Bango la "Mwizi Mkenya!" Mlimani City ni Ubaguzi!, Udhalilishaji!, na Very Undiplomatic Gesture!.

EEEEh, mbona hii ni issue yakawaida sana. mbona wezi wa tanzania huwa wanabebeshwa mabango na wanapigwa picha huyo wa kenya si ni mwisi kama aiba akuje na abebeshwe mabago maana yeye yuko mwisi na watu ya kenya waone kuwa mtu yao ni mwisi. Hakuna uzalilishaji hapo alicho fanya ni wizi kutoka kenya. Mbona wachina wakikamata punda wanawapiga picha na wana alocate kama ni mtz au mnigeria wanaweka jina. Hapo wanamsaidia huyo dad from her self maana tabia yake ni mbaya wizi. Tena anapingana na sera ya Kazi tu anapaswa achukuliwe hatua.
 
Wanabodi,

Nimesoma mahali kutokea kwa tukio la wizi eneo la Mlimani City,
CnWQ33pXgAA_4-N.jpg:small

Msichana kutoka Kenya atuhumiwa kwa wizi M. City, atembezwa na ...
mwizi huyo ni mwanamke kutoka nchini Kenya. Baada ya kukamatwa, kabla hajakabidhiwa kwa vyombo husika, walimtia kibano, kisha kumshikisha bango lililoandikwa "Mimi ni Mwizi Kutoka Kenya!" na kumtembeza ili watu wamuone!.

Hata kama kweli ni mwizi, lakini kitendo alichofanyiwa huyu dada sio tuu ni udhalilishaji wa hali ya juu, ni kinyume cha haki za binaadamu!, na pia ni ubaguzi wa hali ya juu wa kikanda, unaoweza kujenga chuki sio tuu dhidi ya mwizi aliyekamatwa, bali kwa Wakenya wote, hivyo hapa aliyedhalilishwa sio bidada mwizi kutoka Kenya pekee, bali nchi nzima ya Kenya na Wakenya wote walioko nchini kufuatia binti yao kukamatwa akiiba, hivyo kujenga posibilty ya kila Mkenya kuwa mwizi!, jambo ambalo sio zuri kidiplomasia, hivyo linapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa wahusika wakuu wa udhalilishaji huu kuchukuliwa hatua kali, ya mwanzo ikiwa ni kutimuliwa kazi, na kupandishwa kizimbani kwa udhalilishaji wa raia wa Kenya asiye na hatia!.

Waungaji Mkono Udhalilishaji Huu.
Najua kuna watu wata support udhalilishaji huo, kwa hoja kuwa kweli bidada huyo ni mwizi kwa sababu ameshikwa ready handed, na pili kweli ni bidada huyo ni raia wa Kenya, hivyo kwa vile ni kweli ni mwizi na ni kweli ni Mkenya, then alichofanyiwa ni haki yake!. Na wengi wataokasuppot hili, wataunganisha na uchungu wa kuibiwa, hivyo kwao hata adhabu ya kushikishwa tuu bango, ni ahabu ndogo, wangewish apate kipigo haswa cha mbwa mwizi, hadi auliwe kwa kipigo au hata kuchomwa moto!. Hawa sitawalaumu, ni levels tuu za uelewa masuala ya haki, kwao mwizi hana haki, hata mwizi wa kuku, adhabu ya kifo kwa kuchomwa moto kwao ni adhabu stahili au stahiki!.

Utawala wa Sheria (The Rule of Law).
Sisi Tanzania ni nchi ya haki inayofuata mfumo wa utawala wa sheria, "the rule of law" tunafuata mfumo wa sheria tuliorithi kutoka kwa Waingereza, mamlaka pekee yenye kuweza kum declare mtu ni guilt ni mahakama pekee, hivyo everybody is "presumed innocent until proven guilt" tena "by the court of competent jurisdiction", hivyo kitendo cha kumshikisha bango kumuita mwizi ni kumhukumu an innocent victim bila kumfikisha kwenye vyombo halali vya kisheria!.

