Baphomet: Sanamu la Shetani linayozua vurugu USA

Baphomet: Sanamu la Shetani linayozua vurugu USA

View attachment 863720

Rannie Rodil akiigiza Baphomet katika tamasha ya Son Of Monsterpalooza 2013 mjini Burbank, California.



Binadamu tangu zama za kale amekuwa akijenga, kuchonga na kuweka sanamu za aina nyingi kwa sababu mbalimbali.

Baadhi hutumiwa kuwaenzi watu maarufu na kuwakumbuka, na nyingine huabudiwa kama miungu.

Kwa muda mrefu hata hivyo, imekuwa ni nadra kuona sanamua ambayo moja kwa moja inahusishwa na shetani au ibilisi.

Lakini ukifika Marekani, mambo ni tofauti.

Kuna sanamu moja kubwa ya shaba ambayo inahusishwa na ushetani.


Ni sanamu ya, Baphomet ni kiumbe mwenye kichwa kinachofanana na cha mbuzi lakini ameongezwa maungo ya ajabu.

Ni kiumbe huntha mwenye mabawa, na kwenye sanamu hiyo inayotumiwa kwa sasa huoneshwa akiwa na watoto wawili wanaotabasamu.

Sanamu inayotumiwa kwa sasa ina urefu wa karibu futi 9, na iligharimu $100,000 (£64,000) kuitengeneza.

Sanamu hii imekuwa ikitumiwa kuwapiga vita wale walio na imani za Kikristo na imani nyingine zenye kumcha Mungu mmoja. Ni sanamu hii ambayo imekuwa ikitumiwa kuendesha vita dhidi ya kuwekwa kwa sanamu za Kikristo na dini nyingine katika majengo maarufu, bustani na maeneo ya umma nchini Marekani.
View attachment 863722

Agosti 17, sanamu hiyo ya kiumbe anayefahamika kama Baphomet ilipelekwa katika jimbo la Arkansas anakotoka rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton.

Wanaotumia sanamu hiyo ni watu wa kundi linalofahamika kama Satanic Temple (Hekalu la Shetani) ambalo ni kundi la 'kidini' na kisiasa ambalo hupinga kuingizwa kwa dini katika masuala ya serikali.

Kundi hilo liliandaa maandamano ya watu 150 waliyojumuisha waabudu shetani, watu wasioamini Mungu yupo na Wakristo pia.

Maandamano hayo yalifanyika nje ya jengo lililo makao makuu ya jimbo la Arkansas katika mji wa Little Rock.

Walikuwa wamekerwa na hatua ya kuwekwa sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu katika uwanja wa makao makuu hayo.

Satanic Temple walisema sanamu hiyo inakiuka Sheria ya Kwanza ya Marekebisho ya Katiba nchini Marekani ambayo huzungumzia uhuru na haki za kidini.

"Ikiwa kutakubaliwa kuwepo kwa sanamu ya dini moja basi kunafaa kuwa na uhuru kwa wengine kuweka sanamu za kidini, na ukizuia basi kusiwe na sanamu yoyote ile," mwanzilishi mwenza wa tawi la Satanic Temple katika jimbo la Arkansas Ivy Forrester alinukuliwa na wanahabari siku hiyo ya maandamano.
View attachment 863725
Sanamu ya Baphomet inayotumiwa na Satanic Temple


Ndoto yao ni kuwa na sanamu ya kudumu, lakini siku hiyo hawakuruhusiwa na sheria kuiweka kwa muda mrefu. Kuna sheria ya Arkansas ya mwaka 2017 inayohitaji sanamu ya kuwekwa maeneo ya serikali iwe na udhamini wa mbunge ambaye atawasilisha mswada iidhinishwe kupitia bunge.

Sanamu hiyo ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilidhaminiwa na mwanasiasa wa Republican, Seneta Jason Rapert. Hata hivyo, chini ya saa 24 baada ya kuwekwa, mwanamume mmoja alivurumisha gari na kuugonga mnara huo na kuubomoa.

Maandamano ya Satanic Temple Arkansas yalisababisha kuandaliwa kwa maandamano mengine ya kuwapinga yaliyoandaliwa na makundi ya Kikristo na wanachama wa Republican. Wakristo walikuwa wamebeba karatasi zilizokuwa na ujumbe kutoka kwenye Biblia.

