Bango la "Mwizi Mkenya!" Mlimani City ni Ubaguzi!, Udhalilishaji!, na Very Undiplomatic Gesture!.

Unafiki ni kitu kibaya sana... Naona watu mnatetea ujinga eti kadharilishwa kwa namna ipi labda?!!.. Mtu kaiba tena mlimani city sehemu ambayo kama umewahi kufika kwa miundombinu ya pale ilivyo mtu huwezi kupakaziwa umeiba... Ukiambiwa umeiba mlimani city wewe ni mwizi kweli huyo sio Wa kwanza madada wengi tu wamekuwa wakikamatwa na wengine hukiri pale pale kuwa waliiba kweli na kutoa mpaka bidhaa hapo hapo.... Acheni kutetea ujinga nendeni duka husika mkachukue video clip ya CCTV camera muone alivyoiba...

Suala lingine kuhusu bango.... Acheni unafiki jamani kwani huyo dada akitolea front page gazetin na kuandikiwa mwizi kutoka Kenya akamatwa m.city kungelikuwa na tofauti ipi na kushikishwa bango....

All in all kiafrika mwizi huna haki mikonon mwa waibiwa.. Huwezi kutuibia halafu utupangie tukufanye nini.

Tena tushukuru hajapgwa fire

exactly, atakuwa mwizi aliyekubuu, sehemu kama mlimani city na security iliyopo pale lakini alipata ujasiri wa kuiba, kweli hapana chezea kenyan women
 
Kwani wakenya walimtuma? Hakuna haja ya kututea wezi Kwa kisingizio cha diplomasia. Wabebeshe mabango hata mwezi mzima tuwafahamu iwe Mkenya, wamsoga au wa chato.
Tupunguze mihemko jamani, hili ni suala la kijamii lenye kuhitaji tafakuri ya kina. Pasco is right. Vipi ikiwa huyu mtuhumiwa akapelekwa mahakamani na baadaye ikaja kugundulika ni mgonjwa wa akili? Mtaendelea kuhemka?
 
Mwizi ni Mahamakama ndiyo imethibitisha au watu wamejifanya mahamakama na kumuhukumu, tuwe na utaratibu wa kufuata taratibu na sheria za nchi, je kama huyo msichana ana ugonjwa wa akili?
 
WE UNASEMA NN ATI? Kwan cha ajabu ni kipi? Huyo si mwizi kweli au kasingiziwa? Au we unatetea wezi?? Na si kweli anatokea Kenya au we ulitaka wezi wote watokee Tandale?
Acha atangazwe ili ajulikane mapema kabla hajaleta madhara zaid ya wizi, Watu wengi tumemjua kupitia hiyo picha, je wasingemtangaza then kesho akakuibia wewe, ungefurahi, au una kauhusiano nae hivyo imekugusa??...ngoja na mie niendelee kuituma kwenye magroup ya whatsapp wamjue vizuri ila wawe na tahadhari pindi wamwonapo...huku kwetu wezi wanachomwa moto kabsa..nini kutangazwa bana.. dada unakuwa mwivi kah, SHAME ON HER!!!
Shida ndio iko hapo...ni mwizi kweli?
Ana akili timamu?
Zipi ni sababu za kuiba?

Huko Italia mwaka fulani nyakati za Mafia, mama mmoja aliamriwa na watu waliomteka nyara binti yake akaibe mkufu kwa sonara ili binti yake aachiwe. Mama wa watu akakamatwa akiwa ameuficha kwenye 'kofuli' anajaribu kutoka. Kwenye sekeseke la kumkabili mwizi, mlinzi alijikuta ameibiwa gobole lake na Mafia wakajitwalia dhahabu zao kiulaiiiiini. Yule mama aliachiwa baada ya kuthibitika kuwa binti yake alitekwa...hapo utaona haja ya kuacha sheria iamue na kuhukumu. Mbona tunahemuka?
 
