Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,682
- 119,318
Wanabodi,
Nimesoma mahali kutokea kwa tukio la wizi eneo la Mlimani City,
Msichana kutoka Kenya atuhumiwa kwa wizi M. City, atembezwa na ...
mwizi huyo ni mwanamke kutoka nchini Kenya. Baada ya kukamatwa, kabla hajakabidhiwa kwa vyombo husika, walimtia kibano, kisha kumshikisha bango lililoandikwa "Mimi ni Mwizi Kutoka Kenya!" na kumtembeza ili watu wamuone!.
Hata kama kweli ni mwizi, lakini kitendo alichofanyiwa huyu dada sio tuu ni udhalilishaji wa hali ya juu, ni kinyume cha haki za binaadamu!, na pia ni ubaguzi wa hali ya juu wa kikanda, unaoweza kujenga chuki sio tuu dhidi ya mwizi aliyekamatwa, bali kwa Wakenya wote, hivyo hapa aliyedhalilishwa sio bidada mwizi kutoka Kenya pekee, bali nchi nzima ya Kenya na Wakenya wote walioko nchini kufuatia binti yao kukamatwa akiiba, hivyo kujenga posibilty ya kila Mkenya kuwa mwizi!, jambo ambalo sio zuri kidiplomasia, hivyo linapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa wahusika wakuu wa udhalilishaji huu kuchukuliwa hatua kali, ya mwanzo ikiwa ni kutimuliwa kazi, na kupandishwa kizimbani kwa udhalilishaji wa raia wa Kenya asiye na hatia!.
Waungaji Mkono Udhalilishaji Huu.
Najua kuna watu wata support udhalilishaji huo, kwa hoja kuwa kweli bidada huyo ni mwizi kwa sababu ameshikwa ready handed, na pili kweli ni bidada huyo ni raia wa Kenya, hivyo kwa vile ni kweli ni mwizi na ni kweli ni Mkenya, then alichofanyiwa ni haki yake!. Na wengi wataokasuppot hili, wataunganisha na uchungu wa kuibiwa, hivyo kwao hata adhabu ya kushikishwa tuu bango, ni ahabu ndogo, wangewish apate kipigo haswa cha mbwa mwizi, hadi auliwe kwa kipigo au hata kuchomwa moto!. Hawa sitawalaumu, ni levels tuu za uelewa masuala ya haki, kwao mwizi hana haki, hata mwizi wa kuku, adhabu ya kifo kwa kuchomwa moto kwao ni adhabu stahili au stahiki!.
Utawala wa Sheria (The Rule of Law).
Sisi Tanzania ni nchi ya haki inayofuata mfumo wa utawala wa sheria, "the rule of law" tunafuata mfumo wa sheria tuliorithi kutoka kwa Waingereza, mamlaka pekee yenye kuweza kum declare mtu ni guilt ni mahakama pekee, hivyo everybody is "presumed innocent until proven guilt" tena "by the court of competent jurisdiction", hivyo kitendo cha kumshikisha bango kumuita mwizi ni kumhukumu an innocent victim bila kumfikisha kwenye vyombo halali vya kisheria!.
Wizi ni Tabia ya Mtu sio Tabia ya Nchi
Wizi ni tabia ya mtu, mtu yoyote anaweza kuwa kuwa mwizi, kama lengo lilikuwa ni kumdhalilisha ili kumuaibisha mwizi huyo mbele ya umma kuwa bidada ni mwizi, then bango lingeishia kwa maneno "mimi ni mwizi!" hakukuwa na sababu kuiweka nchi yake yote ya Kenya, kuonyesha yeyote anayetoka Kenya, ana possibility kuwa mwizi!.
Haki za Binaadamu.
