, na hata tourism ya Gombe, kuna uzalishaji mkubwa tu wa chakula, kama kibondo na kasulu, pia kuna mazao kama Pamba na Kahawa na Mawese.

Jambo jingine magari yanapo haribika kutokana na barabara mbovu au kuchukua muda mrefu kusafiri kati ya sehemu moja kwenda nyingine nako ni kudumaza uchumi. sasa sijui fikra zako zilizojifinya kwenye vitu vinavyoonekana tu kwako zinatoka wapi?
 
..mbona naona kama kinachokusudiwa ni ukarabati?

.tuwe makini kidogo hapa, maana tusipokarabati hizi barabara tunaweza kulazimika kuzijenga upya huko mbeleni.

NB:

..nasubiri kwa hamu Dr.Kawambwa atakapowasilisha bajeti ya wizara yake. lakini nadhani in the end itapitishwa tu.
 
Duu nimepita juzi nikienda Moshi na hizo barabara 4 kwa kweli ni miyeyusho tuu..badala ya kupanua kwa kutumia changarawe zinazowekwa chini kislammi juu yake wanatumia udongo..sasa na malori yetu haya itakuwaje? mmm
 
Ndg Mzizi wa Mbuyu,

Mbona linapofanywa jambo jema bado unalalamika, wapi ambako ungelikuwa wewe ungeona panafaa.
Ni vyema kuwa na utamadumu wa kuyaona mabaya na mazuri pia!
 
Back
Top Bottom