Satanic Temple waliwasilisha ombi la kushirikishwa kwenye kesi ya kupinga mnara huo wa Amri Kumi za Mungu iliyowasilishwa na shirika la haki za kiraia la American Civil Liberties Union, lakini baadae kundi hilo liliwasilisha ombi kutaka wasishirikishwe kwenye kesi hiyo.

Sanamu ya Detroit
Sanamu hiyo ya Baphomet ilizinduliwa mara ya kwanza katika mji wa Detroit, Michigan kukiwa mipango ya kuiweka nje ya makao makuu ya jimbo la Oklahoma ambapo kulikuwa kumewekwa mnara mwingine wa Amri Kumi za Mungu mwaka 2015.

Mnara huo ulizinduliwa 25 Julai mwaka huo, ambapo kupitia taarifa, Satanic temple walisema: "Tulichagua Baphomet kwa sababu ni kiumbe ambaye huhusishwa na Shetani na maana inayohusishwa naye inafaa sana akiwekwa kando na sanamu inayowakilisha dini nyingine."

Sherehe ya kuuzindua ilikuwa ya faragha, na ukumbi uliotumiwa uliwekwa siri kubwa kwani Wakristo walikuwa wameandamana awali kuipinga mjini. Picha zilizopakiwa kwenye Facebook zilionyesha uzinduzi wake ulifanyika karibu na Mto wa Detroit.

Kabla ya uzinduzi huo kufanyika, waumini takriban 200 walihudhuria ibada ya misa katika kanisa la St. Joseph mjini humo kupinga sanamu hiyo. Wengine 50 walifanya maombi mjini katika eneo ambalo awali Satanic Temple walikuwa wamepanga kuuzindulia mnara huo.

Mwanamume yule yule aliyeuharibu mnara wa Arkansas anadaiwa kufanya vivyo hivyo na kuubomoa mnara mwingine kama huo wa Amri Kumi za Mungu nje ya makao makuu ya jimbo la Oklahoma.

Satanic Temple walisitisha juhudi zao za kutaka kuweka sanamu ya Baphomet huko baada ya Mahakama ya Juu ya Oklahoma kuamua kwamba Sanamu ya Mnara wa Amri Kumi za Mungu ilikuwa imewekwa kinyume cha sheria, hivyo wakawa wameshinda vita bila kupigana.
Mahakama ilisema ni kinyume cha sheria kutumia mali ya umma kwa manufaa ya dini yoyote ile.


View attachment 863727

Jina Baphomet lilitoka wapi na asili yake wapi?
Jina hili asili yake ni enzi ya kukomesha uasi katika Kanisa Katoliki katika miaka ya 1100, kwa Kiingereza Inquisition, na kuteswa kwa wapiganaji wa kidini kwa jina Knights Templar waliokuwa wanateswa ili wafichue siri zao na wakubali kuifuata dini kwa mujibu wa viongozi wa kanisa wa wakati huo.

Kwa mujibu wa waandishi wa enzi za vita vya kidini maarufu kama Crusade, wapiganaji hao walikiri kumuabudu mungu wa wapagani kwa jina Baphometh.

Baadhi ya wasomi hata hivyo huamini kwamba "Baphometh" ni upotoshaji wa jina "Mahomet" - ambalo hutumiwa kumrejelea Nabii Muhammad, jambo linalozua utata zaidi.

Lakini kadiri miaka ilivyosonga na mafumbo na siri kuwahusu Knights Templar kuzidi, ndivyo ufafanuzi wa neno hilo na maana yake ulivyozidi kutofautiana.

Moja ya ufasiri wa neno hilo unapatikana katika kitabu cha Da Vinci Code chake Dan Brown ambapo, neno Baphomet limefafanuliwa na kutafsiriwa kama "Sophia" au busara.

Baphomet kwa mujibu wa Levi
View attachment 863728
Picha maarufu zaidi ya Baphomet ilichorwa na mwanamizungu wa Ufaransa Eliphas Levi mwaka 1856 katika kitabu chake cha Transcendental Magic: Its Doctrine and Ritual.

Alichora kiumbe huntha mwenye mabawa na mwenye pembe na mwenge ulio katikati ya pembe hizo kichwani.

Kuna mchoro pia wa pembe nane kwenye paji la uso.

Mikononi kumeandikwa maneno ya Kilatini SOLVE (tenganishwa) na COAGULA (fungamanisha) - ambazo ni nguvu za kuunganisha na kutenganisha ambazo zilitwaliwa kutoka kwa Mungu.

Mchoro wa Levi ulihamasisha zaidi sanamu inayotumiwa na Satanic Temple.

