Bango la "Mwizi Mkenya!" Mlimani City ni Ubaguzi!, Udhalilishaji!, na Very Undiplomatic Gesture!.

Pasco umegonga bull, lile bango linamuhukumu kinyume cha sheria na haki za binadamu, she is INNOCENT until proven otherwise; tukubali tumekosea na Wakenya will not take kindly to this kind of actions; je tuendako watanganyika walioko Kenya watakuwa salama au tunawatengenezea mazingira gani haya?! Tukumbuke kiendacho hurudi; wahusika wachukue hatua stahiki.
Kama watanzania wameenda kenya kutuwakilisha
kwa kuwaibia wakenya,basi wadhalilishwe kwa vitendo vyao
vya wizi ili warudi nyumbani wakutane na mkono wa sheria.

Siungi mkono mhalifu kwenda nchi za watu kufanya uhalifu
afu tuseme eti anaiwakilisha nchi.
Ni aibu ukienda nchi ya watu ukajikuta unaangaliwa
kwa jicho la tatu kisa waliokutangulia walifanya matendo ya aibu
na wewe unabebeshwa msalaba usiokuhusu.Ndo maana
maana hapo mwanzo nikasema unaweza kuta kitendo hiki kafanyiwa
na wakenya wenzake ili kuepuka kuhukumiwa kama kundi
na badala yake kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe.
 
WE UNASEMA NN ATI? Kwan cha ajabu ni kipi? Huyo si mwizi kweli au kasingiziwa? Au we unatetea wezi?? Na si kweli anatokea Kenya au we ulitaka wezi wote watokee Tandale?
Acha atangazwe ili ajulikane mapema kabla hajaleta madhara zaid ya wizi, Watu wengi tumemjua kupitia hiyo picha, je wasingemtangaza then kesho akakuibia wewe, ungefurahi, au una kauhusiano nae hivyo imekugusa??...ngoja na mie niendelee kuituma kwenye magroup ya whatsapp wamjue vizuri ila wawe na tahadhari pindi wamwonapo...huku kwetu wezi wanachomwa moto kabsa..nini kutangazwa bana.. dada unakuwa mwivi kah, SHAME ON HER!!!

Umenichekesha sana hadi nimetoa machozi!!!!!!!
 
Naunga mkono hoja, hakika huo ni udhalilishaji mkubwa hapakuwa na sababu ya kumbebesha hilo bango na maandishi yenyewe yana ukakakasi sana kama ulivyosema kidiplomasia haiko sawa.
Kifupi mtuhumiwayoyote anatakiwa kufikishwa vyombo vya sharia Period.Polisimuwasakewahusika. Hili halikubaliki!
 
Watu wanakuza hili jambo bila.sababu zamsingi. Angeiba mtu kutoka moshi se wangeandika vivyo hivyo sasa hapo tatizo lipo wapi? Huyu hakuja kuiwakilisha kenya amekuja.yeye.kama yeye ila ilikuwa lazima kumidentify tu.
Ukweli ni kuwa kutetea wezi ni.rahisi sana hasa kama hujawahi kuibiwa ama kushuhudia mtu wako wakaribu akiibiwa. Vp wale walokuwa wanapita njia za mwendo kasi walivokuwa wanaandikwa mpaka na makabila,kazi na dini zao? Hiyo njia.ni nzuri kupeleka ujumbe kokote kuwa ukibainika ni.mwizi utawekwa hadharani hata kama.umetoka wapi. Naunga mkono 100%+ kwa alichofanyiwa na ingekuwa mapendekezo yangu angekatwa na mkono.kabisa.
 
Pasco huwa Unapenda sifa za ajabu ajabu!! Hivi unawafahamu wa Kenya wanavyo tufanyia wa Tz au unajipendekeza tu? Mwizi yoyote awe Rais, awe Mmarekani, awe Mrasia,NK ni kuuwa tu, bora yake kapewa bango lenye uzito wa 1/6KG.
 
