Barabara nne Chalinze - Segera hadi Tanga

Unajua mtu angeniambi wanajenga kilosa kupitia handeni kwenda tanga kwa lami ningemuona ana akili au Dar Bagamoyo kukutana na hiyo ya msata segera, badala ya kupita chalinze, ingeleta mantiki, lakini kuna barabara miaka nenda miaka rudi ni hizo hizo. sasa nguvu za kiuchumi tutaziongeza vipi ikiwa sisi wenyewe tuna dumaza hayo maendeleo
 
yaani umeanza bila kusubiri budget au kwakuwa walisha mtafuta mfadhili? basi kila Mkoa uruhusiwe kwenda kutafuta wafadhili wenyewe na tusifuate national priorities

Mkuu hili ndo ninalo liona na ninalo liogopa!

Ule umoja udugu na mshikamano taratibu vinajengewa mazingira ya kupotea! Hata kama mtu huoni wivu jamani? kwanini hapo tu ndo maji, barabara nne? wakati uzarishaji sifuri? kwanini watu wa Kigoma wanaachwa mataani ili hali kuna ardhi nzuri vyakula vya kumwaga? Kwanini si Tabora na kwingineko?

Siwaelewi jamani bora tujitenge tu kila watu wakazane kivyao vyao kuliko dhahabu za mwanza, sangara mawese ya Kigoma, viishie kufaidisha wengine ili hali wasukuma na waha wanatembelea ndala zilizo isha visigino.. vumbi mpaka uvunguni! grrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Telling the truth we need such roads,but not in expenses of underdeveloped parties of the country.whoever is doing this funding allocations is wrong ,if is president involved is wrong,seems to be putting his personal interests before nation.I regret to say this but consequently we end up fighting in long run............kujilimbikizia
 
Mkuu hili ndo ninalo liona na ninalo liogopa!

Ule umoja udugu na mshikamano taratibu vinajengewa mazingira ya kupotea! Hata kama mtu huoni wivu jamani? kwanini hapo tu ndo maji, barabara nne? wakati uzarishaji sifuri? kwanini watu wa Kigoma wanaachwa mataani ili hali kuna ardhi nzuri vyakula vya kumwaga? Kwanini si Tabora na kwingineko? Siwaelewi jamani bora tujitenge tu kila watu wakazane kivyao vyao kuliko dhahabu za mwanza, sangara mawese ya Kigoma, viishie kufaidisha wengine ili hali wasukuma na waha wanatembelea ndala zilizo isha visigino.. vumbi mpaka uvunguni! grrrrrrrrrrrrrrrrr

Mzee maneno mazito sana hayo! Basi tu wakubwa hawataki kutusikia!
Jana Mbunge Selelii aliliongelea pia suala la barabara hii kuwa ni tatizo.
 
Ni wafadhili wameamua kuiendeleza barabara ambayo wameijenga tangu mwanzo. Wanaona umuhimu wa hiyo barabara. Ni kiungo kati ya Dar na Nairobi. Vile vile, ni barabara inayohusika na utalii wa ndani na wa nje. Ni barabara muhimu sana kwa uchumi wa nchi. Magari yanayosafiri kati ya Dara - Arusha - Nairobi kwa mwaka mmoja yanaweza kuzidi jumla ya magari yote yanayotumia hizo barabara nyingine mlizotaja.

La msingi zaidi ni hili: Si kweli kwamba barabra nyingine hazijengwi kwa vile fedha zinaishia kwenye barabara ya Dar hadi Tanga. Tunao uwezo wa kujenga barabara nyingi, lakini fedha zinaibwa na viongozi. Fedha zinazoibwa miaka mitano zingetosha kujenga barabara muhimu zote mlizotaja.

Lalamikieni tatizo la msingi, ambalo ni wizi wa fedha za umma.
 
Pesa za kujenga hayo mabarabara yote mliyotaja zipo, tatizo ni kuwa watu wanaoishi maeneo hayo hawajui kama zipo hivyo zinaliwa tu na wajanja. kigoma zoto kaamka tayari ujenzi umeanza na wengine wafuate nyayo!