Ni jinsia mbili kwa pamoja, nusu mnyama na nusu binadamu.

Saluti ya vidole viwili
Sanamu hiyo ina vidole viwili vilivyoelekezwa juu mkono wa kulia na viwili vinavyoelekezwa chini mkono wa kushoto, maana yake "kama ilivyo juu, na chini iwe pia".

Maneno hayo na ishara hiyo ya vidole ni maarufu miongoni mwa wenye kuamini katika mizungu na mafumbo.

Chanzo chake ni kazi za kale za msomi Hermes Trismegistus, ambaye vitabu vyake vilikuwa maarufu sana enzi ya Kipindi cha mwamko-sanaa na mageuzi ya kidini, maarufu kama Renaissance and Reformation barani Ulaya.

Maneno hayo pia hutumiwa kuhusiana na sayansi, vitu vyote na Mungu, lakini Levi aliandika kwamba kwa kutumia ishara hiyo, Baphomet wake alikuwa anaashiria kuwiana sawa kwa fadhila na haki.

Watoto wawili
Lucien Greaves, msemaji wa Satanic Temple anasema lengo lao ni kwamba watoto watatazama kazi hiyo ya sanaa kama salama, isiyofaa kuzua wasiwasi wowote.

"Sura ya mbuzi huyo haioneshi chochote. Si ya kishetani wala ya kutisha - kama wanavyodai baadhi ya watu - ukiitazama bila kuongozwa na mzigo wa utamaduni.


Lakini watoto hawafai kumuoogopa Shetani?

"Sifikiri watoto wanaokutana na sanamu hii bila kutiwa hofu na propaganda wanaweza kuona chochote cha kuwatia wasiwasi," anasema Greaves.

"Lakini si kwamba tunapinga kuwaingiza watoto kwenye mitazamo ya kidini. Mara nyingi watoto hulazimishwa kuingia kwenye dini. Hilo ni jambo hatutaki kulifanya kamwe."

Caduceus
Kwenye tumbo la Baphomet kuna ishara ya kale ya Kigiriki ya nyoka wawili walio kwenye fimbo. Fimbo ambayo ilibebwa na Hermes na maafisa wa kueneza matangazo au kutoa matangazo rasmi waliotumiwa kutoa matamko rasmi.

Ishara hiyo kwenye sanamu hiyo inaashiria biashara, mashauriano na kutendeana, na iliingizwa kwenye Baphomet na Levi.

"Kwetu ni ishara ya maridhiano ya vitu viwili tofauti - kwa mfano kuwa na sanamu ya Kishetani karibu na sanamu ya Kikristo," anasema Greaves.

"Tunafikiri ni ujumbe wenye nguvu sana kuwa na sanamu hii ikiwa karibu na sanamu ya Amri Kumi za Mungu. Unaweza kuwa na mambo mawili tofauti kwa pamoja bila mzozo."

Maziwa
Baphomet wa Levi alikuwa huntha mwenye maziwa, lakini "tuliyaondoa maziwa hayo" anasema Greaves. Anasema hawakutaka wajipate kwenye mdahalo kuhusu jinsia ya kiumbe huyo wao jambo ambalo lingewafanya watu kupoteza maana halisi.

Badala yake anasema watoto wawili, mvulana na msichana, ndio wanaowakilisha jinsia.

'Pentagram'
View attachment 863729
Kwenye paji la uso la Baphomet na kwenye kiti cha enzi alichokikalia kuna mchoro wa nyota ya pembe tano, ishara ambayo mara nyingi hutambuliwa kama ishara ya shetani.

Mara nyingi huonekana ikiwa imepinduliwa.

Msalaba wa Peter pia hupinduliwa.

Greaves anasema lengo lao ni kuwafanya watu wabadilishe mtazamo wao na kuacha kuongozwa na waliyofunzwa na utamaduni wao. Waangazie mambo kwa kuzingatia ushahidi uliopo.

Anasema mtazamo huo huwazuia watu kuchukua msimamo huru kuhusu masuala kama vile ndoa za wapenzi wa jinsia moja na haki za kutoa mimba pamoja na huduma nyingine za uzazi wa mpango.
View attachment 863730
Mwenge kati ya pembe
"Mwenge wa maarifa ndio kama upembe wa kati - na inatukuza juhudi za kutafuta elimu na maarifa. Tunathamini hilo sana," anasema Greaves.