Dah waha great thinkers wa kizazi hiki nao chai tupu! Sijui km mleta uzi unajua jinsi wakenya wanatochukulia sisi watz?? Hatulipizi baya kwa baya ila hukuna haja ya kuandika essay ndefu isiyo na tija kumteta mwizi!Kenyan ni wezi every where na wanaukabila sana,na mtz ukifanya nao kazi ndio utajua ila km hujafanya nao kazi lazima utaandika essay ndefu kuwatetea km hii
 
Sio Mugabe na Trump pekee, bali hata rais wao Kenyatta amewahi wasema raia wake kwa wizi. Tena ni baada ya Mugabe na Trump kusema, ni kama alikuwa anaunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

Bila kusahau kauli ya Jacob Zuma kuhusu hulka za najirani zetu hawa - wana tatizo si bure!

Mmesahau yule msichana/mwanamke aliye tiwa mbaroni huko Hotelini Iringa juzi juzi hapa alikutwa na rundo la funguo bandai kwenye mkomba wake - CCTV ndiyo ilisadia kuwanasa/kuwarecord wakifanya uharifu binti huyo alikuwa akishirikiana na wanaune aliyo kuja nao kutoka Kenya, kama si CCTV sina shaka Hotel Management wange watilia shaka wafanyakazi.

Wanawake wa huko wana guts za ajabu sana - unawezaje kuingia nchi ngeni ukawa na ubavu wa kufungua fungua vyumba vya Hoteli bila wasi wasi - je Mungiki kama hao wakukute chumbani peke yako si wanakumaliza!
 
Kuna vitu vya kutetea lakini hivi vya utetezi wa wezi ni vya kupuuza...mtu kaiba kweli halafu katoka kenya huo si ndio ukweli wenyewe??..sasa hapo kosa liko wapi au ulitaka bango liandikwe mwizi toka burundi??..halafu ungeanza na utetezi wa haki aliyeibiwa ningekuelewa sana lkn moja kwa moja umeanza kwa nguvu kutetea haki ya mwizi .dah

Kama phrase "Mwizi kutoka Kenya" ingekuwa ni aina fulani ya pekee ya wizi, ningeona pengine kudhalilishwa kisaikolojia kwa huyo mwizi kusingehitaji utetezi wa kiwango kilichotumika. Kwani bango lingesomeka "Mimi ni mwizi" lingeathiri vipi na kwa kiasi gani feelings zako dhidi ya kitendo cha wizi alichokifanya huyo mwizi?
 
W
Nimesoma mahali kutokea kwa tukio la wizi eneo la Mlimani City,
CnWQ33pXgAA_4-N.jpg:small

Msichana kutoka Kenya atuhumiwa kwa wizi M. City, atembezwa na ...
mwizi huyo ni mwanamke kutoka nchini Kenya. Baada ya kukamatwa, kabla hajakabidhiwa kwa vyombo husika, walimtia kibano, kisha kumshikisha bango lililoandikwa "Mimi ni Mwizi Kutoka Kenya!" na kumtembeza ili watu wamuone!.

Kitendo alichofanyiwa huyu dada sio tuu ni udhalilishaji wa hali ya juu, kinyume cha haki za binaadamu, na pia ubaguzi wa hali ya juu, unaoweza kujenga chuki sio dhidi ya mwizi aliyekamatwa, bali kwa Wakenya wote, hivyo hapa aliyedhalilishwa sio bidada mwizi kutoka Kenya, bali nchi nzima ya Kenya kuonekana ni wezi!, jambo ambalo sio zuri kidiplomasia, hivyo linapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa wahusika wakuu wote waliohusika na udhalilishaji huu kuchukuliwa hatua kali, ya mwanzo ikiwa ni kutimuliwa kazi, na kupandishwa kizimbani kwa udhalilishaji wa raia wa Kenya asiye na hatia!.

Kuna watu wata support udhalilishaji huo, kwa hoja kuwa kweli ni mwizi kwa sababu ameshikwa ready handed, na pili kweli ni raia wa Kenya, lakini sisi Tanzania tunafuata mfumo wa sheria tuliorithi kutoka kwa Waingereza, mamlaka pekee yenye kuweza kum declare mtu ni guilt ni mahakama pekee, hivyo everybody is "presumed innocent until proven guilt" tena "by the court of competent jurisdiction", hivyo kitendo cha kumshikisha bango kumuita mwizi ni kumhukumu an innocent victim bila kumfikisha kwenye vyombo halali vya kisheria!.