Swali la Kizushi kwa wanajamii. NI WANGAPI KATI YENU MLIOENDA KWENYE MIKUTANO YA KIJIJI AU SERIKALI ZA MITAA MWEZI WA TATU? Kama tupo hatufiki ............ lakini mjue kwamba maeneo haya ndipo wanapokula fedha nyingi sana za maendeleo ya pale ulipo.
 
Wana Jamii,

Barabara ni miundo mbinu
Miundo mbinu ni Kipaumbele kwa wakati huu-kwa Tanzania na hii inajulikana!

Kwa mfano kesho; wahisani, watoa misaada,wakopeshaji, na kama bado zimebaki hizo "$2bn" Zikakusanywa- Tutaweza kujenga babarabara zote? Kwa Mkupuo? Assuming hela zipo za "kumwagwa"? Vipaumbele vingine vitakuwaje? Vipaunyuma?

Assuming tumeuza malighafi zote...

Kweli tupo makini kuendesha mipango kama hii, hata kwa kuvurumishwa?
Mambo huwa yanaenda na wakati/nyakati
Nyakati imefikiwa na wakati ndio huu

Wahandisi kazi kwenu(sio ufisadi)kuhakikisha hili linafanyika na kwa ubora wa juu kabisa-Watanzania tujitolee, kizalendo, tuone haya yanafanyika kwa ajili ya vizazi vinavyokuja.

Tutalalama mpaka lini?

Jana hawakujenga barabara tukalalama-leo tunajenga barabara , tunalalama

Kikuu niataendelea kusema humu...Mda wa kuchezewa watu akili hususani Mtanzania unafikia kikomo...(tupo pamoja)ahadi za sasa hivi kama hazitatatekelezeka kwa njia za ufisadi...na sio vinginevyo hazitasamehewa kamwe(tuwe pamoja) tutawashinda hata kama sio kuwamaliza

Tutawafikisha Mahakamani, na tukiwahukumu basi 'viboko kumi na mbili kuingia na vingine kumi na mbili' wakitoka-Live kwenye lundinga zote

Lisemwalo lipo...Barabara hiyo inakuja, Ufisadi huo unakuja, mwishowe viboko vitakuwa vinawangoja!

Ahsante.
 
Lazima sisi Watanzania tutambue kwamba bara bara zetu kuu ni vizuri zikalingana na zile za majirani zetu. Juzi juzi tu viongozi wa Afrika Mashariki waliweka "jiwe la msingi" ktk barabara inayojengwa kati ya mji wa Arusha na Namanga. Upande wa Kenya wanajenga Namanga-Athi River ili iwe ya kiwango hicho hicho.

Ukishafika Arusha ukataka kuendelea mpaka Dar es Salaam, mji mkuu (?wa biashara) wa Tanzania, unatakiwa kuendesha ktk bara bara ya kiwango hicho hicho! La sivyo utaanza kudharau Tanzania kwamba ni junior partner ktk Jumuiya ya Africa Mashariki! Kwa hiyo upanuzi wa barabara ya Segera-Chalinze uko ktk mtindo huo huo. Tuukubali sisi JF.

Kuhusu barabara za vijijini na zile za kuhakikisha mazao yanasafirishwa kutoka huko kwenda mijini, na pia pembejeo na zana za kilimo zinafikia wakulima, nakubaliana kwamba hizi ni muhimu sana. Lakini nyingi zitakuwa ni za kiwango cha changarawe na kupitika kwa misimu yote. Ni jukumu la Serikali za Wilaya (Halmashauri) kuunganisha vijiji vyao na barabara hizi. Fedha zitengwe au ziombwe toka Serikali Kuu kwa madhumuni hayo, na siyo kwa madhumuni ya kununua magari ya usafiri, majoho na kofia kwa madiwani.