Levi mwenyewe aliandika kwamba mwenge wa maarifa uolikuwa unawaka katikati ya pembe za Baphomet ni mwanga wa kusawazisha vitu vyote. Ni taswira ya roho iliyo juu ya vitu vyote vinavyoonekana, kama zilivyo ndimi za moto, ingawa bado imeunganishwa na vitu hivyo, mfano moto unavyoendelea kung'aa juu ya mafuta au kijiti.

Maandiko
Kulikuwa na mpango wa kuongeza maandiko kwenye mchoro wa nyota ya pembe tano ya moja ya nguzo saba kuu za Satanic Temple: "moyo wa huruma, busara na haki unafaa daima kuongoza zaidi ya neno lililoandikwa au kutamkwa."
View attachment 863732
Nyuma ya sanamu hiyo, kutakuwa na nukuu kutoka kwa kitabu cha Cain chake Lord Byron unaosema: "Kisha, nani alikuwa Ibilisi? Yule hangekuruhusu wewe uishi milele, au yule ambaye angelikuumba uishi milele, katika raha na nguvu za elimu na maarifa?"

Satanic Temple ndio nani?
Kwa mujibu wa tovuti yao (The Satanic Temple) Satanic Temple wanaamini kwamba "kimsingi watu kuteseka au kuumia ni vibaya, na chochote kile kinachopunguza madhilana mateso ni kizuri."

Hawaamini katika kutenda mabaya.

Wanasema: "Huwa tunakumabtia kukufuru kama njia halali ya kujieleza na kuonyesha uhuru wa mtu binafsi dhidi ya imani za kitamaduni zisizo na tija."

"Msimamo wa Satanic Temple ni kwamba dini inaweza, na inafaa kutenganishwa na ushirikina. Hivyo basi, huwa hawaendelezi imani katika Shetani binafsi. The Satanic Temple - Wikipedia

"Kukumbatia jina la Shetani ni kukumbatia mtazamo wa kutumia fikira na kujiondoa kutoka kwa mfumo wa kuamini katika nguvu za kipekee za kutoka nje ya dunia na utamaduni uliopitwa na wakati wenye msingi wake katika ushirikina."
Bro hapa kwenye "huntha" umemaanisha nini ?

Maana navyolijua mimi hilo tamko sijui ndio hivyo hivyo ulivyolitumia ama. Msaada tafadhali.

Ila naendelea kusoma uzi wako......!
 
Chief samahani kdg

Kabla ya mimi kukujibu
naomba kidogo nikuulize swali


Unaposema kuwa Dini,ipo nyuma katika kuiendesha Dunia,na hili limesimamiwa na watu wachache sana,ambao hawataki kujulikana!!!!

Hapa naomba uchambuzi wa ndani na ushahidi wa kutosha

Kisha swali ni

Miaka maelfu iliyopita,Kabla kukua kwa Makanisa uliyoyataja
Je!Hao hao waendesha Dunia kama ulivyodai,walikuwepo?!!
au kabla ya Issa(Yesu)عليه السلام?!!!

Kisha naomba jambo moja tu kwako

Uislam haupo katika mfumo huo uliousema,nina hakika kbs,Uislam huujui hata harufu Bro


Ila naomba radhi kama nitakuwa nimetumia maneno yasiyofaa kwako

nataraji udadavuzi kutoka kwako Bro na jibu la swali langu

Shukran sana
kabla sijakujibu,una uhakika uislamu haupo katika mfumo huo...??
 
kabla sijakujibu,una uhakika uislamu haupo katika mfumo huo...??
mkuu..sikia nikwambie kity..dini zimekuja majuzi juzi snaa...na tunaona kuwa kuna kundi dogo ( namanisha secret society) ambalo ndo liliokubaliana juu ya uhifadhi wa hiyo siri ya jinsi dunia au ulimwwngu unavyofanya kazi...

Kwanza kabisa ili uendane sawa na mimi naomba usome hidden doctrine au msahafu unaoelezea vizuri kabsaa hii kitu inayoitwa ROYAL DESCENDANT...

ukishaijua hii ndo utajua kuwa dini zimetoka wapi...unless other wise tufungue thready ya Royal descendant ndo tutamalizia kule...
 
Hilo halina shaka kabisa

Naomba tu,unidadavulie kwa yale niliyohitaji kwako Bro

Ubarikiwe sana
Halina shaka kabsaa kuwa mnacontribute indirectly au unakataa kuwa hamuhusiki?? kwa wewe muumini wa kawaida utakataa kwa kigezo cha kutokuwa na mfumo wa sadaka wa lazima lakini pychologically unahusika bila wewe kujijua..
 
