Mtindo wa magari ya polisi au breakdown kuziba service road asubuhi ndio suluhu kwa madereva kuchepuka?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Kumekuwa na huu mtindo wa magari ya polisi au breakdown kuziba service road asubuhi kwenye barabara ya bagamoyo ili wale wanaochepuka warudi kuunga na foleni kama wengine.

polisi.jpg
Ni kwamba wamekosa njia kabisa ya kupunguza foleni asubuhi mpaka kuamua kuziba service road? Halafu cha kuchekesha ni kwamba ni service road ya upande mmoja tu wa kulia ndio huwa inafungwa (ukiwa uelekeo wa kwenda Mwenge), huku ya upande mwingine magari yakichepuka kama kawaida! Sasa hapo wamesuluhisha nini?

polisi 1.jpg

Kutumia service roads wakati barabara kuu haina tatizo ni kosa, na wanahatarisha maisha ya watembea kwa miguu lakini suala la foleni asubuhi ni kichomi na utaratibu wa kuruhusu magari asubuhi ni mbaya, ndio maana madereva wanaona bora kuchepuka tu.

polisi 2.jpg

Trafiki/Polisi mnaweza kufanya vizuri zaidi ya hivi.
 
Back
Top Bottom