Wizi ni Tabia ya Mtu sio Tabia ya Nchi
Wizi ni tabia ya mtu, mtu yoyote anaweza kuwa kuwa mwizi, kama lengo lilikuwa ni kumdhalilisha ili kumuaibisha mwizi huyo mbele ya umma kuwa bidada ni mwizi, then bango lingeishia kwa maneno "mimi ni mwizi!" hakukuwa na sababu kuiweka nchi yake yote ya Kenya, kuonyesha yeyote anayetoka Kenya, ana possibility kuwa mwizi!.

Haki za Binaadamu.
Hata kama ni kweli kweli bidada yule ni mwizi, hata mwizi anastahili heshima kwa kutokudhalilishwa utu wake kwa kumfanya a subject to ridicule!. Hata wauwaji pia huwa wanastahili heshima na utu, na hata wanaohukumiwa kunyongwa, wananyongwa kwa utu na heshima fulani, na hata ikitokea siku yako ya kunyongwa ikifika, kabla adhabu hiyo haijatekelezwa, anakuja daktai kukupima kuhakikisha ni mzima na uko bukheri wa afya, ikikutikana unaumwa hata kichwa tuu, utatibiwa kwanza, upone ukiwa mzima kabisa ndipo ashabu itekelelezwe!. Kwa msio jua, hata ile siku Saadam Husein alinyongwa, alivishwa suti!, hata Osama kabla hajazikwa baharini, aliswaliwa Kiislamu na kuzamishwa kwa kuelekezwa upanda wa Kibla!.

Diplomasia.
Tanzania tunapojianjaa kuingia kwenye Mtangamano wa nchi za Jumuiya ya Afika Mashariki, yunatakiwa kuanza kujihesabu sisi wote ni watu wamoja, hakuna Mtanzania, Mkenya, Mganda, Mrwanda. Mrundi au Msudani, we are all one!, hivyo vitendo vyovyote vya kumbagua mtu kwa utaifa wake ni ubaguzi, tukumbuke tuna Watanzania wengi nchi za wenzetu, na huko pia wanafanya uhalifu, kama ndio kwanza tunaanza kushikishana mabango ya mimi mwizi, tunakwenda wapi?!.

Uzalendo
Kuna baadhi ya matukio yakitokea, tunapaswa kuyanyamazia kwa kutanguliza uzalendo ili kuificha siri ya jinsi tunavyowatendea wenzetu, lakini watu wanaojitanabaisha kuwa ni watetezi wa haki za binaadamu, kunapotokea mizania ya kutanguliza nini mbele kati ya uzalendo na ukiukwaji wa haki za binaadamu, natanguliza haki kwanza, ndipo uzalendo kwa nchi yangu unafuatia!. Tanzania tunapaswa tutende haki kwanza, ndipo tuje kwenye uzalendo.

Chuki Dhidi ya Wakenya.
Pia najua kuna members humu wenye chuki dhidi ya Wakenya, hivyo watautumia uzi huu kushangilia chuki zao!, chuki hizi zinatokana na wenzetu Wakenya kuwa sharp zaidi katika kuchangamkia fursa, na wako faster to grab oppotunities, huku sisi Watanzania ni wavivu, hatujitumi, na tuko slow kuchangamkia fursa, hali inayopelekea hata baadhi ya fursa nyingi ambazo ni zetu Watanzania zimeshikwa na Wakenya, kisa Watanzania tumelala!.

Kinachotakiwa kwetu sisi Watanzania sio kuwachukia Wakenya kwa mafanikio yao, bali ni kwa sisi kuchangamka na kushindana nao!, tunapoelekea kwenye utangamano, tutafikia kipindi tutakuwa nchi moja, ndani ya serikali moja tukitumia pasipoti moja, na sarafu moja, ajira ni popote!, Watanzania tusipochangamka, then kila mahali, kila sekta, kila ajira nzuri zitakuwa ni Wakenya!.