Halina shaka kabsaa kuwa mnacontribute indirectly au unakataa kuwa hamuhusiki?? kwa wewe muumini wa kawaida utakataa kwa kigezo cha kutokuwa na mfumo wa sadaka wa lazima lakini pychologically unahusika bila wewe kujijua..
Bro
nimekuambia shaka ondoa

au kama utakuwa na fursa,juu ya kunidhibitisha hayo

itakuwa umenena vema sana
 
Nikwambie kitu...

Samahani lakini sipendi uone kama nakukwaza ila napenda ujue namna mambo yalivyo..

Unajua kazi kubwa au mchango mkubwa wa kanisa katoriki na washirika wake kina nani naniii( madhehebu mengine) katika role ya ukuaji wa sayansi ..??

Unajua kazi kubwa ya Islamic religion katika role ya ukuaji wa sayansi na technlojia mpaka kukufikisha hapa ulipo...??

Unajua hata hiyo simu na nguo unazovaa ni matokeo ya sayansi ?? ( shifting negative awareness to positive awareness and knowlege ya grup dogo la wanadamu ) ambayo yanafanywa na kundi la jamii ya watu flani..


naombe nikwambie kitu......

digging reality is too costful sana..sana tena snaa..

Kuna watu wanarisk maisha kwa ajili ya wewe ule nini leo..kila kitu unachokifanya nyuma yako kuna kundi linalowezesha yote hayo na hutakaaa ulijue mpka unakufa ( kama ukiamua)..

Kanisa au taasisi za dini zimeshikilia kila tafiti unayoijua wewe katika ulimwengu huu kwa faida wanayoijua wao hata kama ni baada ua miaka Milioni ijayo..

Leo hii unaona maabara kubwa kabsaa duniani zilizoko switzerland,America na kwingineko zinategemea hela au michango ya pesa kubwa snaa toka kwa watu...

Yani wewe na mimi ndo wawezeshaji wakubwa wa hayo yote ila indirect form..

Njia waliyobuni ni kumwandaaa na kumteka Mwanadamu ili awezesha advancement ya kila kitu..hilo grup la watu wachache wanaofanya excavation kwenye maaeno ya siri haliwezi kumudu garama zote...

Ndipo mpango kabambe ukaanzishwa wa kuwapa watu illusion kuwa kuna mtu mmoja anaitwa Mungu na anafanana na wewe kabsaa kwa hiyo inabidi kila mmoja amwabudu na tuwe yunajitoa kwa halu na mali na anapaswa kuogopwa na hutakiwi kuhoji uwepo wake..

Kuanzia hapo saikolojia ikawaingia wanadamu na wakaaanza kila wakitutana wanatoa sadaka( kwamba wanamtolea bwna) ..

taratibu naona unaanza kunielewa.....

lets go.....



Ukusanyaji wa pesa ya kufundi wao watu ambao lengo lao kubwa ni kuraise awareness and conciousness juu ya universal energy fild ambayo imeshikilia mambo yote..

Ndo mana vatcan imeandaaa watu maaalumu( Watawa= mapadre,maaskofu,masiter,makadinari, wachunguji katika madhehebu tofauti) ili wakusimamie zoezi endeleve la ukusanyaji wa pesa ambayo ni mwendelezo mpka mwanadamu anakutwa na mauti ndo mwisho wake wa kujitolea ,ili hali kuendelea kupata pesa ya kufund miladi mikubwa hiyo..

Vivyo hivyo katika islamic religion..there is indirectly way mnachangia..

Kwa hiyo ndo mana unashangaaa vatcan inapeleka wapi pesa. ..

Ni lini pesa wanayochanga waumini inaenda wapi..?? (kwamba wanapewa masikini au ndo wanazidi kunyonywa zaidi...think critically)

Bada ya hapo kanisa kama kanisa likaamua kuanza kumiliki na kujenga vitega uchumi vyote ili kila mtu ahusike kwenye universal contribution ya pesa( funding system) ili kukamilisha mambo yao..