Wizi ni tabia ya mtu, mtu yoyote anaweza kuwa kuwa mwizi, kama lengo lilikuwa ni kumdhalilisha ili kumuaibisha mbele ya umma kuwa bidada ni mwizi, then bango lingeishia kwa maneno "mimi ni mwizi!" hakukuwa na sababu kuiweka nchi yake yote ya Kenya, kuonyesha yeyote anayetoka Kenya, ana possibility kuwa mwizi!.

Haki za Binaadamu.
Hata kama ni kweli kweli bidada yule ni mwizi, hata mwizi anastahili heshima kwa kutokudhalilishwa utu wake kwa kumfanya a subject to ridicule!. Hata wauwaji pia huwa wanastahili heshima na utu, na hata wanaohukumiwa kunyongwa, wananyongwa kwa utu na heshima fulani, na hata ikitokea siku yako ya kunyongwa ikifika, kabla adhabu hiyo haijatekelezwa, anakuja daktai kukupima kuhakikisha ni mzima na uko bukheri wa afya, ikikutikana unaumwa hata kichwa tuu, utatibiwa kwanza, upone ukiwa mzima kabisa ndipo ashabu itekelelezwe!. Kwa msio jua, hata ile siku Saadam Husein alinyongwa, alivishwa suti!, hata Osoma kabla hajazikwa baharini, aliswaliwa Kiislamu na kuzamishwa kwa kuelekezwa upanda wa Kibla!.

Diplomasia.
Tanzania tunapojianjaa kuingia kwenye Mtangamano wa nchi za Jumuiya ya Afika Mashariki, yunatakiwa kuanza kujihesabu sisi wote ni watu wamoja, hakuna Mtanzania, Mkenya, Mganda, Mrwanda. Mrundi au Msudani, we are all one!, hivyo vitendo vyovyote vya kumbagua mtu kwa utaifa wake ni ubaguzi, tukumbuke tuna Watanzania wengi nchi za wenzetu, na huko pia wanafanya uhalifu, kama ndio kwanza tunaanza kushikishana mabango ya mimi mwizi, tunakwenda wapi?!.

Uzalendo
Kuna baadhi ya matukio yakitokea, tunapaswa kuyanyamazia kwa kutanguliza uzalendo ili kuificha siri ya jinsi tunavyowatendea wenzetu, lakini watu wanaojitanabaisha kuwa ni watetezi wa haki za binaadamu, kunapotokea mizania ya kutanguliza nini mbele kati ya uzalendo na ukiukwaji wa haki za binaadamu, natanguliza haki kwanza, ndipo uzalendo kwa nchi yangu unafuatia!. Tanzania tunapaswa tutende haki kwanza, ndipo tuje kwenye uzalendo.

Ni matumaini yangu, vyombo husika vitaliona hili na kuchukua hatua stahiki kuhakikisha tukio kama hili halijirudii.

Nawatatakia Furahi Dei Njema.