Nimesoma taarifa nyingi za hivi karibuni ambazo zinanipa impression kuwa hawa madiwani wa ccm, wengi wanadhani wakishachaguliwa, basi ni lazima waungane na wale "wakubwa" ktk juhudi za "kula" viji"EPA" vyao na vi-Richmond vyao. Madiwani na viongozi wa vijiji wa aina hii hawafai. Wananchi wawakatae ktk uchaguzi ujao. Badala yake wachaguliwe viongozi waadilifu wenye Uzalendo na ujasiri wa kuwakomboa wananchi maskini na wanyonge ktk hali ya sasa. Uadilifu, uzalendo na ujasiri wa kuleta mabadiliko mema, vianzie ktk mioyo ya viongozi wa mitaa na kata.

kilasara
 
Rafiki yangu mmoja ananipigia simu kuniuliza, Hivi viongozi wetu wanao uelewa wa kutosha?? hivi kama ni upanuzi wa barabara si wangefanya Chalinze -Dar? anaendelea.

Najaribu kutafuta majibu ili nimjibu. Mtaalamu mmoja ananidokeza kwamba barabara ya Segera - Chalinze iko out of standards, yaani ni nyembamba. anaendelea kunidokeza kwamba wakati wa ujenzi wa barabara hiyo wajanja walipunguza upana wa barabara ile ili wapate ulaji. inasemekana barabara ile ilipunguzwa nusu mita ya upana halisi. imagine 174km x 0.5

Lakini kulikuwa na ulazima wa kuifanyia upanuzi sasa hivi? nami nimebaki nikijiuliza.
 
Barabara ya Chalinze hadi segera haikuwa na matatizo yoyote ya kufanya kuwepo na ulazima wa kuijenga upya kwa kiwango cha njia nne kwa sasa. Njia mbili kwenda Segera na njia mbili Kurudi Chalinze.

Bado barabara nyingi za mikoani ziko katika hali mbaya sana, kwa kiwango ambacho kusafirisha chakula kutoka Malinyi kwa mfano hadi kimfikie mlaji Kariakoo gharama zake huwa ni kubwa sababu ya ubovu wa barabara.

Serikali ijayo itakayopewa utawala 2010 ione uonevu wanaofanyiwa Watanzania wengi na irekebishe hali hii bila ya kusita.

Barabara zisizopitika vijijini ziimarishwe na miradi mpya isiyokuwa na manufaa yoyote kwa taifa isimamishwe kama huu mradi Chalize - Segera
 
Huo mchezo kwa makandarasi unaitwa kula sentimita.

Tanzania na nchi nyingi za ulimwengu wa tatu tumeonewa sana kwa mchezo huu wa kula sentimita kwenye ujenzi wa barabara.
 
Hatuna la kumjibu, bajeti imeshapitishwa tena kwa kishindo. Serikali ijayo 2010 bado itakuwa ni hii hii ama sawa na hii. Kwanza fikiria hili, 'Mkuu wa Kaya anatoka kando kando ya barabara hii, Katibu wa CCM Taifa naye wa huko huko, Ben kajenga Lushoto huko huko, Kawambwa kama mkuu wa kaya, Kigoda Handeni(Kamati ya uchumi na fedha), karibu Wenyeviti wote wa vyama vya upinzani, barabara ni hii, Anne Kilango, Aloyce Kimaro, Ole Sendeka, Lowasa'.... NATANIA TUUU!!! Ila nikipata nafasi nitamwambia Spika.
 
Kwani hamjui kuwa viongozi wetu siyo Business oriented? Huwa hawafikirii athari ya miaka 100 ijayo wanajali kura za mwaka ujao. Nchi imeuzwa kila mahala. Mbuga, barabara, mahoteli, madini kila sehemu ni ujinga mtupu. Kama suala ni Bandari ya Tanga bandari yenyewe dhoflihali.

Ni kweli mkuu kwaba mafisadi karibu wote wametoka huko. hushangai kiwanda cha mbolea kujengwa Kilimanjaro kilimo Ruvuma? Upuuzi mtupu na ubinafsi uliokithiri.

Ipo siku atutakamata mashine hapo ndipo watakaposema!
 
Back
Top Bottom