Njia kuu za kuingia na kutoka jiji la Dar ni Morogoro Road na Kilwa Road.
Kinachosikitisha ni kwamba njia ya Kilwa haina mbadala mzuri pale magari yanapoziba njia, labda mtu apite Magogoni au darajani .
Tofauti kubwa unapopita Morogoro RD barabara za mchepuko ziko nyingi: 1. Selander Bridge, Kigogo Rd, Kawawa Rd, au pengine mpya inayozinduliwa Tanzanite Bridge.
Tuseme serikali haoni hilo ni tatizo kwa njia hii, jinsi foleni za magari zinavyoumana. Hasa gari likiharibika njiani, mtu anaweza kukaa masaa 4 au zaidi ili kufika nyumbani.
Nafikiri ni vizuri kuongeza barabara za mchepuko kwa njia zinazokwenda kusini ya Dar. Moja, ni kupasua na kujenga daraja kupitia TEC pale kwenda Kijichi ni karibu sana. Pili, Tandika Azimio kupasua kwenda Kiburugwa ingesaidia sana.
Jambo lingine ni barabara ya Kijichi - Zakhiem ni mbovu sana kuanzia Kijichi mpaka shule ya Msingi Muungano kulikoni.
Pia Tatizo la kipande cha Kichemichemi mpaka Kibonde maji wanasema kuna bomba la mafuta la TAZAMA. Je, hakuna suluhisho miaka hii yote. Mbona sehemu zingine hili bomba limevuka barabara kulikoni hapa pana shida gani ngumu haitatuliki?