Hapa tuu tulipo, tuna mabenki yao matatu, kule kwao hatuna hata benki yetu moja!, kwenye soko letu la hisa DSE, tunamakampuni yao zaidi ya 6!, kule kwenye soko lao, hatuna kampuni ya Kitanzania hata moja!.

Dawa sio chuki bali kushindana!.

Hitimisho.
Ni matumaini yangu, vyombo husika vitaliona hili na kulichukulia sio tukio simple la wizi, bali ni tukio sensitive la udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za msingi za binaadamu, hivyo kuchukua hatua stahiki kuhakikisha tukio kama hili halijirudii.

Nawatatakia Furahi Dei Njema.

Pasco.
Pasco wa jf sio mtetezi wa wezi, bali ni mzalendo na mpigania haki za binaadamu anayeamini haki, utu na uhai, unathamani kuliko materia thing yoyote inayoibiwa!.

Someni hapa chini kisa cha
Mwizi anusurika kufa mabibo hostel |

Rejea nyingine za Pasco kwenye utetezi wa haki za binaadamu ni hizi
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality ...
Chan. Ten:Inastahili Pongezi kwa "Freedom of Expression, Watangaza ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ..
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili .
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki .
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote .
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Naibu Spika Anna Makinda ni Dikteta! |
Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu Unaofanywa na ...
Kutoka Geneva: Prof Mchome atoa msimamo kuhusu mpango wa ..
Je, Kila utumbuaji ni wa haki, au kuna kumkomoa Kikwete .
Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani! | J
Kitendo Cha Rev. Mtikila Kugomea Arrest!, Kinastahili Pongezi ...
Wito kwa Baba *****: Watendee Haki Kina ***** Wote Ili Nao Wapate ...
Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu wali-teswa ...

Hakuna udhalilishaji wa Kenya kama nchi wala kwa Wakenya ambao hawajahusika na wizi huo hapo.Bango alilobebeshwa huyo mdada ni lenye nafsi binafisi ya mhusika 'mimi ni mwizi' na si ya wingi kwa maana ya 'sisi wakenya ni wezi',na kwa kuwa aliyeiba ni raia wa kenya ni vizuri tumtabue kuwa kumbe mwizi wetu ni mkenya.Binafsi nakubaliana na adhabu hiyo.
Kwa wale tunaokumbuka mlimani city kumekuwa na matukio ya wizi sana pale na kwa hadhi ya sehemu ile ambayo hutembelewa na foreigners wengi,watanzania tumekuwa tukionekana si watu waliostaharabika kwa wenzetu hawa,ambapo pia wamekuwa mstari wa mbele kutukashifu kwa tabia hizo chafu,kwa picha hii inaonyesha kuna mamiruki wanaotoka huko nje kuja kutuchafulia hadhi na ustaharabu wetu Watanzania.
"Happy Tanzania"
 
Akiwa mgonjwa Wa akili atakua hajaiba?. Kwanza mgonjwa Wa akili hachukui Kwa kujificha wakati mwingine hutumia nguvu pia
 
Wezi wanavishwa matairi wanachomwa moto wewe unaleta ujinga hapa eti kushikishwa bango ni udhalilishaji...wabebeshwe tu mabango hamna namna tumechoka@ Pasco.
 
Mwizi ukimpata kwenye angle wee tambaa na kichwa chake maana ukichelewa kidogo tu akipata upenyo anakuzawazisha mazima!
 
