Barabara Mbadala Kilwa Road

Nsibwene

Senior Member
Mar 2, 2017
198
129
Njia kuu za kuingia na kutoka jiji la Dar ni Morogoro Road na Kilwa Road.

Kinachosikitisha ni kwamba njia ya Kilwa haina mbadala mzuri pale magari yanapoziba njia, labda mtu apite Magogoni au darajani .

Tofauti kubwa unapopita Morogoro RD barabara za mchepuko ziko nyingi: 1. Selander Bridge, Kigogo Rd, Kawawa Rd, au pengine mpya inayozinduliwa Tanzanite Bridge.

Tuseme serikali haoni hilo ni tatizo kwa njia hii, jinsi foleni za magari zinavyoumana. Hasa gari likiharibika njiani, mtu anaweza kukaa masaa 4 au zaidi ili kufika nyumbani.

Nafikiri ni vizuri kuongeza barabara za mchepuko kwa njia zinazokwenda kusini ya Dar. Moja, ni kupasua na kujenga daraja kupitia TEC pale kwenda Kijichi ni karibu sana. Pili, Tandika Azimio kupasua kwenda Kiburugwa ingesaidia sana.

Jambo lingine ni barabara ya Kijichi - Zakhiem ni mbovu sana kuanzia Kijichi mpaka shule ya Msingi Muungano kulikoni.

Pia Tatizo la kipande cha Kichemichemi mpaka Kibonde maji wanasema kuna bomba la mafuta la TAZAMA. Je, hakuna suluhisho miaka hii yote. Mbona sehemu zingine hili bomba limevuka barabara kulikoni hapa pana shida gani ngumu haitatuliki?
 
Bagamoyo Road sio njia ya kutoka na kuingia Dar? Vipi Nyerere Road? Kwanini umesema ni njia hizo mbili tu ulizozitaja ndo za kuingia na kutoka Dar?
 
Hizo njia za chocho kwa Kilwa Road ulitarajia zipite wapi zitokee wapi? Ukitoka Mbagala, ukafika Mission, geografia hairuhusu kuwa na njia za chocho!

Ukifika Mtongani zipo za chocho kiaina lakini hazikufikishi popote kwa sababu ukivuka tu kwa Azizi Ally, kulia unakutana na Uwanja wa Sabasaba, TPDC Mess, na TIA huku kushoto unakutana na Kambi ya Jeshi ya Twalipo!

Kutoka Twalipo unakutana na Salvation Army, JKT, Pollice Barracks, Polisi Ufundi, mara umetokea Bendera 3 close na Bandari. Kulia nako hali ipo hivyo hivyo!!

Hiyo Morogoro Rd unayosema ni kwa sababu along the road, zaidi ya 95 ni makazi binafsi, na kwahiyo kuna mitaa!!
 
Kwani kambi hazihamishiki?
 
Njia ya kwenda kusini inakuja kuongezwa huku Kimbiji na stendi ya magari yote itakuwa hapo.
Acha utani bana,Kimbiji unapajua ww?
Yaani uishi Mbagala stand Kimbiji?
Are u seriously?
Alafu ya Mgari ya kwenda Kusini,kusini ipi Mbuyuni?
 
Ipo ramani ya barabara kutoka nyuma ya polisi mbagala maturubai, mangaya ambayo sasa imejengwa kwa lami, kupitia mtaa wa Serenge transfomer,kuvusha bonde hadi mashine ya maji mtoni chini,unakutana na barabara ya mtoni Azimio kwenda buza.Hilo jukumu la Tanroads
 
Back
Top Bottom