Elections 2010 Bango hili la kampeni za uchaguzi la CCM silielewi

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,338
6,463
Bango moja la JK liko pale nyuma ya Ocean Road hospital au kama unaelekea NIMR au kwa Mkemia Mkuu wa serikali; lina picha ya JK na mwanamke ambaye inasemekana ni mama yake mzazi, halafu lina maandishi 'upendo wa mama, chagua ccm chagua JK'.

Sasa je, nimchague JK kwa sababu anapendwa au alipendwa sana na mama yake? Hili linaashiria kuwa Urais mwaka huu ni suala la kifamilia? Je, wamelenga watanzania wa aina gani wenye umri wa kupiga kura kwa bango hilo?
 
JK ameona viongozi wengi wa kiafrika jinsi walivyobinafsisha Ikulu kuanzia Misri na kwingineko kama Gabon n.k Aona mrith wake sasa atakuwa Ridhiwani na ndiyo maana wametutangazia uraisi ni suala la kifamilia
 
Afadhali yako bango moja limekukwaza mimi kichefuchefu kila bango nilionalo. kuna mabango ya
afya
wawekezaji
maabara
Hv si angejiunga na wasanii wenzake wa ze comedy
 
Mkuu basi yapo mawili ya aina moja, lingine kama hilo salenda opposite na stanbic bank Head office, hili bango linanikera sana hasa nikipita hapo asubuhi kwenda ofisini natamani nisisimame karibu nalo, hata mimi silielewi ina maana upendo wa mama yake ndiyo kigezo cha sisi kumchangua? je kuna uhusiano gani na uongozi wa taifa na mama yake? jamani aliye karibu na Makamba na Kinana tunataka maelezo, haya ni baadhi tu ya mabango yanayokera wananchi.
 
linaashiria kuwa Urais mwaka huu ni suala la kifamilia?
ndiyo kabisa, wife wake yupo mikoani, mtoto naye mikoani baba nae mikoani.....na akimaliza mwaka 2015...usishangae rizy nae kugombea urais....kisha mama nae atafuata 2025....
 
ndiyo kabisa, wife wake yupo mikoani, mtoto naye mikoani baba nae mikoani.....na akimaliza mwaka 2015...usishangae rizy nae kugombea urais....kisha mama nae atafuata 2025....

Too late.

Watanzania wa leo hawatembei wakiwa wamelala tena. (Mazuzu ni wachache kuliko waelewa)

Yeye ahesabu zake atambae.
 
Lile Bango la opp. na Stanbic mtoto wangu alidhani ni picha ya muigizaji gwiji wa filamu kwenye Jangwa la KALAHARI... "The Gods must be crazy" Xi na Mama yake Lol kweli tuna kazi kubwa mwaka huu...
 
Bango moja la JK liko pale nyuma ya Ocean Road hospital au kama unaelekea NIMR au kwa Mkemia Mkuu wa serikali; lina picha ya JK na mwanamke ambaye inasemekana ni mama yake mzazi, halafu lina maandishi 'upendo wa mama, chagua ccm chagua JK'.

Sasa je, nimchague JK kwa sababu anapendwa au alipendwa sana na mama yake? Hili linaashiria kuwa Urais mwaka huu ni suala la kifamilia? Je, wamelenga watanzania wa aina gani wenye umri wa kupiga kura kwa bango hilo?

Mkuu pole, mimi si hilo yaani yoote sasa yananikera sana, hivi mipesa yote iliyotumika kutengeneza mapicha ya kikwete huyu huyu msanii wetu wa myaka mitano nani asiye mfahamu hasa hapa bongo darisalaam, hadi kila baada ya hatua 10 iwekwe sanamu|picha yake? naiita sanamu make ukubwa wa hiyo mipicha kama sanamu vile!

Yaani huu ni ufisadi wa kutisha kwakweli ukilinganisha na hali duni ya shule na hospitali zetu afu watu wanapoteza mamilioni kutengeneza sanamu za msanii! grrrrrrrrrrrrrrr..
 
Mie jama nataka nichangie campaign za Jk kwa kudhamini bango moja lenye picha yake na wazee wa DSM pale karimjee hall alipowahutubia kuhusu mgomo wa wafanyakazi.
Msaada wangu una sharti dogo tu, kwamba yawekwe maneno ya kiongozi mkakamavu na jasiri mwenye msimamo thabiti Jk, 'WAFANYAKAZI HATA WAANDAMANE KWA MIAKA NANE MISHAHARA HAITAPANDISHWA NG'O!!'
 
Hivi kweli kuna mpango mdhubuti wa kuwaondoa hawa CCM vizuri kwenye uchaguzi huu...

Nawashauri chadema pia wachague mawakala wenye misimamo na uchungu wa nchi.... kwani wengi wanahongwa vijisenti na kuchakachua kura
 
Nyie akina Makamba na wenzenu wote wa hiko chama si bora mngejiita nyi nyi em tuu,kuliko kutuambukiza na sisi kusema si si em,tupotezeeni tafadhali,nyie bakini na nyi nyi em yenu tuu!!
 
Afadhali yako bango moja limekukwaza mimi kichefuchefu kila bango nilionalo. kuna mabango ya
afya
wawekezaji
maabara
Hv si angejiunga na wasanii wenzake wa ze comedy
mimi nachukia rangi yeyote ya kijani na njano.
 
Hayo mabango Kikwete aliyaweka ya kumtangaza (kwa wale wasiomjua, kama wapo), ila sasa naona yanachefua kila mtu. Yaani yamekula kwake.
 
Namie nimeiona kapiga bonge ya bugaluu, nadhani alikua anawakumbushia wale washikaki wake wa zamani mapigo yake, nafikiri picha nzuri angeweka ile wakati yupo msoga anawinda mbayuwayu.

Lakini kiukwelii CCM watueleze picha hizo za mgombea moja ni madawati mangapi ya watoto wanao kaa chini mashuleni?hivi kulikua na haja ya picha za huyu bwana mkubwa kuwa nyingi kipindi hiki kuliko 2005?

Jee? mabango hayo katika Wilaya Moja hatuwezi kupata vitanda japo kumi vya wajawazito? mama zetu watazaa na kulala sakafuni mpaka lini jamani?
IMG_6845.jpg
 
Huyu jamaa mimi ananitia kichefu chefu na hv nina mimba changa basi tena..
Hata nikiwa nimefungua TV walianza kumuonesha tu, na makampeni yake wanamweka mda mrefu, nasikia vibaya na kuzima TV.
Naamini hata mwanangu tumboni anaichukia CCM.
 
hivi kuna haja ya kuweka picha nyingi hivi??huyu si tunamjua ndo rais anayemaliza muda wake sasa picha zote hizo za nini??
 
Back
Top Bottom