Katika kila kitu sasa hivi wanacontrol wao ndo mana ukusanyaji wa pesa umekuwa mkubwa na miladi inakimbia kwa kasi kwani mpkaa sasa ni kiwango kidgo sana unachowachangia directly kanisani ila mara nyingi unachangia kupitia social network ( miladi ambayo inaendeshwa kwenye jamii)


akwa hiyo mkuu unatakiwa ujue kuwa kuanzishwa kwa makanisa kuna lengo kubwa moja tu nalo ni kumcontrol mwanadamu kifikra zaidi asihoji juu ya source ya mambo yote haya.

The bible as well as the Quran ni man made scriptures zenye lengo moja ola kututawanya tu namna ya kucontribute kwenye universal system na ndo mana kutokana na upungufu mkubwa wa elimu hiyo tunajikuta tunaweka mbele zaidi mambo ya udini..

Nadhani utakuwa unaelewa sasa kuwa NASA inapata wapi pesa ya kuendesha mambo ya Space,hivyo hovyo kwa CERN PROJECT na mpango wao wa kugundua Anti matter kupitia Hydron collider system chamber yao..

Mkuu unajua hali za michango ikoje kwenye nyumba za ibada za waislamu? au hiyo michango hukusanywa wapi na nani?
 
Kwa maelezo yake kulola aliwai kuoneshwa shetani alivyo hivyo dai lako kuwa shetani hawezi kuonekana litakuwa lina utata. Pili kwa sisi tunaoamini Biblia Shetani alimtokea Yesu na wakahojiana kwa muda. Maana yake walionana the same kwa Eve. Tunaaarifiwa kuwa shetani anaweza kuchukua sura tofauti tofauti kulingana na muktadha. Ni sawa na watoto wake mapepo au majini ambao wanaweza kuwa wanawake wazuri, wanaume wazuri au etc
lifecoded
Uyo yesu ulikua naye au umekuta hadithi tu??
 
we jamaaa acha kukalili maandiko..una uhakiksa kuwa shetan alimtokea eva kwa umbo kama unavyodhani la kibanadamu..???

Acha kuangalia movie za imagination story ukajua yule bro( shetani) ni kama mtu kabsa...

Are you seriuzly..??
...unadhani anaonekana kama binadamu...??

halafu hao wanaojifanya kutoa ushuhuda kuwa walikutana na Bro( shetani) 🙂 kama wanavyodai....hakuna kitu kama hicho ..ile ni njia ya kuuza CD zao zenye hayo maelezo yanayojaribu kumdadavua bro ,ila bro hayuko kama unavyofikiria....

hizo ni propaganda wabongo tunapenda kuamini kupitia masimulizi...

mi nakupa homework jaribu kutafuta ushuhuda wa kweli wenye evidence juu ya shetani kama hao wanaotupanushuhuda wakupe na video yake..kama utawaona wakifanya hivo...
...

kama shetani ana umbo la binadamu mi najichoma moto
Mi nakunywa sumu
 
Nimetoa ushuhuda wa mtu Moses Kulola( Unluckily he is dead). Pia nikasema mashetani yaweza jitokeza kama mapepo au majini watoto/ watenda kazi wa shetani if yes mbona kuna watu washakutana nao wengi tu na wanasimulia kesi zinazofanana.

Pia sisi biblia inatufundisha kuwa shetani anaweza jigeuza malaika wa nuru. Na tunasoma na kuamini kuwa malaika washawatokea watu mbalimbali ktk biblia ina maana shetani yupo na anaweza kuchukua physical form sawa na malaika. Sasa kuamini haya au kutokuamini kila mtu na lwake lakini Mimi ndivyo ninavyoamini kuwa yupo ila hana nguvu kwa Yesu Kristo.
Sisi tunataka kujikomboa kwenye matango pori mwenzetu unakazana kuyatafuna.
 
Kuna watu wanachanganya kwenye mambo haya magumu na yenye siri kubwa juu ya uwepo wa shetani na Mungu.

Shetani hawezi kuonekana kama Mungu hajawahi kuonekana ,kumbuka both spirits are the same by mode of existance according to Spiritual analysis..

Hakuna mtu ambae amewahi kumuona shetani hata kama ni freemasoni wa degree ya namna gani..

I swear kwa damu yangu..hizo zote ni propaganda za kumfanya mwanadamu azidi kuamini uwepo wa shetani ili akazane kutafuta uhusiano kati ya mafanikio ya haraka na uwepo wake.kitu ambacho badae wakifika huko kwa wenye ukimwengu huu wanawaelekeza jinsi alama hizo zinavyofanya kazi...

Kiukweli ,there is no such kind of a thing kuwa shetani ana umbo la namna hiyo..nakataaa kwa evidence zote..na kama kuna mwenye proof naomba nifanye nao battle kwa hili.