Hata kama ni kweli kweli bidada yule ni mwizi, hata mwizi anastahili heshima kwa kutokudhalilishwa utu wake kwa kumfanya a subject to ridicule!. Hata wauwaji pia huwa wanastahili heshima na utu, na hata wanaohukumiwa kunyongwa, wananyongwa kwa utu na heshima fulani, na hata ikitokea siku yako ya kunyongwa ikifika, kabla adhabu hiyo haijatekelezwa, anakuja daktai kukupima kuhakikisha ni mzima na uko bukheri wa afya, ikikutikana unaumwa hata kichwa tuu, utatibiwa kwanza, upone ukiwa mzima kabisa ndipo ashabu itekelelezwe!. Kwa msio jua, hata ile siku Saadam Husein alinyongwa, alivishwa suti!, hata Osama kabla hajazikwa baharini, aliswaliwa Kiislamu na kuzamishwa kwa kuelekezwa upanda wa Kibla!.
Diplomasia.
Tanzania tunapojianjaa kuingia kwenye Mtangamano wa nchi za Jumuiya ya Afika Mashariki, yunatakiwa kuanza kujihesabu sisi wote ni watu wamoja, hakuna Mtanzania, Mkenya, Mganda, Mrwanda. Mrundi au Msudani, we are all one!, hivyo vitendo vyovyote vya kumbagua mtu kwa utaifa wake ni ubaguzi, tukumbuke tuna Watanzania wengi nchi za wenzetu, na huko pia wanafanya uhalifu, kama ndio kwanza tunaanza kushikishana mabango ya mimi mwizi, tunakwenda wapi?!.
Uzalendo
Kuna baadhi ya matukio yakitokea, tunapaswa kuyanyamazia kwa kutanguliza uzalendo ili kuificha siri ya jinsi tunavyowatendea wenzetu, lakini watu wanaojitanabaisha kuwa ni watetezi wa haki za binaadamu, kunapotokea mizania ya kutanguliza nini mbele kati ya uzalendo na ukiukwaji wa haki za binaadamu, natanguliza haki kwanza, ndipo uzalendo kwa nchi yangu unafuatia!. Tanzania tunapaswa tutende haki kwanza, ndipo tuje kwenye uzalendo.
Chuki Dhidi ya Wakenya.
Pia najua kuna members humu wenye chuki dhidi ya Wakenya, hivyo watautumia uzi huu kushangilia chuki zao!, chuki hizi zinatokana na wenzetu Wakenya kuwa sharp zaidi katika kuchangamkia fursa, na wako faster to grab oppotunities, huku sisi Watanzania ni wavivu, hatujitumi, na tuko slow kuchangamkia fursa, hali inayopelekea hata baadhi ya fursa nyingi ambazo ni zetu Watanzania zimeshikwa na Wakenya, kisa Watanzania tumelala!.
Kinachotakiwa kwetu sisi Watanzania sio kuwachukia Wakenya kwa mafanikio yao, bali ni kwa sisi kuchangamka na kushindana nao!, tunapoelekea kwenye utangamano, tutafikia kipindi tutakuwa nchi moja, ndani ya serikali moja tukitumia pasipoti moja, na sarafu moja, ajira ni popote!, Watanzania tusipochangamka, then kila mahali, kila sekta, kila ajira nzuri zitakuwa ni Wakenya!.
Hapa tuu tulipo, tuna mabenki yao matatu, kule kwao hatuna hata benki yetu moja!, kwenye soko letu la hisa DSE, tunamakampuni yao zaidi ya 6!, kule kwenye soko lao, hatuna kampuni ya Kitanzania hata moja!.
Dawa sio chuki bali kushindana!.
Hitimisho.
Ni matumaini yangu, vyombo husika vitaliona hili na kulichukulia sio tukio simple la wizi, bali ni tukio sensitive la udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za msingi za binaadamu, hivyo kuchukua hatua stahiki kuhakikisha tukio kama hili halijirudii.
Nawatatakia Furahi Dei Njema.
Pasco.
Pasco wa jf sio mtetezi wa wezi, bali ni mzalendo na mpigania haki za binaadamu anayeamini haki, utu na uhai, unathamani kuliko materia thing yoyote inayoibiwa!.
Someni hapa chini kisa cha
Mwizi anusurika kufa mabibo hostel |
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality ...