What if angekuwa mwizi kUtoka tanzania? Acheni watu walipie matendo yao. wewe hujawahi kuibiwa ukaona inavyouma? Huko polisi hata ukimpeleka mwizi hakuna la maana wanafanya. Acha waadhibiwe tu kikubwa wasiwaue
 
Mwizi ni adui wa raia wema. Mbona polisi wana wawekea mabango wahalifu na kuwapiga picha kwa kumbukumbu zao. Mbona China ina toa orodha ya wahalifu toja nchi mbali mbali duniani. Wakenya ni wadhalilishaji wakuu kwao hata hapa huwapiga mno viboko watoto wetu katika shule zinazo endeshwa na wao.
 
What if angekuwa mwizi kUtoka tanzania? Acheni watu walipie matendo yao. wewe hujawahi kuibiwa ukaona inavyouma? Huko polisi hata ukimpeleka mwizi hakuna la maana wanafanya. Acha waadhibiwe tu kikubwa wasiwaue
Kuadhibiwa aadhibiwe ndio lakini si kumbebesha bango linalowakilisha kwamba wakenya wote ni wazi.
 
Haikuwa haki kabisa! Wamefanya kinyume na utu! Wezi wangapi wanakamatwa hapa, hatujawahi kuona bango likisema , mm ni mwizi kutoka Moshi, Mwanza....!

Nalaani udhalilishaji
Kweli mkuu. Hapa Nairobi kuna vijana wa kitanzania wengi sana hukamatwa wameiba lakini hawabebeshwi mabango ya kudhalilisha nchi namna hii.
Hata mwaka juzi kuna rafikiangu nilisoma nae alichomwa moto hadi kufa hapa Kenya kwa kuiba pikipiki. Lakini hatukuona akibebeshwa bango.
 
Maelezo mareeeeefu ati ya kumtetea mwizi, kwa kua ni mwanamke, kwa kua ni mkenya au kwa kua unamjua?

Haki za binaadam my foot, wakati anaiba hakujua kua hatendi haki kwa binaadam wenzie??

Mwizi sio raia wa Tz, kwanini asitajwe utaifa wake??

Amekamatwa papo kwa hapo hlf useme sio mwizi mpk mahakama iseme kwa hiyo alikua anawahifadhia??

Acheni ujinga wenu bhana, msitake kuhalalisha haramu iwe halali, hilo haliwezekani na kamwe halitawezekana.
Hapo ndio nachoka na sheria eti mpk uchunguzi umalizike wakati nimemkuta anachukua sio chake kabisa na kukiri nimkamate nimpeleke mahakamani waje wengine wasiomuona alivyochukua na kukiri, wamtetee kua hajachukua wakati mie ndio nimemuona na nimemkamata...sheria upuuzi ndio maana wanauliwa tuu!!!
 
Kweli mkuu. Hapa Nairobi kuna vijana wa kitanzania wengi sana hukamatwa wameiba lakini hawabebeshwi mabango ya kudhalilisha nchi namna hii.
Hata mwaka juzi kuna rafikiangu nilisoma nae alichomwa moto hadi kufa hapa Kenya kwa kuiba pikipiki. Lakini hatukuona akibebeshwa bango.
Kwahiyo mkuu mtu kuchomwa moto hadi kufa kwako lilikua jambo jema ila kubebeshwa bango na kuanishwa uhalisia wako ndio linaonekana kukukera kabisa!!!aisee
 
Kwahiyo mkuu mtu kuchomwa moto hadi kufa kwako lilikua jambo jema ila kubebeshwa bango na kuanishwa uhalisia wako ndio linaonekana kukukera kabisa!!!aisee
Alichomwa moto baada ya kushikwa na wananchi wenye hasira kali.

Ninachokipinga mimi ni kumtumia huyo mwizi aliyekamatwa milimani city kuwawakilisha wakenya wote.
 
Back
Top Bottom