Hivi watanzania sijui nani kawaloga? ujuaji mwingi sana na kujiona wamestaaribika sana. Mtu kaiba, nchi anayotoka ni Kenya, watu wamekuwa waungwana hawajampiga, ila wamemuadhibu kistaarabu kwa kujitanganza, watu mnaleta upuuzi wa haki za binadamu, angekuwa binadamu huyo angeiba? Mlishasikia ni namna gani watanzania wakiiba huko Kenya yanayowakuta?? Acheni siasa watanzania, ndiyo maana hatupigi hatua.
Mkuu umenena ukweli.mtupu. Kuna watu wanadhani wanashule sana au wamestaarabika sana kumbe tu nikwasababu hayajawahi mfika. Ukikataa kumuita mkenya basi tusisema kuwa mwanakmke kwani pia inaweza leta shida kwa watu wanaohali mabo ya kijinsia kwasababu inaweza onekana ametumwa na wanawake wenzake. Je hilo linawezekana? Mimi nimeshangaa tu kuona kuwa hajaumizwa mpaka hapo alipo nna sio vinginevyo. Mwizi hawezi kuwa rafiki yangu na siwezi mtetea. Naogopa tu pale ambapo sina ushahidi kuwa kweli kaiba ili nisije mhukumu mtu asiyegusika ila ikithibitika kuwa kweli kaiba,ntaleta na msemeno wakukata mkono na mguu kabisa.
 
1. Bango limeandikwa "Mimi ni mwizi kutoka Kenya" SIO "Mimi ni mwizi mwanamke"!
Ingekuwa hivyo neno "mwanamke" nalo lingekuwa limetumika kwa nia mbaya, kwa sababu kitendo cha wizi kilichofanyika na jinsia ya aliyefanya hicho kitendo havina uhusiano wowote.

2. Context inaonesha phrase "kutoka Kenya" imetumika kwa nia mbaya, kwa sababu ilikuwa an unnecessary qualifier na haina uhusiano na kitendo kilichofanyika. Yapo mazingira ambayo yangeruhusu kutumika kwa jina "Kenya" bila kuonesha kuwepo kwa nia mbaya. Mfano ni pale basic 'biographical data' zinapotolewa to fully identify the person.

3. Unaposema "... ila akithibitika" una maana gani? Ni wapi na lini mtu anathibitika kutenda kosa?
 
Nilikuwa naandika comment as this lakini umemaliza!! Pasco ona hii hapa chini
Sasa Pasco unalalamika anadhalilishwa na wewe unaweka picha yake na bango humu, huoni nawe unaendelea kumdhalilisha.

Unatakiwa uongezwe kama mshitakiwa kwenye hii kesi ya udhalilishaji
 
Mi kurudia hilo picha ndio nimezidi kumuona huyu Pasco ni kichwa maji..ila kwa utetezi huo wa nguvu nyingi kwa hawa wezi wa Kenya ningeomba utembelee huku Mombasa
 
Mbona magazeti huwa yanaandika mwizi wa bank ya NMB raia wa ..... amekutwa na hatia. BTW hata rais wao uhuru aliwahi kukiri kuwa wananchi wake ni hatari kwakwiba
 
Wanabodi,

Nimesoma mahali kutokea kwa tukio la wizi eneo la Mlimani City,
CnWQ33pXgAA_4-N.jpg:small

Msichana kutoka Kenya atuhumiwa kwa wizi M. City, atembezwa na ...
mwizi huyo ni mwanamke kutoka nchini Kenya. Baada ya kukamatwa, kabla hajakabidhiwa kwa vyombo husika, walimtia kibano, kisha kumshikisha bango lililoandikwa "Mimi ni Mwizi Kutoka Kenya!" na kumtembeza ili watu wamuone!.

Hata kama kweli ni mwizi, lakini kitendo alichofanyiwa huyu dada sio tuu ni udhalilishaji wa hali ya juu, ni kinyume cha haki za binaadamu!, na pia ni ubaguzi wa hali ya juu wa kikanda, unaoweza kujenga chuki sio tuu dhidi ya mwizi aliyekamatwa, bali kwa Wakenya wote, hivyo hapa aliyedhalilishwa sio bidada mwizi kutoka Kenya pekee, bali nchi nzima ya Kenya na Wakenya wote walioko nchini kufuatia binti yao kukamatwa akiiba, hivyo kujenga posibilty ya kila Mkenya kuwa mwizi!, jambo ambalo sio zuri kidiplomasia, hivyo linapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa wahusika wakuu wa udhalilishaji huu kuchukuliwa hatua kali, ya mwanzo ikiwa ni kutimuliwa kazi, na kupandishwa kizimbani kwa udhalilishaji wa raia wa Kenya asiye na hatia!.

