Ni kitu gani kilikuwa kinafanyika shuleni uliona cha kawaida, lakini umekuja kugundua ilikuwa unyanyasaji na udhalilishaji?

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
Tukiwa shule, tulikuwa tukifikiria ni kawaida kwa walimu au wanafunzi kufanya mambo ya udhalilishaji au ya kingono, au hata kutoa kejeli kwa wanafunzi wengine.

Lakini baada ya kuwa mtu mzima umegundua kwa vitendo hivyo sio vya kawaida ni vya udhalilishaji. Matendo haya si tu yanakatisha tamaa bali pia yanaweza kusababisha madhara ya kisaikolojia ambayo yanaweza kudumu maisha yote.

Kupitia ufahamu huu, ni muhimu kuchukua hatua kuzuia unyanyasaji wa kijinsia shuleni na kuhakikisha mazingira salama na yenye heshima kwa wanafunzi wote.
 
Kutenga wanafunzi kutokana na ufaulu wao, lengo lilikuwa zuri sana lakini wengi waliachwa na makovu kutokana na kutaniwa na kuchekwa.

Au kulikuwa na waalimu wanamuita mtoto mbele ya darasa na kuanza kuzomewa na wengine...
 
Tukiwa shule, tulikuwa tukifikiria ni kawaida kwa walimu au wanafunzi kufanya mambo ya udhalilishaji au ya kingono, au hata kutoa kejeli kwa wanafunzi wengine.

Lakini baada ya kuwa mtu mzima umegundua kwa vitendo hivyo sio vya kawaida ni vya udhalilishaji. Matendo haya si tu yanakatisha tamaa bali pia yanaweza kusababisha madhara ya kisaikolojia ambayo yanaweza kudumu maisha yote.

Kupitia ufahamu huu, ni muhimu kuchukua hatua kuzuia unyanyasaji wa kijinsia shuleni na kuhakikisha mazingira salama na yenye heshima kwa wanafunzi wote.
Wakati nasoma shule ya msingi, wavulana tulikua na tabia ya kuja na vipande vya vioo vidogo shuleni, kisha tunavizia wadada na kuwachungulia kwa kuweka kioo chini ya miguu yao, tulikua tunajiona wajanja sana kufanya hivyo, ila sasa hivi nikifikiria hicho kitendo, naona tulikua tunafanya udhalilishaji mkubwa kwa kina dada, Mungu atusamehe.
 
Kuna jamaa alimchungulia demu wa shule akaja nisimulia, alikula mbata moja akazimia.
 
Viboko / Mboko zile umeinama ka unachuma mchicha unaambiwa shika vidole gumba kabla tu ya kushika ushapata tatu za motooo
 
Walimu wa Kiume kuvuta mikanda ya Sidiria ya Watoto wa kike kwa begani.
Shuleni kwetu Kuna Mwalimu alikuwa anapenda kuwatukana Wavulana Mijusi halafu Wasichana alituita Vitumbua

Kuwatenga Wanafunzi kwenye Mdarasa kutokana na Ufaulu
Kuwafinya Watoto wa kike mapajani kwa kuingiza mikono ndani ya sketi
Kupika na kufanya usafi kwenye Nyumba za Walimu, wanatutuma hadi Sokoni na kutubebesha Mizigo

Mambo ni mengi aisee ambayo siku hizi nayaona ya ovyo mno
 
For the first time leo ndio nimeona comment yako mkuu, by the way I do love you...😘
 
viboko kuwa too much na adhabu nyingine kichurachura, kushika masikio, kubeba mawe
 
Back
Top Bottom