Pasco.
Pasco wa jf ni mzalendo ila pia ni mpigania haki za binaadamu ni hapa chini ni rejea ya baadhi ya mada zake kutetea haki na kupinga, unyanyasaji, udhalilisha na ubaguzi wa aina yoyote!.
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality ...
Chan. Ten:Inastahili Pongezi kwa "Freedom of Expression, Watangaza ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ..
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili .
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki .
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote .
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Naibu Spika Anna Makinda ni Dikteta! |
Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu Unaofanywa na ...
Kutoka Geneva: Prof Mchome atoa msimamo kuhusu mpango wa ..
Je, Kila utumbuaji ni wa haki, au kuna kumkomoa Kikwete .
Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani! | J
Kitendo Cha Rev. Mtikila Kugomea Arrest!, Kinastahili Pongezi ...
Wito kwa Baba *****: Watendee Haki Kina ***** Wote Ili Nao Wapate ...
Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu wali-teswa ...
Pasco,
Nakusalimu kijana. Pili pamoja na kwamba sikufahamu nimekupa nafasi katika kundi la waungwana waliostaarabika na wanaostshili heshima siku zote kwa kutambua kitendo kilichofanywa na wapuuzi kwamba ni cha udhalilishaji.
Wazazi wako waliokelea na kukupeleka shule wanastahili heshima kuu.
Bila shule na malezi uliyoyapata katika mazingira mema ya kibinadamu usingeliliona tendo hili kwamba halifai
Kuna wale wasiojua chochote hata shule zao za shida wanajua kubeba visimu na kuandika ujinga unaotoka vichwani mwao bila kujua kizuri na kibaya katka misingi ya kibinadamu.
Peruzi nakala ya jf utawaona wengine wameishakuuliza kama umewahi kuibiwa.
Haki za binadamu zinapinga udhalilishaji,kama ulivyoeleza sio taifa la Kenya lilioiba au kumtuma mwanamke huyu kuiba.
Kuna vyombo vya sheria husika na makosa ya jinai na hushughulikia maswala haya katika utaratibu na kanuni xilizopangwa.
Kumfunga mtu bango na kumzomea is an assassination of character which is liable for prosecution, otherwise wangemwacha huru baada ya kuchafua image yake.
Diplomasia kama ulivyoieleza ni jambo linalowekwa mbele na nchi zinazofungama mfano jumuiya ya Afrika mashariki tunaimba kila siku kufungamana kiutamaduni,kiuchumi, kisiasa na kimaendeleo kwa ujumla, sasa unapomfanyia matendo kama haya Raia kutoka katika nchi za Jumuiya unakuwa unafanya nini? Kesho wako amefanyiwa hivyo Kule Nairobi wale wanaololoma utawasikia maana walisema wahenga debe tupu ndio lenye kelele.
Nimeeleza haya sababu najua choko choko za nchi,Niliona rangi zote wakati Mhe Jakaya walipotupiana maneno na Gen Kagame maana naishi Rwanda.
Siku zote treat an alien in your country with great Care.
Hivyo nawashauri wale waropokaji wayachukulie maswala mengi ya wageni kwa busara sababu wengi wao ni Buguruni Mbagala mbagala tegeta hawajavuka mipaka unawexa teswa nchi ya watu ukasikia kufa.
A,W,W.
 
Safari yetu Wabongo bado ndefu sana! Huyo mwanadada amshukuru Mungu kwa yeye kuumbwa mwanamke na kwa kujikwaa kwenye eneo lenye watu ambao kidogo wameuona mwanga. Vinginevyo, angekuwa mwanaume halafu amekamatwa na wale ambao hawajauona mwanga, pengine hivi tunavyoongea angekuwa ameshashawahishwa kuzimu kwa matairi na moto wa petrol!
 
Hivi watanzania sijui nani kawaloga? ujuaji mwingi sana na kujiona wamestaaribika sana. Mtu kaiba, nchi anayotoka ni Kenya, watu wamekuwa waungwana hawajampiga, ila wamemuadhibu kistaarabu kwa kujitanganza, watu mnaleta upuuzi wa haki za binadamu, angekuwa binadamu huyo angeiba? Mlishasikia ni namna gani watanzania wakiiba huko Kenya yanayowakuta?? Acheni siasa watanzania, ndiyo maana hatupigi hatua.
 
wakenya huwa siku zote wanawaza kuwaibia watanzania kama wanaona ni udhalilishaji wasingekuwa wanatangaza mlima kilimanjaro upo kwao ,wasingtangaza olduvai gorge ipo kwao hivyo ni sahihi kuwaonyesha tumechoka na wizi wao ndio maana mugabe aliwaumbua
 
Just remember this: two wrongs don't make a right!

Calling her a thief was probably not of great concern, but tying the act of theft (that she committed) to her Kenyan citizenship was definitely offensive to the nation of Kenya, because the two bundled matters have nothing to do with each other!
 
Back
Top Bottom