Waungaji Mkono Udhalilishaji Huu.
Najua kuna watu wata support udhalilishaji huo, kwa hoja kuwa kweli bidada huyo ni mwizi kwa sababu ameshikwa ready handed, na pili kweli ni bidada huyo ni raia wa Kenya, hivyo kwa vile ni kweli ni mwizi na ni kweli ni Mkenya, then alichofanyiwa ni haki yake!. Na wengi wataokasuppot hili, wataunganisha na uchungu wa kuibiwa, hivyo kwao hata adhabu ya kushikishwa tuu bango, ni ahabu ndogo, wangewish apate kipigo haswa cha mbwa mwizi, hadi auliwe kwa kipigo au hata kuchomwa moto!. Hawa sitawalaumu, ni levels tuu za uelewa masuala ya haki, kwao mwizi hana haki, hata mwizi wa kuku, adhabu ya kifo kwa kuchomwa moto kwao ni adhabu stahili au stahiki!.

Utawala wa Sheria (The Rule of Law).
Sisi Tanzania ni nchi ya haki inayofuata mfumo wa utawala wa sheria, "the rule of law" tunafuata mfumo wa sheria tuliorithi kutoka kwa Waingereza, mamlaka pekee yenye kuweza kum declare mtu ni guilt ni mahakama pekee, hivyo everybody is "presumed innocent until proven guilt" tena "by the court of competent jurisdiction", hivyo kitendo cha kumshikisha bango kumuita mwizi ni kumhukumu an innocent victim bila kumfikisha kwenye vyombo halali vya kisheria!.

Wizi ni Tabia ya Mtu sio Tabia ya Nchi
Wizi ni tabia ya mtu, mtu yoyote anaweza kuwa kuwa mwizi, kama lengo lilikuwa ni kumdhalilisha ili kumuaibisha mwizi huyo mbele ya umma kuwa bidada ni mwizi, then bango lingeishia kwa maneno "mimi ni mwizi!" hakukuwa na sababu kuiweka nchi yake yote ya Kenya, kuonyesha yeyote anayetoka Kenya, ana possibility kuwa mwizi!.

Haki za Binaadamu.
Hata kama ni kweli kweli bidada yule ni mwizi, hata mwizi anastahili heshima kwa kutokudhalilishwa utu wake kwa kumfanya a subject to ridicule!. Hata wauwaji pia huwa wanastahili heshima na utu, na hata wanaohukumiwa kunyongwa, wananyongwa kwa utu na heshima fulani, na hata ikitokea siku yako ya kunyongwa ikifika, kabla adhabu hiyo haijatekelezwa, anakuja daktai kukupima kuhakikisha ni mzima na uko bukheri wa afya, ikikutikana unaumwa hata kichwa tuu, utatibiwa kwanza, upone ukiwa mzima kabisa ndipo ashabu itekelelezwe!. Kwa msio jua, hata ile siku Saadam Husein alinyongwa, alivishwa suti!, hata Osama kabla hajazikwa baharini, aliswaliwa Kiislamu na kuzamishwa kwa kuelekezwa upanda wa Kibla!.

Diplomasia.
Tanzania tunapojianjaa kuingia kwenye Mtangamano wa nchi za Jumuiya ya Afika Mashariki, yunatakiwa kuanza kujihesabu sisi wote ni watu wamoja, hakuna Mtanzania, Mkenya, Mganda, Mrwanda. Mrundi au Msudani, we are all one!, hivyo vitendo vyovyote vya kumbagua mtu kwa utaifa wake ni ubaguzi, tukumbuke tuna Watanzania wengi nchi za wenzetu, na huko pia wanafanya uhalifu, kama ndio kwanza tunaanza kushikishana mabango ya mimi mwizi, tunakwenda wapi?!.