Simply because his presence is unprovable hence his image is non identifiable.

..........

kuna kitu watu wanachanganya kati ya alama kama mafuvu( skull and bones),misalaba(cross signs), alama za X ,pembe,pete n.k ambazo ni alama zinazomuwezesha mwanadamu kuingia au kusynchronise na universal energy( high energy flow system ) ambayo inamfanya mwanadamu apate maarifa mengi pamoja na namna ya kuistudy nature ilivyo..

Alama hizo wala sio za shetan ila ni alama ambazo wajuzi wa zamani(Ancients) walikuwa wanazitumia kupata nguvu za kila aina ya kitu wanachokitaka..

Ila watu wasioelewa jinsi zinavyofanya kazi wanakimbilia kusema ni alama ya shetani..

Kanisa katoliki linatumia misalaba madhabahuni pamoja na vyombo vyote vya altareni vina alama na maumbo kama ya misalaba( obelisk) katika kutrap nguvu( energy) from higher worlds..ila watu wanamisinterprete kuwa ni alama za kishetani...

sio kweli..narudia tena na kukazia sio kweli..

Ipo siku nitatoa elimu zaidi naman misalaba inavyofanya kazi na kwanini wakristo au watu wanaoamini juu ya uwepo wa mungu wameambiwa kuvaaa misalaba na kuitumia kwenye makaburi tofauti na alama zingine..
tunasubiri somo mkuu
 
Hizi kitu hizi ni kuwa makini sana, maana sioni mwanga mbele wakati giza ni totoro na wanasema NURU NA GIZA HAVICHANGAMANI.
 
Nikwambie kitu...

Samahani lakini sipendi uone kama nakukwaza ila napenda ujue namna mambo yalivyo..

Unajua kazi kubwa au mchango mkubwa wa kanisa katoriki na washirika wake kina nani naniii( madhehebu mengine) katika role ya ukuaji wa sayansi ..??

Unajua kazi kubwa ya Islamic religion katika role ya ukuaji wa sayansi na technlojia mpaka kukufikisha hapa ulipo...??

Unajua hata hiyo simu na nguo unazovaa ni matokeo ya sayansi ?? ( shifting negative awareness to positive awareness and knowlege ya grup dogo la wanadamu ) ambayo yanafanywa na kundi la jamii ya watu flani..


naombe nikwambie kitu.
.....

digging reality is too costful sana..sana tena snaa..

Kuna watu wanarisk maisha kwa ajili ya wewe ule nini leo..kila kitu unachokifanya nyuma yako kuna kundi linalowezesha yote hayo na hutakaaa ulijue mpka unakufa ( kama ukiamua)..

Kanisa au taasisi za dini zimeshikilia kila tafiti unayoijua wewe katika ulimwengu huu kwa faida wanayoijua wao hata kama ni baada ua miaka Milioni ijayo..

Leo hii unaona maabara kubwa kabsaa duniani zilizoko switzerland,America na kwingineko zinategemea hela au michango ya pesa kubwa snaa toka kwa watu...

Yani wewe na mimi ndo wawezeshaji wakubwa wa hayo yote ila indirect form..

Njia waliyobuni ni kumwandaaa na kumteka Mwanadamu ili awezesha advancement ya kila kitu..hilo grup la watu wachache wanaofanya excavation kwenye maaeno ya siri haliwezi kumudu garama zote...

Ndipo mpango kabambe ukaanzishwa wa kuwapa watu illusion kuwa kuna mtu mmoja anaitwa Mungu na anafanana na wewe kabsaa kwa hiyo inabidi kila mmoja amwabudu na tuwe yunajitoa kwa halu na mali na anapaswa kuogopwa na hutakiwi kuhoji uwepo wake..


Kuanzia hapo saikolojia ikawaingia wanadamu na wakaaanza kila wakitutana wanatoa sadaka( kwamba wanamtolea bwna) ..

taratibu naona unaanza kunielewa.....

lets go.....


Ukusanyaji wa pesa ya kufundi wao watu ambao lengo lao kubwa ni kuraise awareness and conciousness juu ya universal energy fild ambayo imeshikilia mambo yote..


Ndo mana vatcan imeandaaa watu maaalumu( Watawa= mapadre,maaskofu,masiter,makadinari, wachunguji katika madhehebu tofauti) ili wakusimamie zoezi endeleve la ukusanyaji wa pesa ambayo ni mwendelezo mpka mwanadamu anakutwa na mauti ndo mwisho wake wa kujitolea ,ili hali kuendelea kupata pesa ya kufund miladi mikubwa hiyo..

