Jina "Baphomet" limetoka wapi na asili yake ni wapi?

Jina "Baphomet" limetoka wapi na asili yake ni wapi?

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,778
Reaction score
8,204
👉Jina hili asili yake ni kutoka katika enzi za kukomesha uasi katika kanisa katoliki katika miaka ya 1100,: ambapo kwa kiimgereza nyakati hizo ziliitwa inquisition, pia ni wakati ambapo kulikuwa na mateso juu ya wapiganaji wa kidini kwa jina walifahamika kama KNIGHT TEMPLAR walikuwa wakiteswa ili wafichue siri zao na wakubali kufuata dini kwa mujibu wa viongozi wa kanisa wa nyakati hizo.

👉Kwa mujibu wa waandishi wa enzi za vita vya msalaba yaani CRUSADE, wanasema kwamba wapiganaji hao (Knight atemplar) walikiri kumwabudu mungu wa wapagani kwa jina Baphometh.

👉Hata hivyo, baadhi ya wasomi wanaamini kwamba "Baphometh" ni neno la upotoshaji lililo tokea kimakosa kutoka kwenye jina "Mohamet" ambalo hutumiwa kumrejelea nabii Muhammad, ambapo ni jambo linalo zua utata zaidi.

👉Lakini kadri miaka ilivyo songa mafumbo na siri kuhusu alama hiyo kuhusishwa na Knight Templar yaliendelea kuzidi na ndivyo ufafanuzi kuhusu alama hiyo ulizidi kutofautiana.

👉Moja ya ufasiri wa neno hilo "Baphomet" unapatikana katika kitabu cha Da Vinci Code kilicho andikwa na Dan Brown ambapo neno "Baphomet" limefafanuliwa na kutafsiriwa kama neno linalo maanisha "Sophia" au busara.

BAPHOMET KWA MUJIBU WA LEVI.

👉Picha maarufu zaidi ya Baphomet ilichorwa na (mchawi) mwana mizungu wa Ufaransa Eliphas Levi mwaka 1856 katika kitabu chake cha "Transcendental Magic: its Doctrine and Ritual."

Ambapo alimchora kiumbe HUNTHA mwenye mabawa na mwenye pembe na mwenge ulio katikati ya pembe hizo kichwani.

Kuna mchoro pia wa pembe nane kwenye paji la uso.

👉Mikononi mwake Baphometh kumeandikwa maneno ya kilatini SOLVE (tenganishwa) na COAGULA (fungamanisha) - ambazo ni nguvu za kuunganisha na kutenganisha ambazo zilitwaliwa kutoka kwa Mungu.

👉Mchoro wa mwanamizungi Eliphas alevi ndio ulio sababisha kutokea ama kuundwa kwa sanamu inayotumiwa na Satanic Temple au watu wa Hekalu la Shetani

Baphomet ni mwenye jinsia mbili kwa pamoja,na nusu mnyama na nusu binadamu.

.SALUTI YA VIDOLE VIWILI KATIKA ALAMA YA BAPHOMET

👉Alama au sanamu ya Baphomet ina vidole viwili vilivyo elekezwa juu mkono wa kulia na viwili vilivyo elekezwa chini mkono wa kushoto, ambapo maana yake ni "kama ilivyo jui, na chini iwe pia".

👉Maneno hayo "kama ilivyo juu ndivyo ilivyo chini" ni maneno ni maneno maarufu miongoni mwa wenye kuamini katika Mizungi na mafumbo (mysticisms and esotericisms)

👉Chanzo cha maneno hayo ni kazi za kale za msomi Hermes Trismegustus, ambaye vitabu vyake vilikuwa maarufu sana enzi za kipindi cha mwamko wa sanaa na mageuzi ya kidini, maarufu kama Renaissance and Reformation barani Ulaya.

👉Maneno hayo pia hutumiwa kuhusiana na sayansi, vitu vyote na Mungu, lakini Levi alisema kwamba kwa kutumia Ishara hiyo, Baphomet wake alikuwa ana maanisha kuwiana sawa kati ya Fadhila na haki (katika Kabbalah).

ITAENDELEA
 

Attachments

  • Screenshot_20250411_132046~2.jpg
    Screenshot_20250411_132046~2.jpg
    229.2 KB · Views: 41
DUNIA INA MENGI SANA AMBAYO SISI WAMATUMBI WA BUZA HATUYAJUI KWA UNDANI
 
Back
Top Bottom