Uzalendo
Kuna baadhi ya matukio yakitokea, tunapaswa kuyanyamazia kwa kutanguliza uzalendo ili kuificha siri ya jinsi tunavyowatendea wenzetu, lakini watu wanaojitanabaisha kuwa ni watetezi wa haki za binaadamu, kunapotokea mizania ya kutanguliza nini mbele kati ya uzalendo na ukiukwaji wa haki za binaadamu, natanguliza haki kwanza, ndipo uzalendo kwa nchi yangu unafuatia!. Tanzania tunapaswa tutende haki kwanza, ndipo tuje kwenye uzalendo.

Chuki Dhidi ya Wakenya.
Pia najua kuna members humu wenye chuki dhidi ya Wakenya, hivyo watautumia uzi huu kushangilia chuki zao!, chuki hizi zinatokana na wenzetu Wakenya kuwa sharp zaidi katika kuchangamkia fursa, na wako faster to grab oppotunities, huku sisi Watanzania ni wavivu, hatujitumi, na tuko slow kuchangamkia fursa, hali inayopelekea hata baadhi ya fursa nyingi ambazo ni zetu Watanzania zimeshikwa na Wakenya, kisa Watanzania tumelala!.

Kinachotakiwa kwetu sisi Watanzania sio kuwachukia Wakenya kwa mafanikio yao, bali ni kwa sisi kuchangamka na kushindana nao!, tunapoelekea kwenye utangamano, tutafikia kipindi tutakuwa nchi moja, ndani ya serikali moja tukitumia pasipoti moja, na sarafu moja, ajira ni popote!, Watanzania tusipochangamka, then kila mahali, kila sekta, kila ajira nzuri zitakuwa ni Wakenya!.

Hapa tuu tulipo, tuna mabenki yao matatu, kule kwao hatuna hata benki yetu moja!, kwenye soko letu la hisa DSE, tunamakampuni yao zaidi ya 6!, kule kwenye soko lao, hatuna kampuni ya Kitanzania hata moja!.

Dawa sio chuki bali kushindana!.

Hitimisho.
Ni matumaini yangu, vyombo husika vitaliona hili na kulichukulia sio tukio simple la wizi, bali ni tukio sensitive la udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za msingi za binaadamu, hivyo kuchukua hatua stahiki kuhakikisha tukio kama hili halijirudii.

Nawatatakia Furahi Dei Njema.

Pasco.
Pasco wa jf sio mtetezi wa wezi, bali ni mzalendo na mpigania haki za binaadamu anayeamini haki, utu na uhai, unathamani kuliko materia thing yoyote inayoibiwa!.

Someni hapa chini kisa cha
Mwizi anusurika kufa mabibo hostel |

Rejea nyingine za Pasco kwenye utetezi wa haki za binaadamu ni hizi
IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality ...
Chan. Ten:Inastahili Pongezi kwa "Freedom of Expression, Watangaza ...
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ..
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know ...
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili .
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki .
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote .
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Naibu Spika Anna Makinda ni Dikteta! |
Je, Huu Sio Uvunjaji wa Haki Za Msingi za Binaadamu Unaofanywa na ...
Kutoka Geneva: Prof Mchome atoa msimamo kuhusu mpango wa ..
Je, Kila utumbuaji ni wa haki, au kuna kumkomoa Kikwete .
Kagoda: Kamwe haitafikishwa Mahakamani! | J
Kitendo Cha Rev. Mtikila Kugomea Arrest!, Kinastahili Pongezi ...
Wito kwa Baba *****: Watendee Haki Kina ***** Wote Ili Nao Wapate ...
Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu wali-teswa ...
  1. PASCAL mie naona vyote vulivyoeleza ni vizuiri na vina mashiko haswa.Lakini uje tabia za watu zinajengwaje jenwaje.Ni hiyo ni muhimusana.Tena ukumbuke watu kama watu wanamaono namitizamo tofauti alafu hweleweki leo yuko hivi kesho vingine.Wakati mwingine hata yule aliyemshikisha hilo bango huenda naye ni mwizi.weli kufanya kazi kwake hapo mlimani city hajawahi kuibba kweli hata kalmu au bidhaa ndogondogo
 
Back
Top Bottom