Chan. Ten:Inastahili Pongezi kwa "Freedom of Expression, Watangaza ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ..
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili .
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki .
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote .
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Naibu Spika Anna Makinda ni Dikteta! |
Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu Unaofanywa na ...
Kutoka Geneva: Prof Mchome atoa msimamo kuhusu mpango wa ..
Je, Kila utumbuaji ni wa haki, au kuna kumkomoa Kikwete .
Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani! | J
Kitendo Cha Rev. Mtikila Kugomea Arrest!, Kinastahili Pongezi ...
Wito kwa Baba *****: Watendee Haki Kina ***** Wote Ili Nao Wapate ...
Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu wali-teswa ...

Rejea nyingine za Pasco kwenye utetezi wa haki za binaadamu ni hiziNimeishi hapo Mabibo hostel, Block F kwa miaka 4, kumetokea incidents nyingi za wizi na watu kuuliwa!, kiukweli nothing justifies taking someones life kwa wizi wa kitu chochote, material thing!, iwe ni simu, laptop au pc, kitu chochote cha thamani, kwa hakuna kitu chochote duniani chenye thamani zaidi ya life!, ila wanafunzi wa hapo kutokana na mob psychology, wanageuka sio binadamu tena, ni ma wild beast!, kama vichaa!.
Wakati nikiwa mwanafunzi wa UDSM, nikiwa naishi hapo Mabibo Hostel, kuna mwanafunzi aliuliwa kwa kusingiziwa tuu mwizi na demu wake!, baada ya fema kutoa kilio cha mwizi!, watu walimshushia kipigo huyo kijana bila hata kuuliza kaiba nini?, by the time wale auxilary polisi wamefika eneo la tukio, wanafunzi walikuwa ni wengi wamemzingira huyo kijana na hawakumwacha mpaka walipohakikisha wameua!, huku wakishangilia kwa hamasa na furaha ya ushujaa wa kuua mwizi!.
Kesho yake baada ya kujulikana aliyeuwawa ni nani, na aliyepiga yowe la mwizi ni nani, ndipo room mate wa yule girlfried wake akaumia kwa kitendo alichotendewa huyo mvulana wa watu!, akaleak data kuwa kijana yule, hakuwa mwizi, bali alikuwa ni boyfriend aliyepigwa tuu kibuti!, akaja kuomba msamaha, akafukuzwa kama mbwa!, jamaa akagoma kutoka room na kusema hatoki hadi msamaha wake ukubaliwe!, demu akamwambia, usipotoka nakuitia mwizi!, jamaa akagoma, akaitiwa mwizi na kilichomkuta ni kifo!.
Incident nyingine kama hiyo ilitokea tena, nikajaribu kuwazuia watu wasiue kwanza, angalau tuulize nani kaibiwa na kaibiwa nini!, watu wenye uchu wa kuua wakataka kunigeukia mimi kwa kunipa kipigo eti ndio natetea wezi!, nikawakumbushia tukio la kifo cha yule kijana aliyesingiziwa mwizi, japo hawakutulia waliendelea kupiga ila at least nilifanikiwa to save his life japo alishapigika sana!. Kiukweli japo Mabibo Hostel ni jamii ya wasomi wa chuo kikuu, lakini kwenye mob psychology, wana loose all senses of reasoning na kuachana kabisa na utu, na badala yake kugeuka wananyama kabisa!, hawana tofauti yoyote na wale wahuni wa Manzese!.
Poleni kuibiwa, but its shame mwizi wa kuku kupigwa hadi kifo au kuchomwa moto huku watu wamehamasika na kushangilia kuitoa roho ya binadamu mwenzao kwa wizi wa kitu kidogo kama kuku!, huku mujizi ya rrasilimali zetu, kama yale mabilioni ya EPA, yakiachwa bila kufanywa chochote huku serikali yetu, ikiyaomba majizi hayo kurejesha kile ilichokwapua as if waliazima tuu ile mihela!.