Vivyo hivyo katika islamic religion..there is indirectly way mnachangia..

Kwa hiyo ndo mana unashangaaa vatcan inapeleka wapi pesa. ..


Ni lini pesa wanayochanga waumini inaenda wapi..?? (kwamba wanapewa masikini au ndo wanazidi kunyonywa zaidi...think critically)

Bada ya hapo kanisa kama kanisa likaamua kuanza kumiliki na kujenga vitega uchumi vyote ili kila mtu ahusike kwenye universal contribution ya pesa( funding system) ili kukamilisha mambo yao..

Katika kila kitu sasa hivi wanacontrol wao ndo mana ukusanyaji wa pesa umekuwa mkubwa na miladi inakimbia kwa kasi kwani mpkaa sasa ni kiwango kidgo sana unachowachangia directly kanisani ila mara nyingi unachangia kupitia social network ( miladi ambayo inaendeshwa kwenye jamii)


akwa hiyo mkuu unatakiwa ujue kuwa kuanzishwa kwa makanisa kuna lengo kubwa moja tu nalo ni kumcontrol mwanadamu kifikra zaidi asihoji juu ya source ya mambo yote haya.

The bible as well as the Quran ni man made scriptures zenye lengo moja ola kututawanya tu namna ya kucontribute kwenye universal system na ndo mana kutokana na upungufu mkubwa wa elimu hiyo tunajikuta tunaweka mbele zaidi mambo ya udini..

Nadhani utakuwa unaelewa sasa kuwa NASA inapata wapi pesa ya kuendesha mambo ya Space,hivyo hovyo kwa CERN PROJECT na mpango wao wa kugundua Anti matter kupitia Hydron collider system chamber yao..
Nimepitia hizi hoja na nimefurahi sana. Naona ziliandikwa mwaka ambao nilikuwa kwenye box ya uumini wa kiislamu. Sasa na mimi najiuliza mipesa inayotolewa na waislamu kwa anili ya kuhiji hua inaenda wapi? Kwa kutoka kwenye dini nimefahamu bila shaka kwamba sijui wala sikuwahi kujua lolote!

Sent from my moto g power (2021) using JamiiForums mobile app
 
Kuna kitabu kinaitwa Baphomet: The temple mystery revealed cha Tracy Twyman. Humo historia ya Baphomet imehusishwa na vitu vingi lakini vingi vikiwa vinahusiana na Esoteric Christianity, Early Christian cults waliowekwa kwenye group moja liitwalo Gnostics...Hawa Gnostics walikuja kuangamizwa na Kanisa Katoliki. Inasemekana Knight Templar walijifunza elimu fulani kutoka kwenye mojawapo ya wakristo hao...hasahasa kutoka Kwa waliojulikana kama Ophites. Hawa Ophites moja ya mambo yao ilikuwa ni venerations of the snakes, tamaduni ambayo ni ya zamani zaidi ya ukristu, inarudi nyuma zaidi hadi Misri kwenye mafundisho ya Asclepius na Hermes au Thoth (Tehuti). Huyu Tehuti aliabudiwa kama Mungu wa Maarifa na Sayansi...Alama yake ni staff entwined by two snakes. Elimu ya huyu Tehuti imesurvive kama Hermeticism, ikimaanisha elimu ya Hermes.

Pia Hawa Templar waliwahi kupigana na majeshi ya ukombozi ya kiislam yaliyoongozwa na Saladin, lakini pia inasemekana kuwa baadaye walikuja kuwa na urafiki wa siri, ambapo hawa Templars walijifunza mambo flani kutoka kwao ikiwa ni sehemu pia ya mafundisho ya Hermes lakini yaliyosurvive kupitia mystics of Islam wanaoitwa sufis, hasahasa Hashashins, yaani watumiaji wa hashish ...stori yake ni ndefu sana...lakini Kwa kifupi ilihusishwa na baptism of wisdom, ubatizo wa busara, ubatizo wa pili, wa moto au wa roho (fire = spirit)...wisdom inayohusishwa na roho mtakatifu, njiwa/dove/columbia, Divine Sophia, Mother Goddess, Mama aliyezaa kila kitu, Mama wa Mungu, Madonna of the virgin birth, aliyezaa bila kutungwa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom